Tundu Lissu on KLH News Exclusive!

Status
Not open for further replies.
Tunashukuru sana Geeque na MKJJ kwa mahojianao.....duhh mshikaji nimeisikia ile warning ya one minute........anyway si haba, wako watakao jitokeza kuku-support

Inshallaah
hahahahaahha yeah Mazee si umesikia ndio hivyo lakini kitu kizuri ni kwamba ameongea vya kutosha. Tunashukuru pia wasikilizaji wote ambao mmeweza kujiunga na kusikiliza hayo mahojiano.
 
ok basi baba....

fair game sawa?

Mwafrika wa kike,

Mbona umebadili nilichoandika? Mimi nimeandika hivi:
"Mbona magoli kidogo hivyo? Nifungeni hata magoli 20 bora ninacheza fair na kwa juhudi zangu zote."

Sasa bora imegeuzwa kuwa mbona? Nafikiri ni typing error kwahiyo nakusamehe!!
 
Duh! Mazee Gee!

Heshima mbele mkuu, I mean siasa pembeni lakini I got it bros maana hii yako ni kazi kweli, na ndio kumkoma nyani kweli kweli tena mchana kweupee,

Wakuu wote wawili Geeque na Mzee Mwenzangu MMJ, SALUTE!
 
Mwanakijiji,

Nina uhakika unajua wazi kwamba Tundu Lisu ni mkurugenzi wa sheria, haki na katiba wa CHADEMA. Ni haki kuelezea vyeo vyake vyote ili kuwapa wananchi nafasi ya kumuelewa kabla ya kuanza kujadili uchambuzi wake.
http://www.chadema.net/uongozi/sekreta.php

Hata mimi ambaye uandishi uko mbali sana najua hiyo ni requirement moja hasa pale suala analojadili lina uhusiano na hicho cheo chake ambacho umekificha.

Pamoja na kutokuwa na wasiwasi na integrity ya Tindu Lisu na kuheshimimu mchango wake huko nyuma hasa kwenye suala la wananchi wanaodhaniwa kufukiwa kwenye mashimo ya madini Mwanza, lakini ni vizuri kujua katika hili suala anazungumza kama nani.

Mwanakijiji, unatisha, sioni kama una tofauti na akina Rweyemamu.
Sikutegemea hata siku moja niliseme hili Mwanakijiji juu yako kwani kuna michango yako asilimia kama 80 ninaiheshimu sana.

Lakini haya mambo ya kuficha ukweli makusudi, ni uwongo ambao ukiachiwa utaendelea kukua siku hadi siku.

Hivi wewe una matatizo gani hasa?Hapa cha muhimu ni habari kwamba Tindu Kissu atakuwa akihojiwa radioni muda uliotajwa.Hivyo vyeo vyake sio muhimu zaidi ya atachokieleza.Na kama una wasiwasi kuhusu integrity yake,hulazimishwi kusikiliza mahojiano hayo.Cha uwongo hapo ni kipi?Kusema kwamba Tindu ni mwanaharakati wa mazingira au...?

Huhitaji kuwa mwandishi wa habari kutambua kuwa kwa mtu mwenye nyadhifa mbalimbali,chguo la kumtambulisha linaweza kuwa kwenye jambo/wadhifa unaomtambulisha zaidi kwenye jamii,na kwa hapa Lissu nafahamaika zaidi katika jamii kama mwanaharakati wa mazingira na mwanasheria kuliko hizo nyadhifa zake unazotaka ziwekwe hadharani.Acha fikra za kizembe,CV is nothing compared to hoja.
 
Suala la mkataba ni la kisiasa na limeibuliwa na vyama vya siasa. Kwahiyo nafasi ya Lisu kwenye siasa ni muhimu mno kwenye hili suala kuliko hata hicho cheo cha mazingira.

Kwahiyo kwa upeo wako,kwa vile suala la Buzwagi limeibuliwa na vyama vya siasa basi vikundi visivyo vya kisiasa (eg NGOs,wanaharakati,nk) havina ruhusa kuzungumzia?Mbona hujasema lolote kuhusu Balozi za nje zinavyogusia suala hilo?Au vipi kuhusu yule askofu aloitaka serikali iangalie suala hilo?

Hivi kwa mtizamo wako,suala likizungumzwa na mwanasiasa inamaanisha kuwa halipaswi kugusiwa na mwananchi mwingine?Lisu ni MTANZANIA,ana kila haki kama mie au hata wewe (ukitaka) kujadili mustakabali wa nchi yake.
 
Nakubaliana na anayosema Lisu na hata mimi nataka kupigana na hao mafisadi lakini ufisadi wa kweli utaondoka tu pale tutakapokuwa tayari kupigana na haya madhambi ya kila aina tokea sehemu yoyote bila kujali chama.

Tusipoliangalia hili tutaondoa mafisadi wa CCM na kutengeneza mafisadi wa chama kingine. Ndio maana wengine tunataka fair game kwenye haya mapambano ya fikra.

Tuna mifano mingi sana Afrika, ninayoyaona hapa JF hayanipi tumaini kwamba kwa TZ hata tukibadili chama kutakuwa na mabadiliko kwa mwananchi wa kawaida.

Ee bwana ee,acha longolongo zako.Kama unayoyaona hapa JF hayakupi matumaini nenda huko kwa akina Karamagi ukapewe matumaini.Unacholalamika hata hakieleweki.Ulitaka Lissu atambulishwe kwa cheo chake,hilo limefanyika bado unaendelea kusononeka.What's going on,baindamu?
 
Ee bwana ee,acha longolongo zako.Kama unayoyaona hapa JF hayakupi matumaini nenda huko kwa akina Karamagi ukapewe matumaini.Unacholalamika hata hakieleweki.Ulitaka Lissu atambulishwe kwa cheo chake,hilo limefanyika bado unaendelea kusononeka.What's going on,baindamu?

Jadili hoja yangu na sio kunijadili mimi maana kwa kufanya hivyo unapoteza muda wako kumjadili mtu ambaye hata humfahamu.

Haya ni mapambano ya fikra na kila mtu ana za kwake. Kama unaamini kwamba utangulizi wa Mwanakijiji ulikuwa sahihi basi toa hoja yako.

Mtu yeyote anayepinga baadhi ya mambo yanavyoendeshwa hapa basi ni fisadi,ni CCM, hiyo ni argument iliyofilisika maana haiendani na facts wala data zozote.

Kwa watu wa technology wanajua garbage in, garbage out, ndio maana
ni muhimu mno kuweka facts na data zote inavyotakiwa ili upate outcomes nzuri ya mjadala au kitu chochote.

2010 haiko mbali na ndio tutaona kama startegy za kushambulia watu badala ya hoja zitawafikisha wapi?
 
Kwahiyo kwa upeo wako,kwa vile suala la Buzwagi limeibuliwa na vyama vya siasa basi vikundi visivyo vya kisiasa (eg NGOs,wanaharakati,nk) havina ruhusa kuzungumzia?Mbona hujasema lolote kuhusu Balozi za nje zinavyogusia suala hilo?Au vipi kuhusu yule askofu aloitaka serikali iangalie suala hilo?

Hivi kwa mtizamo wako,suala likizungumzwa na mwanasiasa inamaanisha kuwa halipaswi kugusiwa na mwananchi mwingine?Lisu ni MTANZANIA,ana kila haki kama mie au hata wewe (ukitaka) kujadili mustakabali wa nchi yake.

Mimi nilivyofundishwa ni kwamba kwenye jambo lolote unaloliongelea lazima utoe wazi interests zako zingine zozote zilizopo kwenye hilo jambo. Mimi pia naamini hiyo ndio njia pekee ya kuwa fair kwa wale wanao kusikiliza.

Lisu ana right ya kujadili huo mkataba kama tulivyo na right watu wengine. Lakini pia chini ya sheria zote za uongozi bora duniani anatakiwa kuweka wazi interests zake kwenye hilo jambo.

Ilikuwa ni makosa kwa Mwanakijiji kutokusema Lisu ni kiongozi wa chama cha siasa. Bahati nzuri baadaye alirekebisha na hilo mimi nimelikubali.

Kama unaamini tofauti? Well, akili ni mali, kila mtu ana zake. Sitatumia bunduki, matusi waka kejeli kukushawishi ukubali hoja zangu. Kama hoja imeshindwa kufanya kazi, basi tunaendelea kukata ishu zingine.
 
Mtanzania,
nimesoma toka huko kwa page one, argument yako ilikuwa valid na majibu imepata kwisha......usi waste muda na talent yako kujibizana na watu ambao hawajafuatilia hii kitu toka mwanzo, kwa ufupi watu kama wewe ambao "wanaonekana" ni CCM wanahitajika hapa ili kuwe na balance!!!!. Kama umesoma Plato mwanafunzi wa Socrates, angesema nini kuhusu huu mpambano wa kifikra??. Kumbuka kwamba kuna wale wanao-lose mijadala kabla hata hawajajua wapo ndani ya mjadala!........looks like somebody bin someone, somewhere, lost already!!!!!!.
Go Eli and NY Giants!!.
 
Missed it again. Mkuu MKJJ utapandisha lini kijijini?
Ndio nasikiliza list ya Slaa...am catching up. Hee heee naona una watu studio wanakupigia makofi siku hizi kama Jerry Springer hehee....tamu.
 
Mazee Deef!

Muziki safi mkuu, yaani leo nimekula mziki kule kwa mazee Geeque, na sasa kwako safi saaan! keep it up!

My pleasure mkuu na shukrani. Hakikisha tu kazi inafanyika....maana nimesikia sikia balozi wetu bila kupitia kiredio hiki protokali hazifanyiki hahaaa....(joke).
Inaonekana wewe umefurahia ngoma za Sanghoma, Mkhomboti dizaini...
 
Ilikuwa ni makosa kwa Mwanakijiji kutokusema Lisu ni kiongozi wa chama cha siasa. Bahati nzuri baadaye alirekebisha na hilo mimi nimelikubali.

tatizo ni wewe kuassume kuwa nisingelimuuliza kuhusu mtazamo wa kisiasa au mimi sifahamu kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Chadema. Kama ungesikiliza hadi mwisho halafu ungekuta sijamuuliza basi ulikuwa na sababu ya kulalamika. Next time, kosoa baada ya matangazo, lakini kuassume kuwa kwa sababu fulani nisingewaambia watu kuwa Lissu ni kiongozi wa Chadema pia ni kuniunderestimate.. kuna vitu vingine unaviweka kama dramatic portion of the show..
 
My pleasure mkuu na shukrani. Hakikisha tu kazi inafanyika....maana nimesikia sikia balozi wetu bila kupitia kiredio hiki protokali hazifanyiki hahaaa....(joke).
Inaonekana wewe umefurahia ngoma za Sanghoma, Mkhomboti dizaini...

defunc.. mzee tunajaribu jaribu si unajua tena... kwa vile yalikuwa matangazo marefu I'll probably air them on tuesday or wednesday.. namalizia makala kidogo ..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom