Tundu Lissu nae!!

Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.

Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.

Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.

Ni ushauri tu lakini

i have to prove that firsthand!
 
kwahiyo wewe unaona ni kawaida tu, yaani mbunge yuko kwenye kikao, afu anapewa sumons afu akae kimya, spika alitakiwa kuwa na busara, kwakumwambia kwasababu uko kwenye kudiscuss sensitive issue, basi naahirisha mjadala. Wana jf sisiem ni wajanja sana, walijua bila kumwondoa kwenye mood mh. Lissu ingekua balaa, kwahiyo ni hila za kimakusudi zilifanywa na sisiem kumdhoofisha lissu. Lakini pamoja na hilo kama mwanasheria aliebobea bado aliendelea kujaribu kupambana. Katika mapambano silaha yoyote ile unaitumia hata kama ni fimbo, jiwe au tawi la mti.

sure mkurugenzi!
 
wewe umetumwa nini,yaani kwa namna yoyote mnatafuta kuwarudisha nyuma wapigania uhuru wetu,wewe sawa na wabunge wengi wa chama chako nadhani mnafikiri kwa makalio wala si kichwa kama unahisi Tundu kakurupuka wewe umefanyaje!!mwanaume mzima akili kama za Kilango!!umenchefua tu yaani!

...hata mie nataka kutapika!!!
 
Tatizo, hata bunge lenyewe linaendeshwa kishabiki Zaidi kuliko kufuata taratibu; na wakati mwingine waheshimiwa uchwara wanaropoka utafikiri mabinti wa uswasi walio kata tamaa na maisha; hawatafakari ,awafikilii nini kinatoka vinywani mwoo;

Kwa Bungew hili; taifa litadidimia mara dufu; Ni heri mara billions bunge la Mzee Six
 
kwa hiyo kuku anzaaa yai au yai linazaa kuku??kati ya summons na kuomba muongozo wa spika nini kilianza??

unaudhi
unakera
unaleta hasira
nyambafuuuuuu

hizi ndizo busara zangu zakwako zikowapi??wewe

to be honesty kaumaza anapost pumba, na mkuu son of soil punguza jaziba, ban inaweza kukukumba
 
siku hizi JF badala tushauriane na kurekebishana tunapokosea watu wanakutusi na kukukejeli. This is not fair, kama sred haikugusi na huitaki ipotezeee tu....napata wasiwasi na maana halisi ya great thinkers ya JF
 
Jamani hapa hoja hujibiwa kwa hoja, matusi na kashfa si sehemu ya kujenga hoja, kama huna la kuchangia nibora uipotezee thread kuliko kuongea ushabiki na upenzi kama wa simba na yanga.

Kama sijakose hii ni mara ya nne sasa toka siku ya bunge la kwanza kumona lisu akiomba muongozo kwa jazba na kukurupuka na mara zote mama makinda amekuwa anambeat vibaya kwa kuonyesha hajui anachoomba.
mfano jana amepewa samansi kimakosa wakati bunge linaendelea lakini kama msomi wa sheria angeatafakari kwanza namna ya kuhandle issue ile na si kukurupuka na kuanza kuomba eti dharura, na alipotakiwa asome kifungu alichemka kwanza akaambiwa kaa chini soma jipange tena, na hata baada ya kujipanga akasoma kifungu ambacho aliulizwa je kinafit kwa unavyoomba, akabaki ametoa macho.

Wito bado mapema mno atulie, au achukue mifano ya wenzake zito na dr walivyofanya

Hivi wewe unapopigwa jiwe unatafakari kwanza au unakwepa .... kama utalala chini; utaruka; or whatever???? anza kuwalaumu hao waliompa samansi kimakosa - walikuwa na maana gani???? ilikuwa imepangwa - when you are provoked you can act anyhow ...........
subiri wakosee kimakusudi kwa Zitto na Dr. ndipo utajua kuwa safari hii UPINZANI UMEAMUA KWANI CCM WAMEZIDI MNO KUFANYA HILA NA UJANJA UJANJA ..... ujanja wa kuiba kura wanaleta hadi bungeni .............very strange!! - just my comment to u r comments.
 
Watanzania tuna upeo mdogo sana wa kutafsiri mambo. Tunatafsiri mambo mengi kwa vey narrow premises.Mtu akihoji mamlaka makubwa ya kikatiba ya Rais ya kuteua watu wengi kwenye nafasi tofauti za uongozi anaambiwa anahoji mamlaka ya JK wakati urais ni taasisi ya kushikwa na mtanzania yeyote mwenye sifa kwa nyakati tofauti chini ya katiba ile ile.

Hoja ya Mheshimiwa Tindu Lissu ilikuwa kuhoji kitendo cha hadhi na mamlaka ya Bunge kuingiliwa na mtu kutoka nje ambaye ni wa mhimili mwingine wa dola. Hoja hii ina uzito wa kulifanya Bunge lihalalishwe kuahirisha kujadili hoja iliyopo na kujiadili hoja hiyo ya kulirudishia Bunge heshima yake.

Kuna wajinga wame-construe hoja hiyo very narrowly kwamba inamhusu Mheshimiwa Tindu Lissu personally wakati inaihusu taasisi nzima ya Bunge. Kwa bahati mbaya sana miongoni mwa wajinga hao ni kiongozi mwenywe mkuu wa taasisi iliyodharauliwa, yaani Spika wa Bunge! Kwa mwendo huu Watanzania tunahitaji elimu bora kwani tuko dull kichizi.
 
Kuna dhana mbili za kuangalia hapa. TL pamoja na Spika wote wamekurupuka kwa mantiki kwamba TL hakujiandaa kutoa hoja kwani alionekana kubabaika. Pili Spika alionekana kuwa bias sana na maamuzi yake, hakutaka ku-extract kutoka kwa mlalamikaji huenda angegundua mengi, unless atuambia picha nzima alikuwa anaifahamu.
Dhana ya pili ni taswila gani Spika angependa kuijenga dhidi ya Bunge analoongoza. Je, ni bunge la kubezwa? Kama ambavyo summons ya TL ilivyotolewa! Je, ni bunge linaloweza kukiwajibisha chombo chochote kwa kuzingatia sheria zilizopo?
Naamini TL alikuwa sahihi kuonyesha hofu yake juu ya Bunge kudharauliwa (kwa kuzingatia kanuni zilizopo). Basi lilikuwa ni jukumu la Bunge kumtoa hofu memba wake japo kwa dk 10.
NB: kuitwa mahakamani si jambo dogo ndugu zangu!
 
Kwa kitendo walichofanya hiyo mahakama kuu ya Dodoma sio fair, inakuaje mbunge anapelekewa summons ndani ya kikao? kwanini wasingemsubiri atoke nje? na position ya Tundu Lissu kama Chief Whip anatakiwa awepo mjengoni wakati na anatakiwa awe na concetration kubwa ya kuhandle isssue maana yeye ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani ijnakuaje wanaanza kumtumia virus {summons}. au ndio lengo lao CCM kumzinguzingua na aonekana ni mkurupukaji na hafai... kwa hili hawakufanya haki na ukizingtia Bunge ni moja ya mihimili mitatu ya dola inayofanya kazi bila kuingiliwa inkuwaje mahakama inaliingilia bunge?
Uliyepost hii thread jaribu kufikiri ndio kama wewe, mfano upo kwenye sherehe halafu hapohapo unatumiwa ujumbe uende shambani.... utajisikiaje???
 
Acheni ujinga mheshimiwa alichemka. Alitaka kusikilizwa kwa manufaa ya uma. Uma wake na uma wa bunge zima ni upi. Was that important. Mimi huku niliko nilishangaa kuona ametoa mipua yake ati anataka kuahirisha bunge kwa umaarufu wa jazba. CHADEMA wasipo angalia wataonekana wacheza majoka bungeni na nje ya bunge. Wasomi waliopo CHADEMA wajifunze kujenga hoja kwa utafiti na kuondoa jazba kama za kijinga. Bungeni ni mahali pa maana bwana. Sio mahali pa mijadala ya kitoto....unauliza kirefu cha SADC bungeni kwa manufaa ya nani??
 
Acheni ujinga mheshimiwa alichemka. Alitaka kusikilizwa kwa manufaa ya uma. Uma wake na uma wa bunge zima ni upi. Was that important. Mimi huku niliko nilishangaa kuona ametoa mipua yake ati anataka kuahirisha bunge kwa umaarufu wa jazba. CHADEMA wasipo angalia wataonekana wacheza majoka bungeni na nje ya bunge. Wasomi waliopo CHADEMA wajifunze kujenga hoja kwa utafiti na kuondoa jazba kama za kijinga. Bungeni ni mahali pa maana bwana. Sio mahali pa mijadala ya kitoto....unauliza kirefu cha SADC bungeni kwa manufaa ya nani??

ilikuwa ni interview ile mkuu, hata kama wewe unapoenda kufanyiwa usahili sehemu ni lazima utakuwa na detail kidogo kuhusu ofisi unayoenda kuomba kazi.... bado hujawa mzoefu wa kufanyiwa interview.. thats why unakurupuka na kuandika ujinga hapo kwenye highlight.... na ilikuwa trick nzuri sana si unaona alivyochemka?
 
Tundu Lissu na wenzake ma Novice wa Chadema wanatafuta Cheap popularity bungeni hawajaenda pale kutatua matatizo ya wananchi wao.
 
Mheshimiwa huyu wa Singida asipoangalia vema umaarufu wake utamomonyoka vibaya. Mfano. kwa kitendo chake cha jana bungeni kuomba bunge liahirishwe kwa kuwa jaji amem-issue summons ni kituko cha ajabu kuweza kufanywa na mwanasheria na msomi mahiri kama yeye.

Ili kuweza ku-maintain status yake ni lazima afanye utafiti kwa kila anachotaka kukifanya na kukiongea ktk ulimwengu huu wa siasa. Akitanguliza ushabiki na kutaka kujenga jina haraka haraka inawezekana mwaka 2015 jimbo lake likawa na mbadala.

Aige mwenendo wa Bosi wake Dr Slaa. Kila alichokuwa anataka kukiongea(Bungeni) alikuwa anafanya utafiti wa kina na akikiongea kinakuwa na mashiko.

Ni ushauri tu lakini

Hapo blue imekaaje? na hapo red je? hujui unachozungumza mkuu pumzika....
 
Tundu Lissu na wenzake ma Novice wa Chadema wanatafuta Cheap popularity bungeni hawajaenda pale kutatua matatizo ya wananchi wao.

na wabunge wa CCM wameenda kufanya nini? unapozungumza jambo uwe na facts za kueleweka, hebu angalia kazi inayofanywa na John Mnyika, Halima Mdee ( mpaka wnyekiti serikali za mitaa wanazuia wannchi wasiende kutoa kero zao), ongea ukiwa na uhakika sio kuongea kishabiki zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom