Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

CUF walipumbazwa lakini baada ya sindano za kutosha za wadau wameelewa somo sasa tupo pamoja.
Nimeipitia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu nikashindwa kuelewa ni kwanini CUF haikuiunga mkono CDM.Wanasiasa ni watu wanafki sana hasa ukimsikiliza Maalimu na Jussa ndiyo unashindwa kuelewa wanataka nini haswaa
Tatizo la CUF Wakikusanyika hawaongelei facts, wanatumia muda mwingi kumtukana Nyerere (lanatullah), mwisho wa siku wanasema wanataka muungano au mkataba na nchi ile ile ya Nyerere.
Narudia, wametumia muda mwingi kutukana watu badala ya kutafuta ukweli.
Nondo kama hizi anazoteremsha Mchambuzi hawana muda wa kuzisoma.
 
Katika hali inayoshangaza wznz ambao wamekuwa wandai hati ya mkataba ya mwaka 1964 wamejikuta wakijikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

Nahodha Vua amenukuliwa akisema hati hiyo ipo UN na haijawahi kurudi. Sijui UN walikuwa na sababu gani ya kubaki nayo.
Yahya Hamis Hamad katibu wa bunge kutoka znz anasema, hati ipo moja Ikulu Dar. Haiwezi kutolewa kwasababu uwezekano wa kupotea upo.

Hawa wawili ni wznz ambao kwao muungano ulikuwa Mwiba na wanataka mamlaka.

Hivi kama kipande cha karatasi hakiwezi kulindwa hadi Dodoma, kuna sababu ya Rais kutoka nje ya Ikulu?
Kuna sababu za Watanzania kula usingizi? Serikali haiwezi kulinda ukurusa mmoja wa karatasi vipi nchi?

Haya ndiyo mazingaombwe na ulaghai unaoendelea Dodoma.
 
Ndugu yangu utabadilika lini? Eleza basi kitu cha maana japo siku moja. Hapa watu wanajadili mambo muhimu wewe unaleta hadithi za mitaani. Hiyo kauli tumeisikia miaka 30 kipi cha ajabu.
Lakini pia kama ni koti mbona wznz wapo Dodoma wakishona hilo koti?

Tafadhali usihahribu mjadala, kama huna la kusema soma tu, ni sehemu muhimu ya elimu.

Maneno yote ya nini mkulu,

Hio nilioweka hapo ilikuwa kama jingle (Angalizo tu) na linahusiana na mada hii kwani huo ni MSIMAMO WA ZNZ katika kadhia hii ya mvungano wenu.

Kama hu msema kweli unaweza niambia inaharibu vipi mtitiririko wa mada husika? kama si chuki binafsi na ukweli kukuchoma?

Pole sana kama imekuchoma LAKIN ukweli laazima usemwe. Na huko mjengoni Dodoma pamoja na kula cha MJINGA lakin msimamo ni huo huo. 2/3 haipatikani NG'O kwa hili.

POLE SANA

Tatizo la CUF Wakikusanyika hawaongelei facts, wanatumia muda mwingi kumtukana Nyerere (lanatullah), mwisho wa siku wanasema wanataka muungano au mkataba na nchi ile ile ya Nyerere.
Narudia, wametumia muda mwingi kutukana watu badala ya kutafuta ukweli.
Nondo kama hizi anazoteremsha Mchambuzi hawana muda wa kuzisoma.

Ahali yangu Nguruvi3,

Siku zote nakwambia kama utapunguza chuki dhidi ya Znz na waZnz na kujiepusha na ushabiki wa Vyama na kujitenga na kulalamika na kunung'unika kuna mengi sana utajifunza.

Kwa kukusaidia kumbuka kuwa JF sio sehemu sahihi au kuwa ni sharia mtu lazima apite hapa kupata NONDO, Kama Mchambuzi angetaka kuwa mtu makini na KUIPENDA TZ NA WATZ basi hizi unazoziita nondo ANGEZIPELEKA KWENYE TUME YA WARIOBA YA KUPOKEA MAONI YA KATIBA MPYA na hivyo hivi sasa wenye meno wangekaa kule Dodoma kuzijadili. Hapa ni sehemu tu au barza ya kupashana habari na kuilimishana kwa muhimili USIO RASMI.

Wewe humjui na kumfahamu Nyerere zaidi ya kumsikia na kumsoma lakin ujafanya nae kazi. Nikuulize suala dogo tu.
1. HUU MKANGANYIKA UNAOSUMBUA WATU HUKO DODOMA KUHUSU MUUNGANO ALIUANZISHA NANI?

2. Je unajuwa kwanini Nyerere huyo huyo alitumia nguvu zake nyingi sana KUZIKA HOJA YA SERIKALI 3 NA KUUNDWA KWA SERIKALI YA TGK wakti wa uhai wake? (alimzuia Jumbe na hata Wabunge wale wa G55).

Ujiulizi alikuwa na Siri gani?

Huko nyuma kwenye post yangu katika uzi huu POST No 21 niliandika hivi.

Waarabu tuna usemi unaonena. ''NI RAHISI SANA KUWADANGANYA WATU. LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAAMBIA WATU KUWA WAMEDANGANYWA''

Na vile vile Mwimbaji mashuhuri wa Reggae Robbert Nesta Marley (maarufu kama Bob Marley) kwenye wimbo wake wa "Redemption song" alisema YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME"

Nikiwaambia waTanganyika Nyerere aliwadanganya sana na alisimamia kidete kuhakikisha HAMUWEZI KABISA KUUNDA Serikali ya TANGANYIKA pamoja na Znz kuwasaidia sana kuwaombea Serikali Hiyo katika mjadala wa kwanza kuhusu Muungano wenu.

Kumbuka kuwa waZnz wapo wawazi sana na hawamwogopi mtu yoyote kwa lolote zaidi ya Kumuogopa Mungu tu. Muulize Spika Sitta nini kilimtokea alipopeleka ile muswada wa madadiliko a katiba kule Znz, tena mchana kweupeeeeeeeee?

Pole sana

Katika hali inayoshangaza wznz ambao wamekuwa wandai hati ya mkataba ya mwaka 1964 wamejikuta wakijikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

Nahodha Vua amenukuliwa akisema hati hiyo ipo UN na haijawahi kurudi. Sijui UN walikuwa na sababu gani ya kubaki nayo.
Yahya Hamis Hamad katibu wa bunge kutoka znz anasema, hati ipo moja Ikulu Dar. Haiwezi kutolewa kwasababu uwezekano wa kupotea upo.

Hawa wawili ni wznz ambao kwao muungano ulikuwa Mwiba na wanataka mamlaka.

Hivi kama kipande cha karatasi hakiwezi kulindwa hadi Dodoma, kuna sababu ya Rais kutoka nje ya Ikulu?
Kuna sababu za Watanzania kula usingizi? Serikali haiwezi kulinda ukurusa mmoja wa karatasi vipi nchi?

Haya ndiyo mazingaombwe na ulaghai unaoendelea Dodoma.

Chuki nyingine hazina msingi hata kidogo. Kwani taarifa za Bunge hilo zinatolewa kila siku.

Waliodai Hati za Muungano SIO WAZNZ bali ni wajumbe wa Bunge hilo wakiwemo wa TGK ambao ndio wengi zaidi. Na hata ni wao waliogundua kuwa kulikuwa na makosa katika Sahihi na Jina la Msekwa (limeandikwa "Msekwa") na la Nyerere zimeongezwa harufu US kwa computer.

Suala la Znz kuwa hati hiyo ya Muungano wa ilithibitishwa na BLM, limeshapatiwa majibu kwani Mwanasharia mkuu wa Znz Mh Othman amekana kuwa hajawahi kuona kitu kama hicho ofisini kwake na Hata Nahodha alikiri kuwa pamoja na yeye kuwa Chief minister hajapata kuona kitu kama hicho. Sasa watu wanajikanyaga kutaka kuweka mambo sawa.

Kumbuka kuwa viongozi takriban wote wa kamati 12 za bunge hilo akina Job Ndugai, paul Kimiti, Anna Abdallah, Ummy Mwalimu na wengineo wanasisitiza msimamo wa Bara ni Serikali 2 na sio Tatu. Na hata wakipiga kura za kamati upande wa Bara wanapata 2/3 lakin kikwazo upande wa Znz 2/3 haipatikani na haitapatikana NG'O.

Msimamo wa Znz ni kama muungano basi uwe shirikisho au Serikali 3. Serikali mbili wanazozitaka watu wa TGK haiwezekani.
Kwani Muungano ni kama Koti tu.... likikukera unalivua.

Pole sana.

Mchambuzi: Unasikitisha sana kuona kuwa unakumbatia wazo la Utanganyika na kujaribu kadri ya uwezo wsko kujenga hoja dhaifu kupindukia kuusifu Utanganyika. Hebu jiulize kidogo unadai eti Wananchi wakaongeza uelewa na kuitaka Tanganyika, Hawa wananchi unaowataja ni wanasiasa pekee au watanzania wenye hali zote? Kama ni wote, takwimu hizo umezipata wapi kuthibitisha kuwa Watsnzania wote su hata asilimia 90 wanataka Utanganyika au hata 51% Wakiutaka Utanganyika. Kwanini Mchambuzi unawasingizia wananchi kuwa Wanataka Utanganyika wakati ukweli ni kwamba Wanasiasa peke yao ndiyo wanayoitaka Tanganyika tena na wenyewe ni Wanachadema pekee?. Wewe unayejiita eti mchambuzi, mimi nathibitisha pasipo shaka kuwa hulitendei haki jina na sifa ya Mchambuzi. Naomba ujibu kwa hoja Faida 5 tu za Utanganyika kwa mwananchi wa Tanzania bara pia uoneshe hasara 5 tu kwa kuwepo Tanzania ambapo kila mtanzania zinamgusa moja kwa moja kama vile; Kutokuwepo Tanganyika Mwananchi hapati sukari, hapati ardhi ya kulima, Hapati madawa hospitalini, haruhusiwi kutumia barabara, haruhusiwi kuwa kiongozi au hata kuchagua kiongozi, haruhusiwi kusafiri nadani na nje ya nchi yake, Nawachukia sana watu wanaotukuza Utanganyika kwavile tu hawakubaliki aidha Zanzibar au Tanzania bara hivyo kutafuta kupiga bao ktk eneo moja tu la nchi. Watu kama Mchambuzi kilaza walaaniwe na wafungiwe jiwe kubwa shingoni na kutupwa ktkt ya bahari yenye kina kireeeeeeeefu.
 
Njoo kwenye uzi juu ya gharama za muungano kwenye jukwaa la Great Thinkers. Wenzako wa hoja wengi wamekimbia kule baada ya kulemewa hoja.

Kuhusu takwimu za tume ya katiba, hilo nalo tumelijibu, nenda kule great thinkers kwenye uzi wa "mtazamo kuhusu hotuba ya JK bungeni. Wenzako wa hoja pia wamekimbia mjadala ule baada ya kulemewa.

Kuhusu nawakilisha mawazo ya nani juu ya Tanganyika, nawakilisha mawazo yangu binafsi. Hilo moja, sasa katika hilo, nimejikuta sipo peke yangu. Tembelea vijiwe vya bajaji na bodaboda kwa wananchi wa kawaida utasikia hoja zao juu ya haja ya Tanganyika. Tembelea vyuo vikuu ukae na wanafunzi na usijitambulishe ki-ccm, ongea nao kama raia wa kawaida, utawasikia kuhusu umuhimu wa Tanganyika. Tembelea taasisi mbalimbali za umma (TRA, ofisi ya waziri mkuu, ofisi za bunge, ofisi ya makamo wa rais etc), utawasikia kuhusu Tanganyika. Tafuta ndugu yako wa karibu ambae ni mmoja wa wapiganaji wetu (nadhani unaelewa naongelea taasisi gani), kaa nae akueleze juu ya maoni ya wengi, utaisikia Tanganyika.

Katika uzi huu, tupo hapa kujadili jinsi gani mkataba wa muungano ulichakachuliwa na nini yamekuwa madhara kwa muungano, lawama zote zikienda kwa CCM kama tutakavyojadili tena humu, TANU kwa kuanzia. Mjadala wa gharama na takwimu, tembelea nyuzi nilizotaja hapo juu.

Mwisho nadhani unazo updates kwamba Sitta amekiri kwamba saini za Nyerere na Msekwa zimechakachuliwa. Nini kitafuata? Usikae mbali na uzi huu, tutajadili na kuchambua.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.

Tusemezane.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi: Unasikitisha sana kuona kuwa unakumbatia wazo la Utanganyika na kujaribu kadri ya uwezo wsko kujenga hoja dhaifu kupindukia kuusifu Utanganyika.
Hebu jiulize kidogo unadai eti Wananchi wakaongeza uelewa na kuitaka Tanganyika, Hawa wananchi unaowataja ni wanasiasa pekee au watanzania wenye hali zote? Kama ni wote, takwimu hizo umezipata wapi kuthibitisha kuwa Watsnzania wote su hata asilimia 90 wanataka Utanganyika au hata 51% Wakiutaka Utanganyika. Kwanini Mchambuzi unawasingizia wananchi kuwa Wanataka Utanganyika wakati ukweli ni kwamba Wanasiasa peke yao ndiyo wanayoitaka Tanganyika tena na wenyewe ni Wanachadema pekee?.

Wewe unayejiita eti mchambuzi, mimi nathibitisha pasipo shaka kuwa hulitendei haki jina na sifa ya Mchambuzi. Naomba ujibu kwa hoja Faida 5 tu za Utanganyika kwa mwananchi wa Tanzania bara pia uoneshe hasara 5 tu kwa kuwepo Tanzania ambapo kila mtanzania zinamgusa moja kwa moja kama vile;

Kutokuwepo Tanganyika Mwananchi hapati sukari, hapati ardhi ya kulima, Hapati madawa hospitalini, haruhusiwi kutumia barabara, haruhusiwi kuwa kiongozi au hata kuchagua kiongozi, haruhusiwi kusafiri nadani na nje ya nchi yake, Nawachukia sana watu wanaotukuza Utanganyika kwavile tu hawakubaliki aidha Zanzibar au Tanzania bara hivyo kutafuta kupiga bao ktk eneo moja tu la nchi.

Watu kama Mchambuzi kilaza walaaniwe na wafungiwe jiwe kubwa shingoni na kutupwa ktkt ya bahari yenye kina kireeeeeeeefu.
Ndugu yangu, mbona hushambulii hoja unashambulia watu?
Tanganyika ipo, cheti cha kuzaliwa cha Pinda kimeandikwa Tanganyika.
Watu wanaoikataa Tanganyika walaaniwe na kutupwa katika kina kirefu cha bahari.

Labda nawe tukuulize takwimu zipi ulizopata zinazosema Watanganyika wanataka serikali 2?
At least wanaotaka serikali 3 wana hoja.
Tume ya Warioba imekusanya maoni na wengi wamesema serikali 3
Tume tano zilizoundwa hapo awali, kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi imeshauri serikali 3

Tupe tume moja tu iliyowahi kupendekeza serikali 2, na takwimu hata za watu 1000 tu.

Faida moja ya ni uwepo wa fiscal autonomy, hasara kubwa ni kutokuwepo fiscal autonomy.

Faida na hasara zinamgusa kila mtanzani. Narudia mfano huu, halmashauri 41 zimetengewa jumla ya Tsh Milioni 500 kwa ujenzi wa nyumba za Walimu, wastani wa sh 12.5Milioni kwa kila moja.
Kiasi hicho ni sawa na kujenga nyumba moja ya mwalimu.

Kuna kitu kinaitwa bunge la Jamhuri ya Tanzania. Hili lina wabunge kutoka halmashauri 41 nilizosema na nyingine nyingi.
Kuna wabunge kutoka znz wanaoiwakilisha zanzibar.

Zanzibar ina fiscal utonomy na ni nchi inayojitegemea kwa mujibu wa marekebisho ya katiba yao ya 2010.
Ina kila kitu nchi yoyote inachokihitaji.

Wabunge hao ni 81 na kwa mujibu wa wabunge wenyewe, kila mmoja analipwa Tsh milioni 10.
Gharama ya wabunge wake inapaswa kwenda znz kwasababu uwakilishi wao haumhusu Mtanganyika.
Kwanini tumbebeshe mtanganyika kodi ya sukari na chumvi ili kumhudumia mtalii kutoka nchi jirani?
Jibu lake ni moja hatuna fiscal autonomy hivyo tunawabebesha walipa kodi gharama zisizo wahusu na huu ni mfano mmoja rahisi sana

Kwa maneno machache, mshahara wa mwezi mmoja wa mbunge mmoja kutoka znz anayekuja Dodoma kwa shughuli za utalii ni 10Milioni, sawa na pesa zilizotengwa kwa ajili ya halamshauri moja na sawa na nyumba moja ya mwalimu.

Milioni 10/mwezi ni pesa za mlipa kodi ambaye ametengewa milioni 12 kwa halmashauri. Ukienda mbali zaidi utaona mtalii mmoja anaweza kujenga nyumba 100 kwa mwaka katika halmashuri inayojenga nyumba moja kwa mwaka.
Watalii wapo 81 nadhani unaweza kuona ni kiasi gani mkulima na mfanyakazi wa Tanganyika anavyoumia.

Ukumbuke kuwa wabunge hao watalii wanakuja kwa jina la JMT. Znz haina mchango mwingine zaidi ya hapo.
At least kwa miaka 10 Prof Humphrey ameonyesha hawajachangia chochote. Study ya kina Malyamkono inaonyesha zaidi kuwa si kwamba kuna huduma za muungano tu,bali kodi za walipa hoi zinavuka bahari kwenda nchi jirani kwa tune ya dollar milioni 850.

Kila pesa za serikali ni pesa ya mwananchi, iwe kodi, msaada au mkopo. Unaposema wananchi hawakosi sukari, apparently inaonekana ni kweli,kwa undani si chumvi tu ni zaidi ya hapo.

Na mwisho naomba nikuulize, hiyo Tanzania bara ni nchi gani? Ilianza lini na kutokea wapi?
 
"Tungejua kama hali ya aina hii itajitokeza, basi tungeanza na kura ya maoni, tungewauliza wananchi kama wanautaka muungano na kama ndiyo, basi uwe wa aina gani au serikali ngapi, mtu angesema moja, mbili, tatu na kadhalika," alisema Pinda jana kwenye Viwanja vya Bunge mjini hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom