Tundu, Zitto wasisitiza chadema ni shwari

Baadhi ya WanaJF si wakweli kwani wao walikuwa wanashinikiza Zitto afukuzwe sasa leo wanageuka kinyonga kwa kusema afadhali hakuna mpasuko chadema,nilisema toka mwanzo kuwa humu kuna watu wanafata mkumbo tuu hawana uhalisia, si wake si waume!Tatizo ni shule za vichochoroni walizopitia bila kuelimika.
 
Hii ni sawa na kumuuliza mumeo/mkeo eti una nyumba ndogo? Harafu mnaosema amen mbona hamtafakari saaaana? Kuna dhambi na kishawishi cha dhambi, zitto asiwadanganye. Kama anakitakia mazuri chama cha CDM angekuwa bega kwa bega na wenzake na maamuzi ya chama, nini maana ya mpasuko? Ni kuwa na fikra tofauti. Na Tindu lisu hawezi kusema kuwa kuna mgogoro maana tamko hilo litaua chama. Tamko has nothing to do with us we need to build our confidence on what we see from you not what we hear from you.
 
Upo mgongano wa mawazo na si mgogoro!ingawa wakati mwingine mgongano wa mawazo huzaa mgogoro!lakini CHADEMA bado haijafika huko!ikifika huko wala haitakuwa siri tena kila mtu atajua kama ilivyokuwa kwa NCCR MAGEUZI 1996.

Kaka bora uzibe ufa maana ukiuacha itakulizimu kujenga ukuta. Mimi nasema lazima kila mwana chadema atii matakwa ya wengi chamani sio wengine kujidai eti wasipokubali wenyewe basi maamuzi hayo ni batili hata kama yuko mkwenye kundi la wachache. Hiyo tabia ife otherwise no move to change
 
Ni kweli kabisa mkuu,na hiyo ndiyo maana ya democrasia(wengi wape),Zitto alipaswa kufuata kile kilichoamriwa na wengi!!!
 
Hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA imeelezwa kwamba ni shwari na hakuna matafaruku utakaotokea.Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,Tindu Lissu,pamoja na Naibu katibu mkuu wa chadema Zitto kabwe walisema hayo kwa nyakati tofauti walipohojiwa kufuatia hatua ya wabunge wa 10,akiwemo naibu katibu mkuu wake,Zitto Kabwe kutokana na kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akihutubia bunge.
"Hakuna mgogoro wowote baina ya viongozi wa chama bali kilichopo ni taratibu za kinidhamu na sio mgogoro wala mgongano wowote"alisema.Akizungumza jana,Lissu alisema hakuna mpasuko,mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliyopo ndani ya chama hicho.
Kwa upande wake zitto kabwe alisema,hakuna mgogoro wowote ndani ya chama hicho na kwamba taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja.Zitto alisema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya chama hicho na wengine kufikia hatua ya kusema uongo kwa nia ya kuleta chokochoko ,na akasisitiza haoni mgogoro wowote na kutaka wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu.Zitto alisema wakati umefika kwa watanzania kujenga tabia ya kuimarisha vyama na sio kubomoa kama ulivyo sasa ambapo jambo dogo linakuzwa.[Mwananchi,6 Desemba 2010,pp 5]

My take
Mnaokodolea macho na kuombea chadema iingie kwenye mgogorona hatimaye kufa kabisa,hamta fanikiwa kamwe!CHADEMA ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo na kushamiri kwa kasi zaidi,hari zaidi na nguvu zaidi.Mungu ibariki CHADEMA,mungu ibariki Tanganyika.

Kuna watu humu wana zile uniform za kijani na njano, wengine wanawakilisha sisiemu biii, wanajifanya wanaleta hoja, nyingine hoja feki, lengo ni kuwapumbaza wana-CDM na kuweka mpasuko chamani!
Kauli za TL na ZK ni faraja kwa wana-CDM!
Big up
 
Hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA imeelezwa kwamba ni shwari na hakuna matafaruku utakaotokea.Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,Tindu Lissu,pamoja na Naibu katibu mkuu wa chadema Zitto kabwe walisema hayo kwa nyakati tofauti walipohojiwa kufuatia hatua ya wabunge wa 10,akiwemo naibu katibu mkuu wake,Zitto Kabwe kutokana na kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akihutubia bunge.
“Hakuna mgogoro wowote baina ya viongozi wa chama bali kilichopo ni taratibu za kinidhamu na sio mgogoro wala mgongano wowote”alisema.Akizungumza jana,Lissu alisema hakuna mpasuko,mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliyopo ndani ya chama hicho.
Kwa upande wake zitto kabwe alisema,hakuna mgogoro wowote ndani ya chama hicho na kwamba taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja.Zitto alisema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya chama hicho na wengine kufikia hatua ya kusema uongo kwa nia ya kuleta chokochoko ,na akasisitiza haoni mgogoro wowote na kutaka wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu.Zitto alisema wakati umefika kwa watanzania kujenga tabia ya kuimarisha vyama na sio kubomoa kama ulivyo sasa ambapo jambo dogo linakuzwa.[Mwananchi,6 Desemba 2010,pp 5]

My take
Mnaokodolea macho na kuombea chadema iingie kwenye mgogorona hatimaye kufa kabisa,hamta fanikiwa kamwe!CHADEMA ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo na kushamiri kwa kasi zaidi,hari zaidi na nguvu zaidi.Mungu ibariki CHADEMA,mungu ibariki Tanganyika.

Mkuu TUKUTUKU, Heshima kwako

Ni Tundu Lissu siyo Tindu, ni hilo tu kwa leo
 
hivi zitto ni nani hata kunyumbisha chama? WATANZANIA SI WAJINGA KUVAMIA TOPIC ZA KIDINI ambazo wachovu kama zitto na jk wamekuwa wakijikinga na udhaifu wao wa kinafki! there is no any legitimacy for zito and his mates in this war of liberation .zito kalale na jiunge na ccm na hatukuhitaji
 
Sisi wote tulijua hakuna mgogoro. Yanayotokea ni mambo ya kawaida isipokuwa yanakuzwa na vyombo vya habari na baadhi ya mawakala wao kwa nia ya kuua upinzani. Najua kauli hiyo ya pamoja imewaudhi sana maadui wa upinzani. Bravo Zitto & Lissu
 
Si hitaji kuwa na Elimu ya Chuo kikuu kujua Zitto anaipeleka CHADEMA pabaya! Nyie ongeeni tu lakini Zitto sio mwenzetu! yuko kimaslahi binafsi zaidi.
 
hali ya kisiasa ndani ya chadema imeelezwa kwamba ni shwari na hakuna matafaruku utakaotokea.mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,tindu lissu,pamoja na naibu katibu mkuu wa chadema zitto kabwe walisema hayo kwa nyakati tofauti walipohojiwa kufuatia hatua ya wabunge wa 10,akiwemo naibu katibu mkuu wake,zitto kabwe kutokana na kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya bunge wakati rais kikwete alipokuwa akihutubia bunge.
“hakuna mgogoro wowote baina ya viongozi wa chama bali kilichopo ni taratibu za kinidhamu na sio mgogoro wala mgongano wowote”alisema.akizungumza jana,lissu alisema hakuna mpasuko,mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliyopo ndani ya chama hicho.
kwa upande wake zitto kabwe alisema,hakuna mgogoro wowote ndani ya chama hicho na kwamba taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja.zitto alisema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya chama hicho na wengine kufikia hatua ya kusema uongo kwa nia ya kuleta chokochoko ,na akasisitiza haoni mgogoro wowote na kutaka wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu.zitto alisema wakati umefika kwa watanzania kujenga tabia ya kuimarisha vyama na sio kubomoa kama ulivyo sasa ambapo jambo dogo linakuzwa.[mwananchi,6 desemba 2010,pp 5]

my take
mnaokodolea macho na kuombea chadema iingie kwenye mgogorona hatimaye kufa kabisa,hamta fanikiwa kamwe!chadema ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo na kushamiri kwa kasi zaidi,hari zaidi na nguvu zaidi.mungu ibariki chadema,mungu ibariki tanganyika.

si kweli moto ulioko huku tunaujua sisi wa ndani wewe wa nje huwezi jua tundu lisu ni mtu mzima na mwanataaluma hawezi kiri hadharani kuwa cdm kuna hali mbaya
 
Pamoja na mambo mengine i.e. tofauti za kimitazamo............Mh.Zitto amekuwa MWIBA mkali sana kwa Majambazi CCM...............hivyo ni vema CDM wakalijua hilo na wassingie kwenye mitego ya vyombo vya habari............
 
si kweli moto ulioko huku tunaujua sisi wa ndani wewe wa nje huwezi jua tundu lisu ni mtu mzima na mwanataaluma hawezi kiri hadharani kuwa cdm kuna hali mbaya

Mkuu hiyo habari uliyonayo ni nzuri sana.Lakini cha kusikitisha utaki kuitoa,tuambie basi nini kinaendelea huko ndani!kukaa kimya kipindi kama hiki si busara!tafadhari tujuze ulichonacho!!!
 
Zilikuwa ni dili za makanjanja kukichafua chama coz walitumwa na mafisadi na wameshindwa sasa!
 
Wakuu mnaokubali kupumbazwa na gazeti la Mwananchi kuhusu Zitto nawaonea huruma. Pale mwananchi yupo mhariri mmoja aliacha kazi ya Public Relations Tumaini University Iringa. Ni swahiba mkubwa wa Zitto. Upupu wote mliouona na kuusikia kutokea Mwananchi unaomhusu Zitto, mara usikie anajiuzulu mara usikie kaandika barua ya kujiuzulu mara usikie Zitto atofautiana na Mbowe huyo mhariri anashirikiana na Zitto na ni werevu kweli wa kusoma alama za nyakati. Zitto anaelewa kuwa hata mtoto wa darasa la saba hawezi kwenda barabarani kutangaza walivyopishana kauli na babake nyumbani, lenyewe linatoka linaenda TBC linatangaza walivyopiga kura na kulazimisha umma ukubali upuuzi wake wakati anajua kuwa ni utovu wa nidhamu. Mgogoro upo na Zitto ni wa kuangaliwa kama ukoma. Ningekuwa Mbowe saa nyingi kasharuidisha kadi ili ashirikiane vizuri na Kafulila na James Mbatia NCCR MANUNUZI. Shuwaini mkubwa!
 
Hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA imeelezwa kwamba ni shwari na hakuna matafaruku utakaotokea.Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,Tindu Lissu,pamoja na Naibu katibu mkuu wa chadema Zitto kabwe walisema hayo kwa nyakati tofauti walipohojiwa kufuatia hatua ya wabunge wa 10,akiwemo naibu katibu mkuu wake,Zitto Kabwe kutokana na kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akihutubia bunge.
“Hakuna mgogoro wowote baina ya viongozi wa chama bali kilichopo ni taratibu za kinidhamu na sio mgogoro wala mgongano wowote”alisema.Akizungumza jana,Lissu alisema hakuna mpasuko,mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliyopo ndani ya chama hicho.
Kwa upande wake zitto kabwe alisema,hakuna mgogoro wowote ndani ya chama hicho na kwamba taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja. Zitto alisema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya chama hicho na wengine kufikia hatua ya kusema uongo kwa nia ya kuleta chokochoko ,na akasisitiza haoni mgogoro wowote na kutaka wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu. Zitto alisema wakati umefika kwa watanzania kujenga tabia ya kuimarisha vyama na sio kubomoa kama ulivyo sasa ambapo jambo dogo linakuzwa.[Mwananchi,6 Desemba 2010,pp 5]

My take
Mnaokodolea macho na kuombea chadema iingie kwenye mgogorona hatimaye kufa kabisa,hamta fanikiwa kamwe!CHADEMA ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo na kushamiri kwa kasi zaidi,hari zaidi na nguvu zaidi.Mungu ibariki CHADEMA,mungu ibariki Tanganyika.

Kinachoendelea hivi sasa ni taratibu za kinidhamu (angalia italic, bold & underline zangu).

Na hata adhabu zikija kutolewa kwa wale watakaopatikana na hatia, bado hautakuwa mgogoro wala ngongano, bali itakuwa ni maamuzi yaliyotolewa kwa kufuata taratibu.
 
Back
Top Bottom