Tusafiri au Tusisafiri kuja Arusha kwa mazishi ya mashujaa kesho?

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wadau nimepata taarifa za kushtua sana hapa kwamba jeshi la polisi limepiga marufuku mazishi ya kitaifa kesho kwa nashujaa waliouawa kwa kupigwa rusasi za motoi na polisi wiki iliyopita.Inasemekana wamesema miili ikiagwa katika viwanja vya NMC kutakuwa na uvunjifu wa amani.Wakasema eti watatumia kila silaha kupambana na watakaokiuka agizo hilo la polisi.Ninajua watu wengi wako njiani kuja kushuhudia na kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.
Watu mlioko Arusha mkiwemo viongozi na ile kamati ya mazishi tufahamisheni mapema kama kweli polisi imeamua hivyo na mtuambie cha kufanya.
 
nani wa kuvunja amani?wao wakae huko huko vituoni kwao waone kama fujo zitatokea
 
Wadau nimepata taarifa za kushtua sana hapa kwamba jeshi la polisi limepiga marufuku mazishi ya kitaifa kesho kwa nashujaa waliouawa kwa kupigwa rusasi za motoi na polisi wiki iliyopita.Inasemekana wamesema miili ikiagwa katika viwanja vya NMC kutakuwa na uvunjifu wa amani.Wakasema eti watatumia kila silaha kupambana na watakaokiuka agizo hilo la polisi.Ninajua watu wengi wako njiani kuja kushuhudia na kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.
Watu mlioko Arusha mkiwemo viongozi na ile kamati ya mazishi tufahamisheni mapema kama kweli polisi imeamua hivyo na mtuambie cha kufanya.

Hiyo nguvu wangeitumia kupambana na majambazi tungewaona wa maana sana. Wanakuwa na jeuri ya kuwafyatulia risasi raia wema kwa kuwa wanajua hawana silaha yoyote, lakini wakisikia tukio la uporaji hata kama wezi wanatumia mapanga hawatii mguu hadi wapate uhakika kwamba jamaa wameshasepa. Ni aibu kubwa kuwa na jeshi la polisi la namna hii, nadhani hawa jamaa hawajapigana vita muda mrefu inabidi ufanyike mpango waende somalia kusaidia utawala wa sheikh sharif, wakapambane na al-shabab kama wanadhani wao wana nguvu na uwezo wa kupambana na raia.
 
Kwa Polisi hakuna tofauti kati ya Jambazi na anaekaidi AMRI YAO. Ndio maana kuna semi. Nguvu kidogo na Nguvu zaidi. Hivyo basi kama wapo waandamanaji wapya haya shime tena (ili mpime nguvu ya dola kwa mara nyingine) na wapo watakaotoka kenya tena kwa mara nyingine. (maskini Black Man - urafiki wake na FM umepotezea maisha)
 
mmmmh,me nilitaka hata wasiwepo kujidai wanalinda amani maana watu wanaweza kukasirika wakiwaona na yakawa mengine tena huko,God forbid
 
Kwa Polisi hakuna tofauti kati ya Jambazi na anaekaidi AMRI YAO. Ndio maana kuna semi. Nguvu kidogo na Nguvu zaidi. Hivyo basi kama wapo waandamanaji wapya haya shime tena (ili mpime nguvu ya dola kwa mara nyingine) na wapo watakaotoka kenya tena kwa mara nyingine. (maskini Black Man - urafiki wake na FM umepotezea maisha)
Wewe ni Kibaraka wa ccm kwa kila post yako...Nakushangaa unajiita Mwanamageuko, anyway, nadhani unamaanisha huna msimano!
 
Du! hii nchi aisee!!
So polisi wamepata tarifa za kiintelijensia kama kawaida yao au?
 
Polisi nimesikia wanaogopa kupigwa. Si unajua polisi na bunduki ni sawa na samaki na maji kwa hiyo hawathubutu kuja bila mabomu na bunduki msibani. Na wanaona kuja mikono mitupu watauawa na wanaona kuja na bunduki wananchi watawazomea na kuwafukuza . Kwa hiyo Polisi hapa wako njia panda.

Ila ukweli ni kwamba wakileta za kuleta kesho itakuwa zamu yao na watu wamejipanga na ndo maana wameambiwa sio lazima waje na silaha kwani ni ibada
 
Sasa wanataka nini hawa polisi jamani, yaani hata mazishi wanazuia mkusanyiko? Hawa shwaini ni nini tena?
 
Sidhani kama watazuia hata ibada.
Kama watafanya hivyo, nita prove kwamba polisi wa tanzania ni wauaji na hawana nia nzuri kwa wananchi wanaowalinda bali ni mamluki wa watawala

chonde chonde polisi msithubutu kuvunja ibada ya kuwaaga hawa mashujaa, tena kwa ushauri wenu msikaribie kabisa eneo la tukio, mana watu wanahasira na nyie sana. "THE SOCIETY NOW DAYS BRAND U AS KILLERS/ASASSINS RATHER THAN PROTECTORS. Msilete balaa jamani.
 
Kwa Polisi hakuna tofauti kati ya Jambazi na anaekaidi AMRI YAO. Ndio maana kuna semi. Nguvu kidogo na Nguvu zaidi. Hivyo basi kama wapo waandamanaji wapya haya shime tena (ili mpime nguvu ya dola kwa mara nyingine) na wapo watakaotoka kenya tena kwa mara nyingine. (maskini Black Man - urafiki wake na FM umepotezea maisha)

wewe umetumwa, ni mmoja wa vibaraka wa mafisadi mitandaoni, kazi yako kuikatisha tamaa mapambano ya haki na mabadiliko Tz, sitaki kuhangaika na wewe U KNW THE TRUTH UNAJARIBU TU KUFICHA HISIA ZAKO.
 
MIMI NINGESHAULI HILI SUALA SERIKALI INGESHUGHULIKIWA KUANZIA IBADA MPAKA MAZISHIHIA YAO KULIKO KUACHIA CHADEMA NA WAO KUTOA VITISHO TUUU. iNAKUWA KAMA SERIKALI HAIPO KARIBU NA WANANCHI WAKE. HATA KAMA NI UKILAZA WA HAWA CCM UMEZIDI SASA.
 
:Cry:
That is absolutely bad news

Jamani hata ibada ya mazishi kwao nongwa?

Hivi hawa polisi wanakaa mbinguni na huwa wanashuka mara moja moja kwa hiyo hatuwezi kuvurugana nao mpaka kwenye mikutaniko?

Si ndo hawa wanakaa kwenye "vibanda umiza" kajumba kale ka mchana hukai ndani (bati) na vyumba viwili baba, mama, watoto, wakwe et.al wako humo humo ndani? nna wasi wasi wanagongana sana kwenye vijumba vyao mpaka akili za kiubinadamu zinawatoka
 
Kwa Polisi hakuna tofauti kati ya Jambazi na anaekaidi AMRI YAO. Ndio maana kuna semi. Nguvu kidogo na Nguvu zaidi. Hivyo basi kama wapo waandamanaji wapya haya shime tena (ili mpime nguvu ya dola kwa mara nyingine) na wapo watakaotoka kenya tena kwa mara nyingine. (maskini Black Man - urafiki wake na FM umepotezea maisha)

Wewe una matatizo sana idadi ya polisi ni ngapi na wananchi ni wangapi? Je siku wakituchosha nani atawalinda polisi.
 
Back
Top Bottom