Tunduma patifuka vurugu

Yaa, nami nipo katika maeneo haya kwa ujumla uhalibifu umefanywa kwenye jengo la mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma ambapo gari jipya Land cruser pick up double cabin limeharibiwa vibaya, compyuta za ofisini pamoja na laptop zimeibiwa, nyaraka zilizokuwa makabatini na kwenye maeneo mengine ofisini zimebebwa na wananchi na kuchomwa moto, Mabati na saruji vilivyokuwa stoo vimeibiwa na vitu vingine kuharibiwa, kamati ya ulinzi na usalama imeenda huko wakati tayari hali imekuwa shwari, naendelea kufuatilia nipo karibu nao
 
Nchi haitotawalika,hakuna kulala mpaka kileweke kama mbwai mbwai kuni jua sikutishi nchi haifai....mafisadi hawaibi laki wanaiba billioni.
 
Nasikia chadema wameshindwa kuwalipa malimbikizo yao waalimu na kuwapa posho wanazostaili ndio maana wamegoma....chadema tafadhari acheni kuleta vurugu walipeni waalimu haki zao
 
Hbari za kuthibitika toka Wilayani Tunduma ni kwamba wanafunzi toka baadhi shule wameandamana kuishinikiza serikali iwasikilize walimu na kutatua madai yao, katika maandamano hayo kulitokea purukushani na polisi hali iliyosababisha vurugu kubwa na uharibifu wa mali na majengo ya Halmashauri yamechomwa moto

source; mimi mwenyewe niko hapa Tunduma kikazi
hizi ni baadhi ya pic
 
hizi ni baadhi ya pic
Naona taratibu milipuko inaanza kuzoeleka!! Ipo siku watu watakuwa wanaibeba kuihamishia kwa wakuu wa wilaya na mikoa. Na kutakuwa na kugawanya chochote kile walichotuibia wenzetu ikiwa ni pamoja na uhai wao.
 
Hivi hawa Chadema kodi zooooooote hizi wanazokusanya pamoja na kujichotea kwenye mifuko ya hifadhi za kijamii inashindwa kuwalipa haki zao walimu mpaka wanagoma?
 
Back
Top Bottom