Tuongee asubuhi Star Tv: Kufungiwa gazeti la MwanaHalisi

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Kuna mjadala unaendelea Star Tv juu ya kufungiwa gazeti la MwanaHalisi. Dotto Bulendu anaongoza mjadala na ana wageni watatu. Kuna mmoja anaitwa Moses huyu ameegemea kwenye serikali zaidi akiunga mkono kufungiwa kwa gazeti hilo.Ana munkari sana na anajiita mzoefu wa habari wa miaka 14. Anikazi Kumbemba hakubaliani na kufungiwa huko.

Ninapata wasiwasi kuwa ana maslahi na waliolifungia gazeti.Mlioko huko Mwanza mtuambie huyu ni nani?
Amenichefua kutaka kuikingia kifua serikali isiyotaka kurekebishwa.
 
Dotto Bullendu mwongoza kipindi akiwa na wageni Edwn Soko ambaye ni mwandishi wa habari, Akinkzi kumbemba Mwanafunzi wa SAUT, na Moses sijapata jina lake la pili.

ukweli ni kwamba woote waliopo studio live na hata tuliowengi huku nje mtaani na hata wanataaluma wakubwa duniani plus wanadiplomasia (mabalozi wa nchi zenye uwakilishi hapa kwetu) soote kwa umoja wetu tunalaani kufungiwa mwanahalisi na kunyongwa kwa uhuru wa habari kwa maslahi ya tasnia nzima ya habari na upeo kwa wasomaji.

cha ajabu ni kwamba kati ya wachangiaji woote namwona huyu Moses anafagilia sana kufungiwa mwanahalisi kuwa habari zake ni za kichochezi na hivyo serikali imetenda haki kulifungia.

Siamini macho yangu kumwona Mtu anayejiita naye ni mwandishi wa habari akitetea uovu huu kwa jina la uchochezi. Hivi Moses umealika mapovu ya nini hapo studio.......? Huyo moses ni mapovu yaani hakuna anachotetea eti ni bora limefungiwa na wengine wakome...

Changieti ndugu zangu kwa mliokaribu na tv angalieni star tv mumwone huyu mapovu.
 
Sina uhakika hata Dotto Bulendu kama anamfaham vzr huyu jamaa otherwise asingemwlika kwenye kipindi chake, angalia anavochafua mjadala na sasa hivi anasema eti amekasilika Moses ni janga la hicho kipindi hata Dotto mwenyewe ameshamgundua
 
huyo moses ni mapovu ya Omo hana anachooonhea zaidi ya kufurahia kufungwa mwanahalisi si dhani kama anajua anachokisema
 
naona huyu jamaa anataka kuniondolea mudi ya kuangalia hiki kipindi,tafadhali doto uwe unaangalia watu wa kuleta studio huyo jamaa anayefurahia kufungia mwanahalisi ni kilaza wa mwisho,atakuharibia kipindi mdhibiti tafadhali.
 
Hawa wanaojifanya kulitetea mwanahalisi la sadist kubenea wananichefua kwelikweli.vihere here na vibaraka hawa.
 
Naomba sana Mosses atuambie ni habari ipi mwanahalisi waliandika ikiwa ya uchochezi atoe mifano sio kuongea mambo kiujumlajumla kiasi hicho.Pia atoe ufafanuzi tofauti ya habari za kiuchunguzi na kichochezi huenda nae anachofanya hapo studio ni uchochezi dhidi ya mwanahalisi na wasomaji wa habari.
 
Kuna jamaa hapa analichambua mwanahalisi jinsi wanavoandika ujinga wao kwa ku relate matukio,anasema tena wafutwe kabisa,hawafai na sadist kubenea wao
 
Naomba sana Mosses atuambie ni habari ipi mwanahalisi waliandika ikiwa ya uchochezi atoe mifano sio kuongea mambo kiujumlajumla kiasi hicho.Pia atoe ufafanuzi tofauti ya habari za kiuchunguzi na kichochezi huenda nae anachofanya hapo studio ni uchochezi dhidi ya mwanahalisi na wasomaji wa habari.

ametoa mfano wa ile habari waliyozusha mwanahalisi ya tar 7.oct 08 kuwa ridhiwani anataka kumpindua baba yake,halafu ndani taarifa inahusu tabo mbeki na jakob zuma wa af kusini,.sadist kubenea ni kituko tu hana lolote.
 
Sadist kubenea kwa kuwa anamchukia mtu fulani basi anamalizia hasira zake gazetini,nyambaf kabisa.,
 
Mwanahalisi ni gazeti la umbeya..Mwanahalisi lina haki gani kuchafua watu.
 
Kwenye kundi lako la wapumbavu you are number one .Unaeleta upumbavu hapa na kama ma CCM yana haki na mara zote hukimbilia Mahakamani mbona msiende huko mkashitaki kwa nini mnafungia na kukaa kimya ?Shenzi type

na wewe pia,neno to neno yakurudie,bweha.
 
moses anaonekana kcisa ame2mika huyu mana ana hasira na jaziba za ajabu ajabu na anaöekana hajiamin kabisa ndo mana mara nying anaogopa eye contact na camera yan ni typical magamba style jins anavyo2mia nguvu zote kupingana na ukweli ambao uko wazi!
 
ametoa mfano wa ile habari waliyozusha mwanahalisi ya tar 7.oct 08 kuwa ridhiwani anataka kumpindua baba yake,halafu ndani taarifa inahusu tabo mbeki na jakob zuma wa af kusini,.sadist kubenea ni kituko tu hana lolote.

Sasa habari kama hii Mwahalisi inaambiwa ni gazeti la kichunguzi umbeya mtupu...
 
Kwa taarifa za ndani ni kuwa mwanahalisi kwa sasa halina mfadhili,hivo anauza gazeti kwa kichwa cha habari.amekosana na mabwana zake kibao akina mengi,na wengine.
 
Sasa habari kama hii Mwahalisi inaambiwa ni gazeti la kichunguzi umbeya mtupu...

tatizo wanaolisoma hawatafakari,wanameza mazima mazima,wabongo si unawajua wavivu kushughilisha akili zao?
 
yuko sahihi,usitake kila mtu aamini ujinga wa mwanahalisi na mabwana zake,ameokoteza habari za kutunga af kaandika ili auze gazeti af achekewe,piga kufuli kubwa.

Hivi chukua mfano wa toleo la mwisho ambalo limeandika mawasiliano yote aliyoyafanya Rama na Dr. Uli. Kubenea amaejaribu kutafuta habari zote toka daftari la wapiga kura na namba yake ya simu.

Serikali ilipaswa kutuambia kuwa namba hiyo si yake na wala hakuna mfanyakazi wa TISS anayeitwa Ramadhani, then ilifungie badala ya kufanya ilichofanya.

Ukitaka kuthibitisha madai hayo jaribu kutuma pesa kwenye namba hiyo halafu uone inaandika jina gani?

Kujua namba ya mtu siku hizi ni rahisi mno. Kubenea kafanya utafiti.Serikali ingeukataa utafiti wake kwa kutoa hoja na si viroja.
 
Back
Top Bottom