Tusitupe Majina Ya Ukoo

PlanckScale

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
550
169
Naomba nitoe kero langu ...

Hivi inakuaje wabongo wengi sikuizi wameacha kutumia majina yao ya ukoo (kibantu)? Labda nakosea, lakini nilivyoku primary miaka ya sabini, sikumbuki wabantu kujiita "John Lucas", "Peter Alfred", "Maria Moses" n.k. Hapa pia nawakosoa hata wale wabantu wanao jiita "Amina Abdallah" au "Jabir Mohammed".

Sawa unaweza kuwa mkristo au muislamu, lakini jina laukoo lakibantu kwanini ulitupe??

I may be too much of an "African fundamentalist, but I think jina la ukoo (au la kikabila, au la familia) lina make a strong connection to where you come from - your history, your culture, your people,etc. Unless I see you face-to-face, I think if you tell me your name is "Beatrice William", I will automatically assume your European! Sorry, but I have yet to meet a white European with a name similar to kinjekitile or Mwamseka…

What are we becoming? Yes, we should take from other cultures that which will help us better ourselves, but let's not dwell on those attributes that will disconnect us from our land. Remember our ancestors (and especially here in East Africa) worked this land for centuries…


Asante
 
Yaani you are spot on!! Kama ulikuwa akilini mwangu.

Hata mimi sipendi majina ya aina hiyo ila ukiuliza wenyewe wanasema eti ni kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa wao kubaguliwa kwa misingi ya kikabila!!

Kingine ambacho sipendelei ni haya majina ya kizungu ya siku hizi; unakuta mtoto anaitwa "Cherise" au "Chantal" au mengine kama hayo. Pia "Happiness" "Gift" na kadhalika.

Tuamke jamani, tuwe na "sense of identity". Kwani ukimuita mtoto wako Lusekelo haileti maana hiyo hiyo kwa kizungu? Au "Furaha"

Inachekesha kwa kweli, huku kwenye nchi za Magharibi unakutana na Mtanzania mwenzako jina lake Peter Gabriel, sasa wa huku wanamwuliza, inakuwaje uitwe hivyo? Au wazazi wako kuna aliye na asili ya huku?
 
Umesema kweli. Wengi wetu sasa tumefulia katika jambo hili. Yaani mzungu ametuzingua, kutuzuga na kutuzinga akili mpaka hata tunapigania kuibadili ngozi ya miili yetu iwe nyeupe kama mzungu. Majina ya ukoo/ ya kiafrika ni ya maana sana. Ndiyo utambulisho wetu: wa kiutamaduni, mila na desturi. Tunapofuta majina haya tunafuta mila na utamaduni wetu na hat aidentity yetu.

Hakika waafrika wengi hawapendi tena kuyatumia majina haya kwa kuiga uzungu. na wale wanayoyatumia sasa wamebadili namna ya kuyatamka au kuyaandika: yanatamkwa kizungu na kuandikwa kizungu. Yaani tumekwisha kabisa.

Kwa nini hatujali chetu sisi wabongo?? Mbona majina yetu ni mazuri sana na tena yana maana nzuri tu? Nakumbuka miaka ya huko nyuma nilisoma na jamaa yangu mmoja kutoka Cuba (mweusi) alikuwa anatamani sana kuwa na jina la pili (la ubini) kama langu kwani yeye jina lake lilikuwa lina-sound kizungu. Yaani kila wakati alikuwa anataka awe na jina la kibantu. Nikamwambia akirudi kwao afanye process ya kubadili jina. Na nikampendekezea aitwe Kalumanzila. Alifanikwa! Mpaka ninapoandika hivi huyo jamaa anitwa (jina la pili) Kalumanzila. Ana furaha tele kujitambulisha kama mwafrika.
 
Mimi ni mmoja wapo nita muincourage mwanangu asitumie kabisa majina ya ukoo.
 
Nadhani ni ulimbukeni tu ndio wawafanya wayatelekeze majina ya koo zao. Lazima ujivunie asili yako na kujitambulisha nayo!!
 
kaka uko sawa kabisa, nakumbuka mwalimu wangu mmoja yeye ni mkenya aliponda sana class alisema kuna siku wakiwa kenya walikuwa wanamsubiri mbongo mmoja akiitwa francis nathan, basi wao wanajua ni mzungu, alipofika jamaa ni mweusi tii mara ya kwanza walikataa si yeye ikabidi atoe kitambulisho wakashangaa. anasema siku ya mwisho ya semina wakamwambia kwamba kutokana na jina lake wakadhani ni mzungu
 
Mh lakini kuna majina mengine ya ukoo kuyatamka tu inabidi uende tuition akaaa mie nabaki na hili hili langu la Sharleen Davis mpaka mwisho.
 
... Nikamwambia akirudi kwao afanye process ya kubadili jina. Na nikampendekezea aitwe Kalumanzila. Alifanikwa! Mpaka ninapoandika hivi huyo jamaa anitwa (jina la pili) Kalumanzila. Ana furaha tele kujitambulisha kama mwafrika.

Hiyo story imeninyaka kishenzi!
 
MAJINA YA UKOO TUWE TUNAAANGALIA NA MAANA ZAKE.
HEBU FIKIRIA JINA KAMA HILI "ANDUSAMILILE" MAANA YAKE AMENIKAZIA MACHO, JE KUNA UBAYA GANI NILIKIPIGA CHINI NA KUTUMIA JINA LA MTU NIMPENDAE KAMA SOKOINE AMBAYE HAYUKO KWENYE UKOO WETU/ WANGU?
MI NAONA CHA MUHIMU TUTUNZE NA TUYATHAMINI MAJINA YETU YA kiafrika
 
Sio ulimbukeni haya mambo ya kujuana kujuana kwenye makazi hata nafasi za masomo zinaathiri sana mimi kukubali majina ya ukoo. Mimi nilikosa kazi nzuri kama nini kwa vile tu jina langu la ukoo linafanana na 1 wa share holders....imagine....walisema kuwa nimependelewa kupata ile nafasi.
 
majina mengine ya ukoo ni nuksi - so better not to use them - mtoto unampa jina then anarithi tabia za ajabu ajabu kama wizi, uvivu, ubishi nk

So kabla ya kuamua kulitumia angalia history ya ukoo wenu - kama ni wezi, wavivu, vilaza plse don't use that name kwa mwanao.
 
sio ulimbukeni haya mambo ya kujuana kujuana kwenye makazi hata nafasi za masomo zinaathiri sana mimi kukubali majina ya ukoo. Mimi nilikosa kazi nzuri kama nini kwa vile tu jina langu la ukoo linafanana na 1 wa share holders....imagine....walisema kuwa nimependelewa kupata ile nafasi.

pole sana kaka.
Lakini naamini kuna nafasi nzuri kabisa inakungoja wewe.
Piga goti milango ya baraka iko wazi kwa ajili yako.
 
Heshima kwako Nguli.

Majina ya ukoo wakati mwingine yanaweza kukusababishia matatizo makubwa hasa kwenye ajira.Niliwahi kukataliwa kupata madaraka kwasababu wafanyakazi niliokuwaniwasimamie wengi walikuwa wanatoka katika kabila langu.Kitambulisho kikubwa yalikuwa majina ya ukoo.Asikudanganye mtu majina ya ukoo hayana mpango kabisa.

Majina mengine ya ukoo ukiyatamko ni matusi makubwa kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili,Mfano nilikuwa na rafiki yangu mmoja jina lake la ukoo ni ma....ro,mwingine jina lake Mende sasa kila siku haishi kutaniwa ilibidi abadili jina kukwepa utani.


Sio ulimbukeni haya mambo ya kujuana kujuana kwenye makazi hata nafasi za masomo zinaathiri sana mimi kukubali majina ya ukoo. Mimi nilikosa kazi nzuri kama nini kwa vile tu jina langu la ukoo linafanana na 1 wa share holders....imagine....walisema kuwa nimependelewa kupata ile nafasi.
 
Muanzisha mada ebu niweke sawa.

Kusudi lako watu wawape watoto wao majina tulozoea kama 'Ali' na 'charles', lakini wahakikishe mashuleni wanawaandikisha waki-include majina yao ya ukoo.

(1) Mfano Charles John Wachamba, na sio Charles John tu pekee.

(2) Au unamaanisha right from unapompa jina mtoto umpe la kibantu kwa mfano Mwakipumbu Mwakipesile Mwanjenje (1st, 2nd, surname names respectively).

Sasa hiyo namba (2) hapo juu si itakua jina litahitaji mistari miwili au zaidi maana kuna majina yameshiba kweli ya kibantu!
 
majina mengine ya ukoo ni nuksi - so better not to use them - mtoto unampa jina then anarithi tabia za ajabu ajabu kama wizi, uvivu, ubishi nk

So kabla ya kuamua kulitumia angalia history ya ukoo wenu - kama ni wezi, wavivu, vilaza plse don't use that name kwa mwanao.


Na ukimpa hilo la "Shanene" au "Sharon" ndio hata rithi tabia za huko lilikotoka hilo jina?
 
Back
Top Bottom