Tupime utendaji wa Mawaziri wetu

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wadau, wakati sasa umefika tutafute namna ya kupima uwezo wa Mawaziri wetu maana huwa nashawishika kuamini kuwa Mawaziri wengine ama wana damu tu ya kunguni (hawapendwi) au si wawajibikaji au pengine hawana 'vipawa' vya uongozi.

Nimefuatilia mafanikio ya Wizara alizoongoza Waziri Dk Shukuru Kawambwa tangu awamu iliyopita na nimeshindwa kuona/kupima mafanikio ya utendaji wake kwenye Wizara hizo. Waziri Dk Kawambwa ni muungwana sana kwa kumuangalia na hata kauli zake; hata hivyo mafanikio ya Wizara alizoongoza naona kama amefeli kama Waziri na nadhani kazi ilinyomfaa zaidi ni Dipolomasia au Uhadhiri na si Uwaziri.

Awamu iliyopota alikuwa Waziri wa Miundombinu. Wizara hiyo (wakati huo ikijumuisha na Ujenzi) ilionekana kupwaya mno na miongoni mwa jambo ambalo Waziri Dk Kawambwa alishindwa kabisa kulitatua ni suala la TRL. Migogoro baina ya Wafanyakazi wazawa na Mwekezaji RITES haikuisha na hatuelwi kama kweli Mkataba ule wa TRL na RITES bado upo au ulivunjwa kama ilivyotangazwa maana nimesikia kuwa Wahindi wa RITES bado wapo. Sula hilo Waziri Dk Kawambwa lilimshinda kabisa.

Awamu hii Dk Kawambwa ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu ambayo pia inahusisha Elimu ya Juu. Kinachoendelea sasa Vyuo Vikuu- UDOM na MUCE ni maandamano na malalamiko lukuki kiasi kwamba nilimsikia mwanafunzi mmoja akisema kuwa bila kugoma Serikali huwa haiwasaidii hadi hapo wanapogoma ndipo Serikali inaingilia.

Suala la UDOM lilipopamba moto sana Waziri Dk Kawambwa aliingilia kati na ilibidi afanye ziara UDOM. Mimi nilidhani kwa ziara yake kule UDOM basi mambo yangeisha, lakini badala yake baada ya muda mfupi migomo ikaanza tena, tena safari hii hata Wahadhiri nao wagoma hadi hapo Waziri Mkuu alipoingilia kati! Nashindwa kuelewa, hivi Mawaziri wetu hawana mandate ya kutatua matatizo ya Wiazara zao hadi Waziri Mkuu aingilie kati? Sasa kuna haja gani ya kuwa na Waziri kwa Wizara husika?

Nawasilisha.:frusty:
 
Wadau, no comments? Ni kweli tunaridhika na utendaji walioshindwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom