Tundu Lissu: Wenje asiposhinda kesi ya matokeo, najiuzulu ubunge

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,251
1,467
Yanayojiri Ubunge jimbo la Nyamagana Jiji la Mwanza.

Ndugu zangu yule Mwanasheria nguli na mahili(International Lawyer) hivi karibuni ameahidi kujuhuzulu nafasi yake ya ubunge.

Haya yalijiri pale mahakama kuu ya Tanzania kanda ya ziwa Mwanza mara baada ya kesi ya kupinga ushindi wa ubunge wa Mabura,Stanislaus.

Baada ya mahakama kuomba vielelezo vya ushindi wa Mabula,Alikimbilia halmashauri ya jiji na kuleta mabox ya kura na kusema ndiyo ushahidi wake wakati mshindi anayedai kuporwa ushindi wake mh.E.Wenje akileta fom namba 21 zilizosainiwa na mawakala wote zikionesha wazi alishinda(kwa mujibu wa form)

Hakimu aliomba mh.Mabula kuwasilisha vielelezo vingine nje ya box kwa kuwa kwanza bix ni mali ya tume na mahakama haifanyi kazi ya tume ya kufungua mabox.

Mh.Mabula alisema yeye alivichoma vielelezo vingine baada ya kuona havina maana tena(kwa maelezo yake nje ya mahakama)

Baada ya hapo Wakili anayemtetea Mh.Ezekiel Dibogo Wenje ndugu Tundu Antiphas Mung'wai Lissu nje ya mahakama alimfuata Mbunge huyo wa ccm na kumuahidi kwamba kwa kuja na mabox akishinda hiyo kesi atalazimika kumnunulia gari yenye thamani ga pesa za kitanzania 25 ml pamoja na kujiuzulu ubunge katika jimbo lake.

Kesi inasubiri kupangiwa hakimu na kusikilizwa kwa awamu ya mwisho.Hii ni baada ya siku ya jumanne wiki iliyopita umati mkubwa wa watu na wafuasi wa Chadema na Ukawa kujaa eneo la mahakama wakisubiri kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo na kuambiwa kuwa siku hiyo haitasikilizwa tofauti na taarifa zilizokuwa zimetolewa siku ya tarehe 02/02/2016 ambapo haikusikilizwa kwa kuwa ilikuwa wiki ya sheria.

Stay tuned,get informed.
 
Lisu akujiuzulu weye utafaidi nini?? Au ndo mshaamua mshindi ni huyo wa ccm? Andika kichwa cha habari chenye mantiki. Nilikimbilia nkidhani kuwa Lisu kashikwa kichaa kumbe ni mwandishi kichaa!
 
Ni kweli Wenje na kafulila walinyang'anywa ubunge kwa nguvu,tena we Mabula hukushindaaaaa hayo mabox ya kura yalikua ya wizii kilicho halali Ni Ni karatasi za matokeo
 
Ushahidi wa mabox ya kura ...mmmmhhhhh.kwani yanahifadhiwa wapi na uhakika wa mtu kutokucheza nao upo kweli..?????Tuna imani na mahakama kutoa haki.
 
JF bana raha iyo international lawyer imenichekesha sana. JF hata ukitukanwa ama kutaniwa usikasirike kabisa. Watu humu tulikuwa maadui
 
Kiukweli wabunge wengi walishindwa kwa kurudia kuhesabu kura
Zile fomu zikipitiwa hakika UkAWA watakuwa na wabunge wengi tu
 
Hivi hawa kina Mabula et al wana japo uelewa wa wanachokifanya mahakani? Hugo wakili wake naye hana ufahamu wa aina ya vielelezo katika kesi za uchaguzi au naye ni ngimbaro wa sheria? Masanduku ya kura mahakamani? Hebu aandike kuwa ameshindwa na ampishe Wenje mshindi halali.
 
Ndugu zangu yule Mwanasheria nguli na mahili(International Lawyer) hivi karibuni ameahidi kujuhuzulu nafasi yake ya ubunge.

Haya yalijiri pale mahakama kuu ya Tanzania kanda ya ziwa Mwanza mara baada ya kesi ya kupinga ushindi wa ubunge wa Mabura,Stanislaus.

Baada ya mahakama kuomba vielelezo vya ushindi wa Mabula,Alikimbilia halmashauri ya jiji na kuleta mabox ya kura na kusema ndiyo ushahidi wake wakati mshindi anayedai kuporwa ushindi wake mh.E.Wenje akileta fom namba 21 zilizosainiwa na mawakala wote zikionesha wazi alishinda(kwa mujibu wa form)

Hakimu aliomba mh.Mabula kuwasilisha vielelezo vingine nje ya box kwa kuwa kwanza bix ni mali ya tume na mahakama haifanyi kazi ya tume ya kufungua mabox.

Mh.Mabula alisema yeye alivichoma vielelezo vingine baada ya kuona havina maana tena(kwa maelezo yake nje ya mahakama)

Baada ya hapo Wakili anayemtetea Mh.Ezekiel Dibogo Wenje ndugu Tundu Antiphas Mung'wai Lissu nje ya mahakama alimfuata Mbunge huyo wa ccm na kumuahidi kwamba kwa kuja na mabox akishinda hiyo kesi atalazimika kumnunulia gari yenye thamani ga pesa za kitanzania 25 ml pamoja na kujiuzulu ubunge katika jimbo lake.

Kesi inasubiri kupangiwa hakimu na kusikilizwa kwa awamu ya mwisho.Hii ni baada ya siku ya jumanne wiki iliyopita umati mkubwa wa watu na wafuasi wa Chadema na Ukawa kujaa eneo la mahakama wakisubiri kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo na kuambiwa kuwa siku hiyo haitasikilizwa tofauti na taarifa zilizokuwa zimetolewa siku ya tarehe 02/02/2016 ambapo haikusikilizwa kwa kuwa ilikuwa wiki ya sheria.

Stay tuned,get informed.
Huyo mabula tayari keshashindwa yaani ushahidi ni kubeba mabox ya kura?huo ni ukichaa kabisa,yaani ni sawa na dokta akwambie anataka apime choo yako wewe unaenda unabomoa choo unapeleka hospital
 
Lisu akujiuzulu weye utafaidi nini?? Au ndo mshaamua mshindi ni huyo wa ccm? Andika kichwa cha habari chenye mantiki. Nilikimbilia nkidhani kuwa Lisu kashikwa kichaa kumbe ni mwandishi kichaa!
Nitaachaba na siasa na sitapiga kura tena maana nina imani na Lissu 100% .

Pitia maandishi yangu tena mkuu.
 
Back
Top Bottom