Tundu Lissu: Ngeleja amelidanganya bunge

Napata maswali mengi kichwani mwangu, hebu hili bunge la 10 ni nini hatima yake? Na nini matumaini ya watz kwenye bunge hili?
 
Iwapo itafanyika reshuffle Ngeleja atakuwa majeruhi, naona aanze kupaki mizigo yake mapema.
Hawa mawaziri wababaishaji wajue Bunge hili ni la vijana wapambanaji tena vichwa! Wakumbuke kufanya homework yao kabla ya kukurupuka na majibu ya kijuujuu.
 
Tatizo ni kwamba hakuna wa kuwawajibisha wezi waongo katika hii nchi. maadili ya uongozi 0% ... .... ulizeni ni viongozi wangapi wametaja mali zao baada ya uchaguzi?
 
Mawaziri wote hudanganya bunge mara kwa mara. Ni wabunge tu huwa hawako makini na au walikuwa hawathubutu kuwaumbua mawaziri. Mwezi wa sita na saba ndo uongo mwingi zaidi. Chadema wanaweza kupata umaarufu sana kwa kufuatilia tu kauli za mawaziri bungeni.

Natamani angepatikana mtu anachambua sheria zote zilizotungwa na kusainiwa kipindi cha JK. Udanganyifu uliomo humo unatosha kuvunja bunge na serikali!
 
Hivi kwa utaratibu huu wa kila waziri anaposema uongo anatetewa na spika maana yake nini? Ule usemi kwamba Anna Makinda amepewa uspika ili kurahisisha mambo yao ndo huo tumeanza kuushuhudia. Ajue wazi kabisa historia itamsuta sana.
 
Iwapo itafanyika reshuffle Ngeleja atakuwa majeruhi, naona aanze kupaki mizigo yake mapema.
Hawa mawaziri wababaishaji wajue Bunge hili ni la vijana wapambanaji tena vichwa! Wakumbuke kufanya homework yao kabla ya kukurupuka na majibu ya kijuujuu.

Ndugu yangu huyu jamaa hawezi kujeruhiwa, katoka mbali na Rostam Aziz, ni wakina Rostam waliompa kazi pale vodacom na ndo hao waliompa kazi ya kusimamia maslahi yao pale nishati na madini. Hana chochote cha kufanya kule zaidi ya kusimamia maslahi yao, ndo maana hata January Makamba alitaka kumfunika.
 
Nadhani kuna kila sababu ya kuangalia uwezekano wa kuandaa maandamano makubwa ya kuelekea nyumbani kwa huyu mama spika kumuonyesha kuwa wananchi haturidhiki na utendaji wake wa kutumikia mafisadi badala ya walala hoi wa nchi hii.
 
utashangaa akileta ushahidi ataambiwa ampelekee spika ofisini!
Hilo la kwamba watamalizana ndani kwa ndani mbona Makinda ameshalisema leo. Soma hii taarifa:

TUNDU LISSU YAMKUTA YA LEMA

tundu-lissu.jpg

Na Mwandishi wetu,
Dodoma

"Alisema yeye Spika kwa kutumia vyombo vyake pamoja na kamati ya Maadili Mbunge huyo pamoja na Waziri Ngeleja wataitwa ili kila mmoja kubainisha ukweli wake na kisha yeye kutoa taarifa kwa Bunge."

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amempa siku nne Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuthibitisha kauli yake kuwa Waziri Nishati wa Madini William Ngeleja, amesema uwongo bungeni.

Akitoa uamuzi huo leo Spika Anne Makinda, Lissu anatakiwa kuthibitisha kwa kuwasilisha uthibitisho unaoonyesha Ngeleja amesema uwongo ifikapo Ijumaa wiki hii.

Spika Anne alisema kuwa pia, atatolea taarifa juu ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (Chadema), kudai Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema uwongo bungeni, katika Mkutano huu wa Bunge.

Katika tukio la jana Lissu aliomba muongozo wa Spika mara baada ya Waziri Ngeleja kujibu swali la mbunge huyo.

Katika Swali hilo la nyongeza mbunge Tundu Lissu alitaka kujua ni kwanini mwekezaji aliyepewa leseni ya kutafuta madini wa kampuni ya Shanta Maning kujenga kiwanja cha ndege katika maeneo ya wakazi bila kulipa fidia.

“Mheshimiwa Spika naomba kujua ni kwanini mwekezaji huyo amechukua ardhi ya wakazi kwa nguvu na pia kujenga uwanja wa Ndege katika eneo hilo” alisema Lissu.

Akijibu swali hilo Waziri Ngeleja alisema ujenzi wa kiwanja hicho pamoja na meneo yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo yapo kisheria na hivyo hakuna kosa kwa mwekezaji huyo kujenga kiwanja hicho.

‘’Mweshimiwa Spika napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Tundu lissu kuwa mimi mwenyewe nilifika katika eneo hilo 2008 na maeneo yote yapo kisheria” alisema.

Kufuatia jibu hilo Mbunge huyo Tundu lissu alioomba muongozo wa Spika kwa kutumika kanuni ya 63 (i) na 64 (iA) na kudai kuwa katika jibu lake Waziri Ngeleja amesema uongo bungeni.

Akizungumzia kuhusiana na suala hilo Spika alisema mbunge Tundu lissu atatakiwa kuandika maelezo yake na kuyawasilisha kwake ili yafanyiwe kazi.
Alisema yeye Spika kwa kutumia vyombo vyake pamoja na kamati ya Maadili Mbunge huyo pamoja na Waziri Ngeleja wataitwa ili kila mmoja kubainisha ukweli wake na kisha yeye kutoa taarifa kwa Bunge.

Ndio maana walimuweka makinda walilitambua hili. Pinda kadanganya wamempotezea leo hii Ngeleja kadanganya naye watampotezea.
 
Ndio maana walimuweka makinda walilitambua hili. Pinda kadanganya wamempotezea leo hii Ngeleja kadanganya naye watampotezea.
Nimewahi kuonya cdm wajipange na namna spika atavyokuwa anaitetea serikali tena penye uozo.sijui kama cdm wamejipanga kwa hili ili tusionekane wapiga kelele tu!
 
Just ask me-self, till when? Right now Tz, sarcastically, has turned everything good into a merely mavi. In most conuntries....uwaziri was/is a title with some dignity attached to it except Tz why? Rais na majority ya mawaziri wake ni aibu, Bunge nalo linaharakisha kukosa uhalali, in short...now ni uhuni mtupu. I'm mercifully tired.

Mapinduzi au mabadiliko chanya yana njia mbili. Aidha yaanzie ndani (yaani watawala, ambayo ni aghalabu sana kutokea) au yaanzie nje (watu/raia, taasisi za kiraia, au wapinzani (ambayo ni kawaida). Sasa CCM na serikali yake nadhani wanahimiza walio nje ya wigo wao wayalete hayo mapinduzi au mabadiliko.... kwa kutazama mambo yalivyo sasa.
 
Kweli mkuu,hawa watawala hawana hofu ya nguvu ya umma,wanaogopana wenyewe! Huwa sipendi kutamka hili lakini mpaka yatokee machafuko mazito nchi nzima ndio wataheshimu umma,wapo wanaodhani hatujafikia that situation kusababisha hayo,sasa sijui wanataka situation gani itokee zaidi ya hapa tulipo.inatia hasira mno udikteta ndani ya "democrasia"
 
Baada ya kuletewa ukweli what next with speaker Makinda?ushahidi wa Lema umeenda wapi?na huu ataupeleka wapi?

Uuupuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuzziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
tusisahau Naibu wizara ya ujenzi nako ameelezwa ya kwamba amedanganya ya kwamba barabara toka dodoma hadi sehemu ya kwanza ya mgao ktk barabara ya dodoma babati na hili nalo spika akayeyusha jap (nwwuj) aliyeyusha pia
 
Back
Top Bottom