Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
"Ukicheka na Nyani utavuna mabua". Usemi huu unazidi kudhihirika katika nchi yetu hasa katika suala la wafanyakazi kuendelea kukandamizwa bila ya kuwa na mtetezi. Wafanyakazi hawa ndio wamekuwa walipa kodi kwa serikali kwa asilimia 100 kuliko chanzo kingine chochote cha kodi. Hili serikali imefanikiwa kuwanyamazisha wafanyakazi.
Sasa kanakwamba hilo la kodi halitoshi, Serikali imeamua kuwatikisa tena wafanyakazi kwa kuwalazimisha kusubiri pesa zao za akiba mpaka ufike umri wa kustaafu. Hivi kwanini serikali inapanga maisha ya mtu mmojammoja. Kesho itakuja na sheria nyingine ya matumizi ya mshahara.
Kwa hili tafadhali wafanyakazi wasitarajie kupata mtetezi asiyekuwamfanyakazi na anaeumizwa moja kwa moja na sheria hii. Sheria hii imepitishwa Bungeni kwa urahisi kabisa pasipo kuzua mijadala na ndio maana watanzania wengi wameshtuka na kushangaa kusikia sheria hiyo ilipitishwa muda mrefu Bungeni, April mwaka huu.
Kama ni suala la kuweka akiba, mfanyakazi wa leo anajua kuna mabenki mengi nchini atakwenda kuhifadhi pesa za watoto wake. Kumekuwa na utetezi potofu juu ya sheria hii kuwa itasaidia mfanyakazi kukopa Nyumba. Je, mahitaji ya wafanyakazi ni nyumba tu? kuna ambao tayari wameshajenga kwa njia wanazozijua wenyewe na mahitaji yao si nyumba tena.
Na kama suala ni kumlinda mfanyakazi asijekudhalilika uzeeni, basi suala hili liwe ni hiari ya mfanyakazi mwenyewe lakini kwa wanaotaka kuchukua pesa zao, waachwe wachukue. Kwa hili serikali ndio inajifanya kuwajali wafanyakazi, mbona wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mpaka leo wapo wamelala pale makao makuu ya stesheni Dar wanaokoteleza vyakula, serikali haiwaoni? Mafao yao yako wapi?
Wafanyakazi ujumbe ni kuwa "ukicheka na Nyani utavuna Mabua".