Tupendane: Matukio 08 wakristo,wayahudi na waislamu waliyookoana ktk mazingira usiyotarajia

Tusibaguane

JIFUNZE HAPA

1:WAISLAM WA SYRIA na WAALMENIA WA UTURUKI
Armenians_marched_by_Turkish_soldiers_1915.jpg

Chini ya utawala dhalimu wa OTTOMAN uturuki waliamua nchi nzima iwe ya waturuki na ya kiislamu na kufyeka makabila yote na wakristo. Waalmenia zaidi ya million 2.5 wengi wao wakristo walikuwa wahanga wa kwanza. wengi walikimbilia syria nchi ambayo wayahudi,wakristo na waislamu waliishi kwa upendo. Waislamu waliwapokea wakristo hawa na kuwahifadhi hadi syria ikaitwa MBINGU SALAMA/Safe heaven. Fadhila zinalipwa leo maana waislamu wa syria wakikimbia vita dhidi ya ISIS wanapokelewa na jamii ya WAALMENIA waliopo ULAYA, CANANDA na US wakikumbuka wema waliwafanyia.

2:KIJANA WA KIISLAMU REFIK (17) ALIYOOKOA FAMILIA ZA KIYAHUDI
iStock_000032313968_Small.jpg

Kabla ya msako wa kuwauwa wayahudi. Albania wakristo,wayahudi na waislamu waliishi kwa upendo. Myahudi mmoja Moshe Mandil alikuwa amemuajiri kijana huyu wa kiislamu. baada ya msako wa HItler kuwaua wayahudi. Kijana huyu aliichukua familia hii na kuificha nyumbani kwao milimani. Sio huyu tu wayahudi wengi walihifadhiwa na waislamu na kuwaokoa maisha.

3:MAKASISI WA KIGIRIKI
iStock_000091235591_Small.jpg

Hapa wakristo na wayahudi waliishi vizuri kabisa. Wanazi walioingia waliomba list ya Wayahudi wote ili wawaue. Kadrinari aliyaandikia makanisa yote na makasisi barua kuwa Wawatengenezee Wayahudi VYETI FEKI VYA UBATIZO ili waonekane ni wakristo ili wasiuwawe. Kuna kisiwa kimoja nchini hapo kilikuwa na wayahudi 257 aliwaadaa wanazi kuwa kuna wayahudi wawili tu. Msako mkali wa SHOOTING SQUARD haukuwaona hata mmoja wote walifichwa na wananchi.

FAIDA: Mwaka 1953 lilipotokea tetemeko ugiriki Taifa la kwanza kutoa msaada tena haraka lilikuwa ni ISRAEL.

4:UOKOAJI WA WAYAHUDI DENMARK
iStock_000007460704_Medium.jpg

Hapa SHOOTING SQUARD ya WANAZI ilimuhitaji mfalme atoe tangazo kuwa wayahudi wote wavae ngue zenye alama kama nyota hapo juu ya njano(david star) ili wawatambue kirahisi maana wakristo/warutheli na wayahudi walikuwa karibu mno. Cha ajabu wa kwanza kuvaa hivyo alikuwa Mfalme mwenyewe na kuwataka watu wote wavae hivyo. Hii iliwachanganya wanazi. Walipokuja kwa kasi kuua walichelewesha huku maelfu ya wayahudi wakitoroshwa na meli za wavuvi. Ikiwa ni idadi kubwa kabisa. Hadi leo matajiri wakubwa na wanaoifanya denmark iwe juu kitechnolojia na kiuchumi ni hawa jamaa.

5:MSIKITINI PARIS PALIPO GEUZWA MBINGU SALAMA KWA WAYAHUDI
640px-Grande_Mosqu%C3%A9e_de_Paris.jpg

Wanazi walipoichukua PARIS 1940. Msako wa wayahudi ulianza na maelfu wakubwa kwa watoto walikamatwa na kupelekwa kambi za mateso Ujerumani. Ni huu msikiti uliowaficha kwa kuwapa chakula,malazi na hata fursa ya kuoga mamia ya wayahudi wenye asili ya Afrika kaskazini na kuwaokoa.

6:Tahrir Square
800px-Tahrir_Square_-_February_9_2011.jpg

Katika hali ambayo haikutarajiwa Wakristo waliweka tofauti zao pembeni wakaungana na waislamu kumuondoa madarakani Mubarack. Hii ilithibitishwa zaidi siku ya kuondoka baada ya ushindi Ijumaa February 2011, Waislamu walitoa mikeka yao na kuanza kuswali huku wakristo wamewazunguka kuwalinda. Hata baadae wakristo walipoanza kuvamiwa na wachache wenye nia mbaya waliibuka waislamu kuwalinda.

7:SHOMRIM - ASKARI MAALUMU WA KIYAHUDI WALIOJITOLEA KUWALINDA WAISLAMU
Stamford_hill.jpg

Baada ya jamaa mmoja kuchomwa kisu LONDON (MWANAJESHI) na ikasemekana Alichomwa na waislam. Ilizuka vurugu kubwa huku misikiti ikichomwa moto, makundi ya vijana yakiwachoma visu waislamu kama kisasi. Kikundi kimoja cha Wayahudi SHOMRIM kilijitolea kuwalinda waislamu na kuwasaidia polisi. Polisi haya jamii pamoja na waislamu wachache walishirikiana kushika doria usiku na mchan kuwalinda waislamu wasiuwawe huko. Kikundi hiki cha WAYAHUDI kimekuwa MACHO na MASIKIO ya polisi na kimekuwa msaada kwa watu wa imani zote hasa waislam.

8:HII YA WAKRISTO WA NA WAISLAM WA CAMEROON ITAKUSHANGAZA ZAIDI
726px-LamidoGrandMosque.jpg

BOKO HARAM wanaojiita waislam ila cha ajabu huko wanashambulia MISIKITI na MAKANISA. Hii imewafanya waislam na wakristo cameroon kuwa wamoja na kuweka tofauti zao kidini. Sasa WAKRISTO wakiwa wanasali waislamu wanawalinda nje hadi ibada iishe, Waislamu wakiwa wanaswali basii wakristo nao wanapeana zamu ya kuwalinda waislamu hadi ibada iishe. Mfano huo msikiti unaitwa lamido Grand hicho kitu hufanyika.

MODS: Hii sio ya kidini isipelekwe jukwaa la dini hii ni mada ya KIJAMII.

karibuni: Sema chochote
HHili ni funzo boa kabisa.
 
yani lipo moja kubwa ambalo katu halitotajwa kwa kuwa watu wako na malengo ya kuwatenganisha wadamu kutoka ktk asili yao ya utu na kupenda ili tu wao wapate kusimamisha imani zao ambazo hata yesu na muhammad hawajawahi zifundisha.
subiri mtawaona.
 
nimeipenda hii makala;kw nn ss hatuwezi kuendelea kuishi kwa upendo na amani tena kama zama hizo?hata kama chanzo ni wanasiasa,kwani wao hawana dini?
 
nimeipenda hii makala;kw nn ss hatuwezi kuendelea kuishi kwa upendo na amani tena kama zama hizo?hata kama chanzo ni wanasiasa,kwani wao hawana dini?
Historia inaonyesha hata Jerusalem ilipokuwa chini ya Islamic calphate, caliph Umar aliwataka waislam wawavutie wakristo nawayahudi wakati huo kuhamia uislam kwa kuishi maisha ya mfano sio nguvu. Hivyo kila mtu aliendelea na dini yake, kwa amani tena wakilipishwa kodi kidogo kuliko mtawala aliyekuwepo. Kuishi kwa amani za kidini kumekuwepo tangu zamani sana. Lakini siku za hivi karibuni dini zimeingiliwa na watu au vikundi vyenye malengo binafsi ya kimaslahi,siasa etc.
Ni kazi yetu kuomba amani na upendo huku tukikosoana katika tofauti zetu za kidini kwa amani upendo na uvumilivu wote.
 
Back
Top Bottom