Tupinge malipo ya rada kama tulivyopinga dowans(richimondi)

Viongozi wetu pamoja mkuu wa inchi aliyepita wanayo change yetu na tunajua zilipo. Membe awaambie warudishe tu nasi hatunasababu ya kuwashitakli. Wasipofanya hivyo leo wakija watawala wengine watawashitaki au kuomba change hata kwa watoto wao japokuwa wao watakuwa wamekufa.
 
My God, sasa nini kinachofuata,? Watanganyika wake upppppppppppppp. Kuna haja gani ya kungoja 2015 kuwaondoa hawa? Situfanye hata sasa?kuna mambo mengi sana yamefichwa.

Mfumo wetu wa habari umeshikwa na watu hawa hawa wasio waadilifu. Wakati wote kile tunachokiona na kusikia sio reality. What happen here is what we call mind control through media, they are hiding the truth, katika nchi yetu politics inatupeleka pabaya, hakuna mwenye uchungu na hii nchi, inabidi watanzania tufikie wakati wa kusema sasa basi, its over.
 
KAMA umefuatilia japo kwa juu juu kile ambacho kinachosemwa na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe "fedha zetu za rada" unaweza kujikuta umeamini mambo yafuatayo. Kwamba, kampuni ya BAE Systems ambayo kutoka kwao tulinunua rada ya kuongozea ndege (Watchman Traffic Control System), imeamriwa kurudisha fedha na mahakama.



Asante kwa uchanbuzi wako. Je, unafahamu lolote kuhusu makubaliano kuhusu BAE na SFO ya namna ya kutoa fedha hizo? Je, unafahamu ni pande ngapi zilihusika katika makubaliano hayo?

Ninachofahamu, kabla ya makubaliano ya BAE na SFO kufikiwa, SFO kwa kushirikiana na DFID iliwasiliana na Serikali ya Tanzania (ikiwasilishwa na Wizara ya Fedha ) na kufanya mazungumzo ya namna ya fedha hizo zitakavyotolewa na nani apatiwe. Makubaliano hayo ndio msingi wa hukumu ya Jaji Bean wa Mahakama ya Southwalk Crown Court, na ndio sababu iliyomfanya kuamua kutoza faini ya Mahakama kidogo ili sehemu kubwa ya fedha zile zirudi Tanzania kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania, ambayo SFO, DFID, Serikali ya Tanzania walikuwa wameshayaainisha na ndio yaliyokuwa msingi wa makubaliano na BAE.

Ndio maana, katika Bunge la Uingereza, Waziri mdogo wa DFID alikaririwa akijibu swali kwa niaba ya Serikali ambapo aliainisha wazi msimamo wa Serikali ya Uingereza wa kuunga mkono fedha hizo zirudishwe Tanzania. Hakulitoa jibu lilie hewani. Suala la kwamba fedha hizi zirudishwe Tanzania linaungwa mkono na Serikali mbili za Uingereza na Tanzania.

Kuhusu watuhumiwa, hili ni suala tofauti kabisa na litaweza kushghulikiwa wakati wake ukifika. Kwa sasa muhimu ni hela yetu kwanza kurudi nchini maana watuhumiwa wa kwanza waliotoa rushwa hiyo wameamua kusameheana, hawa watuhumiwa wetu tunaweza kuwashitaki bado hapa nchini. Hata hukumu ya BAE haijawavua hatia watuhumiwa wa nchini kwetu. Hivyo, katika hili naunga mkono kuwa PCCB wabanwe wawafikishe hawa Mahakamani. Hili sio jukumu la Waziri Membe, ni la PCCB. Hata makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza hayakusimamiwa na Waziri Membe bali Wizara ya Fedha. Jukumu la Wizara ya Mambo ya Nje ni kutumia diplomasia ya kiserikali na ya umma (Public Diplomacy) kuhakikisha fedha zinarudi. Wengine wafanye majukumu yao.
 
viongozi wakuu wetu kusema uongo haiwatii uoga, ni fasheni.
Wakati wowote na bila uoga wao usema uongo. Hii si mala ya kwanza hivyo sishangai
 
Nafikili ujumbe kama huu ni kuutuma kupitia email yake.Niko natafuta email ya Membe nitamtumia tu
 
737753731_hPjyU-M.jpg

Kumekuwa na imani isiyo rasmi kuwa waziri wa mambo ya nje kwa kawaida ndiye rais mtarajiwa, hata Mkapa na Kikwete walianzia kwenye wizara hiyo hivyo ukiongezea na fununu za mitaani si dhambi tukisema waziri wa mambo ya nje wa sasa Bernard Membe amelalia mlango wazi wa kuwa binadamu wa tano kukalia kiti cha urais wa Tanzania na imani hata wapambe wake wanampamba hivi.
Tangu kuibuka kwa sakata la rada na jnsi kasi ya Membe katika kulishughulikia tayari malalamiko yameanza kusikika kila pembe ya nchi watu wakihoji juu ya uwezo wa rais huyu mtarajiwa katika kutetea maslahi ya taifa.
Membe haonyeshi hamu ya serikali kuwashughulikia watanzania waliohusika kwenye dili la rada na hata waingereza wanapogoma kulipa hizo fedha yeye anazungumza kisiasa kuwa lazima watulipe lakini ukipima mchoko wa kauli zake unamaizi kuwa ni kama anacheza makida ule mchezo wa kitoto kwa maana hata mimi ningekuwa nadaiwa kisha anayenidai haonyeshi kuwa kweli anataka nimlipe fedha zake basi sitamlipa hivyo ndivyo Membe anavyofanya.
Mimi nilitegemea atumie vizuri nafasi hii kujing’arishia nyota yake ya kwenda Ikulu lakini naona ameanza kupwaya mapema kwa kauli zake za kisiasa, hakuna haja ya kuwabembeleza wezi wala madalali wa Tanzania walioshirikiana na wezi dawa ni kuwashughulikia ipasavyo mpaka wajue kuwa Tanzania si shamba la bibi lakini naona Membe anatuchezea akili labda nimalize kwa kumtaka Membe mara atokezapo mbele ya umma na vyombo vya habari hatutaki tena mchezo wa kitoto bali tunataka tuambiwe ni lini? juma ngapi? na tarehe ngapi? wezi walikwapua jasho letu wataturudishia vinginevyo nitashawishika kuweka kulikoni? kwenye uwezo wa Membe kutetea maslahi ya Taifa.

NOVA KAMBOTA
0717 709618 / +255717 709618
novakambota@gmail.com
Nova Tzdream -
 
Hivyo, fedha hizo Paundi milioni 25.5 (Mahakama iliweka faini ya paundi laki tano), ni fedha za hisani kwa watu wa Tanzania.
Katika hukumu yake, Jaji Bean anasema hivi baada ya maelezo marefu ya kuelezea hiyo kesi: "The victims of this way of doing business, if I have correctly analysed it, are not the people of the UK, but the people of Tanzania"; yaani "wahanga hasa wa biashara ya namna hii, kwa jinsi nilivyoelewa, siyo watu wa Uingereza; bali watu wa Tanzania".

Mkuu Ogwari, je hapo juu ulimaanisha paundi millioni 29.5, au??
 
I find this article very interesting and highly articulated. This is how Tanzanian need to evaluate issue na sio kudandia dandia tuu, Membe ameshindwa kumlaumu mwanasheria mkuu kwa kushindwa kuwasimamisha mahakamani wote walio husika katika kuliingiza taifa kwenye hasara.

PCCB is the toothless watchdog, wameshindwa kufile kesi kwa watu wote muhimu waliousika katika kesi hii... Nasimama upande wa BAE rudisheni pesa moja kwa moja kwenye mikono ya Watanzania kwa kuinvest kwenye project ambazo zitawasaidia direct Watanzania. Serikali kama inataka pesa zao iende kuwadai kina Mkapa na kundi lake ambao ndio waliotuingiza kwenye huu mkenge.
 
viongozi wa tanzania wameshindikana kwa maneno ya uongo kutufanya watanzania wajinga!eti muda huu wanajifanya watanunua madawati!napata hasira mie yaani membe hata kumshukuru bi CLEAR SHOT aliyekua waziri alilamika sana juu ya deal hili la rada
 
Asante kwa uchanbuzi wako. Je, unafahamu lolote kuhusu makubaliano kuhusu BAE na SFO ya namna ya kutoa fedha hizo? Je, unafahamu ni pande ngapi zilihusika katika makubaliano hayo?

Ninachofahamu, kabla ya makubaliano ya BAE na SFO kufikiwa, SFO kwa kushirikiana na DFID iliwasiliana na Serikali ya Tanzania (ikiwasilishwa na Wizara ya Fedha ) na kufanya mazungumzo ya namna ya fedha hizo zitakavyotolewa na nani apatiwe. Makubaliano hayo ndio msingi wa hukumu ya Jaji Bean wa Mahakama ya Southwalk Crown Court, na ndio sababu iliyomfanya kuamua kutoza faini ya Mahakama kidogo ili sehemu kubwa ya fedha zile zirudi Tanzania kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania, ambayo SFO, DFID, Serikali ya Tanzania walikuwa wameshayaainisha na ndio yaliyokuwa msingi wa makubaliano na BAE.

Ndio maana, katika Bunge la Uingereza, Waziri mdogo wa DFID alikaririwa akijibu swali kwa niaba ya Serikali ambapo aliainisha wazi msimamo wa Serikali ya Uingereza wa kuunga mkono fedha hizo zirudishwe Tanzania. Hakulitoa jibu lilie hewani. Suala la kwamba fedha hizi zirudishwe Tanzania linaungwa mkono na Serikali mbili za Uingereza na Tanzania.

Kuhusu watuhumiwa, hili ni suala tofauti kabisa na litaweza kushghulikiwa wakati wake ukifika. Kwa sasa muhimu ni hela yetu kwanza kurudi nchini maana watuhumiwa wa kwanza waliotoa rushwa hiyo wameamua kusameheana, hawa watuhumiwa wetu tunaweza kuwashitaki bado hapa nchini. Hata hukumu ya BAE haijawavua hatia watuhumiwa wa nchini kwetu. Hivyo, katika hili naunga mkono kuwa PCCB wabanwe wawafikishe hawa Mahakamani. Hili sio jukumu la Waziri Membe, ni la PCCB. Hata makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza hayakusimamiwa na Waziri Membe bali Wizara ya Fedha. Jukumu la Wizara ya Mambo ya Nje ni kutumia diplomasia ya kiserikali na ya umma (Public Diplomacy) kuhakikisha fedha zinarudi. Wengine wafanye majukumu yao.

Hapo kwenye bold:Huu ni uchambuzi wa Mwanakijiji kwenye one of the weekly papers zilizotoka jumatano hii nadhani ni Mwanahalisi
 
asante kwa uchanbuzi wako. Je, unafahamu lolote kuhusu makubaliano kuhusu bae na sfo ya namna ya kutoa fedha hizo? Je, unafahamu ni pande ngapi zilihusika katika makubaliano hayo? Ninachofahamu, kabla ya makubaliano ya bae na sfo kufikiwa, sfo kwa kushirikiana na dfid iliwasiliana na serikali ya tanzania (ikiwasilishwa na wizara ya fedha ) na kufanya mazungumzo ya namna ya fedha hizo zitakavyotolewa na nani apatiwe. Makubaliano hayo ndio msingi wa hukumu ya jaji bean wa mahakama ya southwalk crown court, na ndio sababu iliyomfanya kuamua kutoza faini ya mahakama kidogo ili sehemu kubwa ya fedha zile zirudi tanzania kwa manufaa ya wananchi wa tanzania, ambayo sfo, dfid, serikali ya tanzania walikuwa wameshayaainisha na ndio yaliyokuwa msingi wa makubaliano na bae. Ndio maana, katika bunge la uingereza, waziri mdogo wa dfid alikaririwa akijibu swali kwa niaba ya serikali ambapo aliainisha wazi msimamo wa serikali ya uingereza wa kuunga mkono fedha hizo zirudishwe tanzania. Hakulitoa jibu lilie hewani. Suala la kwamba fedha hizi zirudishwe tanzania linaungwa mkono na serikali mbili za uingereza na tanzania. Kuhusu watuhumiwa, hili ni suala tofauti kabisa na litaweza kushghulikiwa wakati wake ukifika. Kwa sasa muhimu ni hela yetu kwanza kurudi nchini maana watuhumiwa wa kwanza waliotoa rushwa hiyo wameamua kusameheana, hawa watuhumiwa wetu tunaweza kuwashitaki bado hapa nchini. Hata hukumu ya bae haijawavua hatia watuhumiwa wa nchini kwetu. Hivyo, katika hili naunga mkono kuwa pccb wabanwe wawafikishe hawa mahakamani. Hili sio jukumu la waziri membe, ni la pccb. Hata makubaliano kati ya serikali ya tanzania na uingereza hayakusimamiwa na waziri membe bali wizara ya fedha. Jukumu la wizara ya mambo ya nje ni kutumia diplomasia ya kiserikali na ya umma (public diplomacy) kuhakikisha fedha zinarudi. Wengine wafanye majukumu yao.
umesema fedha ya rada irudswe serikalini halafu pcb ibanwe ili iwafikishe watuhumiwa wa ndani mahakamani. Labda nikufahamishe tu kwamba hosea wa pcb na chenge si kwamba tu wote ni wasukuma bali pia wanatoka eneo moja kule bariadi. Nakuachia utafakari mwenyewe.
 
umesema fedha ya rada irudswe serikalini halafu pcb ibanwe ili iwafikishe watuhumiwa wa ndani mahakamani. Labda nikufahamishe tu kwamba hosea wa pcb na chenge si kwamba tu wote ni wasukuma bali pia wanatoka eneo moja kule bariadi. Nakuachia utafakari mwenyewe.
Ushauri wangu ni kuwa, tujadili masuala na sio watu. PCCB ni taasisi. Siamini katika ukabila, udini, ukanda. Naamini katika utaifa zaidi ndivyo nilivyolelewa na kukuzwa kabla mabadiliko ya mfumo wa Elimu kuingiza huu 'usasa' hayajafanyika. Lakini nimeelewa ujumbe uliojificha nyuma ya kauli hii. Ni ujumbe mzito.
 
My God, sasa nini kinachofuata,? Watanganyika wake upppppppppppppp. Kuna haja gani ya kungoja 2015 kuwaondoa hawa? Situfanye hata sasa?kuna mambo mengi sana yamefichwa.Mfumo wetu wa habari umeshikwa na watu hawa hawa wasio waadilifu. Wakati wote kile tunachokiona na kusikia sio reality. What happen here is what we call mind control through media, they are hiding the truth, katika nchi yetu politics inatupeleka pabaya, hakuna mwenye uchungu na hii nchi, inabidi watanzania tufikie wakati wa kusema sasa basi, its over.
Sawa, tukiwaondoa tuwaweke nani? Tafakari.....!
 
Hapa inavyoelekea ''....la mdimu'' anajitafutia umaarufu wa kurahisishiana kazi 2015,
ndo maana kibaraka wake ''ugonjwa-sugu'' ashaanza kupaniki baada ya kuona mkuu wake anapewa fact
 
Membe for 2015

Kama membe ni jizi namna hii kuanzia pesa za Libya basi tupindue nchi na VIONGOZI 90% wa CCM wawekwe kwenye kikaango na tuwakamue utajiri wetu hasa ule walioUPORA na kuukimbizia nje ya nchi.

Nakwambia MAHABUSU zitajaa.
 
Na. Lula wa Ndali (Raia Mwema)

KAMA umefuatilia japo kwa juu juu kile ambacho kinachosemwa na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe “fedha zetu za rada” unaweza kujikuta umeamini mambo yafuatayo. Kwamba, kampuni ya BAE Systems ambayo kutoka kwao tulinunua rada ya kuongozea ndege (Watchman Traffic Control System), imeamriwa kurudisha fedha na mahakama.


Pili, fedha hizo zinazorudishwa kiasi cha Paundi milioni 30 hivi, ni zile ambazo tulilipia zaidi ya bei ya rada na hivyo ni “chenji” ambayo ni halali yetu.


Vile vile unaweza kuwa umeaminishwa kwamba fedha hizo ni mali ya serikali; kwani ni serikali ndio ‘iliyoingizwa mjini’ , na hivyo ni muhimu fedha hizo kurudishwa “kwa serikali”.


Pia unaweza kuwa umeaminishwa kwamba BAE inataka kuziingiza fedha hizi kupitia NGO ya Uingereza au hata NGO za Tanzania.
Kama wewe unaamini jambo lolote ama yote kati ya hayo manne, basi, wewe ni miongoni mwa watu ambao hawataki kutafuta ukweli. Yaani unazugika kirahisi, na yumkini ni miongoni mwa watu ambao ukisikia imesema “serikali imesema” basi huitaji kuhoji tena unaitikia tu “naam”.


Naomba mniruhusu nifyatuke kidogo leo. Kama kuna Mtanzania ambaye amewahi kupitia jengo lolote la shule (si lazima awe ameingia na kuketi darasani) na anaamini lolote kati ya hayo, basi, mtu huyo huwa kama mbwa mbele ya chatu; kwani hujikuta akilaanika kifikra kiasi cha kupata kigugumizi cha mawazo. Mambo yote hayo manne hakuna hata moja ambalo ni la kweli.


Kwanza, fedha ambazo BAE imekubali kuzitoa kwa ajili ya “kuwanufaisha watu wa Tanzania” hazikuamriwa na mahakama yoyote ya Uingereza.


Baada ya Taasisi ya UchunguzI wa Makosa makubwa ya Ulaghai (SFO) ya Uingereza kuendesha uchunguzi ulioonesha kuwa rada ya Tanzania iliuzwa kwa bei ghali na kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa hasa kwa kuwepo ushahidi ulioonesha kuwa BAE ilimlipa dalali Shaileth Vithlani mamilioni ya paundi ili kulainisha watendaji wa serikali na kupitisha dili ya ununuzi, uamuzi ulitakiwa ufikiwe.
Na uamuzi huo ni aidha kuleta mashtaka dhidi ya BAE Systems pamoja na mtu mmoja mmoja ndani ya kampuni hiyo au kuachilia. Wasingeweza kuachilia; kwani ushahidi ulikuwa mkubwa.


Hivyo, BAE Systems wakaamua kukaa chini na SFO na kukubaliana mambo mbalimbali ili kesi isiendelee na wasije kuingia gharama kubwa.


Ikumbukwe kuwa wakati SFO inachunguza BAES na sakata la rada, Serikali ya Marekani nayo ilikuwa inaichunguza BAES kupitia Wizara yake ya Mambo ya Sheria. SFO na DoJ ziliamua kukaa na BAES na kuingia makubaliano ya kumaliza uchunguzi uliokuwa unaendelea.
Kwa upande wa DoJ, BAES ilikubali kulipa zaidi ya dola milioni 400 bila kutoa kinga mwamvuli kwa wote waliohusika au kwa makosa yote. Maana yake DoJ wanaweza bado kuleta mashtaka dhidi ya BAES na watendaji mbalimbali kama kuna ushahidi mpya utaibuka kuhusiana na yale waliyochunguza.


Kwa upande wa SFO wao wakaamua kukubaliana na BAES mambo fulani fulani ili kumaliza uchunguzi wao. Mambo kumi na moja yalikubaliwa kati ya BAES na SFO kuhusiana na upelelezi wao wa sakata la rada la Tanzania.
  1. AES watakubali kosa moja kwa mujibu wa sheria ya Uingereza ya Makampuni ya 1985 (kosa linahusiana na mambo ya kihasibu).
  2. Kukubali kwake makosa kutafanyika katika fomu itakayowekwa ambamo masuala ya kesi yataorodheshwa.
  3. Faini ya kosa hilo itawekwa na mahakama.
  4. Kampuni ya BAES itatoa kama hisani (ex gratia) malipo ambayo yatakuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa Tanzania. Kiasi kitakuwa ni paundi milioni 30 ukiondoa faini zitakazowekwa na mahakama. Namna ya kutoa fedha hizo itakuwa kama itakavyokubaliwa kati ya SFO na BAES. (muhimu kuzingatia kuwa serikali ya Tanzania haitajwi).
  5. SFO haitamshtaki mtu yeyote kuhusiana na utendaji wake kwenye suala hili isipokuwa kwenye masuala ya nchi za Hungary na Czech.
  6. SFO itasitisha uchunguzi wote kuhusiana na BAES.
  7. Hakutakuwa na upepelezi wowote dhidi ya afisa yeyote wa BAES kwa jambo lolote kuhusiana na sakata hili kama lilifanyika kabla ya Feb 5, 2010.
  8. Hakutakuwa na mashtaka yoyote ya madai dhidi ya mtu yeyote ndani ya BAES kwa jambo lolote lilikuwa linachunguzwa na SFO.
  9. Mfanyakazi yeyote wa BAES hatotajwa au kuhusishwa katika kesi yoyote kama mshiriki wa njama zozote katika kesi yoyote ambayo SFO inaweza kuleta ikihusisha watu wengine.
  10. SFO na BAES wote watatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na makubaliano hayo.
  11. Makubaliano hayo yamefanyika chini ya sheria za Uingereza.
Hayo ndio makubaliano. Makubaliano hayo yalishtua taasisi mbalimbali za kisheria; kwani yalionekana kutoa kinga ya jumla kwa BAES kinyume na makubaliano ambayo BAES iliingia na Marekani.


Makubaliano hayo yalipotolewa hatukusikia serikali yetu (Waziri Membe au Mwanasheria Mkuu) kuyapinga. Hakuna kikundi cha wabunge kilichotumwa kwenda kudai SFO isiingie makubaliano hayo; kwani yalionekana kupendelea BAES, lakini yakaingiwa.


Jambo la pili ambalo yawezekana umeaminishwa ni kuwa fedha hizo ni fedha za “serikali”. Kama ambavyo nimedokeza hapo juu, fedha hizo ni hisani toka BAES. Sio malipo ya deni, sio adhabu, sio, sio ishara ya kujirekibisha, na wala si fedha ambazo tulilipa zaidi ya bei ya rada. Hili ni jambo la kueleweka.


Fedha hizi ni fedha za BAES. Fedha ambazo Vithlani alipewa na BAES ili kufanikisha dili la rada ni dola milioni 12.4. Ni muhimu kuzingatia kuwa kampuni ya Vithlani ya Merling International ilisajiliwa Tanzania. Hivyo, kama kuna mtu ambaye serikali ingeweza kumdai fedha yake ni Vithlani.


Hivyo, utaona dola milioni 60 hivi ambazo BAE wamekubali kuwapatia Watanzania zinadizi sana fedha ambazo Vithlani alichukua. Na ndio maana zinawafanya watu watoke mate huko waliko.


Sio fedha za serikali hizi, na serikali yetu haina haki hata kidogo ya kuzidai; lakini serikali ikitaka inaweza kumdai Vithlani au kutaifisha hadi kuku wake na kumrejesha nchini afungwe miaka 1000! Hapo ndio kweli serikali inaweza kujionesha kweli imechukulia suala la rada kwa uzito unaostahili.


Jambo la tatu ni kuwa, Waziri Bernard Membe wanaeneza taarifa kuwa makubaliano hayo yanasema fedha zitaingizwa kwa kupitia NGO ya Uingereza au NGO za Tanzania. Hili si kweli. Makubaliano (kifungu cha tano) yanasema hivi kwa Kiingereza “The company shall make an ex gratia payment for the benefit of the people of Tanzania in a manner to be agreed between the SFO and the Company. The payment shall be £30 million less any financial orders imposed by the court”.


Naamini Membe alitafsiri kwa makusudi ex gratia na kuleta kwenye Kiingereza kuwa as charitable walisababisha baadhi yetu kutafsiri kuwa ni “through a charity” ambayo kwenye Kiswahili tukafikiria ni “kupitia NGO”.


Neno ex gratia ni neno la kisheria sio neno la hivi hivi tu. Lina maana “kama hisani”; yaani mtoaji wa malipo kwa namna ya ex gratia anafanya hivyo bila kuonekana kuwa amelazimika au amelazimishwa au hata bila kukubali makosa yoyote yale.


Mara nyingi hili linatokea katika mahali ambapo mhusika hajakubali makosa au hana makosa, lakini kitu kibaya kimetokea na hivyo dhamira yake inamtuma kutenda hisani kwa yule aliyeumizwa.


Sio lazima iwe ni kwenye jambo baya. Ex gratia yaweza kutolewa hata kwenye jambo zuri kama kuonesha shukrani. La msingi ni kuwa, mtoaji anatoa wakati mwingine zaidi ya kile anachotakiwa kutoa.


Hivyo, fedha hizo Paundi milioni 25.5 (Mahakama iliweka faini ya paundi laki tano), ni fedha za hisani kwa watu wa Tanzania.
Katika hukumu yake, Jaji Bean anasema hivi baada ya maelezo marefu ya kuelezea hiyo kesi: “The victims of this way of doing business, if I have correctly analysed it, are not the people of the UK, but the people of Tanzania”; yaani “wahanga hasa wa biashara ya namna hii, kwa jinsi nilivyoelewa, siyo watu wa Uingereza; bali watu wa Tanzania”.


Utaona kuwa serikali ya Tanzania haikuhusishwa katika sehemu ya kurudishiwa fedha kwa sababu wao siyo waathirika; kwani wao ndio walishiriki kuwaumiza wananchi wao. Sasa wamepata wapi ujasiri wa kudai fedha za waathirika? Iweje walio jeruhi ndio wapewe fedha za pole?


Hili linanikumbusha kisa cha kiongozi mmoja ambaye baada ya kutuhumiwa kumpiga dereva risasi, baadhi ya viongozi wa serikali wakampa yeye ‘pole kwa yaliyomkuta’!


Jambo la nne; nadhani utakuwa umeshapata jawabu kuwa haijaamuliwa mahali popote kuwa fedha hizo ziingizwe kupitia NGO - iwe ya Uingereza au ya hapa nchini. Namna jinsi fedha hizo zitaletwa kuwanufaisha waathirika (Watanzania), ni kwa makubaliano kati ya SFO na BAES - sio mtu mwingine.


Haya yayote yanatufanya tujiulize swali moja kubwa: Kwa nini serikali (kupitia Waziri Membe) imetumia nguvu kubwa (ya kuomba ushirikiano wa wabunge “wote” na kutuma wabunge kwenda Uingereza) kudai kitu cha dezo?


Inakuwaje viongozi wetu wanatumia muda kwenda kubembeleza fedha za hisani zirudishwe kwao wakati wanajua kabisa kuwa kinachorudishwa sio deni wala malipo ya fedha ambazo serikali ilimgawia Vithlani?


Swali hilo ni muhimu; hasa tukiangalia mwitikio wa serikali ile ile kwenye masuala ya ufisadi wa Kagoda kwa mfano. Kagoda walichukua Sh. bilioni 40, lakini hatujasikia timu ya wabunge imejaribu kukaa nao na kuwataka warudishe fedha serikalini, kwanini?


Swali hilo linatufanya tuulize kuhusu mwitikio wa serikali hii hii kwenye suala la Meremeta na mabilioni ya shilingi yaliyochotwa na watu ambao wengine wamekaa humo humo kwenye serikali yao. Kwa nini serikali haikuwadai hawa?


Swali hilo linatufanya tuulize kama kweli hawa watu wana uchungu sana na fedha zetu, kwanini hawakufanya uchunguzi dhidi ya Andrew Chenge ili kuweza kuona mali alizonazo hazijatokana na mipango ya dili hizi; na sio yeye tu; bali na wahusika wengine wote?


Swali hilo linatufanya tuulize kama kweli serikali inaona imeonewa kwa nini haijaleta mashtaka mazito zaidi pamoja na kuifunga kampuni ya Vithlani (kama mwenyewe hajaifunga bado!), na hata kufaitisha mali zake?


Kwa nini katika mashtaka yao dhidi ya Vithlani hakuna mashtaka ya uhujumu uchumi, utapeli, n.k? Hivi kweli tunataka tuaminishwe kuwa kosa kubwa la Vithlani ni hilo la “kumdanganya mpelelezi”?


Hivi kwa nini hiyo serikali haijatoa taarifa yoyote huko Bungeni juu ya harakati za kumsaka Vithlani zimefikia wapi? Kwa nini serikali yetu ilipopeleka ujumbe huko haikupeleka ujumbe wa nguvu Interpol kuulizia na kutilia mkazo suala la kumkamata Vithlani ambaye anadunda tu huko aliko?


Sote tunafahamu sakata la posho za vikao sasa hivi (hatujagusa posho ya mawasiliano!) na jinsi gani mabilioni ya fedha zetu yanapotea kinyemela. Dk. Slaa, juzi, kagusia upotevu wa bilioni zaidi ya 200 ndani ya Jeshi la Polisi na Magereza, kwa nini hatujasikia wabunge wamemuita IGP Mwema kutoa maelezo? Au hizi fedha zinapoliwa na wajanja nchini hatuzihitaji kurudishwa isipokuwa zile za hisani?
Binafsi sitaki tuwe mashujaa wa kwenda kudai vya dezo, lakini vile vilivyo vya haki yetu tunashindwa hata kutoa maelezo! Sitaki kusikia serikali nzima inanyemelea fedha ambazo zinatakiwa kunufaisha Watanzania.


Sitaki kuambiwa kuwa ati leo hii serikali hii hii iliyotetea ununuzi wa kifisadi wa hiyo rada imeshindwa kuliomba radhi Taifa, na badala yake inajifanya kama ‘haijui’ kilichotokea! Na kinachoniudhi zaidi ni kuwa wapo watu ambao wanaamini kabisa Watanznaia hawana uwezo wa kumjulisha moja na moja na kupata mbili. Tatizo ni kuwa kweli wapo wengine wenye shida hiyo!


Sasa mimi nina pendekezo. Serikali iachilie hili suala la BAES na SFO na tusubiri tuone wao watakuja na mtindo gani wa kutuletea fedha kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania.
Na badala yake serikali ibane matumizi yake, ifuatilie fedha zetu katika zile kesi mbalimbali, ifanye uchunguzI dhidi ya Chenge na timu nzima iliyohusika na dili la rada, iongeze mashtaka dhidi ya Vithlani, yakiwemo ya uhujumu uchumi, na iwabane wakohoe hadi senti zetu za mwisho.
Twende tudai kilicho chetu kutoka kwa hawa wenzetu. Hilo la Waingereza wanajuana wenyewe; kwani kama ni uzembe ulikuwa wa kwetu!

swali kwako ongwari,
kwanini unafikiria serikali inapata wakati mgumu sana kumdai pesa zetu za ukweli vithlani ??
 
Back
Top Bottom