uzuri wa chadema huwa hawakosei wala hawataki kurekebishwa
tumeona sasa CCM wanajenga hoja kwamba alikimbia vikao vya kamati sasa ndio anaona ana maoni ya kubishana kipi kiwemo na kipi kisiwemo ni kama kweli Tundu hakuwajibika
chadema wameshikwa pabaya wabishi hao hata kwenye hoja iliyo wazi ni heri tusio na chama. kama mnabisha kuwa Tundu hakukosea basi hakuna haja ya kushika dola mtakuwa wabishi zaidi na hamtashaurika kama CCM
Mnaongea ongea tu hamjui what real happened, Hebu mtafuteni Lissu ana majibu ya Uhakika!
magamba bwana!.....Wakati wa kufunga muswada wa katiba, Waziri wa sheria na katiba Celina kombani alituambia watanzania kwamba anamshangaa Tundu Lissu anafunguka leo na kutoka bungeni na wanachadema wenzake wakati hakutokea kwenye vikao vya kamati ambako angeweza kutoa maoni yake. Kombani alisema, kwa mfano katika kikao cha mwezi juni, 2011 Lissu alikuwa Tarime wakati wajumbe wengine wakikutana kuandaa mchakato huo kwa ajili ya kuwakilishwa bungeni lakini pia Waziri alisema anayo orodha ya mahudhurio kuthibitisha kwamba Lissu hakuhudhuria. Katika hitimisho lake hilo Kombani alisema, wajumbe wengine kama Halima Mdee na wabunge wengine wa upinzani walihudhuria na walitoa maoni yao ambayo yamepokelewa na kufanyiwa kazi.
Kumbuka kamati hii iliundwa baada ya kukataliwa kwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza ili kutatibu mchakato huo upya kabla hujasomwa kwa mara ya pili miongoni mwa wajumbe alikuwa Tundu Lissu ambaye taifa limetangaziwa kwamba hakuhudhuria vikao.
my take: 1. Ni kazi gani muhimu zilimbana Lissu kuliko unyeti wa katiba (moyo wa nchi)
2. lissu analetaje maoni yake bungeni wakati maoni hayo angeyatoa kwenye kamati
3. Lissu angehudhuria vikao vya kamati ya katiba angetuambia alitoa maoni gani ambayo hayakupokelewa.
4. Tundu Lissu huwezi kulitumia bunge kama kamati ndogo unawarudisha nyuma wengine.
5. Lissu tuombe radhi watanzania kwa kushindwa kutuwakilisha kwenye kamati
6. Lissu wewe ulikuwa muhimu sana kuanzia ngazi ya kamati ambako hukuhudhuria
7. tundu lissu ulitoa kipambele kwa mamabo mengine kuliko katiba?
Kwani alijibuje?huyu pipijojo amekurupuka tena sana na wewe naona unaingia kwenye mtego wake halafu unajifanya eti huna chama.!!!!!! jana kwenye mdahalo kuna mtu aliuliza swali hilo na lissu alilijibu kwa ufasaha sana..
pipijojo unaongea usicho kijua.hayo unayosema kombani hajayasema Bungeni bali aliyasema wakati startv alipowakutanisha yeye na lissu katika kpindi cha tuongee asubuhi ambapo lissu alimjibu na kumuuliza hasard ya waliyo yaongea lakini kombani akabaki akichekacheka pasipo jibu lolote.magamba mwaka huu mnalo. mia
hivi suala ni tundu lisu au katiba? Mbona akili zako ndogo sana?