Elections 2010 Tutafakari hili kidogo

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,080
5,058
Kina mama wawili wanakuja nyumbani kwangu na kuniomba kadi ya CCM,wanaiangalia na kuandika namba zake wananirudishia hapo hapo wanaomba kitambulisho cha mpiga kura nacho wananakili baadhi ya mambo na kisha wananirudishia na kunishukuru.
Kabla hawajaondoka ninawauliza kwa nini wanafanya hivyo?Kwa sauti ya upole wananiambia kuwa wanataka wajue watu ambao ni mtaji wa CCM yaani wenye kadi na hati ya kupigia kura.
Kwa haraka silioni kosa lakini natamani nijue angalau yafuatayo,

  1. Kwa nini wafuate watu majumbani badala ya kuwaita kwenye ofisi za chama?
  2. Jambo hili linavunja taratibu zozote?
  3. Je katika siasa za ki mafia halitatuletea matatizo kwa familia ambazo sio wanachama?
Waungwana naomba tujadili
 
uliwapa za nini? ungewaambia huna kadi zote... si cha kadi ya chama au ya kupiga kura kwani kutokuwa na kadi ya chama au ya kupiga kura si kosa kisheria!
 
ndio maana nasema elimu ya uraia inahitajika sana.wew inaelekea una matatizoya kichwa,mtu humjui unampa hivyo vitu kwa sababu gani?hata ungemjua ni kosa kumwonyesha sembuse kumpa.nakupa pole
 
mkuu hapo ulichemka mbaya utampaje mtu kadi na kitambulisho cha kura, kweli elimu ya uraia bado
 
inaelekea mnafahamiana! otherwise usingea toa kabisa
 
inaelekea mnafahamiana! otherwise usingea toa kabisa

Ni kweli hawa ni waarabu wa pemba, kama ulikuwa kweli unataka ushauri usingewapa ila ungeuliza kwanza. lakini bado hakijaharibika kitu, kimsingi umekosea jambo sijui kama kuna sheria uliyovunja! na kama kweli wewe ni mzalendo na nenda katoe taarifa hizi polisi ( japo siwaamini sana nao maana....), kwenye ofisi za tume ya uchaguzi, kwa katibu mkuu wa CCM na kwa vyama vyote vingine vya siasa, ili kama CCM hawajui zoezi (????) hili waelewe kabisa walishaanza kuhujumiwa, na kwa vyama vingine vya siasa wajiweke tayari na kuandaa mikakati ya kuzuia wizi wa kura. Taadhari tu,kesho akija mwingine akikuambia umpe kadi yako ya kupigia kura ili akuhifadhie( maana kama umetoa kadi hiyo ikanakiriwa namba, hili pia lawezekana) hadi siku ya 31-10-2010, mwambie BABAAAAA HAPENDIIIIII!
 
Hukuwauliza juu ya wale ambao hawana kadi wala vitambulisho watawasaidiaje? na kama wao wanatafuta wenye kadi za ccm, je wale wenye kadi za vyama vingine hawana shida nao?
 
Nilishalizungumzia hili katika thread nyingine some days ago. CCM inashirikiana na NEC (Tume ya Uchaguzi, lakini pengine hao wanaopita na kukusanya details hawajui kitu gani hasa kinafanyika baada ya wao kuwasilisha ngazi za juu orodha zenye details za wanachama wao.

Nasikiavyo hawa wanaokusanya details hizo huliupwa kati ya 50,000 hadi 100,000 kufuatana na wingi wa majina yanayowasilishwa.

Baadaye hayo majina – na mengine kutoka kila kituo cha uandikishaji (nchi nzima - na hasa sehemu za miji zinazosadikiwa kuwa na wapinzani wengi) hupelekwa NEC.

Hizo orodha za majina ya wapiga kura ya wana-CCM yakifika kule makao makuu ya NEC, zinatafutwa orodha za majina ya wapiga kura kutoka vituo hivyo na kinachofanyika ni kuyaondoa, (au kuyahamishia kwenda kwenye orodha za majina ya vituo vingine vya mbali), majina yote yale mengine (ambao siyo ya wana-CCM).

Matokeo ya uharamia huu unaofanywa na NEC hauwi wa 100 per cent, lakini kwa kiasi kikubwa majina ya wale siyo wana-CCM yanavurugwa, kwa kuondolewa kabisa au kuhamishiwa katika orodha za vituo vingine.

Ndiyo maana kule jimbo la Temeke mwaka 2005 majina ya wapiga kura zaidi ya laki moja hayakuonekana katika orodha, wengi wao wakiwa wa vyama vya upinzani na hivyo kushindwa kupiga kura.

In fact mtindo huu wa kuwa-defranchise wapinzani ulianza kutumika hasa 2005, na umeigwa kutoka Zimbabwe, Ethiopia (katika uchaguzi wao wa 2005 na mwaka huu pia) na Kenya (wakati wa Moi 1992 na 1997).

Na ndiyo maana CCM haitaki kata kata kuwa na NEC huru, au pia kutomuondoa Chairman wake, L Makame ambaye anazeekea pale – kwani anaridhia hujuma hizo chafu. Nashangaa kwa nini vyama vikuu vya upinzani hawasusii uchaguzi – bila ya wawakilishi wao kuwamo ktk NEC.

Haya ninayowaambieni ni kweli kabisa, chunguzeni sana kwa nini CCM inakazania kufanya hivyo.
 
Ninawashukuru sana wote mliochangia.Ukweli ni kuwa watu hao walifika nyumbani kwangu na wakamkuta bint yangu na sio mimi binafsi kama nilivyoliwakilisaha.
Nimeonana na katibu wa tawi la CCM na nikamuuliza nae akajibu ya kuwa haya ni maelekezo toka ngazi za juu na si ya siri kwani lengo lao nikujua wanachama na potential wapiga kura wao.
Pia alieleza ya kuwa wanajaribu kuwadhibiti wanachama ambao wanaweza kuingia katika kura za maoni lakini si wapiga kura.
Nawashukuru ten na nitwajuza yatakayoendelea.
 
Ninawashukuru sana wote mliochangia.Ukweli ni kuwa watu hao walifika nyumbani kwangu na wakamkuta bint yangu na sio mimi binafsi kama nilivyoliwakilisaha.
Nimeonana na katibu wa tawi la CCM na nikamuuliza nae akajibu ya kuwa haya ni maelekezo toka ngazi za juu na si ya siri kwani lengo lao nikujua wanachama na potential wapiga kura wao.
Pia alieleza ya kuwa wanajaribu kuwadhibiti wanachama ambao wanaweza kuingia katika kura za maoni lakini si wapiga kura.
Nawashukuru ten na nitwajuza yatakayoendelea
.

Kwenye red: Uwongo huo. kura za maoni zinaanza mwaka huu tu, lakini usajili wa wana-CCM ulianza in 2005 elections na pamoja katika chaguzi ndogo baada ya hapo. Wasitufanye mafala. Uchaguzi wa Busanda CUf walilalamika sana kuhusu suala hili.
 
nilishalizungumzia hili katika thread nyingine some days ago. Ccm inashirikiana na nec (tume ya uchaguzi, lakini pengine hao wanaopita na kukusanya details hawajui kitu gani hasa kinafanyika baada ya wao kuwasilisha ngazi za juu orodha zenye details za wanachama wao.

Nasikiavyo hawa wanaokusanya details hizo huliupwa kati ya 50,000 hadi 100,000 kufuatana na wingi wa majina yanayowasilishwa.

Baadaye hayo majina – na mengine kutoka kila kituo cha uandikishaji (nchi nzima - na hasa sehemu za miji zinazosadikiwa kuwa na wapinzani wengi) hupelekwa nec.

Hizo orodha za majina ya wapiga kura ya wana-ccm yakifika kule makao makuu ya nec, zinatafutwa orodha za majina ya wapiga kura kutoka vituo hivyo na kinachofanyika ni kuyaondoa, (au kuyahamishia kwenda kwenye orodha za majina ya vituo vingine vya mbali), majina yote yale mengine (ambao siyo ya wana-ccm).

Matokeo ya uharamia huu unaofanywa na nec hauwi wa 100 per cent, lakini kwa kiasi kikubwa majina ya wale siyo wana-ccm yanavurugwa, kwa kuondolewa kabisa au kuhamishiwa katika orodha za vituo vingine.

Ndiyo maana kule jimbo la temeke mwaka 2005 majina ya wapiga kura zaidi ya laki moja hayakuonekana katika orodha, wengi wao wakiwa wa vyama vya upinzani na hivyo kushindwa kupiga kura.

In fact mtindo huu wa kuwa-defranchise wapinzani ulianza kutumika hasa 2005, na umeigwa kutoka zimbabwe, ethiopia (katika uchaguzi wao wa 2005 na mwaka huu pia) na kenya (wakati wa moi 1992 na 1997).

Na ndiyo maana ccm haitaki kata kata kuwa na nec huru, au pia kutomuondoa chairman wake, l makame ambaye anazeekea pale – kwani anaridhia hujuma hizo chafu. Nashangaa kwa nini vyama vikuu vya upinzani hawasusii uchaguzi – bila ya wawakilishi wao kuwamo ktk nec.

Haya ninayowaambieni ni kweli kabisa, chunguzeni sana kwa nini ccm inakazania kufanya hivyo.
muhh makubwa! 0ngera mkuu kwa kunihabarisha. Nilikuwa gizani. Mara zote huwa nashindwa kufahamu ni kwa nini majina yanakosekana kwenye vituo. Kumbe ndo mchezo huu.
 
Mmmh nina mashaka sana na hilo.

Kuna haja ya kulifatilia kwa kina, kwani hakika wananchi wengi wanaweza wakawa wanaingizwa mkenge pasi kujua athari kubwa itakayowafika mbeleni.

Wapi washtaki?wapi waripoti matendo kama hayo?-ni maswali ambayo wananchi wengi hujiuliza.

Amka: nenda katika chama chochote cha siasa makini utoe ripoti ya matukio kama hayo ambayo huyaelewi. Vyama kama vya upinzani vinaweza kuwa mhimili wa kufatilia na kuchochea uwepo wa uchaguzi huru endapo vikiwa vinapewa taarifa nyeti mapema. Pia zipo asasi za kiraia makini zinazofanya kazi katika masuala ya demokrasia, utawala bora na haki za binadamu, hawa nao ni miongoni mwa mahala makini pa kukimbilia.

Tuamke!kuwa na uchaguzi huru na wa haki ni jukumu la kila mmoja.!!
 
:pound:yatawashinda haoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Kwa kweli CCM wanaboa mpaka basi..Ningekuwa na uwezo ningewapoteza kabisa kwenye hii nchi.aarghh!
 
Kunakosa gani hapo?
Wamemwomba kawaonyesha wakanakili....
Kibaya kitakuja baadae kama watajaribu kumrubuni kwa namna yoyote afanye wanavyotaka...
Kama wamemkuta ana kadi ya chama chao..ni sahihi wakihakiki potential voters jamani hakuna ubaya.
 
Kama mwayajua yote haya, mwaenda kupiga kura ili iweje? Si muwaachie tu waendelee kuiba? Kila siku nasema hakuna upinzani. Ingetokea vyama vyote vikasusia uchaguzi, nini kingefanyika?

Hawana ubavu huo. Wote wanafiki!
 
Back
Top Bottom