Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 8,635
- 7,918
Mkataba kama unavyosema wewe wa mwaka 1964, siyo sheria, Sheria inaitwa "ACTS OFUNION OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR, 1964."Swali la Tatu: Je, Mkataba Ulijengwa kwa Nguvu Ganui ya Kisheria?
Jibu ni kwamba, Mkataba wa Muungano, 1964, ulichukua nafasi ya Sheria Mama, kwa matarajio kwamba, Muungano wetu utapewa nguvu za kikatiba ndani ya mwaka mmoja; Ni hapa ndugu Kobello unapoanza spins zako; Nitafafanua; Unaelezea vizuri sana yaliyojiri huku aidha kwa kujua au kutojua, unaruka mambo mengine muhimu zaidi ya kusaidia kufungua kiini macho hiki cha muungano; Kwa mfano, hoja yako kwamba Katiba ya Tanganyika ilikubaliwa ndio iwe Katiba ya Muda, hakuna anayebisha hili, mpaka hapa tupo sawa; Lakini hauelezei watanzania waliopo humu kwamba, ili hilo lifanikiwe, katiba ya Tanganyika ilitakiwa ifanyiwe marekebisha kwanza, bila ya hivyo, Mkataba wa Muungano, 1964 ungeendelea kuwa nguzo pekee ya kuhalalisha muungano;
Kwa makusudi au kwa kupitiwa, hautaki kujadili yaliyomo katika Mkataba wa Muungano, 1964, hasa pale unapoweka masharti juu ya matumizi ya Katiba ya Tanganyika kuwa Katiba ya Muda ya Jamhuri Mpya ya Muungano wa Tanzania (katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja). Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, ibara ya tatu inasema hivi:
(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:
a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;
c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.
Bila ya Katiba ya Tanganyika kufanyiwa marekebisho katika maeneo haya, ili kuupatia Muungano wetu Uhalali na Nguvu ya Kikatiba, Katiba ya Tanganyika isingekuwa na uhalali au nguvu ya kutumika kama Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na badala yake, ingebakia na nguvu yake kwa upande wa Tanganyika, kama ilivyokuwa kabla ya Muungano baina ya taifa huru la Tanganyika na Zanzibar; Kwa maana hii, basi Mkataba wa Muungano, 1964, ungebakia kuwa ndio nyaraka peke yake ya kuhalalisha muungano wetu, hivyo kuendelea kuchukua nafasi ya Sheria mama katika kipindi cha mpito;
Mbali na marekebisho haya ya Katiba ya Tanganyika ili ipate nguvu za kikatiba kuendesha Muungano wakati wa kipindi cha mpito, pia kulikuwa na sharti lingine ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, sharti ambalo lilikuwa ni muhimu kuliko yote, kwa maana ya kuupatia Muungano wetu sasa nguvu kamili na uhalali wa kisheria wa kudumu; Sharti hili ambalo pia unakwepa kulijadili kwa mtindo wa ku-spin issues, lipo katika kipengelea cha saba cha Mkataba wa Muungano ambacho kinasema hivi:
vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Nadhani sasa tupo tayari kudadisi kwa undani zaidi kuhusu Mkataba wa Muungano, 1964, na nguvu yake ya kisheria;
Na hiyo act ni mjumuisho wa "Union of Zanzibar and Tanganyika Law" kwa upande wa Zanzibar na "Union of Tanganyika and Zanzibar Act, 1964. hizi ndiyo sheria zilizoanzisha muungano.
Ukisema articles of the Union ni sheria, unakuwa upo kisiasa zaidi na si kisheria ... now lets go