Tupeni tathmini, upepo wa ushindi CHADEMA ukoje katika kata hizi?

Tunaomba majibu ya msingi:

1. CHADEMA kimesimamisha wagombea katika kata zote? Ni kina nani?
2. Je, kuna uratibu kutoka makao makuu ili kusaidia kampeni katika kata husika?

Binafsi nimechoka kusikia Darajambili kila siku!

Chaguzi hizi ndogo ni kiashirio (inference) cha hali ya kiasa sasa hivi na hata itakavyokuwa mwaka 2014. Tuache siasa za mitandaoni, tufanye kazi.

Kata ya Moyavizi Mbozi Mashariki Magamba watashindwa kuchakachua kura kwani kijana Mtakati atashinda kwa kishindo.
 
Hivi vipau mbele vya chadema kila mwanacdm au wananchi wanavijua? Hili ndilo litakalotoa mwanga wa ushindi kwa chama hicho. Na matokeo haya yatatoa picha ya tuendako maana hali inaanzia huku chini. Maeda hajatujuza kama wameweka wagombea ktk kata zote. Tueleze tu hata usipotaja majina sawa tu.
 
Anapata support kutoka jimboni, mkoani na hata makao makuu? Msaidieni jamani.

Mkuu, kwa Mbozi mashariki CHADEMA imejipanga vizuri sana kwenye kata hiyo kuna tajiri mmoja wa Magamba ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya magamba katika kijiji cha Ichesa aliwafunga jera vijana wa CHADEMA kwa kusaidiana na polisiccm kupika kesi. CHADEMA wilaya na mkoa walikata rufaa na kuwawekea wakili kwa ghalama za CHADEMA. Vijana wakashinda rufaa hiyo maonezi ya magamba yamefumbua macho watu wa rika zote katika kata ya Moyavizi hawataki kusikia habari za magamba kabisa.
 
Mara nyingi naona Kamanda Tumaini Makene analeta news zilizotoka kwa Mh Mnyika. Ngoja nimtafute Mnyika kwenye twitter aje atupe habari yenye uhakika hata kama itapitia kwa Members wapya wa JF Wassira na Mashishanga
 
anael suala si cdm kujipanga ni sisi watanzania kuichoka ccm.
kama huko mara imetumika mil 300 kwa ajili ya kumng'oa mtu mmoja hiki chama si kimeoza?

Huyu alishakunywa maji ya bendera ya magamba hata upige debe unapoteza muda wako!
 
Tunaomba majibu ya msingi:

1. CHADEMA kimesimamisha wagombea katika kata zote? Ni kina nani?
2. Je, kuna uratibu kutoka makao makuu ili kusaidia kampeni katika kata husika?

Binafsi nimechoka kusikia Darajambili kila siku!

Chaguzi hizi ndogo ni kiashirio (inference) cha hali ya kiasa sasa hivi na hata itakavyokuwa mwaka 2014. Tuache siasa za mitandaoni, tufanye kazi.
Mkuu Kashaija Butege, asante, hii ni hoja ya msingi sana!, ngoja tusubirie majibu.
P.
 
Mkuu Kashaija Butege, asante, hii ni hoja ya msingi sana!, ngoja tusubirie majibu.
P.

Nafikia kuamini kuwa CHADEMA hakijasimamisha wagombea katika kata zote, na kama wamewasimamisha basi vetting haikufanyika kwa undani. Amini usiamini Pasco, uchaguzi huu utaonesha kama kelele tunazopiga humu mitandaoni zinafuatiliwa na viongozi wa CHADEMA, au basi tu wanatuchukulia kama watu wa kijiweni tusio na shughuli za kufanya.
 
Naweza kusema kwa uhakika bila piace of doubt kuwa uchanguzi huu ni taswira ya 2015 national election, Mwekuti Mbowe alisema wanaweza kushinda kata 20 kati ya hizo 29 tusubiri tuone mtinange.
 
mimi nimejibu kwa upande wangu niufahamuo,sasa kwa kuwa hizi ni taarifa pengine mwingine atatoa za upande mwingine mkuu.

Asante. Kazeni mwendo makamanda. Itapendeza kama CHADEMA kitatisha sehemu zote, hasa miko ile ya Mtwara na Lindi. Ningefurahi zaidi kama kitashinda kata iliyoko Bagamoyo. Yaani ningependekeza Bagamoyo wapeleke nguvu kama zilizotumika katika uchaguzi mdogo wa Kirumba na Kiwira.
 
Kaka sikia nikuambie CHADEMA ni Arusha mjini, Moshi Mjini,labda Mbeya Mjini kwine hakuna kitu. Wanataka kuwaaminisha wananchi tu lakini bado hawajajipanga. Wakipata ka kata kamoja basi kelele hizo.

NB: Hawawezi kuchangia thread hii maana iko direct.

wewe i.d.i.o.t nani hawezi kuchangia hii post! CHADEMA tumesimamisha kata zote udiwani, siyo kila kata kuna watu wake humu jf ili upate taarifa, unapata taarifa za arusha kwa sababu watu wake wapo humu na tumejipanga, dodoma nimepata taarifa mambo mazuri mno, japo CCM mnaendelea na zoezi la kugawa pilau kwenye mikutano!
 
Anael
Unataka jibu unalotaka wewe nimesema kuwa CHADEMA imesimamisha wagombea kata zote 29 nchi nzima.
 
wewe i.d.i.o.t nani hawezi kuchangia hii post! CHADEMA tumesimamisha kata zote udiwani, siyo kila kata kuna watu wake humu jf ili upate taarifa, unapata taarifa za arusha kwa sababu watu wake wapo humu na tumejipanga, dodoma nimepata taarifa mambo mazuri mno, japo CCM mnaendelea na zoezi la kugawa pilau kwenye mikutano!

Safi sana kamanda. Kuna mtu asubuhi hii ameniambia kampeni za Bagamoyo zinaendelea vizuri. Mie nitaenda huko kufanya tathmini siku ya Jumamosi.
 
1.Bangata-Arusha
2.Darajambili-Arusha
3.Msalato-Dodoma
4.Mpwapwa-Mpwapwa

5.Magomeni-Bagamoyo
6.Lwenzera-Geita
7.Bugarama-Kahama
8.Mwawaza-Shinyanga

9.Vugiri-Korogwe
10.Tamsta-Lushoto
11.Makata-Liwale
12.Mneromiembeni-Nachingwea
13.Mlangali-Ludewa
14.Luwumbu-Makete
15.Mpepai-Mbinga
16.Mletele-Songea
17.Ipole-Sikonge
18.Kiloleli-Sikonge
19.Miyenze-Tabora
20.Karitu-Nzega
21.Mpapa-Mbozi
22.Myovizi-Mbozi
23.Lubili-Misungwi
24.Kilema-Kusini-Moshi
25.Nanjarou/Reha-Rombo
26.Mtibwa-Mvomero
27.Mahenge-Ulanga

28.Likokona-Nanyumbu
29.Kitangiri-Newala

Taarifa za Kiintelijensia zinasema CCM imeweka mkakati kuweka nguvu zaidi katika kata zilizokolezwa kwa wini mwekundu. CHADEMA chukua hatua acha kubweteka. Wanasema hizo nyingine wana uhakika wa kushinda.

Mlioko viwanjani tujuze hali ikoje mpaka sasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom