Tutafakari haya!

JUANITA

Member
Mar 27, 2010
46
0
SALAAM ALEYKUM NYOTE,


Pamoja na ugeni wangu, naomba kufungua mada ifuatayo nikitaraji michango yenu itanifungua macho zaidi kuhusu nchi yetu tunayoipenda na kuiozesha kwa makusudi katika kila nyanja kana kwamba TUMELAANIWA!:
Kwamba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataraji kuanzisha mradi kamambe wa kujenga barabara ya kudumu (Highway) kuunganisha mikoa ya Ziwa Victoria na ile ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro, Manyara) - barabara itakayopasua Mbuga ya wanyama ya Serengeti, Hifadhi za Maswa, Loliondo na Ngorongoro Conservation area. Hii ikiwa miaka michache baada ya kuwakatia ndugu zetu (!) wa Falme za Kiarabu ili wawe na 'Arabia in Afrika' ya kwao kule Loliondo.

Mradi huu unaopingwa vikali na asasi mbalimbali za Hifadhi na Mazingira za Kimataifa, hapa kwetu haujulikani sana, au si kwa uwazi wa kutuamsha. Hata 'FaceBook' wamejiunga kwa kutoa tovuti ya kuomba wanaopinga mradi huu wajiandikishe. Pia unaweza kupata taarifa kwenye tovuti iitwayo 'STOP THE SERENGETI HIGHWAY'. Highway hii inatarajiwa kuanza rasmi 2012 na kuna tetesi serikali ya China itakuwa mshiriki mkuu.


Athari za kimazingira, uharibifu wa uasili, kuvuruga 'eco-system', kuharibu mwenendo wa tabia za wanyamapori haswa Nyumbu, Pundamilia na wengineo kufuata 'migration routes' ili kupata lishe na vizazi vipya; ni baadhi tu ya yatakayojiri. Fuatilia. Amua. Shukurani.
 
Back
Top Bottom