Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 988
hana Tunu yoyote, naye kapinda tu kama mumewe
tangu adamu isaka na yakobo haya tumeyaona kwa Kikwete, eti mke wa kiongozi naye anakula perdiem na gari la serikali anatumia, tumelaaniwa?!
hana Tunu yoyote, naye kapinda tu kama mumewe
Nimeona maajabu sana. Katika ziara za Waziri mkuu wa Tanzania kanda ya ziwa kaambatana na mkewe. Baada ya kuona Raia hawamuelewi waziri mkuu, Tunu Pinda ikabidi aulize swali kwa niaba ya wakazi wa sehemu husika.
Aliuliza;
Sisi wanawake wa hapa tunapata tabu sana katika kuchota maji hadi nywele za katikati hazikui sababu ya kujitwisha chungu, je serikali itatusaidiaje?.
Waziri akajibu;
Nimeambiwa zinahitajika mil 200 kuondokana na tatizo, hizo mil 200 nitawapeni bila tatizo.
Hii imekaaje?. mia
ni MAGU alikuwa na msafara wa magari kama mia na kitu. Pia aliulizwa swali na mama mmoja kuhusu serekali kutangazia wananchi huduma za kujifungua ni bure ili hali hospt hakuna hata glovis na pamba,Pinda hakuweza kumjibu
Hivi huyo si msaidizi wa Slaa wa kumkumbusha? Kama jibu ni ndio, kwanini iwe mwao kwa Pinda?
Mkewe hana haki ya kumkumbusha? mbona mkitaka michango mnamtumia? au umesahau, alivyopigania michango ya timu ya netiboli ya wanawake Tanzania?
Hivi wewe una mke au mume nyumbani? au bado hujaoa au kulewa? kama huna na bado, basi ukikuwa utayajuwa
majukumu ya mke kwa mume ni yepi.
Ni mume na baba wa mtoto mmoja mkuu ila mke wangu hagusi mambo ya ofisini kwangu as wengine ethically mke akigusa ofisini na feelings zake basi wengine maisha yao yataathirika.......halafu kwa nini mimi namzungumzia PM wewe unaniletea mambo ya mke wa mtu mwingine....huyu ni nani katika nchi hii????
Mmmh na kama ukubwa ndo huu unaoniambia nikikua ntayaona then better nibaki na ujana wangu for good........a clear dermacation between public and private entities as a feature of Beaurocracy ndo najitahidi kuitafuta ........
Mi naongelea a Government icon and you keep dragging this topic into political arena................Cant we check this scenario without a political lens?????
Kuna kazi na kazi. Kazi yako si ya utumishi wa watu. Ungekuwa japo na ki grocery mkeo angekusaidia ukipenda usipende.
Mkuu kazi yangu ninahusika na kuwatumika watu 100%..........ila nauliza tu ni wapi tunaweza kuchora mstari kuwa hapa ni public and official na wapi ni private katika hili?????
Kwa Waziri Mkuu, private ni anapokuwa nyumbani kwake tu. Na hata hapo pia kuna majukumu ya kutumikia umma yanamfata.
Hivi kacheo kako ka utumishi wa umma kamefikia udiwani? ubunge? uwaziri? uwaziri mkuu? au ni mjumbe wa nyumba kumi? Mwenyekiti serikali za mitaa?
Umeona ee!Huko ndo kujitekenya mwenyewe afu unacheka. Waacheni wahangaike tu. very soon wataanza kujifinya wenyewe afu wanalia!
Nywele za katikati????????????????
Yaaa, ni katikati ya kichwa, utosini!