Maty
JF-Expert Member
- Aug 24, 2010
- 2,167
- 725
Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.
Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.
Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?
Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?
Tushirikiane kupeana mawazo wandugu