Tutaendelea kutayarisha Bajeti Mbadala, Ndio Upinzani Makini

Sis wanadamu ni watu wa ajabu sana, tunapenda kulaumu na kulalamika kila wakati, ili mradi tu yanayosemwa / kutendwa yako kinyume na matakwa na itikadi yako. Itikadi na ukweli lazima vitenganishwe katika masuala muhimu yanayogusa nchi. Hakuna aliyekamilifu, na kukubali kukosea ni ushujaa. Watu wengi hawapendi kukosolewa, na huo ndio ukweli. Zitto hongera na mapambano na daima utashinda! Nilikukubali majuzi kwenye Twitt yako uliposema Mhe. Dr. Mgimwa ni Mzee muungwana alivyokubali mapendekezo bila kejeli na vijembe! Humu JF kuna watu wavivu wa kusoma, kusikiliza taarifa, kufuatilia mijadala katika fora mbalimbali, kazi yao ni kudandia thread na kutia comment za kitoto! Tutafika tu, lakini cha moto tutakona!
 
TZ inataka uongozi kama huu, wa kukubali tunapokoselewa na hata kutolea maelezo/kurekebisha
 
CCM wamegeuza a minor issue into a three course meal kwa sababu hawana la maana kujadili. Hata pale walipopewa ufafanuzi bado wameendelea kuimba makosa as if hawajapewa explanations! Mbona ni mara nyingi tu vitabu vya speech za bajeti zinakuwa na makosa? Wametumia muda mwingi kujadili vitu vidogo kama tarakimu kwenye speech ya CDM na matokeo yake bajeti yao imepita bila ya kujadiliwa kwa kina! Sijui ilikuwa ni idea ya nani lakini sasa itabidi wakae mkao wa kunyolewa maana bajeti ya serikali is a time-bomb.

Nilicheka sana kumsikia Zakia Meghji, Vita Kawawa na wengine wakisema Tanzania tusiogope kukopa, hata USA na Japan wanakopa tena kwa kiwango cha juu! Hiki ni kichekesho, yaani ni sawa na kumwambia fundi seremala akope tu kwa sababu hata Bakharesa anakopa! Tayari deni la ATCL limeishia ku-trade off bandari ya Mtwara, haya mengine wata-trade off nini? Uranium?

Zitto, there is nothing to worry about the ranting ya watu kama Ngeleja na 1st class ya Mwigulu. Dawa ni kujipanga vizuri. CCM wanataka kuaminisha watu kuwa CDM are not ready to govern, ni wapiga kelele. Hivyo mnachotakiwa kufanya ni kuwa na macho mengi kwenye utayarashaji wa bajeti. Natambua kuna challenge kubwa ya rasilimali lakini naamini solution inaweza kupatikana.
 
Zitto.

Kwa nini mnawatenga wapinzani wenzenu kwenye maswala muhimu kama haya ya kuunda bajeti hamuoni kama bajeti yenu mnayoiita ya upinzani inakosa nguvu inaoneka ni ya Chadema aina picha ya upinzani...watu kama Prof Lipumba, Dr Sengodo Mvungi ni washauri wazuri upande wa upinzani lakini mnashindwa kuwatumia mnaonekana wabinafsi watu wanashindwa kuwatofautisha na CCM.
Tangu lini watu wenye mitizamo tofauti wakaunda umoja?
 
Zitto,

First, have my accolades for handling the matter to end with victory on your side. This is how gentlemen setle critique arising from mistakes we partake.

I deserve the auathority to claim being among the founders of this issue who raised a very loud voice through an hypothesis posted here. But so far with this statement you've my pardon and gradually you can regain my trust.

Du!
Thinking in swahili and translating verbatim into pidgin engilsh!
 
Last edited by a moderator:
Kuna jumla ya mapendekezo 10 katika Bajeti Mbadala ya mwaka huu yamekubaliwa na Serikali. Tunatendelea kutoa mawazo zaidi ili kuboresha nchi yetu na kuwaonyesha Watanzania kuwa tukikabidhiwa dola tunaweza kuendesha nchi bila mashaka yeyote.
Kwanza ninawapongeza kwa kukubalika kwa baadhi ya mapendekezo yenu. Mhe. Zitto, umeeleza mapendekezo 10 ambayo yamekubaliwa na serikali, lakini hapa umetaja mawili,
1. Tozo za SDL
2. Kuuziana assets
3. ...........
4. ...........
..............
..............
10. ........

Kwa faida ya WanaJF na Watanzania, ninashauri uweke hayo maoendekezo 8 yaliyokubaiwa na serikali.

Pia kuna wachangiaji wanajadili uhalali wa Bajeti Mbadalakama ni CDM au ni ya wapinzani wote, na wengine wamependekeza mngekuwa mkivishirikisha vyama vyengine vya upinzani katika kushughulikia masuala nyeti kama hili la bajeti, kwa njia ile ile mlivyofanya wakati wa kukusanya sahihi za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Tulilojifunza katika tukio lile ni kuwa pamoja na tafauti zao, bado wapinzani wanaweza kuwa na sauti na shauri moja. Msisahau kuwa Umoja ni Nguvu.
 
Here we go! Tutaendelea kusukuma hoja kwa manufaa na maendeleo ya watu, by any means necessary. Forward we go brothers in the struggle for the second liberation.
 
Umakini wa chadema tumeupima kwenye bajeti yao iliyowasilishwa bungeni, hizo nyingine ni story ingawa nimekubali kukiri udhaifu wa CDM.

Kingine, bajeti ya taifa kwa mwaka sio sawa na bajeti ya familia au harusi, inahitaji watu makini sana, ushirikiano wa hali ya juu na wataalam mbali mbali. Tatizo la CDM ni tabia yao ya kujifanya kujua kila kitu hata katika mambo yanayohitaji taaluma maalumu.

Kwa Ubinafsi wa viongozi wa CDM, nahakika haitakuja bajeti makini abadan.
 
ZITTO you will be presenting this for only next three years. effective 2015 you will be presenting the Budget for the United Republic of Tanzania, so when you say "Ninaahidi kwamba tutaboresha zaidi miaka inayokuja." usisahau ilo.
 
ZITTO, Again, tuwekee hayo mapendekezo kumi ambayo yamekubaliwa na hao wahuni, ukiweza tuwekee na your expected implications for each item.

Nakukumbusha kwamba msiogope mtu hata mmoja uko bungeni, watanzania tumeishaamua kuwapa nyie uongozi wa nchi yetu.Huo uhuni mnaofanyiwa tunauona msijedhani mko wenyewe, tunathamini sana kazi zenu ndani na nje ya Bunge. Naomba hiyo list. thanks
 
Zitto.

Kwa nini mnawatenga wapinzani wenzenu kwenye maswala muhimu kama haya ya kuunda bajeti hamuoni kama bajeti yenu mnayoiita ya upinzani inakosa nguvu inaoneka ni ya Chadema aina picha ya upinzani...watu kama Prof Lipumba, Dr Sengodo Mvungi ni washauri wazuri upande wa upinzani lakini mnashindwa kuwatumia mnaonekana wabinafsi watu wanashindwa kuwatofautisha na CCM.

Labda kuhusu Mvungi lakini mategemeo yangu ni kwamba Ushauri wa Profesa Lipumba ulizingatiwa wakati wa maandalizi ya bajeti ya serikali kutokana na mahusiano yaliyopo kati ya CCM na CUF.
 
Umakini wa chadema tumeupima kwenye bajeti yao iliyowasilishwa bungeni, hizo nyingine ni story ingawa nimekubali kukiri udhaifu wa CDM.

Kingine, bajeti ya taifa kwa mwaka sio sawa na bajeti ya familia au harusi, inahitaji watu makini sana, ushirikiano wa hali ya juu na wataalam mbali mbali. Tatizo la CDM ni tabia yao ya kujifanya kujua kila kitu hata katika mambo yanayohitaji taaluma maalumu.

Kwa Ubinafsi wa viongozi wa CDM, nahakika haitakuja bajeti makini abadan.

Haitakuja bajeti makini wakati gani?
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom