Tundu Lisu kweli kiboko amchana Kikwete kuhusu kuingilia Idara ya Takukuru

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
Alikuwa anachangia kwenye bunge na akanukuu kauli ya Hosea aliyoitoa kwa balozi ya marekani kwamba rushwa kubwa zinashindikana kukomeshwa kutokana na vingozi wa juu kuzikingia kifua. Anasema Kauli hii inaonyesha hatari iliyopo kama Rais wa nchi anaingilia maamuzi ya takukuru na watumishi kwa kuogopa kufukuzwa wanaacha kuziandama rushwa kubwa.

Bila kumungunya wala kumeza meza maneno anaomba bunge hilo kujadili jambo hilo na wahusika wazomee bungeni kabla hawajakutana na nguvu ya umma. wabunge kama hawa ndio tunaowahitaji na sio wale wa ndiooooooooooooo na kupiga meza za bunge hovyohovyo
 
Safi sana Lissu.............................. Wabunge wa CCM wanatuharibia meza kazi yao kuzipiga kila kukicha kwa kutetea uozo.
 
Tungekuwa na wabunge wa namna hii kweli tunahitaji miaka kumi tu na nchi hii ingekuwa na maendeleo yasiyokuwa na mfano
 
UTASKIA........anauza sura kwenye Runingaaaaaa.........kuna watu huwa sielewi walipataje elimu hadi wakaitwa MAJAJI,MADAKTARI,MAINJINIA,WALIMU,.........YANIIIII
 
Lisu ni kichwa na huwa makamanda wa cdm hawana muda wa kamumunya maneno wanasema kile kilichopo na huwa ni wabunifu sana so keep it up lisu
 
UTASKIA........anauza sura kwenye Runingaaaaaa.........kuna watu huwa sielewi walipataje elimu hadi wakaitwa MAJAJI,MADAKTARI,MAINJINIA,WALIMU,.........YANIIIII
kuna watu mindset zao bado ni zimesetiwa ki single party state.
 
Lisu ni kichwa na huwa makamanda wa cdm hawana muda wa kamumunya maneno wanasema kile kilichopo na huwa ni wabunifu sana so keep it up lisu

Kweli kabisa RED ONE yaani LISU na CDM kweli kiboko wanaita shoka shoka na sio panga la kukatia kuni na wako straight forward nasio wabunge wa CCM ambao uanza kwa kumshukuru Rais, then waziri mkuu , then mh spika ,halafu wapiga kura baadaye wake/waume zao muda ukiisha wanaunga mkono hoja . tutafuka kweli?
 
Jamaa ana'dhamiri sahihi na nchi yetu, huwezi unamfananisha na kina Komba. Kwa kifupi Tundu lissu ni sawa na wabunge 100 wa SisiEmu.
 
Back
Top Bottom