Tuongee asubuhi on star tv friday 04/03/2011

Paul Mabuga

Member
Nov 25, 2010
10
2
Waungwana ijumaa wiki hii tutaangalia "Pamba: Ruzuku ya pembejeo imeongezeka, Uzalishaji Unashuka."

Mantiki hapa ni kwamba wakati serikali ilikuwa haitoi ruzuku uzalishaji ulipanda na kufikia marobota 700,000 kwa mwaka, lakini wakati ruzuku imeanza kutolewa uzalishaji umeshuka na hata rekodi ya robota chini ya laki tatu kwa mwaka huu. Mwaka huu ruzuku shs bn 8 imetolewa: Je kwa hali hii hizi pesa zinafika kwa wakulima?

Naomba michango yenu na natarajia kuwa -- baadhi itachapwa kwenye screen na kama mtu anaweza ku upload video ya maoni yake walau chini ya dakika mbili na kuituma you tube -- akiipa jina kuanza na Tuongee na kisha neno lolote ninaweza pia kuitumia.

Nawakaribisha jamvini kwa michango yenu waungwana.
Asante.
 
Nioavyo mimi uzalishaji wa pamba umeporomoka kutokana na watu wengi kuachana na kilimo cha pamba baada ya kuona hakiwaletei manufaa kutokana na bei yake kua chini. Miaka ya nyuma wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa walijihusisha na kilimo cha pamba kwa sababu ndicho kilikua chanzo kikubwa cha mapato. Lakini kuanzia miaka ya tisini kuelekea 2000 watu wengi waliamua kujikita kwenye shughuli za uvuvi hasa baada ya sangara kupata soko la nje. Wakulima wengi wa pamba wanatoa sababu kuu mbili zilizowafanya waachane na kilimo cha pamba na kujikita kwenye uvuvi. Mosi, wanasema shughuli za uvuvi zinawaingizia pesa za papo kwa papo "instant earning" tofauti na kilimo cha pamba ambacho huwalazimu kusubiri miezi 7 hadi 8 wavune na kuuza pamba yao. Pili wavuvi wanasema bei ya pamba iko chini ndio maana wamekata tamaa na kujikita kwenye uvuvi ambako wanapata pesa za kutosha. Ushauri wangu kwa serikali naiomba isiishie kutoa ruzuku tu bali isimamie na suala la bei iwe na tija kwa wakulima. SAMIR NASRI. - mwanza.
 
Tatizo moja la msingi ni kwamba mtindo wa serikali wa kushugulikia kilimo una matatizo makubwa. zamani ukisikia ruzuku, maana yake bei ya mbolea ilikuwa iko chini, bei za madawa na mbegu bora ziko chini. siku hizi ukisikia ruzuku, maana yake ni kwamba kuna "wafanyabiashara" wanaopewa uwakala wa kusambaza pembejeo hizo, na hao ndio wanaofaidika na ruzuku hizo. ukisikia serikali imetoa bilioni kadhaa kwa ajili ya kilimo kwanza, ukifuatilia utakuta ni Yusufu Manji ndiye aliyenufaika kwa kupewa tenda ya kuagiza power tiller, nk. kwa hiyo utaona in figures, serikali imefanya wajibu wake wa kumwaga mafedha, kumbe ni kama mtu mwenye bustani anakupa data kwamba ametumia lita elfu kadhaa kumwagilia bustani yake, kumbe maji yote yalikuwa yakiletwa yanachotwa na watu wanayatumia kwa kazi nyingine. hapo huwezi kupata tija katika bustani hiyo. napendekeza serikali ihamasishe wakulima waunde vikundi vya wakulima, na hivi vipewe mafunzo ya ujasiriamali na viandikishwe. kwa kuwa hawa ndio wakulima wenyewe, wapewe hizo pembejeo wenyewe. la pili ambalo lazima liendane na hili, ni kwamba serikali iwe makini katika kusimamia haya, kuhakikisha kwamba inawalinda wakulima wake wasiangukie kwenye midomo ya mamba hawa.
 
Back
Top Bottom