Kumbe hela zipo kila mwaka,wananchi wana lazimishwa kuchangia gharama za kuendesha shule,....mwishoni hela zinarudishwa hazina eti zimebaki,kweli?
Msome Tundu Lissu
Akirejea takwimu za mahesabu ya Tamisemi, alisema kwa mwaka wa fedha 2008/2009 na 2009/2010 zaidi ya shilingi bilioni 30 zilizotengwa na Bunge kwa shughuli za maendeleo zilirudishwa hazina.
Tungependa kujua nafikiri wananchi wa Tanzania wanapenda kujua hizi fedha zimerudi kweli hazina au zimetumika kwa mambo mengine tusiyoyajua.
Na ni sababu gani zilizofanya zisitumike wakati Watanzania nchi nzima wanachangishwa fedha kwa nguvu bila kuwepo sheria, bila kuwepo utaratibu wowote unaotambuliwa na sheria za nchi hii ili kujenga na kuendesha mashule.
Hii ni moja ya sababu ya kupeleka hoja binafsi ya kutaka Bunge liichunguze hii ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili Bunge linalotoa fedha liridhike kwamba kweli hizi fedha hazijatumika kweli au zimetumika kwa mambo mengine, alisema
Hiki kichwa bana.........I concur kabisa 100%
Ili wabunge waweze kuifuatilia bajeti ya serikali kikamilifu na kisha waweze kuibana, ni muhimu kuomba serikali iwe inapatia wabunge vitabu vinavyoitwa Medium Term Expenditure Framework (MTEF). Vitabu ambavyo huwasilishwa kwa wabunge ni vile vye jumla kuu na wala siyo budget details. Hivyo wabunge hupitisha matumizi mabaya bila wao kujua, kisha mambo yakishafanyika eanahoji nani aliidhinisha.
Pili, wabunge wapewe vitabu vya bajeti at least 21 days kabla ya kikao cha bajeti, kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni za kudumu za bunge. Hii itawapa fursa ya kuichambua bajeti na kuihoji badala ya kugonga meza na kuuliza maswali ambayo hayarejei bajeti.
Kwa mfano mbunge anauliza, ni lini daraja la mto X litajengwa, kwenye mjadala wa wizara ya miundombinu, wakati hilo ni swala la TAMISEMI. Au mbunge anauliza lini jimbo lake litaunganishwa kwenye gridi ya taifa badala ya kuelekeza waziri apunguze pesa kwenye kifungu fulani ili zitengwe kuunganisha jimbo lake kwenye gridi ya taifa.
Nachojaribu kusema ni kwamba, matatizo hayo mawili waliyoyataja Tundu na John, na matatizo mengine, yamesababishwa na wabunge kutokuwa makini wakati wa mijadala ya bajeti. Manunuzi ya mashangingi hupitishwa na wabunge. Safari za kifahari za viongozi hupitishwa na bunge. Kisha wabunge wanalalamika serikali inatumia pesa kwa matumizi yasiyo muhimu!!!
Akirejea takwimu za mahesabu ya Tamisemi, alisema kwa mwaka wa fedha 2008/2009 na 2009/2010 zaidi ya shilingi bilioni 30 zilizotengwa na Bunge kwa shughuli za maendeleo zilirudishwa hazina.
"Tungependa kujua… nafikiri wananchi wa Tanzania wanapenda kujua hizi fedha zimerudi kweli hazina au zimetumika kwa mambo mengine tusiyoyajua.
"…Na ni sababu gani zilizofanya zisitumike wakati Watanzania nchi nzima wanachangishwa fedha kwa nguvu bila kuwepo sheria, bila kuwepo utaratibu wowote unaotambuliwa na sheria za nchi hii ili kujenga na kuendesha mashule.
"Hii ni moja ya sababu ya kupeleka hoja binafsi ya kutaka Bunge liichunguze hii ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili Bunge linalotoa fedha liridhike kwamba kweli hizi fedha hazijatumika kweli au zimetumika kwa mambo mengine," alisema