Tuongee Asubuhi: Ongezeko na Majaaliwa ya Vyama Vidogo vya Siasa kuelekea 2015

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za J3 GT's

Jumatatu ya leo tutajadili kuhusu Ongezeko na majaaliwa ya Vyama vidogo vya siasa kuelekea uchaguzi Mkuu 2015. Lengo ni kutathimini kukomaa kwa demokrasia lakini pia mfumo wa siasa za Tanzania katika kumletea ustawi bora wa maisha mtanzania wa hali ya chini na kukuza pato la Taifa:

Katika mjadala huu tunategemea kuwa na

Bw.Kuga Peter Mziray APPT Maendeleo
Bw. Johson Mwangosi SAU

Unaweza pia kuendelea kuchangia katika habari kuu za wikiend ya jana na asubuhi ya leo

  • Sakata la watoto wa Wasirra
  • Uchaguzi Mkuu NEC na nagazi nyinginezo CCM
  • Siku ya Wazee Duniani
KESHO: Bila kusahau kesho mjadala kuhusu TUNANUFAIKAJE NA UGUNDUZI WA GASI, URANI NA MAFUTA Utajadiliwa kwa Uwezo wa Mh.ZZK Studio zetu za DSM. Maswali na mjadala wa wiki iliyopita itashughulikiwa. Invisible unaweza kutusaidia kuiunga hapa kwa ajili ya wachangiaji wapya.


Karibuni
 
Mwanza Mkuu
Kuhusu vyama vingi vidogo, mimi nadhani haifai kuwa na utitiri wa hivyo vyama. Hayo ni mambo ambayo wenzetu waliyaepuka.Kwanini sisi tusifanye the same? Kama tuliiga mfumo wa vyama vingi, kwanini tusiwe na vyama kama viwili tu vyenye nguvu?

Tuweke msisitizo kwenye issue za kitaifa (especially kwenye katiba mpya), ambapo tutakuwa na malengo ya kitaifa, halafu tuwe na vyama kama viwili tu vikubwa, CCM na CUF tayari wao ni kama kitu kimoja, iwe hivyo, halafu kubakie CHADEMA.

Hivyo sijui APPT, SAU na sijui vitu gani ni upotevu tu wa pesa za walipa kodi, na pia vinaweza kutumika kugawa kura na hivyo kutunyima mageuzi ya kweli na maendeleo.

Wenzetu marekani na kwingineko walifanya hivyo. Sisi utitiri wa vyama tunadhani eti ndiyo demokrasia, utafsiri wetu mbaya wa mambo mengi unatucosti sana, same way tulivyokurupukia ubepari bila kutafakari yepi ni mazuri na yepi siyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ningekuwa na uwezo hakika ningevunja vyama vyote vya kisiasa vidogovidogo na kubaki na vyama vikubwa ambavyo vinaonekana kuwa no serious.

Vyama vidogo ndivyo vinavyovuruga maana nzima ya siasa ya vyama vingi. Kuna vyama ambavyo kwa sasa vimelala lakini ghafla huibuka wakati wa uchaguzi.

Navyo hutangaza kushuiriki uchaguzi halafu baadaye siku chache kabla ya uchaguzi utasikia mgombea wake amejitoa na ametangaza kumwunga mkono mgombea wa chama tawala.

Inakuwa kama vile chama kinaongozwa na watoto wa chekechekea. Nashangaa kwa nini Tendwa havifuti vyama vya aina hii kama vya akina dovutwa. Ndiyo maana watanzania wengi sasa hatuna imani na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bw. Tendwa.
 
Another factor to influence a two-party system should be the shared principles and ideals of our people. We have a lot in common than what divides us,we should then stregthen our unity by setting up a constitution for the people and by the people.

In many other countries, the range of beliefs is greater, and disagreements run deeper contrary to our country,were we've enjoyed a unity for quite a long period of time,only recenlty, have we seen what ccm and cuf wants to impose on us.The so called division based on religion and tribalism.

Otherwise we are a one nation with same kind of demands,mainly getting rid of poverty.

We are above all those types of politics(too many political parties and divisions),and our needs and demands should bring us together,where we're stronger than any kind cynicism, and no matter what pundits are saying,our national priorities shall prevail.
 
Utitiri wa vyama vya siasa sio kipimo cha kukua kwa demokrasi,huu ni mpango wa chama tawala CCM kuzigawa kura za wapinzani ili kiendelee kubaki madarakani.

Mbegu ya rushwa katika chaguzi za CCM natunda ni UFISADI katika serikali na taasisi na mashirika ya zote za umma.
 
Mimi sidhani kama ni busara kwa nchi yenye demokrasia changa kama hii kuwa na vyama 19 vya kisiasa, mbaya zaidi baadhi ya vyama hivi utendaji kazi wake ni wamashaka, havionekani mpaka chaguzi zinapokaribia matokeo yake wanapata 0.

Ushauri wangu vyama hivi vingeungana kuing'oa magamba, tunataka changes!
 
Tukizungumzia kukua kwa demokrasia mawanda yake ni mapana, lakini ni membamba katika ongezeko la vyama vidogo vidogo. Ukuaji wa democrasia huendana na mapinduzi ya kisiasa ambapo watu huwa na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa bila vipingamizi.

Mfano mzuri wa ukuaji wa demokrasia ni swala la mgombea huru binafsi ambalo nazani litaviondoa vyama vidogo vidogo kwa maana haitahitaji juwa na chama ndio upate ridhaa ya kuchaguliwa.

Pia ukuaji wa demokrasia sidhani kama ni kuongezeka kwa vyama vidogo vidogo, kwa maana kwamba democratic change haiwezi tokea kwa staili hii maana kuwapo kwa utitili wa vyama ni furaha kubwa kwa watawala kukaa milele madalakani.

Mfano mzuri ni mageuko ya kisiasa nchini kanya kuunganika kwa vyama viwili ndo kufanikiwa kwao katiua kukitoa chama tawala KANU, kwa maana hiyo hakuna haja ya kuwa na vyama utitili ilhali kuna uhitaji wa muunganiko wa vyama katika kuleta mageuko kisiasg na kidemocrasia.

Swali kwa MH. MZIRAI katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 alisema kura zake ziende kwa Jakaya Mrisho Kikwete. Je, HUKU NDIO KUKUA KWA DEMOKRASIA. NA ALIOMBA RIDHAA KWA WANANCHI KWANINI ILHALI ALIJUA KULA ATAMPA KIKWETE?
 
Swala si ongezeko la vyama bali uhuru uliomo ndani ya chama, cha kukemea hapa ni kupitishwa kwa majina katika kulenga mitandao fulani mathalani uchaguzi wa mwaka huu wa CCM, huku vijana wanaoonekana kuwa na uwezo wakipigwa chini na kubeba familia za viongozi na watu wenye uwezo wa kulamba mavimbi ya wakubwa kisha chama kinajivunia kuongeza idadi ya vijana, mi nafikiri tusiwe na vyama vichache afu uhuru wa uchaguzi unabanwa,
 
MImi nafikiri onezeko la vyama hasa vidogo na vinavyibukia ni matokeo ya uchu wa madaraka zaidi ya dhana y ukuaji wa demokrasia....
kupewa haki ya kuchagua au kuchaguliwa haina maana kila mtu anayejisikia aweze kuanzisha chama chake (kama akijisikia)
nakumbuka hoja ya Mwalim Nyerere kipindi anaihutubia NEC (kama mtataka video ntaweka) alisema demokrasia na uhuru wa kisiasa haina maana kuwa tuwe na utitiri wa vyama vingi saana au tuwe na wataka madaraka saana ila ni uhuru wa watu katika kujihisi wako huru katika nchi yao (kwa maana ya uhuru haswaa) na si vinginevyo.

Tunachokishuhudia sasa ni utitiri wa tamaa ya watafuta madaraka...kama mmoja wa wachangiaji hapo juu alivyosema KINACHOTUUNGANISHA NI KIKUBWA KULIKO KINACHOTUTENGANISHA.

Mimi kwa maoni yangu ningeomba sheria ya usajili wa vyama ingelimiti idadi ya vyama na sheria ya ufutaji wa vyama ambavyo havina TIJA KISIASA au vyama vya msimu ingekuwepo au kama ipo ingepewa meno
 
Siku zote chama kinapoongozwa kwa hila au kundi fulani la watu,tatizo hutokea na hapo ndo mambo uenda ndivyo sivyo, katika mjadala wako wa kesho atakapokuwepo Zitto Zuberi Kabwe me nawenzangu hapa site tunamwomba awepo na yule mchambuzi machachari wa huko mwanza ndugu maurice, last time uchaguzi wa arumeru tulimwona akiwakilisha chama,sa kwenye uchaguzi wa chama mbona hatumwoni?

Tunamwomba kesho studio
 
Ongezeko la vyama vingi kiujumla ni kukua kwa democrasia lakini kutokana na sheria za uchaguzi wa nchini yetu ya kuwa mshindi hapatikani kwa kiwango fulani, mshindi anapatikana japo akimzidi mwenziwe kwa kura moja anapewa ushindi.

Sasa kwa hali kama hii inakuwa tatizo kwasababu kunakosesha chama chenye nguvu ambachokitapambana na chama tawala kwasababu ya hivi vyama kura za upinzani wanagawana.Lakin 2ngepata vyama viwili2 vya upinzani apo ingalikuwa vizuri sana.

From ZANZIBAR
 
Demokrasia ni kuruhusu matendo yote yanayompa mtu uhuru wa kufanya atakavyo pasipo kuvunja sheria. Waache watu wachague wapi pa kwenda uhuru usigandamizwe
 
Marekami kuna vyama viwili ni upotoshaji, viko viiingi ila vyenye nguvu ni vitatu! Kwa huk kwetu vyama vingi ni pandikizi.

Vyama vilivyo wahi kutawala marekani ni vitatu! Liberal democtrat, republi na democrats! Lakini kuna vyama viingi saana.

Vyama vidogo hutumiwa saana! Vingi viko kwa manufaa ya chama tawala! Angalia matamko yao mengi! Hubeba chama tawala
 
Tatizo letu Sisi watanzania tumeingia kwenye mfumo ambao wengi hawauelewi ndiyo maana kila mtu akiamka asubuhi anawaza kuanzisha chama cha siasa, hii inatokana na sheria mbovu na nyepesi zinazoruhusu kuanzishwa kwa vyama hivi.

Leo hii kuna vyama vimekuwepo kwa zaidi ya miaka 10 ila havijawahi kuwa hata na mbunge mmoja sasa hii ni Demokrasia au ni kujaribu demokrasia?
 
Nawapata vizuri Star TV hapa St. Petersburg Russia ila bado kuna tatizo la sauti kila mnapobadilishana studio kati ya Mwanza na DAR sauti zinakuwa chini sana hapo Dar sauti ya mtangazaji iko chini.

Hongera.
 
Vyama vingi vya siasa malengo yao ni ruzuku na si kuleta ushindani ktk siasa na kusaidia kupunguza wimbi la umasikini kwa watanzania, ni vyema kuwa na vyama vichache vyenye tija, kuliko kuwa na vyama vingi na kuleta mzigo kwa wananchi kwani vyama hivyo vinatumia kodi zetu kujiendesha na huonekana kipindi cha uchaguzi mkuu tu.
 
tunapoongelea ukuaji wa Demokrasia,ni vema pia tuangalie upande wa pili ndani ya vyama vyenyewe,

Je kuna demokrasia ya kweli ndani yake? Maana tumeona baadhi ya vyama vikiwa na mmwenyekiti huyohuyo ndani ya miaka 20,na pia unakuta mtu huyo huyo anagombea urais kwa miaka yote ishirini bila kuruhusu na wanachama wengine kutumia fursa hiyo ingawa wanakuwepo wengi tu wenye vigezo pengine hata zaidi.

Pale inapotokea mwanachama kutaka kugombea nafasi fulani ndani ya uongozi wa chama kwa mujibu wa katiba ya chama ,ambayo inashikiliwa na kiongozi wa wakati huo,basi mara nyingi hujikuta akifukuzwa uanachama. Kwa kuambiwa ni watovu wa nidhamu.

Je kama hawa ndio viongozi wanaotaka tuwape ridhaa ya kutuongoza kitaifa? Kama hata ndani ya vyama wanashindwa kuiheshimu demokrasia hiyo.baba wa taifa alifanya siasa bila kulazimika kutumia familia yake nikimaanisha yeyote yule ndani ya familia yake awe mke au mtoto.

Lakini ebu tuangalie sasa hivi jinsi gani familia za wanasiasa zinavyopigana vikumbo kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vyao.je huu ndio ukuaji wa demokrasia?

Viongozi wengi wa vyama vyetu vya kisiasa ni kina haambiliki,wababe na nafikiri pia si wawazi sana pale inapotokea wanachama kutaka kujua mchanganuo wa mahesabu na matumizi ya chama,basi wao hugeuka mbogo na kuwatimua.

Kwa hiyo ni vema tunapojadili hili ni vema pia tujadili umuhimu wa kuwa na mgombea binafsi ili kuwaruhusu wale wenye kulazimika kufungua vyama kwa siasa kwa ajili ya uchaguzi waweze kujiwakilisha wenyewe.

Hii itapunguza sana huu utitiri wa vyama vya siasa vya msimu
 
Mi nadhani wassira hawajawatendea haki hao mabinti, kwani mbali na siasa watoto wa kaka yake ni watoto wake tu.

pia hata wangelikuwa watoto wake wa kuwazaa bado nao wanauhuru wa kuwa chama chochote kama yeye alivyofanya yeye kuwa NCCR, kwani ni lazima wazazi wake walikuwa TANU/CCM.

Je hao mabinti wangefanya kitu ambacho yeye angedhani ni bora je asingejisifia kwamba kwao wanaakili sana
 
Back
Top Bottom