Tunu Pinda kamuuliza Mh. Mizengo Pinda swali kwenye mkutano wa hadhara

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Nimeona maajabu sana. Katika ziara za Waziri mkuu wa Tanzania kanda ya ziwa kaambatana na mkewe. Baada ya kuona Raia hawamuelewi waziri mkuu, Tunu Pinda ikabidi aulize swali kwa niaba ya wakazi wa sehemu husika.
Aliuliza;
Sisi wanawake wa hapa tunapata tabu sana katika kuchota maji hadi nywele za katikati hazikui sababu ya kujitwisha chungu, je serikali itatusaidiaje?.
Waziri akajibu;
Nimeambiwa zinahitajika mil 200 kuondokana na tatizo, hizo mil 200 nitawapeni bila tatizo.
Hii imekaaje?. mia
 
Alimuandaa ili aulize hilo swali!! Fedha za miradi ya maji kutoka kwa wafadhili ndio wanagawana kinyemela na kufanyia propaganda za kisiasa!!!
 
Nimeona maajabu sana. Katika ziara za Waziri mkuu wa Tanzania kanda ya ziwa kaambatana na mkewe. Baada ya kuona Raia hawamuelewi waziri mkuu, Tunu Pinda ikabidi aulize swali kwa niaba ya wakazi wa sehemu husika.
Aliuliza;
Sisi wanawake wa hapa tunapata tabu sana katika kuchota maji hadi nywele za katikati hazikui sababu ya kujitwisha chungu, je serikali itatusaidiaje?.
Waziri akajibu;
Nimeambiwa zinahitajika mil 200 kuondokana na tatizo, hizo mil 200 nitawapeni bila tatizo.
Hii imekaaje?. mia

Huko ndo kujitekenya mwenyewe afu unacheka. Waacheni wahangaike tu. very soon wataanza kujifinya wenyewe afu wanalia!
 
Milioni 200 kwa mipango gani? Maneno kamili na halisi aliyosema Waziri Mkuu Pinda yako wapi?

Pinda kasahau habari za pesa ni matokeo?

Bila mipango hata milioni elfu mbili zitaungua bila matokeo, kwani "Mali bila daftari, hupotea bila habari"
 
Walikuwa wanahalalisha safari allowances zao. Hayo matatizo ya maji mama Pinda kayajuwaje kama mumewe hayajui? Kwani mh. Pinda alishindwa nn kulizungumzia hilo katika hotuba yake? Hawa wanatapatapa kwani wanajua, WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA.
 
ni wapi huko?
ni MAGU alikuwa na msafara wa magari kama mia na kitu. Pia aliulizwa swali na mama mmoja kuhusu serekali kutangazia wananchi huduma za kujifungua ni bure ili hali hospt hakuna hata glovis na pamba,Pinda hakuweza kumjibu
 
Nimeona maajabu sana. Katika ziara za Waziri mkuu wa Tanzania kanda ya ziwa kaambatana na mkewe. Baada ya kuona Raia hawamuelewi waziri mkuu, Tunu Pinda ikabidi aulize swali kwa niaba ya wakazi wa sehemu husika.
Aliuliza;
Sisi wanawake wa hapa tunapata tabu sana katika kuchota maji hadi nywele za katikati hazikui sababu ya kujitwisha chungu, je serikali itatusaidiaje?.
Waziri akajibu;
Nimeambiwa zinahitajika mil 200 kuondokana na tatizo, hizo mil 200 nitawapeni bila tatizo.
Hii imekaaje?. mia

Sio ajabu! MAISHA YA VIONGOZI WENGI WA BONGO YAPO KIMAIGIZO IGIZO TU! Tunu Pinda na Mizengwe Pinda wake walikuwa wanatekeleza Comedy yao!
 
Hawa nao wanajipanga kwa ujasirimali wakistaafu...wale mafao yao bila shida!ila iliwasaidia hao wanakijiji maana uoga huu sijui utaisha lini!
 
Ana uhakika gani kuwa kiasi kinachohitajika ni M200 kamili? Giving solution without plan!

Hizi ndio siasa za Tanzania ukitaka kufanikiwa au eneo lako lifikiwe na huduma za jamii kiurahisi wewe cheza na wanasiasa, unazisha event yoyote hata kama mna kikundi cha watu 20 cha kilimo cha nyanya alafu unamwalika waziri katika risala yenu mnachomeka na matatizo mbalimbali yanayowakabili na kama kawa tamko litatolewa na mkuregenzi wa halmashauri au manispaa au jiji itabidi akomae kutekeleza ahadi ya waziri hata kama ilikuwa sio priority (na hapo ujue wakati wanatekeleza kuna wananchi wengine wamelia kwa hela zao za maendeleo kukatwa bila kujua au watazua sababu nyingine ya kwanini mradi wao haujatekelezwa)
 
Alikuwa hajasikia swali aliloulizwa na mmoja ya waliopo mkutanoni, Tunu kalirudia tu.
 
Na uhakika huwa wanatembea tu kuona tz lakini wakija wanauliza maswali wanatuacha na shida zetu wanarudi kwenye viyoyozi dsm.
nilimuona kule ukerewe eti anamuuliza maswali mkurugenzi mtendaji hadharani ....utafikiri hawana ofice huu mtindo pia alikuwa nao jk yeye kesha usahau
 
Back
Top Bottom