Ni ukweli kuwa tupita kipindi kigumu sana katika kutafuta ajira, na maombi mengi tunayatuma na wala hatuitwi kuja kufanya interview, na wakati huohuo maisha ni magumu kwa namna hii mtu lazima alalamike, na kuona kwamba kuna tasisi au mtu anambania kazi, na hivyo kukata tamaa.
Mimi hadi kabla ya kuitwa kwenye interview pengine nilikuwa mtu wa fikra hizo, kwani nimetafuata ajira kwa mda mrefu sana, nimeandika barua nyingi, nimebadilisha CV za kila namna nikifikiri zitasanisaidia kupata kazi, lakini kwa muda mrefu kulikuwa na ukimya utadhani kama sijatuma kitu vile. kumbe ilikuwa ni suala la wakati kwani ikafikia kipindi nimeitwa na sekretarieti ya ajira nafasi tatu tofauti, na nimechaguliwa hapo jana katika interview ya kuanza tuu niliyoifanya katika maisha yangu hapo sekretarieti.
Cha msingi wenzangu tusikate tamaa, pale unapokataa tamaa ndipo ushindi wamwenzako unapoanzia, tusikatishane tamaa kuhusu Sekretariti ya ajira kwani kama kuna matatizo, hakuna taasisi yoyote hapa Tanzania ambayo haitafanya kazi bila matatizo, cha msingi Sekretariti imepunguza matatizo hayo. Cha msingi kuwa na sifa halafu uzitete sifa hizo kwenye interview utapita kama nilivyopita.
From Seniour job Seeker(As then was)