Tutabadilika kwa kufundishwa kuishi na wake zetu kwa njia ya radio

chayoa

Member
Apr 15, 2012
6
3
Kuna matangazo kwenye radio yanayoelezea kuwa hata kulazimisha mapenzi kwa mkeo ni ukiukaji wa haki za binadamu, Hebu niambieni kuwa kuna watu wanabadilika jinsi ya kufanya mapenzi na wake zao kwa kusikia tu tangazo la radio au wanaolipia matangazo hayo wanaharibu pesa zao, Hivi wanafanya tathmini na kujua ni kiasi gani watu wanapokea hayo matangazo, Ambapo mengine yakitangazwa wengine wanafunga radio au wanaondoka kijanja. Kama fedha hizo ni za wafadhili hayo ni matusi na misaada ya aina hiyo haitatusogeza popote, Tutapewa misaada daima dumu lakini tutaendelea kuwa masikini na maendeleo duni. Hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali
 
Kwa hapa Tz mpaka sasa kuna redio moja tu ambayo ni chuo cha suala ulililiweka hapo juu na Redio hiyo ni redio Imaan kama upo dar freq ni 104.4 kila siku sa 5 usiku kuna kipindi kizuri sana. Na sikiliza Redio Imaan ili ikutoe kwenye giza na kukupeleka ktk nuru.
 
Sijawahi kusikiliza radio hiyo, wana vipindi vya mahusiano au wanawarekodi mtu na mke wake wakiwa kitandani wanaombana. kama lile la radio free Afrika, "mi sitaki nimechoka bwana, niache nilale"
 
Sijawahi kusikiliza radio hiyo, wana vipindi vya mahusiano au wanawarekodi mtu na mke wake wakiwa kitandani wanaombana. kama lile la radio free Afrika, "mi sitaki nimechoka bwana, niache nilale"

Yaani mkuu nikilisikia huwa najikuta nimesonya, ni upumbavu mtupu yaani mtu anaguna miguno ya kingono kabisa?!! Sijui tunakoelekea na hii misaada ya akina Cameron. Wizara ya habari nayo ipo ipo tuuu huyu mama sijui kama ataweza kutufanyia lolote! Hebu wapige ban haraka haya matangazo ya ngono haya. "mi nimechoooka bwanaa! niache nilale" "Hebu geuka kidogo basi nikuoneshe" Pumbavu kabisa!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom