Turudi kwenye muungano

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
NI dhahiri sasa Tanzania inahitaji kura ya maoni ili kuamua mustakabali wa Muungano.Tunathubutu kutamka haya kwa sababu ya hali inayotokea nchini wakati wa kuanzisha mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya itakayoridhiwa na Watanzania.Wakati wa mjadala uliolazimika kuendeshwa baada ya bunge kukataa muswada wa awali wa sheria ya marekebisho ya katiba ya nchi Machi mwaka huu, suala

la Muungano liliibuka.
Hoja ikaibuka mjadala ulipoendeshwa jijini Dar es Salaam, ukumbi wa Karimjee, na iliibuka, na hapa kwa nguvu kubwa, mjadala uliofanyika ukumbi wa Sekondari ya Haile Selasie, mjini Zanzibar.Watoa maoni Zanzibar walitaka kwanza kutafutwe ufumbuzi wa mvutano wa muda mrefu kuhusu Muungano na kufikia kuishinikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iachane na muswada huo,

badala yake iitishe kura ya maoni kuwauliza wananchi kama wanataka kuendelea na Muungano.
Hata mwishoni mwa wiki, pale ujumbe wa Serikali ya Muungano ulioongozwa na Samwel Sitta, ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki, hilo liliibuka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipotaka suala la Muungano litafutiwe ufumbuzi kwanza.Na katika msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

(CHADEMA) kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni, kimesema wazi kuwa mfumo wa muungano uangaliwe upya.
CHADEMA imethubutu kwa mara ya kwanza kutaka Tanganyika irejeshwe ili washirika wawili wa muungano wawepo bila kificho kwa kuwa wanaona Zanzibar imeanza kutwaa hata isichostahiki.Katika hali kama hiyo, na kwa sababu kilio cha wananchi kutaka serikali itatue tatizo la muda

mrefu la mfumo wa muungano, hakuna tena namna ya kupuuza kilio hicho.
Katika muswada huo uliowasilishwa bungeni Jumatatu, Serikali imependekeza kuwa sasa ni ruhusa wananchi kujadili muungano, kinyume na pale awali, ila iwe ni katika kuuimarisha na siyo kutaka kubadilisha mfumo wake.Hapa serikali inashikilia mfumo wa muungano wa serikali mbili, msimamo ambao ungekuwa sahihi iwapo

haujapata kulalamikiwa. Umelalamikiwa sana.
Kwanza, kilio hicho hakikuja tu kwa bahati mbaya; kimetokana na wananchi wa upande wa Zanzibar kutoridhika na namna mamlaka ya nchi yao yalivyodhoofishwa kinyume na matarajio yao.Wanalalamika kuwa baadhi ya mambo yanayotambuliwa kama mambo ya Muungano, yaliingizwa kinyemela kutoka yale mambo 11 yaliyotajwa na kujumuishwa katika Hati ya

Makubaliano ya Muungano (Articles of Union) ambayo ndiyo msingi wa muungano.
Kwa miaka yote ya uhai wa muungano, miaka 47, serikali zote mbili zimeendelea kupuuza malalamiko ya wananchi. Hatua za sasa kupitia muswada wa katiba, zinaashiria kutaka kuzima kabisa malalamiko hayo.Hatudhani kwamba hiyo ni sahihi. Haiwezekani kukandamiza madai ya haki ya wananchi. Ni muhimu hoja zao

zisikilizwe na kuzingatiwa kwa sababu hakuna ubaya wowote kutazama upya mfumo wa muungano kama ni kweli uliasisiwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa nchi zilizoungana.
Tunasema huu ndio wakati hasa serikali zetu kufanya uamuzi mgumu ili kumaliza mvutano na tunaamini ikifanya hivyo, itakuwa inaepusha balaa huko mbele twendako.
Chanzo. Turudi kwenye muungano | Gazeti la MwanaHalisi
 
Namuunga mkono mtoa hoja. Ingawa wa Tanganyika wamekuwa na kigugumizi kwa hili lakin ndio ukweli wenyewe.
 
Wananchi wa Pande zote mbili wameshaonyesha kutohitaji huo Muungano. Ni serikali ndiyo inaonekana kuuhitaji huo muungano, kwa faida ya nani mpaka leo hatujui.
Serikali inakiwa kuitisha kura ya maoni ili kuwauliza wananchi kama watauhitaji huo muungano au kipengele cha muungano kiwe kati ya masuala ambayo tunapaswa kuyajadili kwa uwazi, wananchi wanahitaji kusikilizwa maoni yao badala ya kupuuzwa na na kubezwa eti waubezao hawajui umhimu wake.
Sawa hawaujui umuhimu wake, hiyo ni failure mojawapo ya serikali au muungano wenyewe kwa kutoeleweka kwa wananchi wake.
Ningependa kuwahimiza wananchi kuwa tunapoelkea katika majadiliano haya ya katiba mpya basi tuitumie nafasi hiyo kuukataa Muungano siyo muundo, namaanisha tuukatae muungano tulionao katika katiba ijayo.
 
Back
Top Bottom