Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Mchambuzi,

Asante sana kwa kuanzisha thread ambayo ya kuelemisha na kufikirisha. Nimesoma post zote na za wachangiaji wengine, mchango wako na wa wengine binafsi umenifungua sana. Sasa naona si sawa kuwaambia ndugu zetu wa Zanzibar kuwa tuwaache wajitenge kama baadhi ya michango ya thread nyingine tunavyopendekeza, nafikiri uelewa wa masuala ya muungano ni mkubwa kwa wenzetu wa Tanzania visiwani.

Shukrani mzawa halisi;

Naomba nikiri kwamba hata mimi kwa muda mrefu nilikuwa naishi katika hali ya kiza kingi sana huku nikiamini kwamba matatizo ni ndugu zetu wa zanzibar, kumbe ni kinyume chake; Kwa kweli ili mtu uelewe kiini macho hiki, ni lazima utumie muda mwingi sana kusoma na kutafakari mambo mbalimbali; ukitegemea wanasiasa wa bungeni ndio wakusaidia uelewe nini kinaendelea, itakula kwako;

Upo sahihi kuhusu uelewa mkubwa wa ndugu zetu wa ZnZ; Na napenda kuwapongeza viongozi wao kule visiwani ambao katika kipindi chote cha muungano, walikuwa wana waelimisha mambo mengi juu ya muungano huu, tofauti na sisi ndugu zao wabara ambao tulikuwa tunapigwa blah blah nyingi tu; Najua itachukua muda sana kwa UMMA wa watanzania kuelewa suala hili hivyo kufanya maamuzi muhimu, na kutokana na udhaifu huu, wananchi watapigwa blah blah nyingi sana wapinge hoja ya Tanganyika, na wataishia kutuona sisi wenye mwamko wa tanganyika kama ukoma, hivyo kukaa mbali kabisa na sisi; ikitokea hivyo, itakuwa rahisi sana sana kwa the state kutugeuza sisi kuwa their political enemy number one; hizo zitakuwa ni faida za the state za muda mfupi tu kwani hata ikichukua hadi mwaka elfu mbili na mia moja (2100) kwa vitukuu vyetu kuja funguka baadae na kurekebisha taifa lao, siku hiyo itakuja;

Until then, let them politicians enjoy the ride ya kupeleka nchi yetu kuzimu, kwani in the long run, we will all be dead;
 
Mkuu Mchambuzi ni wazi tunakubaliana sana kwenye mengi.However kuhusu mapinduzi,ni wazi kwamba baada ya uchaguzi wa huko zanzibar wa mwaka 1961 mwezi wa january,ASP ilishinda uchaguzi kwa kupata viti 10, ZNP viti 9 na ZPPP viti vitatu.Kwasababu ASP haikufikisha nusu ya kura,ikabidi kutakiwa iwepo serikali ya mseto.Hatahivyo ZPP na ZNP viliungana,na makubaliano(chini ya mwingereza), yakafikiwa kuwa iwepo serikali ya muda(bila ya ASP kushirikishwa) hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika,ambapo ulipangwa kufanyika hapo june 1961(kiukweli Zanzibar ilikuwa haitawaliki).

Kumbuka Abdurahman babu yeye alikuwa ni mwanachama wa ZNP,na kwahiyo kutokana na muungano wao na ZPP,wao ndiyo waliokubaliwa na waingereza kuunda serikali ya mseto.Ambayo iliongozwa na Juma Shamte kama sikosei.Lakini tatizo lilikuja baada ya mwingereza kumshauri awatenge kina Babu kutokana na misimamo yao ya kikomunisti.

Hilo la kutengwa ndilpo lililosababisha Babu akaanzisha chama chake cha UMMA Party,ambapo sasa walishirikiana na ASP kwenye mapinduzi(MORE CREDITS WANAPEWA ASP),lakini chama hicho kikavunjwa rasmi mara baada ya mapinduzi na viongozi hao(kina Babu,Hanga et al),pamoja na wafuasi wao wakajiunga rasmi na ASP chini ya uongozi wa Karume.

Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kiasi kikubwa ulikuwa hauepukiki,hilo kwa kweli historia itamjudge mwalimu Nyerere pamoja na Karume.Chama cha Karume,kilikuwa na wazanzibari weusi,na kilipigwa vita na hivyo vyama vingine na hata mwingereza alishirikiana na Sultan kuwapiga vita(thanks for the revolution),maana hata huo uhuru wa december 1963,haukuwa uhuru wa watu wa Zanzibar,bali ni madaraka ya nchi yalikabidhiwa kwa Sultan.However jambo la msingi hapa,ni kwamba TANU na ASP vilikuwa vikishirikiana kutokana na hilo la bias ya mkoloni na Sultani,ukweli ukiwa kwamba waarabu na wazungu ndiyo walikuwa wakipendelewa na waafrika kuwa daraja la chini.Hayo yalikuwa mojawapo ya sababu za ushirikiano mkubwa kati ya TANU na ASP.

Sina shaka kabisa kuwa nia ya mwalimu ya muungano ilikuwa njema kabisa,kwasababu mwalimu mwenyewe alishawahi kunakiliwa(Gazeti la Tanganyika Standard la desemba 1964), akisema kuwa ni bora uhuru utolewe kwa block nzima ya Afrika mashariki kama muungano mmoja wa kisiasa,na alikuwa radhi kuona hilo likifanyika hata kama ni kwa kuchelewesha uhuru wa Tanganyika.Maneno hayo aliyazungumza kwenye ile iliyokuwa jumuiya ya wapigania uhuru wa Afrika mashariki na kati(Pan African Freedom Movement fo East and Central Africa-PAFMECA).

Kwenye muungano huu kuna confusions nyingi sana,na hilo siwezi kumlaumu sana mwalimu kwasababu yeye alitaka kuu save muungano huu by any means.Muungano huu una "Hati ya muungano",(Iliyozaa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar),ambayo ndiyo ilitiwa saini na mwalimu pamoja na Karume,hati hiyo ndiyo ilitumika kwenye uundaji wa katiba ya muungano hapo 1977(ambapo sasa iliitwa jamhuri ya muungano wa Tanzania), pamoja na katiba ya Zanzibar 1984.

Lakini pia kabla ya hapo,tukumbuke pia kwamba mwaka 1964,bunge la Tanganyika lilipitisha sheria ya muungano,na zikathibitishwa na baraza la wawakilishi,lakini bado ukweli unabaki kwamba hawakushirikishwa kwenye utungaji wa sheria hizo.Tatizo walilokuwa nalo Zanzibar,ni kwamba kulikuwa hakuna katiba,bali nchi ikiongozwa na presidential decrees,ikiwa na maana kwamba atakachosema Karume ndiyo sheria,na yeye ndiye mwamuzi wa mwisho on almost everything.

So again,hapo wa kulaumiwa si mwalimu,kwasababu inawezekana Karume ndiye aliyetoa hiyo amri kuthibitisha sheria hizo za muungano kwasababu Karume alikuwa desparate kufanya lolote ili asipate shida ya kuitawala Zanzibar ambayo kiukweli ilukuwa haitawaliki.Na alikuwa akiwaogopa sana mahasimu wake kina Babu,Hanga na wengineo.

Kwahiyo kazi kubwa ya sheria hizo za muungano,ilikuwa ni kuithibitisha ile hati ya muungano pamoja na kutabanaisha muundo wa muungano pamoja na mgawanyo wa madaraka.Na mwaka 1964,mabadilishano ya hati za muungano yalifanyika,Zanzibar ilipata wawakilishi wa baraza la mapinduzi kwenye serikali ya muungano, na walikuwa saba(Abdulrahman Babu,Idris Abdulwakil,Kassim Hanga,Sheick Nasir Moyo,Sheick Aboud Jumbe,na Sheick Hasnu Makame)

Kwasababu Zanzibar walikuwa hawana katiba,ndipo walipo i adopt katiba ya Tanganyika ambayo lifanyiwa marekebisho hapo mwaka 1965,na ndipo ilipokuja na yle maazimio 11.

Kwa kifupi mkuu,mimi nwashangaa sana wazanzibari wasiojielewa,ndiyo maana mwalimu aliwahi kusema nje ya Tanzania,hakuna Zanzibari,na ni ukweli mtupu,hao kina Jussa wanaopigia kelele wakristo,kesho muungano ukivunjika,watatafuta mchawi mwingine kwasababu kisiwa kile hakipo na hakitatawalika nje ya muungano,huo ni ukweli mtupu.

Wataanza kubaguana wapemba na waunguja,weusi na waarabu,kwasababu dhambi ya ubaguzi imo ndani ya damu zao.Na Sultani naye hatocheza mbali,na kwa kawaida,lazima yeye ndiye atakayeshinda,lakini haina maana kwamba amani itakuwepo,kwasababu pia kuna wale weusi ambao lazima watatengwa kwasababu hawatakuwa na haki sawa na waarabu etc.

It is a very volatile situation,na shida ndipo ilipo.Tatizo kubwa ni kwamba sidhani kama muungano wa serikali tatu utatatua tatizo lolote kama serikali hiyo(ya muungano) haitakuwa na mamlaka ya juu zaidi ya yale ya serikali za Zanzibar na Tanganyika kwenye issue za ulinzi na usalama na mambo mengine ambayo yanalalamikiwa kwasasa hivi kwamba yaliongezwa kutoka kwenye yale 11.Kwasababu kuna issue ambazo ili kuendelee kuwepo na amani,ni lazima zibakie chini ya serikali ya muungano,jambo ambalo sidhani kama wazanzibari wanaopinga muungano wanakubaliana nalo.

Issue hii ni issue inayohitaji mjadala haswa.Lakini pia ni muhimu tusipoteze muda mwingi na rasilimali ku fix the unfixable.Ni wazi mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa,na hivyo ni muhimu tuende na wakati tujadiliane upya kuhusu muungano wetu,tuufanyie marekebisho ama hata kuuvunja ikibidi.
 
Ni kweli, autonomy marekani ipo highly debatable lakini mengi yanapotezewa na states husika kutokana na ukweli kwamba, kuwa a member state in the US kuna faida nyingi kuliko hasara; Ni faida za namna hii, iwapo ndugu zetu wanzazibari wangekuwa na wao wanazipata , mgogoro huu usingefikia hali ya leo;
Zanzibar wana legislature, executive na court system yao.Hii ni sawa na Texas au California.Zanzibar wana state bank, state troopers, revenue authority na rights zote ambazo state kama Texas na California wanazo. Ukiangalia masuala 22 ya muungano, yote yapo under federal law Marekani. Kwa hiyo, based on US as an example, Zanzibar wana nafasi ya kutumia mfumo huu uliopo kupata faida ambazo States za Marekani, au hata India wanazipata.
Kitu ambacho Zanzibar wanakitafuta ni "complete autonomy"
Sidhani kuwa Zanzibar inaisikitikia Tanganyika kwa kukosa autonomy, bali inailalamikia kwa kuchukua baadhi ya vipengele ambavyo vinainyima Zanzibar complete autonomy.

Kuwepo kwa serikali tatu, siyo kwamba kutaipa Tanganyika autonomy, bali kutaiongezea Zanzibar sauti kwenye meza kuu ya muungano. Kama tatizo ni Federation, bado population is the decisive factor and not the economy. Population ya Mainland ni mara kumi ya Zanzibar (just came up with this comparison, for the sole purpose of elaboration). Kwa hiyo federation of two countries is a loss to Tanganyikans.
Kwa hiyo mgogoro hautokani na faida ambazo wazanzibari wangezipata, bali ni kundi nusu la wazanzibari ambao mapinduzi kwao yalikuwa ni njia ya kiuonevu ya kupata uhuru.

Kuhusu katiba ya sasa, tufahamu yafuatayo:

Kwanza, Kamati Maalum ya CCM ilichukua nafasi ya tume ya katiba; Pili, Kamati Maalum ya CCM ilichukua nafasi ya Baraza la kutunga Katiba, na hii ni kama ilivyotajwa ndani ya mkataba wa muungano, 1964, lakini kwa sababu zisizoeleweka, masharti haya yakachakachuliwa na sheria mpya iliyoitwa Sheria ya baraza la kutunga Katiba, 1965; kwa kifupi, misingi iliyowekwa ndani ya Mkataba wa Muungano 1964, mkataba ambao haukutaja neno "shughulii/maamuzi ya kisiasa", haikutaja "chama cha siasa", haikutaja "TANU", "ASP", wala "CCM", lakini bado CCM hijacked Mkataba wa Muungano, 1964 pamoja na yaliyomo, na badala ya baraza la kutunga katiba kupitisha katiba per Articles of the Union, 1964, Bunge la CCM likaipitisha katiba mpya ya 1977; Kabla sijajibu swali lako kuhusu bunge kukiuka katiba ya 1977, nikuulize kwanza, je:

Katiba unayoizungumzia hii ina uhalali gani iwapo tutakubaliana kwamba Mkataba wa Muungano, 1964, ulikuwa ndio sheria mama? Lipi ni tatizo kubwa hapa linalopelekea hali ya nchi yetu kuchafuka kutokana na mgogoro wa muungano – Ukiukwaji wa Katiba ya 1977 au Ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964?
Huo ulikuwa ndiyo mfumo wa kisiasa wa wakati ule. Kumbuka kuwa Halmashauri kuu ya Tanu na baadaye CCM ndiyo iliyokuwa na Madaraka, na ndiyo ilyokuwa na uwezo wa kuitisha constitutional assembly. Kwa hiyo, sioni tatizo when CCM hijacked the wholke process kwa sababu ndiyo chombo kilichokuwa na madaraka. Relevance ya CCM/TANU NEC kuwa na madaraka hayo yalielezewa vizuri sana na Pius Msekwa kwenye toleo la sita la "Taamuli" kwenye article yake ya Towards party supremacy:The changing pattern of relationship between The National Assembly and NEC of TANU before and after 1965.

Apparently watanzania wengi tulikuwa hatujui relationship between the legislature and the National Executive Committee Pre and post 1965.
katiba kutokuwa halali hilo siliungi mkono, ila naunga mkono udogo wa katiba ya 1977 kwenye kuhodhi authority ya kurekebisha vipengele vya muungano. Hilo lilikuwa lipo chini ya NEC na kwa sasa hivi lipo chini ya wananchi, ambao kwa upande mmoja hawatakuwa na nia ya kuuendelkeza muungano kama utaupa upande mmoja nguvu zaidi based on sovreignty ya upande huo.

in my humble view, solution ni shirikisho, na ndio maana hata federation in the United States, na hata Russia kwa kiasi fulani, mambo yao yanakwenda vizuri, na member states na wananchi wao wanaona faida nyingi za kuwepo.
Kwa mtazamo wako, unaona ni sahihi kweli kwa Rais wa Tanganyika kuwa pia Rais wa JMT? Inawezekana, lakini maelezo yake yatakuwa yamejaa kiini macho kuliko uelewa;

Vinginevyo, huu ni mzigo mkubwa sana kwa Rais, lakini anaweza kupunguziwa lawama hizi chini ya mfumo wa serikali tatu – shirikisho;
Mfumo wa shirikisho unategemea na asili ya watu waliopo na malengo yao kiuchumi. Pia mfumo wa shirikisho upo extremely complicated to be used as a general term. Kwa kuwa umemaanisha serikali tatu, sidhani kama umefikiria kwa undani maslahi ya wananchi wa Tanganyika. Kwa sababu ukiangalia, itabidi serikali ya Tanganyika ipoteze electorate power au serikali ya Zanzibar iongeze representative power. Something tht is not beneficial to Tanganyika .

By the way, on a second note .... there's no Tanganyika, so when the president makes decisions, he does it for Tanzania. The problem is more executive than systemic.
 
Kuna hoja ipi hapo?

Ungeuliza kwanini Nyerere aliweka muungano usioeleweka, ningekuelewa.

Tanganyika iko wapi?

Not Nyerere ni CCM uiteteayo na ndio maana tunasema kuitetea CCM kwenye hoja unahitaji uwe na akili za maiti
 
Not Nyerere ni CCM uiteteayo na ndio maana tunasema kuitetea CCM kwenye hoja unahitaji uwe na akili za maiti

Muungano wa Nyerere na Karume ulianza kabla ya CC na ndiyo huohuo ukazaa CCM kwa kuunganisha vyama vya Afro Shirazi Party na TANU. Kama huelewi ni bora uulize kuliko kukurupuka.
 
Mkuu jmushi1,

Ni kweli tunakubaliana katika mambo mengi ya msingi; Nakubaliana na hoja yako kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya mapinduzi; Vile vile naunga mkono hoja yako juu ya nia njema ya Nyerere kuhusu muungano wetu, na hili nililisema katika post namba moja ya mjadala huu; Kwahiyo katika hili, mtazamo wetu pia upo sawa; Umezungumzia kauli za Mwalimu alizozitoa katika mazingira ya PAFMECA; Kuongezea tu, kwamba Mwalimu alinukiliwa na Gazeti la Tanganyika Standard la tarehe 16/11/1964 akisema yafuatayo baada ya kikao kile ya PAFMECA kule Addis Ababa, mwaka 1960:

"Wengi wetu tunakubali bila ya hoja ya shirikisho la nchi za Afrika Mashariki ni jambo linalokubalika; Tumesema hayo kwa imani kuwa mipaka ya nchi iliyopo sasa imetengenezwa na mabeberu, na sio sisi wenyewe, na katika hali hiyo basi ipo kama kizingiti kwa muungano baina yetu; Lazima tuikabili ofisi ya makoloni na kudai uhuru sio wa Tanganyika, na baadae Kenya, Uganda na Zanzibar kila nchi peek yake, bali uhuru tuudai tukionesha sote ni wamoja kisiasa;"

Katika hili tunajifunza nini? Muhimu hapa ni mawili: Kwanza, kwa maneno yake mwenyewe, ndoto ya Mwalimu ilikuwa ni shirikisho/federation state of East Africa ambayo ingejumuisha Zanzibar; Pili, kwa Mwalimu,, Zanzibar ilikuwa ni nchi huru kama ilivyo Kenya, Uganda, na Tanganyika; Msisitizo hapa ni kwamba Mwalimu alitaja Zanzibar katika context of Federation, not Unitary System, na hivyo ndivyo Mkataba wa Muungano, 1964 ukalenga kutimiza;
Kuna kauli nyingine muhimu hapa ya Mwalimu ambayo pengine wale wapinga muungano wataipenda; Ni kauli Nyerere aliitoa na ikachapishwa na Gazeti la Observer la Uingereza, April 20, 1968, miaka minne baada ya muungano:

"Iwapo UMMA wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha; Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana"

Swali linalofuata hapa ni JE: Sababu za baadhi ya wazanzibari kuukana muungano wetu nje ya mapungufu yaliyopo ambayo yanachangiwa sana na ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964, je pia kuna mkono wa influence au ushawishi kutoka nje ya nchi? Kama jibu ni ndio, mimi naungana na Mwalimu kwamba Muungano uvunjwe leo hii, iwapo tu, uamuzi wao unatokana na ushawishi kutoka nje, kwani hili litakuja kutuletea balaa;Vvinginevyo kama tatizo ni mgogoro tu wa kikatiba na ukirekebishwa wazanzibari watakuwa na furaha kuendelea na muungano, basi turekebishe tatizo hili, hasa kwa kuangalia kwamba – Je, since the inception ya Mkataba wa Muungano, 1964, tumejikwaa wapi?

Lakini pia kabla ya hapo,tukumbuke pia kwamba mwaka 1964,bunge la Tanganyika lilipitisha sheria ya muungano,na zikathibitishwa na baraza la wawakilishi,lakini bado ukweli unabaki kwamba hawakushirikishwa kwenye utungaji wa sheria hizo.Tatizo walilokuwa nalo Zanzibar,ni kwamba kulikuwa hakuna katiba,bali nchi ikiongozwa na presidential decrees,ikiwa na maana kwamba atakachosema Karume ndiyo sheria,na yeye ndiye mwamuzi wa mwisho on almost everything.
Ukitumia muda kuelewa kwa undani masharti ya muungano sehemu ya PILI hadi SITA, utaelewa tatizo lilitokea wapi;

Lakini pia una hoja ya msingi kuhusu Karume kwani inavyosemekana, muungano chini ya utawala wake ulionekana hauna tatizo kwa sababu mbili (kwa mujibu wa Shivji): Moja, Zanzibar waliendelea kuwa na chama chao cha siasa yani ASP; Mbili, Karume alipuuzia constitutional restrictions on his power;

So again,hapo wa kulaumiwa si mwalimu,kwasababu inawezekana Karume ndiye aliyetoa hiyo amri kuthibitisha sheria hizo za muungano kwasababu Karume alikuwa desparate kufanya lolote ili asipate shida ya kuitawala Zanzibar ambayo kiukweli ilukuwa haitawaliki.Na alikuwa akiwaogopa sana mahasimu wake kina Babu,Hanga na wengineo.

Mimi nadhani wa kulaumiwa sio Mwalimu wala Karume, bali ni kuangalia mazingira mazima na kujaribu kubaini ni wapi tulijikwaa, hasa sababu zilizopelekea Mkataba wa Muungano, 1964, uanze kuchakachuliwa; Tusisahu pia kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa chini ya katiba ya muda kwa miaka 12 mfululizo (1965-1977), pia kutokana na sababu kwamba Karume aliweka wazi kwamba hapatokuwa na uchaguzi Zanzibar kwa miaka hamsini ijayo; baada ya karume kufariki mwaka 1972, ndipo mchakato wa katiba mpya ukaanza, na miaka mitano baadae Katiba Mpya ikazaliwa lakini hili liliwezekana baada ya TANU na ASP kuungana, vinginevyo CCM isingeweza kufanya iliyoyafanya juu ya Katika ile, lakini na Muungano kwa ujumla;

Kwa kifupi mkuu,mimi nwashangaa sana wazanzibari wasiojielewa,ndiyo maana mwalimu aliwahi kusema nje ya Tanzania,hakuna Zanzibari,na ni ukweli mtupu,hao kina Jussa wanaopigia kelele wakristo,kesho muungano ukivunjika,watatafuta mchawi mwingine kwasababu kisiwa kile hakipo na hakitatawalika nje ya muungano,huo ni ukweli mtupu.

Nje ya Tanzania hakuna Zanzibar? Mwalimu alisema hivyo kweli? Basi hilo lilinipita, vinginevyo sikubaliani na hoja hiyo; Ni kama kusema bila ya Ridhiwani, Hakuna Jakaya; Kauli hii sio sahihi, inatakiwa iwe – Bila ya Jakaya, hakuna Ridhiwani kwa maana ya kwamba, Ni Jakaya ndiye aliyemzaa Ridhiwani, bila ya hivyo, Ridhiwani asingekuwepo katika dunia ya leo; Same applies to Zanzibar na Tanzania; Nyerere itakuwa alijichanganya kwani ukisoma hauli yake niliyoweka kule juu kuhusu kikao cha PAFMECA mwaka 1960, Mwalimu aliitaja Zanzibar sambamba na Tanganyika, Kenya na Uganda; Jina Tanzania halikuwepo; isitoshe, Tanzania ni jina lililokuja baadae kwa njia ya uchakachuaji kwani jina hili lilitokana na sheria iliyopitishwa na Bunge, Sheria namba 24 ya mwaka 1967 ambayo ilimwezesha Rais kubadilisha jina la Tanganyika kuwa Tanzania; Hii ni kinyume na Mkataba wa Muungano 1964, kwani Sio Serikali wa Bunge lilipewa mamlaka per articles of the union 1964, kushughulikia mambo yasiyo ya muungano kama vile jina TANGANYIKA AU JINA ZANZIBAR;

Wataanza kubaguana wapemba na waunguja,weusi na waarabu,kwasababu dhambi ya ubaguzi imo ndani ya damu zao.Na Sultani naye hatocheza mbali,na kwa kawaida,lazima yeye ndiye atakayeshinda,lakini haina maana kwamba amani itakuwepo,kwasababu pia kuna wale weusi ambao lazima watatengwa kwasababu hawatakuwa na haki sawa na waarabu etc.

It is a very volatile situation,na shida ndipo ilipo.Tatizo kubwa ni kwamba sidhani kama muungano wa serikali tatu utatatua tatizo lolote kama serikali hiyo haitakuwa juu ya serikali za Zanzibar na Tanganyika kwenye issue za zulizni na usalama na mambo mengine.Kwasababu kuna issue ambazo ili kuendelee kuwepo na amani,ni lazima zibakie chini ya serikali ya muungano,jambo amabalo sidhani kama wazanzibari wanaopinga muungano wanakubaliana nalo.
Issue hii ni issue inayohitaji mjadala haswa.

Nakubaliana na wewe kwamba kuna mambo ambayo inabidi tuyaelewe kwa kina kabla ya kuyarukia; kwa mfano, historia inatueleza kwamba kwa kitambo cha vizazi vitatu, Zanzibar ilikuwa imegawanyika katika misingi ya:

  • Kikabila
  • Kiuchumi
  • Kijamii

Na hii ilikuwa chini ya himaya ya Uingereza na Utwala wa usultani wa Kiarabu ambao ulidumu kwa karne tatu!!!

Ndio maana ni muhimu sana kuelewa kwamba ndugu zetu hawa wamepitia historia tofauti kabisa na sisi, na uhuru wao waliupata mitaani kwa kazi kubwa sana iliyohusisha mtutu wa bunduki; lakini binafsi nisingependa kuingia kwa undani kuhusu jamii ya ndugu zetu wazanzibari zaidi ya kuelewa tu background yao; tukianza mjadala wa namna hii hatutaumaliza; tuelewe tu changamoto za wenzetu zipo vipi, na sababu zao za kuona muungano una kero, halafu kama nilivyosema awali, tumrejee Mwalimu anaposema kwamba:

"Iwapo UMMA wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha; Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana"

Again, iwapo sentiments zao zina influence kutoka nje, muungano huu ni kuachana nao; lakini kama kiini chake ni kutafuta autonomy huku wakiwa wanautaka muungano uendelee, that's even better;
 
Mkuu Kobello,

Nianze na hoja yako kwamba hauoni tatizo kwa CCM ku hijack the entire project kwa sababu ilikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo; Nianze na maswali hapa: Mamlaka hiyo CCM ilipewa na nani? Je, CCM alikuwa superior to articles of the Union? Naomba upitie vizuri Articles of the Union Section 2 to 6 ili uone jinsi gani Mkataba wa Muungano, 1964, ambao literally ilikuwa ni sheria mama, ulianza kuchakachuliwa; Unajengaje hoja kuhalalisha kilichofanywa na CCM? Naomba niulize tena, huo uhalali/mamlaka unayosema CCM ilikuwa nayo, ilipewa na nani? Kama unakubali kwamba Mkataba wa Muungano ulikuwa ndio sheria mama, kwanini katika mkataba ule hatuoni neno CCM, ASP, TANu, wala lolote kuhusiana na maamuzi ya kisiasa? Mambo haya hayakuwa ya muungano, yalikuwa yawe chini ya nchi shirikishi, per articles of the union 1964;Au labda uniambie kwamba aliyekuwa ana type ule mkataba aliyasahahu hayo kwa bahati mbaya!

Kubali tu kwamba kinyume na Sheria Mama ilivyoagiza i.e. Mkataba wa Muungano, 1964, CCM iliamua kuingia jikoni kwa nguvu na hapo ndipo mchafuko wa muungano ulipoanza; na tusiwazingizie wenzetu wa zanzibar, TANU ilikuwa inatafuta njia ya kujipatia uhalali wa maamuzi juu ya muungano kwa muda, na ikagundua kwamba njia pekee ni kujiunga na ASP ili kuifunika, kisha kuanza kufanya maamuzi ya muungano kutokea Dodoma; baada ya CCM kuamua kuingia jikoni, kinyume na sheria mama, wakateuliwa wajumbe kutoka CCM-NEC ambao hawa waliundiwa kamati ya kuangalia wafanye mambo gani ili kufanikisha azma yao ya kuzidi kukiuka Article of the union na kuwa na aina ya muungano ambao bara ingeupende; In the end, kamati maalum ya chama ikachukua nafasi ya Tume ya Katiba na bunge likachukua nafasi ya baraza la kutunga sheria, kinyume na utaratibu uliokubaliwa ndani ya Articles of the Union, 1964; Yet unasema CCM ilifanya haya kwa uhalali? kwa kweli hizi ni siasa tu Kobello, sio reflection ya uhalisia wa mambo;

Kuhusu zanzibar kuwa na autonomy kutokana na kuwa na legislature, executive na court system yao, ni lazima ukumbuke kwamba haya hayakuja kirahisi, kwani kwa muda mrefu yalikuwa yanaendeshwa kwa kiini macho; ukitaka nifafanue ntafanya hivyo, lakini nadhani unaelewa jinsi gani zanzibar imevipigania hivi over time, halikuwa ni suala la moja kwa moja na rahisi kama unavyotaka tuamini;

Tukiwa bado kwenye hili la autonomy, pia nimependa ulivyoweka numerali ya 22 kama ndio matters of the union; kama unakumbuka vizuri au kama umesoma vizuri mkataba wa Muungano, 1964, kulikuwa na masuala 11 tu yaliyokubaliwa, na yaliyobakia ilikuwa yafuate baada ya katiba mpya kuja, vinginevyo katika kipindi kile cha mpito ambacho maximum kiliwekwa kuwa mwaka mmoja, juhudi kubwa zilikuwa zielekezwe katika uteuzi wa tume ya katiba na baraza la kutunga sheria; cha ajabu ni kwamba, badala yake, mwaka 1965, katiba ile ikawa ya muda, na ikazidi kuchakachua masuala yaliyokuwa yanaipa zanzibar autonomy yake na kuyaweka kwenye muungano, kinyume na makubaliano ya awali ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964;

Na majibu yako kuhusu serikali ya Tanganyika nilitegemea yatajaa Siasa kuliko kitu kingine; umeelezea vyema complications zilizopo, ambazo kwangu mimi its a myth na nimeelezea kwa undani sana katika majibu yangu kwako awali uliponiuliza, je mfumo wa federation - ya serikali tatu una faida gani kiuchumi, kijamii na kisiasa? Majibu yangu yale bado yanasimama hata hapa kujibu hoja yako inayopinga shirikisho;

Mwisho nilitaka nisahahu kujibu hoja yako ifuatayo:
Population ya Mainland ni mara kumi ya Zanzibar (just came up with this comparison, for the sole purpose of elaboration). Kwa hiyo federation of two countries is a loss to Tanganyikans.

Katika majibu yangu kwa Joka Kuu, nilimjibu juu ya suala kama hili, na nitalifafanua tena;

Ukubwa wa Tanganyika na udogo wa Zanzibar unapimwa na nini, land mass? Population? GDP? Whats the righ way kupima ukubwa wa nchi? Mimi nina amini kwamba ni vyema tupime ukubwa wa Zanzibar by Potential GDP, hasa iwapo watakuwa na full autonomy; Kwa mfano, Kuwait ni nchi ndogo sana hata kwa Tanganyika kwa vigezo vya land size na population, lakini kiuchumi, hawa sio wenzetu kabisa, na ningependa tutazame ukubwa wa Zanzibar kwa vigezo hivyo. Kwa mfano:

  • Total Land ya Tangnayika ni almost 50 times of Kuwait;
  • Population ya Tanganyika ni 10 times of Kuwait;
  • Lakini kiuchumi au GDP, Uchumi wa Kuwait ni over 7 times ya Tanganyika;

Naamini kwamba, given rasilimali walizonazo Zanzibar – utalii, mafuta na gesi, more autonomy to Zanzibar itapelekea taifa hili kuwa kubwa sana kiuchumi, pengine kufanana na Tanganyika kama sio kukaribiana na Tanganyika;
 
Mchambuzi said:
Swali linalofuata hapa ni JE: Sababu za baadhi ya wazanzibari kuukana muungano wetu nje ya mapungufu yaliyopo ambayo yanachangiwa sana na ukiukwaji wa Mkataba wa Muungano, 1964, je pia kuna mkono wa influence au ushawishi kutoka nje ya nchi? Kama jibu ni ndio, mimi naungana na Mwalimu kwamba Muungano uvunjwe leo hii, iwapo tu, uamuzi wao unatokana na ushawishi kutoka nje, kwani hili litakuja kutuletea balaa;Vvinginevyo kama tatizo ni mgogoro tu wa kikatiba na ukirekebishwa wazanzibari watakuwa na furaha kuendelea na muungano, basi turekebishe tatizo hili, hasa kwa kuangalia kwamba – Je, since the inception ya Mkataba wa Muungano, 1964, tumejikwaa wapi?
Mkuu Mchambuzi,nadhani mwalimu alisema ikiwa watafanya maamuzi hayo(kujitenga), bila shinikizo kutoka nje,basi tuwaachie wafanye maamuzi hayo,ila kama kuna shinikizo kutoka nje,basi tusikubali.(Hivyo ndivyo nilivyoelewa),i stand to be corrected.
Mchambuzi said:
Nje ya Tanzania hakuna Zanzibar? Mwalimu alisema hivyo kweli? Basi hilo lilinipita, vinginevyo sikubaliani na hoja hiyo
Hilo hapo juu nadhani hukunipata,sikusema mwalimu alisema hayo maneno(directly),bali ni mimi nimesema hivyo kutokana na situation ilivyokuwa volatile.Kama wasingeungana na Tanganyika,Zanzibar isingekuwa moja.Hata Karume mwenyewe baada ya mapinduzi na muungano,alitawala kwa mkono wa chuma,ubaguzi bado ulikuwepo miongoni mwa wananchi wa Zanzibar,lakini yeye aliushughulikia kwa mkono wa chuma.Kwa mfano alipitisha sheria ambayo mzazi(mwarabu)hakutakiwa kupinga ndoa ya mwanae(wa kike) asiolewe na mtu mweusi.Na yeye mwenyewe alifanya the same,alioa wake wanne wa kiarabu kwa nguvu,na alipokataliwa,wazazi wao walihukumiwa kuchapwa viboko.Pia aliwaweka chini ya uangalizi mkali waarabu pamoja na waasia na waajemi.Ndiyo maana yangu ya kusema Zanzibar isingekuwepo bila muungano.Na pia ni kweli mwalimu alisema kwenye hotuba yake alipozungumzia udini,akasema nje ya muungano,kuna "sisi wapemba,hao waunguja", akaendelea kusema pia "nje ya muungano hakuna Zanzibar,bali kuna sisi wazanzibari, na hao wazanzibara"nakumbuka hiyo hotuba as if it was yesterday.
 
Nimeipitia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu nikashindwa kuelewa ni kwanini CUF haikuiunga mkono CDM.Wanasiasa ni watu wanafki sana hasa ukimsikiliza Maalimu na Jussa ndiyo unashindwa kuelewa wanataka nini haswaa.

Ngongo

Nafikiri Lissu alisema mengi mazuri katika hutuba ile lakini kwa maoni yangu ukisoma ile hutuba chini ya kichwa cha habari: KATIBA YA MUAFAKA AU KATIBA YA UHURU? utaona Lissu alielekeza makombora kwa wazanzibari (CUF?) badala ya lawama ya kukiukwa kwa makubaliano ya awali muungano, ambayo Mchambuzi bila ya kupindisha maneno ameyasema.

Kosa ambalo Lissu alilifanya ni kutumia katiba ya 1977 ambayo tayari yenyewe ni utata mtupu kujengea hoja yake hiyo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kuwa yamevunja muungano. Lissu alisahau au kwa makusudi alipotosha.
Lissu anaelewa kuwa Katiba ya Zanzibar si jambo la muungano, wala muundo wa serikali ya Zanzibar si jambo la muungano. Hawa wazanzibari wanaweza kujiamulia muundo upi wa serikali yao uwe ,pia kubadilisha katiba yao au kuifanyia mabadiliko vile wanaona inafaa.

Nina imani Lissu angeungwa mkono na wabunge wazanzibari ndani ya bunge juu ya hoja zake kama angeondoa kipengele cha KATIBA YA MUAFAKA AU KATIBA YA UHURU? katika hotuba yake.

Wazanzibari walishachoka uchonganishi kutoka Tanganyika(Tz bara) na hicho kifungu kinaashiria kusema kuwa mwafaka/mapatano yamekiuka Katiba ya 19977 na hivyo muelekeo wa siasa za maelewano huko visiwani ulikuwa ni jambo baya.

Hata kesho naamini akiamua kuirudia hotuba yake katika upeo na wepesi ambao Mchambuzi ameandika mada yake basi Serikali ya Tanganyika inarudi tu.

Lissu/CHADEMA kama unasoma hapa rekebisha kosa hilo, pia fanyeni mawasiliano na CUF na CCM-Zanzibar(wale wanaotaka mabadiliko ya mfumo wa muungano ili utakapolianzisha tena utakuwa una uhakika wa kuungwa mkono na hoja yako kusonga mbele.
 
Nonda,

Aante sana kwa clip yako; sasa nadhani tumekamilika, kilichobakia mbele yetu sasa ni kuijengea hoja nzuri Tanganyika yetu irudi, kama njia ya kuboresha muungano wetu;
 
Mkuu jmushi1,

Mkuu Mchambuzi,nadhani mwalimu alisema ikiwa watafanya maamuzi hayo(kujitenga), bila shinikizo kutoka nje,basi tuwaachie wafanye maamuzi hayo,ila kama kuna shinikizo kutoka nje,basi tusikubali.(Hivyo ndivyo nilivyoelewa),i stand to be corrected.

Alichosema Mwalimu ni kama nilivyokiweka; alicho maanisha ni kwamba kama kuna shinikizo la nje kwa wazanzibari kutaka wajiondoe, basi waende;

Hilo hapo juu nadhani hukunipata,sikusema mwalimu alisema hayo maneno(directly),bali ni mimi nimesema hivyo kutokana na situation ilivyokuwa volatile.Kama wasingeungana na Tanganyika,Zanzibar isingekuwa moja.Hata Karume mwenyewe baada ya mapinduzi na muungano,alitawala kwa mkono wa chuma,ubaguzi bado ulikuwepo miongoni mwa wananchi wa Zanzibar,lakini yeye aliushughulikia kwa mkono wa chuma.Kwa mfano alipitisha sheria ambayo mzazi(mwarabu)hakutakiwa kupinga ndoa ya mwanae(wa kike) asiolewe na mtu mweusi.Na yeye mwenyewe alifanya the same,alioa wake wanne wa kiarabu kwa nguvu,na alipokataliwa,wazazi wao walihukumiwa kuchapwa viboko.Pia aliwaweka chini ya uangalizi mkali waarabu pamoja na waasia na waajemi.Ndiyo maana yangu ya kusema Zanzibar isingekuwepo bila muungano.Na pia ni kweli mwalimu alisema kwenye hotuba yake alipozungumzia udini,akasema nje ya muungano,kuna "sisi wapemba,hao waunguja", akaendelea kusema pia "nje ya muungano hakuna Zanzibar,bali kuna sisi wazanzibari, na hao wazanzibara"nakumbuka hiyo hotuba as if it was yesterday.

Sasa nimekuelewa mkuu;
 
Mkuu Kobello,

Nianze na hoja yako kwamba hauoni tatizo kwa CCM ku hijack the entire project kwa sababu ilikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo; Nianze na maswali hapa: Mamlaka hiyo CCM ilipewa na nani? Je, CCM alikuwa superior to articles of the Union? Naomba upitie vizuri Articles of the Union Section 2 to 6 ili uone jinsi gani Mkataba wa Muungano, 1964, ambao literally ilikuwa ni sheria mama, ulianza kuchakachuliwa; Unajengaje hoja kuhalalisha kilichofanywa na CCM? Naomba niulize tena, huo uhalali/mamlaka unayosema CCM ilikuwa nayo, ilipewa na nani? Kama unakubali kwamba Mkataba wa Muungano ulikuwa ndio sheria mama, kwanini katika mkataba ule hatuoni neno CCM, ASP, TANu, wala lolote kuhusiana na maamuzi ya kisiasa? Mambo haya hayakuwa ya muungano, yalikuwa yawe chini ya nchi shirikishi, per articles of the union 1964;Au labda uniambie kwamba aliyekuwa ana type ule mkataba aliyasahahu hayo kwa bahati mbaya!

Kubali tu kwamba kinyume na Sheria Mama ilivyoagiza i.e. Mkataba wa Muungano, 1964, CCM iliamua kuingia jikoni kwa nguvu na hapo ndipo mchafuko wa muungano ulipoanza; na tusiwazingizie wenzetu wa zanzibar, TANU ilikuwa inatafuta njia ya kujipatia uhalali wa maamuzi juu ya muungano kwa muda, na ikagundua kwamba njia pekee ni kujiunga na ASP ili kuifunika, kisha kuanza kufanya maamuzi ya muungano kutokea Dodoma; baada ya CCM kuamua kuingia jikoni, kinyume na sheria mama, wakateuliwa wajumbe kutoka CCM-NEC ambao hawa waliundiwa kamati ya kuangalia wafanye mambo gani ili kufanikisha azma yao ya kuzidi kukiuka Article of the union na kuwa na aina ya muungano ambao bara ingeupende; In the end, kamati maalum ya chama ikachukua nafasi ya Tume ya Katiba na bunge likachukua nafasi ya baraza la kutunga sheria, kinyume na utaratibu uliokubaliwa ndani ya Articles of the Union, 1964; Yet unasema CCM ilifanya haya kwa uhalali? kwa kweli hizi ni siasa tu Kobello, sio reflection ya uhalisia wa mambo;

Kuhusu zanzibar kuwa na autonomy kutokana na kuwa na legislature, executive na court system yao, ni lazima ukumbuke kwamba haya hayakuja kirahisi, kwani kwa muda mrefu yalikuwa yanaendeshwa kwa kiini macho; ukitaka nifafanue ntafanya hivyo, lakini nadhani unaelewa jinsi gani zanzibar imevipigania hivi over time, halikuwa ni suala la moja kwa moja na rahisi kama unavyotaka tuamini;

Tukiwa bado kwenye hili la autonomy, pia nimependa ulivyoweka numerali ya 22 kama ndio matters of the union; kama unakumbuka vizuri au kama umesoma vizuri mkataba wa Muungano, 1964, kulikuwa na masuala 11 tu yaliyokubaliwa, na yaliyobakia ilikuwa yafuate baada ya katiba mpya kuja, vinginevyo katika kipindi kile cha mpito ambacho maximum kiliwekwa kuwa mwaka mmoja, juhudi kubwa zilikuwa zielekezwe katika uteuzi wa tume ya katiba na baraza la kutunga sheria; cha ajabu ni kwamba, badala yake, mwaka 1965, katiba ile ikawa ya muda, na ikazidi kuchakachua masuala yaliyokuwa yanaipa zanzibar autonomy yake na kuyaweka kwenye muungano, kinyume na makubaliano ya awali ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964;

Na majibu yako kuhusu serikali ya Tanganyika nilitegemea yatajaa Siasa kuliko kitu kingine; umeelezea vyema complications zilizopo, ambazo kwangu mimi its a myth na nimeelezea kwa undani sana katika majibu yangu kwako awali uliponiuliza, je mfumo wa federation - ya serikali tatu una faida gani kiuchumi, kijamii na kisiasa? Majibu yangu yale bado yanasimama hata hapa kujibu hoja yako inayopinga shirikisho;

Mwisho nilitaka nisahahu kujibu hoja yako ifuatayo:

Katika majibu yangu kwa Joka Kuu, nilimjibu juu ya suala kama hili, na nitalifafanua tena;

Ukubwa wa Tanganyika na udogo wa Zanzibar unapimwa na nini, land mass? Population? GDP? Whats the righ way kupima ukubwa wa nchi? Mimi nina amini kwamba ni vyema tupime ukubwa wa Zanzibar by Potential GDP, hasa iwapo watakuwa na full autonomy; Kwa mfano, Kuwait ni nchi ndogo sana hata kwa Tanganyika kwa vigezo vya land size na population, lakini kiuchumi, hawa sio wenzetu kabisa, na ningependa tutazame ukubwa wa Zanzibar kwa vigezo hivyo. Kwa mfano:

  • Total Land ya Tangnayika ni almost 50 times of Kuwait;
  • Population ya Tanganyika ni 10 times of Kuwait;
  • Lakini kiuchumi au GDP, Uchumi wa Kuwait ni over 7 times ya Tanganyika;

Naamini kwamba, given rasilimali walizonazo Zanzibar – utalii, mafuta na gesi, more autonomy to Zanzibar itapelekea taifa hili kuwa kubwa sana kiuchumi, pengine kufanana na Tanganyika kama sio kukaribiana na Tanganyika;
Sidhani kama unaamini kuwa TANU pre 1965 (kabla ya single party) ilipewa ridhaa na wananchi itawale. Na sidhani kama unaamini kuwa baada ya mwaka 1965 TANU ndiyo kilikuwa chama pekee na wabunge wote wa Tanganyika ambayo katiba yake ndiyo ilipewa mamlaka ya kuwa katiba ya muungano (kifungu cha pili) waliteuliwa na halmashauri kuu ya TANU. Tofauti na sasa ambapo bunge linapata mswaada kutoka kwa rais, bunge lilikuwa likipata muswaada kutoka NEC ya TANU.
Sasa naomba uniambie/elezee kwanini kuipa madaraka katiba ya Tanganyika ambayo iliondoa vyama vingi na kuipa TANU/CCM madaraka ya kibunge (unajua hili?) ni kinyume cha makubalianbo?
 
Mkuu jmushi1,

Alichosema Mwalimu ni kama nilivyokiweka; alicho maanisha ni kwamba kama kuna shinikizo la nje kwa wazanzibari kutaka wajiondoe, basi waende;

Sasa nimekuelewa mkuu;
Mkuu ebu naomba uniwekee hiyo statement ya mwalimu ningeshukuru sana.Nitajaribu na mimi kuitafuta,isipokuwa nakumbuka alisema ikiwa hakuna shinikizo kutoka nje,basi tuwaachie waende,so nika assume the opposite is also true,kwamba kama kuna shinikizo la nje basi tusikubali muungano uvunjike(hakusema hivyo),lakini i am almost certain kuwa alisema endapo hakuna shinikizo la nje basi waachwe waende.
 
Ok Mchambuzi,nimepata hicho kipengele,hapo chini...Kutoka kitabu cha "Mwalimu Julius K.Nyerere",cha William Edgett Smith,kilichotafsiriwa na Paul Sozigwa(uk. 154)

Kama watu wa Zanzibar, bila ya ulaghai kutoka nje, wataona ni bora kuvunja Muungano, mimi siwezi hata kidogo kuwapiga mabomu na kuwaua wananchi wa Zanzibar. Kama waliingia katika Muungano kwa hiari yao, vivyo hivyo wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao.

Hapo nimetafsiri kwamba bila ya shinikizo kutoka nje,wakitaka kuvunja muungano,basi hana shida na hatoweza kuwapiga mabomu wazanzibari,again, i stand to be corrected,pengine ni utafsiri wangu?
 
Kobello,

..nakubaliana na hoja yako.

..lakini lazima tuwe wakweli kwamba mambo yale 11 ya muungano ndiyo kiini cha Tanganyika na Zanzibar kupoteza "autonomy."

..kwa maana nyingine ni kwamba Tanganyika na Zanzibar zilikoma kuwa dola au nchi mbili tofauti, na badala yake zikaunda dola au nchi kubwa inayoitwa TANZANIA.

Joka Kuu

Jina halisi la muungano lilikuwa ni Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama ni jina la nchi basi ni hili. Lakini nia ilikuwa ni kuipoteza Tanganyika au jina Tanganyika lisitumike basi ndio uchakachuaji ulipoanza wa kubadilisha jina. Mazingaombwe na ukiini macho ulianza tokea alfajiri.

The name Tanzania derives from the names of the two states, Tanganyika and Zanzibar, that united in 1964 to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, which later the same year was renamed the United Republic of Tanzania Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia

Tanganyika na Zanzibar zilikoma vipi kuwa dola au nusu dola wakati ziliungana kwa mambo 11 tu? Na mengine Tanganyika ilitakiwa kujifanyia kivyake na pia Zanzibar kujifanyia kivyake yale mambo ambayo si ya muungano.

Umeridhika na Tanzania yako bila ya kusikia mzazi mmoja wa Tanzania kutajwa tajwa?

Wewe unasherehekea uhuru wa Tanzania bara? au uhuru wa Tanganyika?

Hata mifano uliyoitoa ya jumuia, nchi wanachama wa jumuia hupoteza ndio baadhi ya powers lakini haifanyi kuwa nchi hizo zisiwe dola. Chukua mfano wa EU, soma histoia yake.
 
Ndani ya muungano kuna ulaji ndio maana wote wanaotoa povu kinywani kutetea mfumo uliopo wana masilahi binafsi ya ulaji. Si bure eti. Na ukiasikiliza kwa makini hakuna hata mmoja anyetoa hoja. Ni uvuvuzela kwa mbele.
Mungu ibariki Tanganyika
Saa ya Ukombozi ni sasa alisemaga Mtanganyika Mchungaji Mtikila
 
Sidhani kama unaamini kuwa TANU pre 1965 (kabla ya single party) ilipewa ridhaa na wananchi itawale. Na sidhani kama unaamini kuwa baada ya mwaka 1965 TANU ndiyo kilikuwa chama pekee na wabunge wote wa Tanganyika ambayo katiba yake ndiyo ilipewa mamlaka ya kuwa katiba ya muungano (kifungu cha pili) waliteuliwa na halmashauri kuu ya TANU.

Mkuu Kobello,

Kwanza naomba uelewe mimi sio mwanasheria, ni mbabaishaji tu huku uraiani lakini kiini macho hiki kipo wazi kwa mtu wa kawaida iwapo atatumia muda zaidi japo kidogo kudadisi masuala haya;

Nitajibu swali lako hili kwa kirefu kidogo, kwahiyo naomba uvumilivu toka kwako; Tuanze na hicho chama cha TANU; Kwanza naomba uelewe kwamba kujadili TANU katika mazingira ya Muungano ni Kinyume Cha Sheria kwani suala la TANU, ASP, au Vyama Vya Siasa kwa ujumla, hayakuwepo kama masuala ya muungano, haya yalikuwa ni masuala ya nchi shirikishi – Tanganyika na Zanzibar, kuyashughulikia; Kwahiyo, hata kama TANU ilipita uchaguzi husika kwa asilimia 1,000,000,000,000,% , haijalishi, kwani kuingia kwake katika masuala ya Muungano ilikuwa ni ubatili;

Kumbuka kwamba Mkataba wa Muungano, 1964 uliweka kipindi cha Mwaka mmoja kama Kipindi cha Mpito, na katika hili, Mkataba wa Muungano uliweka masharti kwamba liteuliwe baraza la kutunga katiba, na mengine yafuate baadae;

Ebu tuijadili kidogo hiyo Katiba ya Tanganyika;
Hoja yako kuhusu Katiba ya Tanganyika kuwa katiba ya Muda ni sahihi, lakini kidogo kuna upotoshwaji; Nitafafanua; Chini ya Mkataba wa Muungano, 1964, iliamuliwa kwamba kutakuwa na Kipindi cha Mpito kisichozidi mwaka mmoja, ambacho kama unavyosema, Katiba ya Tanganyika ndio iwe Katiba ya JMT; Lakini masuala muhimu zaidi katika sharti hili ambayo, aidha kwa makusudi, kwa kupitiwa, au kutofahamu, umeyaacha. Nitayajadili. Masharti ya Muungano yaliweka wazi kabisa katika ibara ya PILI kwamba, Katiba ya Tanganyika itakuwa ni KATIBA ILIYOREKEBISHWA ili kuweka yafuatayo:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;
c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

Msisitizo hapa: Kwanza, suala la TANU halikuwa suala la ku deal na kitu chochote cha muungano, hivyo TANU, kama ilivyokuwa ASP, majukumu yao yalikuwa huko kwao, sio kwenye muungano, mpaka pale baraza la kutunga katiba litakapoteuliwa na kufanya kazi yake na kuimaliza Per Articles of the Union, 1964; Msisitizo wa pili ni kwamba – unajichanganya unapohusisha katiba ya Tanganyika, Wabunge wa TANU, na Muungano;

Vinginevyo, ni kweli kwamba katiba ya Tanganyika ilipewa mamlaka ya kuwa katiba ya muda ya MUUNGANO, lakini kwa masharti ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba hiyo, ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kama nilivyojadili; Vile vile katika kipindi hiki cha mpito, Rais wa JMT na Makamo wake (Rais wa Zanzibar), kwa pamoja walitakuwa wateue tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya kudumu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Lakini tofauti na masharti haya, bunge la JMT likapitisha sheria ya kuhairisha INDEFINATELY ibara hii ya Saba ya Mkataba wa Muungano, na badala yake, Bunge likapitisha katiba ya Muda ambayo ndiyo ilitengeneza madaraka ya JMT na pia ya nchi mbili shirikishi;

Huu ulikuwa ni uchakachuaji mkubwa wa Mkataba wa Muungano, 1964, na ukaendelea kwa miaka 12, mpaka pale CCM sasa ilipoamua kuingia jikoni na kusimamia mchakato wa katiba kwa kuingia ndoa na ASP kimazingaombwe, kinyume kabisa na Mkataba wa Muungano, 1964.

Naomba pia niseme kwamba, hii hoja yako inachanganya mazingira ya Tanganyika na Tanzania; Ni muhimu tukayaweka haya in their correct contexts, na katika hili, tutazidi kubaini hiki kiini macho kwa undani zaidi; Pre 1965 Period unayoizungumzia, bado ilitambua uwepo wa Tanganyika katika Tanzania; Kwa maana nyingine kipindi cha 1964 – hadi mwanzoni wa 1967, Tanganyika ilikuwepo na ilikuwa inadunda kama Taifa lililo jipatia uhuru miaka sita iliyopita (1961); Ni miaka mitatu baadae, ndipo taifa la Tanganyika likaingia Mkataba wa muungano na taifa lingine linaloitwa Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aprili mwaka 1964;

Katika mkataba huu, iliwekwa bayana kwamba kila upande utakuwa na masuala yake yasiyo ya muungano, huku masuala kumi na moja yakikubaliwa yawe ya muungano; Lakini cha ajabu zaidi, bunge lile lile la JMT unalolizungumzia, ndio lililoua Tanganyika kwa kupitisha Sheria Namba 24 iliyompa madaraka Rais kubadilisha neno Tanganyika, liwe Tanzania; Kwahiyo TANGANYIKA IMEFUTWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA BUNGE LA JMT Namba 24, ya mwaka 1967;

Tofauti na sasa ambapo bunge linapata mswaada kutoka kwa rais, bunge lilikuwa likipata muswaada kutoka NEC ya TANU. Sasa naomba uniambie/elezee kwanini kuipa madaraka katiba ya Tanganyika ambayo iliondoa vyama vingi na kuipa TANU/CCM madaraka ya kibunge (unajua hili?) ni kinyume cha makubalianbo?

Hili swali sijalielewa vizuri, lakini nadhani nimelijibu kwa namna moja au nyingine hapo juu, lakini pia wakati natoa majibu kwa wadau kadhaa humu ndani; nadhani ukinisoma vizuri hapo juu, utapata pia maelezo yatakayosaidia kupatia swlai lako hili majibu; Vinginevyo for starters, mjadala wa TANU/CCM, ASP katika mazingira ya Muungano ni kinyume cha Mkataba wa Muungano, 1964; Na ndio maana hakuna sehemu katika Mkataba wa Muungano, 1964, inayotamka TANU, ASP, CCM, au chaam cha siasa;

Masuala ya Siasa were meant to remain katika kila nchi husika; Lakini tunaona katika historia jinsi gani sharti hili lilikiukwa, kwanza kwa bunge kupitisha sheria mbalimbali za kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuchakachua Mkataba wa Muungano, kwa malengo ya kisiasa – again, masuala ya kisiasa hayakuwa masuala ya muungano;
 
Ok
Mchambuzi,nimepata hicho kipengele,hapo chini...Kutoka kitabu cha "Mwalimu Julius K.Nyerere",cha William Edgett Smith,kilichotafsiriwa na Paul Sozigwa(uk. 154)

Hapo nimetafsiri kwamba bila ya shinikizo kutoka nje,wakitaka kuvunja muungano,basi hana shida na hatoweza kuwapiga mabomu wazanzibari,again, i stand to be corrected,pengine ni utafsiri wangu?

Mkuu, ebu tusaidiane katika hili,pengine sipo sahihi na tafsiri yangu. Kwa uelewa wako, JE:
  • Mwalimu was okay kwa muungano kuvunjika kama ilitokana na influence ya nje? au alikuwa okay kuvunjika kama ilitokana na matakwa ya wazanzibari wenyewe?
 
Alikuwa ok kama ni matakwa ya wazanzibari wenyewe,lakini kama kuna shinikizo kutoka nje,then kutakuwepo na tatizo kwasababu usalama wa Tanganyika nao utakuwa mashakani.Kwahiyo mwalimu was not ok kama muungano ukivunjika kutokana na shinikizo kutoka nje.Hivyo ndivyo nlivyoielewa statement ya mwalimu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom