Tupeane mawazo wapendwa

Usipoachana utakuwa na nyumba ndogo

Hahahahaha dena umenifurahisha asee, hivi hamuwezi mkakaa mkazungumza mkayamaliza na kuendelea kuishi kwa amani kweli? Mi nadhani kwenye ndoa ukimya ni mwingi sana watu hawapati muda wa kuzungumzia matatizo katika ndoa zao. Yaani inawezekana mmojawapo kati ya baba au mama hataki kabisa kukaa chini kuwekana sawa na mwenzie au akiambiwa anakuja juu
 
nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!

Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.

kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.

Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!![/QUOTE]

hahahhaha Susy umenifurahisha hapo kwenye red

ila kweli ndoa za siku hizi zinatukatisha tamaa, yani hata hamu inatoweka
it's not exciting kuolewa anymore sio kama zamani
Ooh Lord, please give me strength
 
Hahahahaha dena umenifurahisha asee, hivi hamuwezi mkakaa mkazungumza mkayamaliza na kuendelea kuishi kwa amani kweli? Mi nadhani kwenye ndoa ukimya ni mwingi sana watu hawapati muda wa kuzungumzia matatizo katika ndoa zao. Yaani inawezekana mmojawapo kati ya baba au mama hataki kabisa kukaa chini kuwekana sawa na mwenzie au akiambiwa anakuja juu

Maty, hapo inategemea.ngoja nisemee upande mmoja
kwa mfano una mwanaume hataki kukaa chini kuongea hata umfanyeje
kwani tatizo nini, tumia njia yoyote ya kumjulisha unachotaka kusema
unaweza kumuandikia barua, mtumie txt msg ndefu kama barua, tuma e-mail n.k at the end of the day atasoma tuuu any of them
na ujumbe utakuwa delivered..sasa kwakuwa yeye kichwa ngumuu ndo hatobadilika ila kama mtu poa atabadilika tuu..
nimesemea hivi mana mara nyingi kwenye mahusiano wanaume ndo wanakuwa wagumu kuwekwa chini kuongelea matatizo ya mahusiano yao.. vikishindikana vyote hivyoo chapa lapa..ndo point inabaki pale pale..TUSICHOSHANEE..
 
kitufe cha asante sikioni kwangu ,ningekiona ningekugongea ila kwa vile kuna like basi nahisi bora nigonge hapo.

Kwa mtazamo wangu, kuachana siku zote siyo jambo linalotarajiwa na wengi pindi wanapoanza mapenzi yao na hatimaye kufunga ndoa. Ila kutokana na sababu mbalimbali zinazorekebishika na zisizorekebishika ndiyo kunapotokea huko kuachana.
Kuachana kunatokana na kukosekana kwa upendo na uvumilivu kwa wanandoa,
lakin mimi naamini siyo kila jambo linavumilika,yapo yanayovumilika na yapo yasiyovumilika hata kwa sekunde moja.

Kuachana wakati mwingine siyo jambo zuri kwa wanandoa na watoto wao,lakin
kuachana wakati mwingine ni jambo zuri tena zuri sana kwa wanandoa pamoja na watoto pia.Lililo muhimu ni kujua sababu ipi/zipi zinawafanya m achane.

Uvumilivu ni mzuri sana lakin siyo kwa kila jambo ksb uvumilivu mwingine ukizidi, unaweza kufika mahali USIWE WENYE MANUFAA KWA NDOA YENU PAMOJA NA WATOTO WENU PIA.

MATATIZO YAPO TU KILA SIKU NA YALIRUHUSIWA/YANARUHUSIWA KUWEPO KWASABABU YANA FAIDA NYINGI SANA(kwa watu wenye upeo mkubwa wa uelewa) KWA BINADAMU KULIKO HASARA ZAKE AMBAZO NI CHACHE SANA.

KWA VILE MATATIZO YAPO, BASI KUACHANA KUNAWEZA KUWA SULUHISHO LA HAYO MATATIZO KWA WANANDOA NA WATOTO WAO, AU PIA ISIWE SULUHISHO,pia ikawa ni moja ya fundisho kwa wakati huo au hata hapo baadaye.

WAPO WATOTO WANAOISHI KWA FURAHA SANA PINDI WAZAZI WAO WANAPOACHANA KULIKO KIPINDI KILE WALICHOKUWA WANAISHI NA WAZAZI WAO WALIOKUWA WANAISHI KWA UGOMVI KILA SIKU,
LAKIN PIA WAPO WATOTO WANAOISHI KWA SHIDA PINDI WAZAZI WAO WANAPOACHANA.

PIA SIYO KWAMBA KILA FAMILIA YENYE WAZAZI WASIOACHANA (WANAOISHI PAMOJA) BASI HATA WATOTO WAO WANA UPENDO,AMANI NA FURAHA MIOYONI MWAO,AU WANAFURAHI UPAMOJA WA WAZAZI WAO.

KWA HIYO LILILOMUHIMU NI KUJUA KWANINI WANANDOA WANAFIKIA HATUA YA KUACHANA.JE MAISHA YA WATOTO BAADA YA KUACHANA WANDOA YATAKUWAJE?.

Na kwavile Kuachana ni jambo la mchakato na siyo jambo la mlipuko/kukurupuka basi naamini lina pande mbili zote, ubaya au uzuri, faida au hasara,furaha au huzuni.
 
Maty unaweza ukawa wewe ni mzungumzaji mzuri na kuweka vitu mezani viongelewe kwa uwazi ,lakini mwenzio hatekelezi na ukimuuliza zaidi atakuambia unafikiri mi ndo sina ya kusema ,unamwambia sema basi anakujibi sioni sababu ya kukuambia.........ni ngumu sana kama upande mmoja ndo unakuwa unajaribu kushirikisha mambo mwingine hautoi support .

Hahahahaha dena umenifurahisha asee, hivi hamuwezi mkakaa mkazungumza mkayamaliza na kuendelea kuishi kwa amani kweli? Mi nadhani kwenye ndoa ukimya ni mwingi sana watu hawapati muda wa kuzungumzia matatizo katika ndoa zao. Yaani inawezekana mmojawapo kati ya baba au mama hataki kabisa kukaa chini kuwekana sawa na mwenzie au akiambiwa anakuja juu
 
Ukiingia kwenye ndoa, usijivue uhusika wako na usitake kumvua mwenzio uhusika wake kwa 100%. Jipeni nafasi wa kila mmoja kuishi maisha yake, na jipeni nafani ya kuishi kama familia.

Vunjeni ukimya na matatizo ya ndoa yatapungua na 'sio kwisha mind you'. Kwa mfano zungumzeni jinsi ya kila mmoja kupoteza 30% ya uhusika wake. Hii mtashare kama common ground ambayo ndio itakuwa msingi wa ndoa yenu. Inaweza kuwa mawili, matatu au hata manne lakini haiishii kwenye tendo la ndoa, kula pamoja, kulea watoto, ibada, michezo, majukumu ya nyumbani ect.
 
Maty....ukiona watu mpaka wamefikia kuachana jua wameshindwana kabisa kabisa kabisa....unaweza ukaondoa huo ukimya unaousemea ukaongea mpaka ukapata kibiongo lakini mwenzio yanaingilia huku yanatokea kule, mie huwa namheshimu mtu aliyeona yamemshinda akaamua aanze njia yake mana kufa kwa pressure n nn?
 
Niliwahi kuanzisha thread ya "We need to talk" majibu yaliyokuwa mengi ni kwamba hakuna aliyetayari sasa mtasolve vipi hayo matatizo???

Hiyo ndo ilikuwa maana yangu MAty kuwa tukae tuzungumze sasa kama hutaki "KUACHANA TU"
 
Dah! mawazo yenu niliyoyapata hapa inaonyesha ndoa ni ngumu sana asee
Maty NDOA kama NDOA sio ngumu ila sisi binadamu ndio tunaifanya ionekane ngumu, NDOA ni jambo takatifu lililobarikiwa na Mwenyezi Mungu kuachana sio solution tatizo tumekosa uvumilivu mama anajifanya mjuaji baba naye anajifanya mjuaji kila mtu ndani ya nyumba anajifanya ana kibesi kuliko mwenzake,wengine walioana ili mradi tu kwa vile fulani kaoa, nakumbuka siku moja padri kanisani aliuliza "Ambaye hajawahi kutoka nje ya ndoa yake anyooshe mkono juu" nakumbuka kati ya watu wote waliokuwa kanisani walionyoosha mikono juu walikuwa watano tu.
 
Maty....ukiona watu mpaka wamefikia kuachana jua wameshindwana kabisa kabisa kabisa....unaweza ukaondoa huo ukimya unaousemea ukaongea mpaka ukapata kibiongo lakini mwenzio yanaingilia huku yanatokea kule, mie huwa namheshimu mtu aliyeona yamemshinda akaamua aanze njia yake mana kufa kwa pressure n nn?

Kama nimwelewa vizuri Maty, anazungumzia ndoa za kisasa ambapo hata ndoa changa zinavunjika.

Swali linakuja je wamechukua hatua gani kuinusuru hiyo ndoa. Ni kweli kuna issue ambazo lazima zivunje ndoa, lakini si kweli kusema kwamba kila ndoa yenye issues lazima ivunjike.
 
Ulokole peke yake hautoshi kusimamisha ndoa...
Ndoa ina nguzo zake, kama kuheshimiana, kusikilizana, Upendo, Hekima etc etc...
Msipotumia hizo nguzo , hata kama mtageuza Biblia kuwa mito ya kulalia kichwani, it wont work out!
Nakuchukia sana kuachana...Kwa namna yoyote, kuachana hakuleti matokeo mazuri, hata kama ni kuokoa uhai wa mmojawapo!
Kugombana kupo kwenye familia kila siku, lakini mimi naichukulia hii kama fursa nzuri sana inayopelekea KUPATANA baadaye, na hakuna tendo zuri kama wawili wakaapo pamoja chumbani na kuweka mambo sawa, maana mnaweza mkaishia kushusha mapazia nje ya ratiba, ha ha haaa!.
 
Ukiingia kwenye ndoa, usijivue uhusika wako na usitake kumvua mwenzio uhusika wake kwa 100%. Jipeni nafasi wa kila mmoja kuishi maisha yake, na jipeni nafani ya kuishi kama familia.

Vunjeni ukimya na matatizo ya ndoa yatapungua na 'sio kwisha mind you'. Kwa mfano zungumzeni jinsi ya kila mmoja kupoteza 30% ya uhusika wake. Hii mtashare kama common ground ambayo ndio itakuwa msingi wa ndoa yenu. Inaweza kuwa mawili, matatu au hata manne lakini haiishii kwenye tendo la ndoa, kula pamoja, kulea watoto, ibada, michezo, majukumu ya nyumbani ect.
Nitafute nikupe zawadi yako ya Pasaka for this useful post
 
unatakiwa kubalance baina ya uvumilivu na mateso, hivi kama nina uhakika mai waifu anamgaia uroda jirani yetu ndio nivumilie tu kwa ajili ya watoto? khaaaa! si nitakufa bila symptoms?,
on the other hand uko right kama makosa yenyewe ni kunuka kikwapa, sijui asubuhi anachelewa kupiga msuwaki, sjui akinuna havai nguo za ndani, n.k , hapa tunapaswa kufikiria watoto
 
nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!

Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.

kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.

Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!!

Viva usingo! unalamba na kuchapa lapa, ha h aha.
 
unatakiwa kubalance baina ya uvumilivu na mateso, hivi kama nina uhakika mai waifu anamgaia uroda jirani yetu ndio nivumilie tu kwa ajili ya watoto? khaaaa! si nitakufa bila symptoms?,
on the other hand uko right kama makosa yenyewe ni kunuka kikwapa, sijui asubuhi anachelewa kupiga msuwaki, sjui akinuna havai nguo za ndani, n.k , hapa tunapaswa kufikiria watoto

Kumbe bado mapointi yanashuka??? Hongera...................
 
PJ umeongea vema ,embu niulize na wale wanaoamini wako sawa kwa yale wanayofanya kwa wenza wao na hata ukijaribu kumueleza dharau kwenda mbele na majibu yake kwamba anatekeleza wajibu wake vema.

Ulokole peke yake hautoshi kusimamisha ndoa...
Ndoa ina nguzo zake, kama kuheshimiana, kusikilizana, Upendo, Hekima etc etc...
Msipotumia hizo nguzo , hata kama mtageuza Biblia kuwa mito ya kulalia kichwani, it wont work out!
Nakuchukia sana kuachana...Kwa namna yoyote, kuachana hakuleti matokeo mazuri, hata kama ni kuokoa uhai wa mmojawapo!
Kugombana kupo kwenye familia kila siku, lakini mimi naichukulia hii kama fursa nzuri sana inayopelekea KUPATANA baadaye, na hakuna tendo zuri kama wawili wakaapo pamoja chumbani na kuweka mambo sawa, maana mnaweza mkaishia kushusha mapazia nje ya ratiba, ha ha haaa!.
 
nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!

Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.

kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.

Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!!

mie nina frnd wangu aliolewa na hawa wachungaji wa makanisa ya kiroho, haikupita miezi 6 ile ndoa ilivunjika, matatizo yaliyoporopmoshwa hapo na frnd wetu ni ya kuchosha nafc, usuluhisho ulikuwa historia kwenye hii ndoa, sasa kila mtu anaishi maisha yake, mchungaji cjui yupo kinshansa huko mdada kashaolewa upya...yaani jamani hizi vurugu cjui zinatupeleka wapi jamani.
 
Back
Top Bottom