Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Kuna mjadala mwingine unaendelea pale manzese kila siku jioni wa kiislamu,ukipita pale mada kubwa wanayo zungumzia ni ukristo,yaaani baada ya kufanya kazi,wao wanakaaa wanawazungumzia wakristo sijui bible ikifungu fulani kinasema hivi mara vile,sasa mm nashangaaa hayo maendeleo yatatoka wapi wakati muda mwingi wamekaaa kutoa majungu tu na kuwatukana wakristo,hivi kweli tutafika?
 
Wana JF na Watanzania wenzangu,

Hili swala la kuanza kuingiza UDINI kwenye mstakabali wa Taifa letu limekuwa engineered na CCM na KIKWETE kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010 mwaka jana.
Believe me or not, CCM na KIKWETE waliliingiza hili swala la UDINI baada ya kuona upepo wa kisiasa umebadilika ghafla pale CHADEMA ilipomteua Dr. W.Slaa kama mgombea wa Urais. Dr. Slaa alikuwa,amekuwa na ataendelea kuwa tishio kwa CCM na vikaragosi vyake. Ili kuzima nguvu za kisiasa za Dr. Slaa na CHADEMA, mkakati uliowekwa na CCM kutaka kummaliza Dr. Slaa na CHADEMA hakukuwa na njia nyingine mbadala isipokuwa kupenyeza UDINI ikizingatiwa kuwa Dr. Slaa mi MKRISTO tena aliyesomea na kubobea kwenye maswala ya Canon Laws(Ueweledi katika sheria za utawala,usimamizi na uendeshaji wa Kanisa Katoliki na mambo yanayohusu Kanisa kwa ujumla).

Kwanza CCM walianza kurushia madongo Dr. Slaa(siasa majitaka) kuwa mtu aliyeikana IMANI yake hafai kuwa Rais. Mara akadaiwa kapora mke wa mtu na upuuzi mwingine kama huo. Kelele zote hizo hazikubadilisha mtazamo wa Wananchi kuhusu Dr. Slaa na CHADEMA na ndipo CCM wakaingiza gia ya UDINI wakiamini kuwa hilo litawasaidia kujinasua na nguvu kubwa ya CHADEMA.

Kila mtu ni shahidi kuwa KIWETE amekuwa akilizungumzia sana hili la UDINI kwa namna fulani ya KINAFIKI kwasababu anajua kabisa kuwa YEYE AKIWA MUISLAMU akishawaweka sawa WAISLAMU wenzake na wakakubaliana naye kuwa kuna UDINI basi WAISLAMU wataingilia kati. Juzi tumeshuhudia pale KARIMJEE HALL WAISLAMU chini ya BAKWATA wakiongozwa na Sheikh wao wakiimbia SERIKALI KUWA IMEKUWA IKIPOKEA AMRI TOKA KWA MAASKOFU(wakristo) NA KAMA IMESHINDWA KUWADHIBITI MAASKOFU BASI WAO WAISLAMU WAPEWE HIYO KAZI YA KUWADHIBITI ILI WAWANYOOSHE!!!

Matamshi hayo yalikuwa ni uchochezi wa wazi kabisa. Mimi niltegemea kuwa Serikali ingelichukua hatua za kuwakamata au hata kuwakemea hao Waislamu kwa tamko lao hilo lakini mpaka sasa ni KIMYA. Hii inaonyesha kuwa hili swala limepangwa. Kama ingelikuwa ni MAASKOFU AU CHAMA CHA UPINZANI wametamka hivo tungesikia kelele za serikali na hata kupigwa mabomu. Lakini maadamu limesemwa na WAISLAMU na ndiyo ajenda ya KIKWETE NA CCM yake hakuna mtu atahoji.

Kwa hiyo inadhihirisha kwamba CCM wako nyuma ya jambo hili. Wanachosubiri kwa sasa ni kuendelea kuchochea na kumwaga Petrol kwenye moto huu wa UDINI mpaka ulipuke na kuenea nchi nzima na kitakachofuata ni KUWAKAMATA VIONGOZI WOTE WA CHADEMA NA MAASKOFU ILI KUTAKA KUIMALIZA NGUVU CHADEMA NA DR.SLAA ili kwa mwaka 2015 CCM wasiwe na upinzani mkali kama Uchaguzi uliopita.

Nimesikia MASHEIKH wakipendekeza kuwa kuwe na Sheria ya kuwazuia Maaskofu kutojihusisha na Siasa kama ilivyo kwa wanasiasa kutenganisha Biashara na siasa! Lakini hawahawa Masheikh wanakaa misikitini wakihubiri siasa!!! Nashangazwa na IQ ndogo ya hawa jamaa ya kutoelewa kuwa Maaskofu hata wao wenyewe Masheikh ni sehemu ya JAMII YA WATANZANIA na maamuzi yoyote ya Serikali au Chama Tawala yanawagusa moja kwa moja. Kama ni kupanda bei za UMEME askofu au Sheikh LAZIMA ALIPE.Kama ni kulipa kodi wanaponunua bidhaa iwe ni chakula,mavazi,malazi lazima watalipa. Hatuna maduka wala huduma special kwa Maaskofu au Masheikh.

Usitegemee kuwa kama hali ya kisiasa ikibadilika na kuwa mbaya iwe kisiasa au kiuchumi,impact hiyo inamgusa kila mmoja bila kujali kuwa ni Askofu au Sheikh. Wote wakiwa viongozi wa kiroho hakuna atakaye kuwa salama whether akiwa msikitini au kanisani kama siasa zikichafuka!Huwezi kuwahubiria watu dini kanisani au mskitini HUKU WAKIWA NA NJAA,HAWAWEZI KWENDA SHULE,HAWANA NGUO ZA KUVAA! Sahau.

Maaskofu na Masheikh ni sehemu ya jamii ambayo lazima iwajibike kwa mambo yote ya kisiasa kwasababu yanaigusa jamii yote kwa ujumla.

WAKATI WA MWALIMU HII REDIO IMANI INGELIFINGIWA MARA MOJA KWA SABABU ZA KUTAKA KUCHOCHEA SIASA ZA UDINI.

NAOMBA BARAZA LA HABARI NA WAZIRI MHUSIKA WAIMULIKE REDIO IMANI NA IKIWEZEKANA IFUNGIWE MARA MOJA KABLA HAIJALETA MADHARA.
 
Hao ni masheikh uchwara wackupe taabu,cc waislaum tulioelimika hatuwezi kudanganywa na hao wapuuzi

Kaka usitukane jambo usilolijua wewe najua nakuelimika kwako huwezi kumzidi prof Mikidadi aliyekuwepo pale. Mnajidai mmeelimika kwa kujua vingereza vya uongo na kusoma Idea za watu unajidai eti umeelika.
Nis comment sana nipe Award zako kaka ili niendelee!
 
Hawa Masheikh wajifunze kupresent maada na siyo jazba na maneno mengi ya uzushi, nawashauri waanze kutatua internal problem zao kwanza. Pili wasifanye mambo km nyimbo za taarabu huyu katoa wimbo na wengine unamjibu kwa kumtungia nyimbo. Toeni hoja zenu zenye maana na sio kudandia za wengine kwa majibu mepesi na yasio na busara.nawashauri anzeni kwanza na kushughulikia elimu kwenye shule zenu na kujifunza kujenga hoja la sivyo mtaangamia kwa kukosa maarifa
 
Wewe waache tu,ipo siku watalia na kusaga meno,kwa kuwa vita havina macho!!
 
Hakuna tofauti kubwa kwa hiyo Radio na thread nyingi za uchechezi humu JF za wakristo za kukebehi, kudharau, kudhalilisha waislamu.... Sasa wameshastuka jasho kwenu, si mnafikiri nyinyi ndio wenye elimu haya sasa wacha wakuonyesheni.
 
Kwa mwislam ambaye amesoma na kuelewa sidhaani kama anaweza kukubaliana na huo mjadala, manake ni uongo mtupu na uchochezi. Hata ukifuatilia wanachosema si kweli maana wao ndo wachawi wa maendeleo yao, fanya tu utafiti mdogo wa shule za sekondari za kiislam kuhusu maendeleo yao utahisi kichefuchefu, manake viongozi ambao hawana elimu dunia wanang'anga'nia kuzisimamia hatimaye kuzipeleka ambako siko.
ILA KWA MKIRISTO aliyesoma anaona ni sahihi kwa maaskofu kuchanganya dini na siasa na kushabikia chama fulani......
 
Unataka mkwere ajustify namna gani kwamba kuna udini Tanzania? bila kuwatuma hao mashehe mbumbumbu kwenye redio na kufanya mihadhara isiyokuwa na tija ? wametumwa hao kuna wakati kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka jana pia nishawahi kusikiliza hiyo redio ikimcritisizi Dr.Slaa kwamba ni mtu anayependa udini sana so kwa hili pia sishangai kabisaaaa..... wako kazini wametumwa nashindwa kuelewa hao wanaojiita kupokea taarifa za kiinterejensia kwa nini wasizitumia kuzuia vitu kama hivi ....full nonsense issues wanaziweka ili kuwahadaa wale wenzangu na mimi wasioweza kuchakatua jambo/mambo na waamini kwamba udini ni kweli upo ..
.

Umenena. Asante
 
Usipotoshe ukweli kwa dai lako la uongo kuwa Uislamu ulienezwa kwa upanga! haya nakuuliza, Uislamu ulipoingia huku kwetu miaka 1000 kabla ya ukristo kuja ni upanga gani huo uliotumika mpaka babu zetu wakasilimu?
Maeneo ya Machame, Usangi, Ugweno, Moshi mjini, Bukoba, Musoma nk, kuna Waislamu pia sasa upanga uliotumika kuwasilimisha umeuhifadhi ktk MUSEUM yako?
2) Indonesia ni nchi yenye idadi kubwa sana ya Waislamu duniani kote, sasa uislamu ulipoingia huko ni upanga upi huo uliotumika?
India, Pakistani, Afganistani, Kosovo, Bosnia, mackedonia, Uzbekistan, Urusi, Chechenia, USA na nchi nyingi duniani wanakoishi waislamu ni upanga gani huo uliotumika?

Labda Ukristo ndio ulioenezwa kwa mtutu wa bunduki ndio maana Wazee wetu akina KINJEKITILE walikataa kudanganywa na Wazungu waliokuja kama Wamisionari kumbe lengo lau ni kuwabatiza na kuwatala!

Usituletee propaganda chafu zilizopitwa na wakati tafuta lingine la kuongea lakini sio upupu!

mmmmm!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, kaazi kweli kweli!!!!!
 
Wana JF na Watanzania wenzangu,

Hili swala la kuanza kuingiza UDINI kwenye mstakabali wa Taifa letu limekuwa engineered na CCM na KIKWETE kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010 mwaka jana.
Believe me or not, CCM na KIKWETE waliliingiza hili swala la UDINI baada ya kuona upepo wa kisiasa umebadilika ghafla pale CHADEMA ilipomteua Dr. W.Slaa kama mgombea wa Urais. Dr. Slaa alikuwa,amekuwa na ataendelea kuwa tishio kwa CCM na vikaragosi vyake. Ili kuzima nguvu za kisiasa za Dr. Slaa na CHADEMA, mkakati uliowekwa na CCM kutaka kummaliza Dr. Slaa na CHADEMA hakukuwa na njia nyingine mbadala isipokuwa kupenyeza UDINI ikizingatiwa kuwa Dr. Slaa mi MKRISTO tena aliyesomea na kubobea kwenye maswala ya Canon Laws(Ueweledi katika sheria za utawala,usimamizi na uendeshaji wa Kanisa Katoliki na mambo yanayohusu Kanisa kwa ujumla).

Kwanza CCM walianza kurushia madongo Dr. Slaa(siasa majitaka) kuwa mtu aliyeikana IMANI yake hafai kuwa Rais. Mara akadaiwa kapora mke wa mtu na upuuzi mwingine kama huo. Kelele zote hizo hazikubadilisha mtazamo wa Wananchi kuhusu Dr. Slaa na CHADEMA na ndipo CCM wakaingiza gia ya UDINI wakiamini kuwa hilo litawasaidia kujinasua na nguvu kubwa ya CHADEMA.

Kila mtu ni shahidi kuwa KIWETE amekuwa akilizungumzia sana hili la UDINI kwa namna fulani ya KINAFIKI kwasababu anajua kabisa kuwa YEYE AKIWA MUISLAMU akishawaweka sawa WAISLAMU wenzake na wakakubaliana naye kuwa kuna UDINI basi WAISLAMU wataingilia kati. Juzi tumeshuhudia pale KARIMJEE HALL WAISLAMU chini ya BAKWATA wakiongozwa na Sheikh wao wakiimbia SERIKALI KUWA IMEKUWA IKIPOKEA AMRI TOKA KWA MAASKOFU(wakristo) NA KAMA IMESHINDWA KUWADHIBITI MAASKOFU BASI WAO WAISLAMU WAPEWE HIYO KAZI YA KUWADHIBITI ILI WAWANYOOSHE!!!

Matamshi hayo yalikuwa ni uchochezi wa wazi kabisa. Mimi niltegemea kuwa Serikali ingelichukua hatua za kuwakamata au hata kuwakemea hao Waislamu kwa tamko lao hilo lakini mpaka sasa ni KIMYA. Hii inaonyesha kuwa hili swala limepangwa. Kama ingelikuwa ni MAASKOFU AU CHAMA CHA UPINZANI wametamka hivo tungesikia kelele za serikali na hata kupigwa mabomu. Lakini maadamu limesemwa na WAISLAMU na ndiyo ajenda ya KIKWETE NA CCM yake hakuna mtu atahoji.

Kwa hiyo inadhihirisha kwamba CCM wako nyuma ya jambo hili. Wanachosubiri kwa sasa ni kuendelea kuchochea na kumwaga Petrol kwenye moto huu wa UDINI mpaka ulipuke na kuenea nchi nzima na kitakachofuata ni KUWAKAMATA VIONGOZI WOTE WA CHADEMA NA MAASKOFU ILI KUTAKA KUIMALIZA NGUVU CHADEMA NA DR.SLAA ili kwa mwaka 2015 CCM wasiwe na upinzani mkali kama Uchaguzi uliopita.

Nimesikia MASHEIKH wakipendekeza kuwa kuwe na Sheria ya kuwazuia Maaskofu kutojihusisha na Siasa kama ilivyo kwa wanasiasa kutenganisha Biashara na siasa! Lakini hawahawa Masheikh wanakaa misikitini wakihubiri siasa!!! Nashangazwa na IQ ndogo ya hawa jamaa ya kutoelewa kuwa Maaskofu hata wao wenyewe Masheikh ni sehemu ya JAMII YA WATANZANIA na maamuzi yoyote ya Serikali au Chama Tawala yanawagusa moja kwa moja. Kama ni kupanda bei za UMEME askofu au Sheikh LAZIMA ALIPE.Kama ni kulipa kodi wanaponunua bidhaa iwe ni chakula,mavazi,malazi lazima watalipa. Hatuna maduka wala huduma special kwa Maaskofu au Masheikh.

Usitegemee kuwa kama hali ya kisiasa ikibadilika na kuwa mbaya iwe kisiasa au kiuchumi,impact hiyo inamgusa kila mmoja bila kujali kuwa ni Askofu au Sheikh. Wote wakiwa viongozi wa kiroho hakuna atakaye kuwa salama whether akiwa msikitini au kanisani kama siasa zikichafuka!Huwezi kuwahubiria watu dini kanisani au mskitini HUKU WAKIWA NA NJAA,HAWAWEZI KWENDA SHULE,HAWANA NGUO ZA KUVAA! Sahau.

Maaskofu na Masheikh ni sehemu ya jamii ambayo lazima iwajibike kwa mambo yote ya kisiasa kwasababu yanaigusa jamii yote kwa ujumla.

WAKATI WA MWALIMU HII REDIO IMANI INGELIFINGIWA MARA MOJA KWA SABABU ZA KUTAKA KUCHOCHEA SIASA ZA UDINI.

NAOMBA BARAZA LA HABARI NA WAZIRI MHUSIKA WAIMULIKE REDIO IMANI NA IKIWEZEKANA IFUNGIWE MARA MOJA KABLA HAIJALETA MADHARA.

Ujumbe wako nkoyi umetulia sana na una hekima za hali ya juu. Big up yaani kwa hapa nimekufagilia sana.
 
Nendeni shule kwanza ndipo mrudi hapa, vilaza wakubwa tanzania hii ni nyie waislam...na hamtaendelea kuwapita wakristu....sahauni.
tutaendelea kuwatibu kwenye hospitali zetu, kuwasomesha watoto wenu maskini, tutawalipia gharama za matibabu india watoto wenu wanaohitaji operation kubwa, hata mkitaka vingine tutawapa maana hamna elimu wala hela na hata tabia ya utoaji hamna...tutawakimbiza mchakamchaka mpaka mwisho....
 
Madai ya hawa jamaa hayakuanza leo, yangekuwa yana mantiki mimi ningesema pengine ni maumivu ya kuonewa. Lakini inahitaji akili ndogo sana kujua kuwa madai yao sio tu ya uongo, bali pia ni ya kipumbavu. Unawezaje kudai kuwa waislamu wamekuwa wakifelishwa! Wanafelishwa na nani? Utaratibu wa kusahihisha mitihani haubagui msahihishaji awe mkristo au muislamu. Wasahihishaji ni watu wa dini zote. Shule za seminari zinafaulisha wanafunzi kwa sababu tu ziko makini kitaaluma, kwani wanapofeli leo wanafunzi wa shule za kiislamu huko Zanzibar ambako asilimia zaidi ya 98 ni waislamu mpaka serikalini nao pia wanafelishwa? Nonsense.

Hizi hospitali za kikristo kwani zilijengwa na serikali? Je, waislamu na dini nyinginezo zote zimenyimwa kujenga hospitali? Je waislamu hawatibiwi kwenye hospital hizo. Huu ndio ufinyu wa ajabu wa baadhi ya viongozi wa dini. Wao wanadhani kila wasemapo jambo maaskofu imewapasa kupinga tu, ali mradi ni maaskofu wamesema.

Lakini ninalolishangaa zaidi, ni serikali kuwanyamazia hawa watu wanaochocheza machafuko waziwazi. Sio kwamba hawajulikani au kwamba ni vigumu kujua wako wapi, ila serikali inajifanya kama haikusikia tu. Kutumia chombo kama redio kuchochea machafuko sio jambo la kuachwa hivi hivi tu. Huku kunyamaza kwa vyombo husika kunatoa tafsiri gani kwa watu wanaofikiri? Sasa kesho redio za kikristo nazo zikianza kujibu upuuzi huo halafu serikali ikawachukulia hatua wataepuka lawama kuwa wana upendeleo na unyanyasaji?
 
Mnajuwa Mkristo wa kwanza kutia nanga pwani ya Kilwa (yeye mwenyewe hajashuka melini), ni Vasco Da Gama, baad ya kushusha wasaidizi wake na kupewa mabaharia wa kuwaendeleza safari yao na waliporudi kwa mara ya pili Kilwa kitu cha kwanza ilikuwa ni kuwapiga wenyeji kwa mizinga kutoka kwenye merikebu zao bila ya huruma! Kisa? CRUSADE!

Na hiyo kurusedi bado inaendelea haijasitishwa. Na sasa ndio inaongeza kasi, kwa sababu tu uIslaam unakuwa kwa haraka kuliko dini yoyote duniani.

Hapa kwetu kinawashngaza nini kuwa tumetawaliwa na mfumo kiristo uliosimikwa na Nyerere? Kama si kweli, kwa lipi zaidi ambalo linamfanya Nyerere awe kwenye safu ya kupewa utakatifu? Utakatifu upi alioufanyia nchi hii? Zaidi ya kuleta mfumo kiristo?

Samahani ndugu yangu Zomba, naomba unisaidie kujua ni kwa jinsi gani Nyerere aliingiza Mfumo wa kikristo Tanzania? nipe mifano halisi ya mifumo hiyo na kwa jisi gani inaonyesha imejikita kwenye ukristo. Pengine utakuwa umenielewesha na kujua ndugu zangu waislam wanachokilalamikia pengine kuna ukweli ndani yake.
 
mashehe wengi hawana shule..uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo sana. weledi wao wa dunia ya leo ni funyu. wanajua kusoma quran tu. uwezo wa kuchambua mambo kisomi hawana. wasikusumbue.
 
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.
Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.
Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa , bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!
Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa “intelijensia” ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

Wana JF naomba kuwakilisha

Nchi hii ni ya waislamu, wacristo na wasio na dini yeyote kama baadhi ya wamasai wanaoamini mlima oldonyo lengai, sasa unaposma serikali ijenge hospitali za dini na vyuo haiwezekani hata kidogo.

Hata dini haijajenga hospitali wala chuo ila waumini wake ndio wamajenga kwa hiyo na waislamu nao wajenge vyuo kama wanavyojenga misikiti. Mbona hawabaguliwi kwenye hivyo vyuo na mahospitali?

Mfano Kilimanjaro hospitali kubwa ni KCMC ya walutheri na Mwanza Bugando ni ya RC, hizi ni huduma za jamii kama zingine.
 
Tatizo wakristu na Waislam kwanza kila kundi linajiona bora na wengi kuliko jingine, bila kujua ukweli kuwa WAPAGANI ndio wengi kuliko hizo dini zenu zilizoletwa na wazungu na waarabu. Kwa mpagani anajua waislam na wakristio ni wasotambua historia yao vema ndiyo maana ni wagomvi sana kwani wao ni kama mashabiki. Wapagani hutukanwa sana na makundi yote lakini kwa kuwa wanajijua wao ni wachezaji(wenyeimani) huwa hawana ugomvi na mashabiki wa waarabu na wazungu, utagombanaje na mazezeta?
 
Naomba nianze kwa kuonyesha masikitiko yangu na hasa katika zama hizi za kikwete, suala hili laudini litatupeleka pabaya kwani sasa hivi uhuru na habari leo ndiyo magazeti yaliyo bize sana kuzungumzia masuala ya udini sijui wana maslahi gani, ni vema wakawa mfano wa kulinda maadili ya uandishi kwa maslahi ya wengi.
 
Status
Not open for further replies.
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom