Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
- Thread starter
- #21
Kubwajinga, Naunga mkono hoja yako ndugu yangu. Kuongeza idadi ya Wabubnge hakuongezi tija yoyote katika nchi yetu bali ni kuongeza tu gharama kubwa zisizo na msingi wowote.
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Shangingi ya Wabunge ni bil. 12.92/- [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Serikali imewapigia pande Wabunge wapya ya Jamhuri ya Muungano wa TZ jumla ya sh. bilioni 12.92 kwa ajili ya kununulia mashangingi mapyaa kama vitendea kazi majimboni kwao. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Katika pande hilo, kila mbunge aliyefanikiwa kutinga Dodoma atalamba jumla ya sh. milioni 40. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Bunge la Tanzania lina jumla ya Wabunge 323 na kwa mtaji huo mabilioni hayo yatamwangwa ili kuhakikisha Waheshimiwa Mama Rahimanino wanapatiwa michuma hiyo kuanza kazi zao rasmi. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Mshiko huo utatolewa kama mkopo na serikali ambapo Wabunge watatakiwa kulipa nusu ya fedha hizo yaani mil. 20 wakati mamilioni yaliyobakia yaani mil. 20 yatalipwa na serikali kama pande la kuongeza motisha ya kufanya kazi. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Utaratibu wa kukopesha Wabunge magari ulikuja baada ya utaratibu wa zamani wa kupatiwa magari kutoka Wilaya zao kuonekana unaongeza gharama kutokana na magari hayo kuharibika mara kwa mara kutokana na kutumika na wafanyakazi wengi kwa kubadilishana. [/FONT]
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Akifagilia hatua hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Bunge, Juma Akukweti alitonya kuwa utoaji mikopo umekuwa ukifanyika hivyo kwa Wabunge na serikali kuchangia gharama za michuma hiyo nusu kwa nusu ili kuwawezesha kuzungukia wapiga kura wao kiulaini. [/FONT]
Hii ni moja ya gharama za wabunge wetu. Hebu fikiria wakipungua mpaka 100 hivi tutaokoa mabilioni mangapi?