Tupeane mawazo wapendwa

lakini Nyamayao mwenye jukumu la kulinda ndoa ni nani huoni ni sisi wengine kutotumia akili zetu tu ndo husababisha yote hayo.

huyu shemeji yangu alichukulia kama kamwona dada na ukoo wake wote, shemeji anapangiwa na mama yake mambo yake ya familia na mambo kibao ya kimaisha, ni yule anaemckiliza mamake so ikapelekea hawa watu kutengana...
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa sio wote wanaoacha/chwa ni malaya au wahuni.

Freema,

Katika Ndoa uwa HAKUNA KUACHWA bali KUNA KUACHA... Na watu wengi wanashindwa kutofautisha na wanachukulia haya maneno ki-juujuu tu..

Mara nyingi panapotokea kutokuelewana katika ndoa, mwanamke uacha - pack the bag and go - right? Also in very few cases, Wanaume ufanya maamuzi ya kuacha - pack the briefcase and go - Hakuna anayeachwa. Aneyafanya maamuzi ya kuondoka maana yake ameacha hajaachwa ...
 
Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.

Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.

Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?

Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?

Tushirikiane kupeana mawazo wandugu

Maisha ya kuishi wote hata kama ni kuvumiliana basi amani na upendo viwepo. Je kuna raha gani kuishi na mtu mmenuniana kisa watoto? Ilhali kama mnaweza kupeana nafasi na mkawalea watoto vizuri huku mkiwasiliana kuhusu suala zima la malezi ya watoto, naona its fair enough hata kwa hao watoto. Siyo kwamba naunga mkono watu kutengana ila inafika wakati inabidi kukubaliana na hali halisi ya maisha.

Sijui kwa nini mimi naamini peace of mind ni kitu muhimu sana kwenye kufanikisha majukumu mbalimbali..hii umenuniana na mtu hata kurudi nyumbani unakuwa kama unalazimishwa wengine mpaka wanatamani wenza wao wafe, kweli haina raha yoyote..Haimaanishi ukitengana mtu ukimbilie kwa mwingine ila ni kutulia na kutafakari kabla ya kuingia mahusiano mengine, halafu kuwapa watoto kipaumbele ni jambo la busara.
 
Freema,

Katika Ndoa uwa HAKUNA KUACHWA bali KUNA KUACHA... Na watu wengi wanashindwa kutofautisha na wanachukulia haya maneno ki-juujuu tu..

Mara nyingi panapotokea kutokuelewana katika ndoa, mwanamke uacha - pack the bag and go - right? Also in very few cases, Wanaume ufanya maamuzi ya kuacha - pack the briefcase and go - Hakuna anayeachwa. Aneyafanya maamuzi ya kuondoka maana yake ameacha hajaachwa ...

Skulmeti, leo upitie pale, mwambie Jesca akupe bia tatu ntakuja kulipa.
 
Unasema watu wanaoachana hua hawafikirii watoto?Kuna wavumiliaji ambao hua wanajifanya wanabaki kwaajili ya watoto ila watoto ndo wanaoishia kuteseka!Si kila mtu anafaa kua mzazi mpaka useme lazima wawepo wote ili mtoto afurahie..kuna wengine mmoja anaweza kuwapa hao watoto mapenzi zaidi ya wanayoweza kupewa na wazazi wawili.Kama hujui mara nyingi watu hua wanamalizia frastruatian zao kwa watoto!We unaposema unavumilia mwanaume anaona unamng'ang'ania!Kama hutakiwi ondoka..au kaa subiria Ukimwi!
 
Ukiniacha hautauona Ufalme wa Mbingu.
 
Maisha ya kuishi wote hata kama ni kuvumiliana basi amani na upendo viwepo. Je kuna raha gani kuishi na mtu mmenuniana kisa watoto? Ilhali kama mnaweza kupeana nafasi na mkawalea watoto vizuri huku mkiwasiliana kuhusu suala zima la malezi ya watoto, naona its fair enough hata kwa hao watoto. Siyo kwamba naunga mkono watu kutengana ila inafika wakati inabidi kukubaliana na hali halisi ya maisha.

Sijui kwa nini mimi naamini peace of mind ni kitu muhimu sana kwenye kufanikisha majukumu mbalimbali..hii umeniana na mtu hata kurudi nyumbani unakuwa kama unalazimishwa wengine mpaka wanatamani wenza wao wafe, kweli haina raha yoyote..Haimaanishi ukitengana mtu ukimbilie kwa mwingine ila ni kutulia na kutafakari kabla ya kuingia mahusiano mengine, halafu kuwapa watoto kipaumbele ni jambo la busara.
hili post ukichanganya na hayo ma lips mie kwisha habari yangu. naomba nikuwe msomaji tu kwenye hii sred
 
ni kweli watoto ndo wanapata matatizo na matatizo yapo mengi na wakati mwingine sio lazima mtu awe malaya

Unasema watu wanaoachana hua hawafikirii watoto?Kuna wavumiliaji ambao hua wanajifanya wanabaki kwaajili ya watoto ila watoto ndo wanaoishia kuteseka!Si kila mtu anafaa kua mzazi mpaka useme lazima wawepo wote ili mtoto afurahie..kuna wengine mmoja anaweza kuwapa hao watoto mapenzi zaidi ya wanayoweza kupewa na wazazi wawili.Kama hujui mara nyingi watu hua wanamalizia frastruatian zao kwa watoto!We unaposema unavumilia mwanaume anaona unamng'ang'ania!Kama hutakiwi ondoka..au kaa subiria Ukimwi!
 
Dear maty yaani leo umegusa mtima muhimu sana katika maisha yetu ya sasa. Kusema ukweli hal hii inatisha na kwa bahati mbaya sana ndio kwaaanza inakamata chati kwa kasi. Sometimes nasema bila kumtanguliza MUNGU katika ndoa na maisha yetu, mambo kama haya ni inevitable kabisa. Na kama ulivyosema ndoa za wenye viwango flani vya elimu mamb ndo huwa magumu zaidi kuliko ndoa ambazo wanaume ndo wenye elimu au mali kuliko wanawake. Kwenye ndoa ambayo wenzi wote wana viwango sawa vya elimu au kipato mara nyingi kuna mambo ambayo katu hayatavumilika na pande yoyote kati yao. Mf. Katika ndoa kama hii kwa wale wanaume wenye tabia ya kunyanyasa wanawake kwa kisingizio kuwa ni mkewe na hapaswi kuuliza, hoji au kufuatilia mambo anayoyafanya yeye kama mume ni wazi akileta ubabe kwa vitu ambavyo ni obvious mke atapata kichwa kuwa asimbabaishe.
hali kadhalika mke anawezakuwa ndo chanzo cha matatizo especially kama naye akikinga mkono kiganja kinajaa....... anawezajikuta analeta hadithi za usawa mpaka kwenye kugawa dozi............jana nilikupa leo nami napumzika (utadhani akitoa anayefurahia ni mpewaji tu). Sasa kwa mwanaume mwenye mke wa hivi ni lazima hatakubali na ataona ni bora atafute amani huko inakopatikana.

Ni tofauti na nyumba ambayo mke ni msomi, mume msomi but kila mtu anajua na kutimiza wajibu wake kama mume/mke na kama Baba/mama. Hawa wataishi kwa amani pamoja na kuwepo kwa migongano ya kawaida, heshima inatawala zaidi na kila mtu anatambua thamani ya mwenzie. Kinyume cha hapo ni kutengana.
wa maisha halisi ya w

Darling maty...........when worse comes to worse sometimes ni bora mkatengana kuliko kuwakuza watoto katikati ya uwanja wa vita. Madhara yake ni makubwa kuliko yale wanayoyapata kwenye utengano kwani huko unawezakupanga mpangilio maalumu. Kulea watoto ndani ya ndoa yenye migongano kila kukisha (sisemi ile ya kawaida) but sometimes watu wanakuwa na irreconciliable issues ambazo nyingine wanashindwa kabisa kuzicontant na kutozionyesha kwa watoto. Mfano kupigana, kutukanana, kunyanyasana n.k. madhara ni makubwa sana kisaikologia kwa watoto wanaokulia ndani ya familia za aina hizo na usijeshangaa mtoto akakua na yeye kuwa violent au na tabia za ajabu kwa familia yake........ni effect aliyoipata wakati anakua na ameichukulia ndivyo ndoa zilivyo au zinavyotakiwa ziwe. Mtoto anayekuwa kwenye familia ambayo mama yake haeshimiwi, ananyanyaswa na mama huyo kukaa kimya naye atachukulia kuwa ndivyo mke mwema anavyopaswa kuwa...so mkewe akiwa tofauti tu ni tatizo. The same kwa watoto wa kike, kama baba ananyanyaswa, anatukanwa au anapigwa watategemea kupata wenzi wenye nidhamu kama baba yao.

So I dont think kuwa mara zote kutengana ni kuwadeprive watoto amani. ila tu kuwe na zingatio kubwa katika kujaribu kuwaelewesha why hali imekuwa kama ilivyo (epuka kuonyesha ubaya wa mwenzi wako kwa watoto)

Maty unauliza maswali mengii............. kuhusu kama ni suluhisho ninawezasema ndio na hapana. Itategemea unapoamua kuachana na mwenzi wako umejipangaje kukabili maisha yako ili usijikute kwenye wakati mgumu utakaokufanya ujutie maamuzi yako. Lakini vile vile kabla hujaamua "mimi sasa basi" ni vema ukachukua muda mzuri wa kukaa na kutafakari ili kujidhihirishia kuwa unachukua uamuzi sahihi na changamoto zake unazijua vema na una mikakati ya kukabiliana nazo. Epuka kuamua kwa hasira. Itakuumiza mwenyewe.

Kuhusu kuoa/olewa tena...............uhmmmmm inategemea na kama uliamua kuufungua tena moyo wako kwa mwingine na kama maamuzi yako ya kuolewa/oa yalishirikisha experiences ulizozipata kwenye ndoa yako ya mwanzo. Usikurupuke kwa kuwa tu kuna jamaa kakutamkia anakupenda na wewe ukataka kumdhihirishie mtalaika wako kuwa "yeye alipokuwa akisema wa nini, kuna walokuwa wanajiuliza watakupata lini" utaumbuka.

Usinisahau kadi ya mwaliko mamito

Nidai ofa ya pasaka mamito lol
 
Back
Top Bottom