Tunu zetu na katiba mpya

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Ni kweli Tumepata tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni katiba! Asante.. sasa nini kufuate katika

Fikira????


Sisi tunaojinasibu kuwa wenye fikira pevu tufanye nini au tunasubiri tusikie tume wanasema nini?

Hasha, mimi binafsi siungi mkono kusubiri tutafakari na kubadilishana mawazo juu ya nini kiingie au kisiingie katika katiba mpya.

Hapa nawaza kuhusu TUNU zetu kuwa moja ya misingi yetu mikuu katika hili.


Sasa najiuliza (na wewe njoo tujiulize kwa pamoja)

Hivi tunu zetu ni zipi?

Kama ningetakiwa kupendekeza jinsi ya kujadili hili nigesema tuliangalie katika sura tatu:

1. Ni zipi TUNU zetu tunazodai kuwa nazo(rejea dira yetu iliyopita)
2. Ni TUNU zipi tunazisimamia kwa sasa (rejea dira yetu ya sasa/hali halisi)
3. Ni TUNU zipi tunataka tujinadi kwazo kwa siku zijazo(rejea dira yetu kwa mbeleni)

Nawasilisha: mimi kwangu zito linahitaji Great thinkers naamini hapa ndipo kwao!
 
Back
Top Bottom