Mkuu wangu habari nzuri tu, mimi hupitia hapa kijiweni japo mara moja kwa wiki kuwasoma wanafalsafa kama nyie.Habari Mkuu wangu Mkandara, ni kitambo sana kimepita!
Sijakuelewa kabisa kwenye uzi huu, kwanini unang'ata pande zote mbili? Mwanzoni kabisa umeonesha kuafikiana sana na alichodai mtoa mada, lakini papohapo unakuja kuafikiana tena na imani ya MgonjwaUkimwi ambayo imebezwa haswaa na mtoa mada, unasimama wapi? Maana hoja zao zipo mbalimbali kabisa, Africanism Vs Umagharibi. Unasimama wapi? Kumbuka kuwa kuna watu wengi nyuma yako, waoneshe pa kusimama usiwaache dailema!
Sisi sio vipofu wa utandawazi, bali hatupaswi kabisaaaa kuugeukia! USIMTUPE MBUZI MTONI KWA KUMUONA NG'OMBE AMEVUKA, UTAMUUA hata kama nae ana kwato!
Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa!
Labda nikufahamishe tu ya kwamba nimeyaunga mawazo yote mawili kwa sababu maalum ambazo zote zinafuata ukweli wa hali halisi iliyopo sasa hivi na pili hatuna haja ya kuendelea kuaminishwa hivo.
Niseme tu ya kwamba kizazi hiki ni VIPOFU kwa maana ya kwamba hawajui UKOLONI MAMBOLEO unafanya kazi vipi japo wanajua maana yake kwa elimu walofundishwa.
Pengine sii ajabu kabisa leo hii hakuna mtu anajua maana ya Ukoloni Mamboleo hivyo tunazidi kutopea ktk lindi la kutawaliwa kiuchumi pasipo kujua. Kuna kipande hiki kinachosema hivi:-
1. Neo Colonialism - Whereby multinational corporations continue to exploit the natural resources of the former colonies; that such economic control is inherently neo-colonial, and thus is akin to the imperial and hegemonic varieties of colonialism practiced by the empires of Great Britain, the United States, France, and other European countries...
Ningependa sana kumsikia Rais au mwanasiasa yeyote atakayeweza kusimama na kuzungumzia Neo - Colonialism, kisha tupime tulipo leo kama haitakuwa tumefanya kama walivyotaka wakoloni tufanye ama tume hivyo!..Nina hakika hadi napoandika hivi wakoloni tayari wameisha fika wanapotaka..
Labda kisome kipande hiki kidogo ambacho Kwame Nkurumah alikizungumzia kuhusu Ukoloni Mamboleo halafu nambie Je, hatufanyi watakavyo?.
Neo colonialism
1. Political control that can be exercised economically, linguistically, and culturally, whereby promotion of the culture of the neo-colonist country facilitates the cultural assimilation of the colonised people and thus opens the national economy to the multinational corporations of the neo-colonial country.