Tuta wabeba kwa mbeleko na machele hawa viongozi wetu mpaka lini?

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
germany_3  MAFISADI WA ZAMANI.jpg

kila nikikumbuka jinsi babu zetu walivyoteswa na wakoloni inatia uchungu sana, waligeuzwa magari na bibi zetu warembo walibakwa na kuuwa na hawa watu, baada ya waafrika wenzetu wenye ujasiri (NYERERE) na wengine kupata maarifa walipambana na kuwaondoa wakoloni.

Baada ya wakoloni kuondoka tuliwapa dhamani ya uongozi waafrika wenzetu , walichofanya ni yale yale ya wakoloni, TUNAWABEBA mabegani (kwa tunaofanya kazi nzito kama vibarua na makuli), kichwani (wasomi wanaofanya kazi mbalimbali) na mikononi (biashara ndogo kina mama) mwetu kupitia hii VAT , INCOME TAX NA USHURUNA AINA NYINGINE ZOTE ZA KODI, kwa kifupi bado tunabeba mkoloni wa leo (viongozi) kama babu zetu tofauti ya mkoloni wa leo na zamini na leo ni rangi tu, wa siku hizi ni weusi

Wao wanapanga jinsi ya kutumia kwenye shughuli za maendeleo yao na familia zao kwa kupitia posho kubwa, misharaha mikubwa, usafiri wa kifahali wenye unlimited petrol supply, ufisadi na nk

na kutenga fedha kiduchu kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya taifa leo, wao wakiwa mawaziri term moja wanatajirika kuliko taifa. na wanatajirika kulika sisi wafanyabiashara tuliofanya biashara kwa zaidi ya miaka ishirini.
wengine tumepiga sana kelele lakini raha ya kubebwa na sisi wananchi imewazidia sasa wamefikia wanaishi hotelini kama wasio na makazi kabla ya kuchaguliwa kwenye hizo nafasi.
mimi leo nawadondosha sito beba tena mkoloni. nitawapiga vita mpaka waondoke kwa wale weupe
 
Back
Top Bottom