Tundu Lisu ni kisiki cha mpingo wapenda haki tunakukubali endeleza tupo nyuma yako

yah najua yule jamaa filikunjombe ni magamba lakini ni kati ya wale wachache wanaeimba'' nilalapo nakuota wewe''
 
lissu anatisha amaongea ukweli bila hata chembe ya unafiki. Nashangaa wabunge wa ccm hasahasa wa tanzania bara wanaacha kuungana na wenzao kuupinga muswada , wakati wa zanzibari wale wa cuf na ccm wameungana . hii ina maana tanzania bara wabunge wa ccm ni waoga na wanafiki
 
Tundu Lissu ni jembe,haogopi kuongea kilichopo moyoni mwake,nampongeza sana kwa hilo.
 
Kizuri cha jiuza, Kazi ya lisu inaonekana na inalipa ndo maana anazidi kungaa ndani ya bunge. Tunachotakiwa kama wananchi wa tanzaniya ya kweli ni kumuunga mkono katika vita hivi ambavyo ni hatari kwa maisha yake.
Mungu ambariki ampe mwangaza zaidi.
 
Kwa kazi inayofanywa CHADEMA kwa kwa kweli mnapaswa kupongezwa. Lakini nachukua nafasi kumpongeza Tundu Lisu hakika umeonyesha uajasiri mkubwa na sio mwoga pamoja na kushambuliwa kila upande na Magamba na washirika wao kutoka bara hadi visiwani huajalegeza msimamamo wala kutetereka. Umeonyesha kuwa wananchi waliokuchagua hawakufanya makosa pia umedhiirisha kuwa wabunge wote wa CCM hawajakaribia hata kidogo uwezo wako wa kuona mambo. Kilichonifurahisha ni kuwa wewe si mnafiki kama baadhi ya wabunge wengine sisi wapenda amani na usawa tunakuombea maisha kwani pia tunajua uanahatarisha maisha yako mbele ya Magamba.

Nimekumbuka ule msemo wa JK kwenye kampeni kuliko Tundu Lisu awe mbunge heri Dr Slaa awe rais, hakika wewe ni kisiki cha mpingo

nakubaliana nawe asilimia zote. mimi pia nakuombea heri
 
Kwa kitu msichokijua.MH TUNDU LISU
Nikati ya jopo la mawakili waliyo mkuwa wanamtetea Rais wa sasa wa South Africa Mh ZUMO na kesi zake.
Ni wakili mwenye uwezo wa juu.
TATIZO KUBWA LA WABUNGE WA CCM NI WIVU
 
TUNDU ANTIPAS LISU NI SAWASAWA NA WABUNGE MIA WA CCM

hakuna ubishi wabunge 100 wa magamba ni sawa na TUNDU LISU mwenyewe

BIG UP BRO,TUKO PAMOJA KWA SALA NA SUPPORT
 
Kwanza upende usipende mh lisu ni intellectual maana mpaka sasa hivi hakuna anayejibu hoja wanaishia kumtukana. Jibuni hoja ukweli unauma. Tais ana madaraka kama mfalme hata kama katiba ya sasa inasema hivyo anayebisha aseme.
Pili ni jasiri anaongea anachoamini hajali yuko peke yake ama na wafuasi. Wengi hawana hili they are just followers.
Tatu very analytical
nne anaongea kwa utulivu sana
namshukuru mungu aliyenipa nafasi ya kuongea na lisu siku moja. Asiye amini tafuta nafasi uongee na lisu uone. Si mchezo anajua mambo maana anasoma
 
Mh lisu hata ukianza likizo sasa hivi hili ulilofanya wengi hata ukiwapa miaka 100 hawawezi.
 
Mbona Sitta (at least anafahamu sheria among magamba) amekimbia na kwenda India kumsalimia
Dr. Mwakyembe, kwanini hakua ahirisha akabaki kuitetea serikali yake ktk
kipindi hiki tete?

Mkuu hawa watu huwa makini sana na hoja zinazoletwa bungeni. Huyu mzee Sitta na Lowassa huwezi kuwaona wamejiandikisha katika hoja tata kama hizi, Kwani wanajua nini kilicho mbele yao. Wana malengo ya baadae hawa ndio maana huwa wajanja sana kuchangia hoja kama hizi. Nikirudi kwa Mh Lissu nadhani anaifanya kazi yake ya uwaziri kivuli ktk hali ya uweledi wa juu mno mpaka magamba wanachanganyikiwa.
 
mama wa katiba yy katika kuhitimisha ametumia muda mwingi kulazimisha kuwa kamanda LISSU ni mpotoshaji in proffession,kisa kamwaga nondo nzito,pia anawaomba wagamba wenzie watumie radio kuwaeka sawa wapiga kura ili wakija hawa wenye nondo wawe wamewekwa sawa.
 
Lissu ndiyo,anafahamu wajibu wake ukweli na haki pia ameamua kuvisimamia. Mungu amtiye nguvu pamoja na wapenda haki na ukweli wote.
 
Kweli jamaa ni kichwa maana hadi leo wenye akili mgando bado hawajaelewa aliwasilisha nini ila sisi tunaoelewa tuampongeza
 
PEOPLE'S POWER NI KWELI kamanda LISSU ni JEMBE la ukweli.Tuanakuombea sana kwa Mungu uzidi kutuongoza,Ila kama huwa unapita humu jukwaani tunaomba uelewe kuwa tuko nyuma yako na waeleze wabunge wote wa Chadema tuko nyuma yao na kiukweli wengine tuna hasira sana na tunaomba mtupe update kile mnachokijadili ili nasi tuelewe hatima yenu ya kutoka nje na kuwapisha hao magamba wajadili mswaada batili kwa watanzania ila ni mswaada wa CCM na CCM B
 
"Kwa Mungu Mwenyezi Muumba Mbingu Na Nchi Na Vitu Vyote Vionekanavyo Na Visivyo Onekana, Tunamkabidhi Ndugu Yetu Mpendwa Mheshiwa Tundu Lisu" Ee Mungu Umlinde, Umuweke Salama Dhidi Ya Watu Waovu Na Umpe Furaha na Amani Yeye Na Familia Yake Na Wazazi Wake Waliomleta Duniani. Hakuna Lolote Baya Litakalompata Chini Ya Ulinzi Wako Mkuu. Amina.

 
Back
Top Bottom