Elections 2010 Tundu Lissu Kuwania Ubunge Singida Kusini - Mashariki

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Tundu Antipas Lissu: Ataka ubunge Singida Kusini-Mashariki

Gazeti MwanaHalisi


MIAKA mitatu iliyopita, katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, yalitokea mambo makubwa mawili yaliyoyobadilisha mwelekeo wa siasa za upinzani nchini.

Kwanza, neno “fisadi” ambalo halikuwa linavuma, lilipata mvumo, tena wa nguvu kubwa hapa nchini. Linamaanisha wala rushwa wakubwa.

Pili, ilitangazwa orodha ya mafisadi maarufu kwa jina la “List of Shame.”
Ingawa Dk. Willibrod Slaa, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu ndiye amekuwa akitajwa zaidi kuhusiana na tukio hilo, wachache wanafahamu kwamba Tundu Antipas Lissu ndiye mhimili mkuu hasa wa mambo hayo.

Huyu ndiye aliandaa orodha hiyo ya mafisadi. Ni huyohuyo aliyeongoza kuingiza neno “fisadi” katika msamiati wa kisiasa Tanzania.

“Ukweli ni kwamba neno fisadi sikulitunga mimi. Limo katika kamusi zetu. Lakini lilikuwa halijavuma kama msamiati wa kisiasa. Lilikuwa likitumiwa zaidi nchini Kenya. Nikalichukua na kulitumia pale Mwembeyanga. Tangu hapo likawa maarufu,” anasema Lissu katika mahojiano yake na gazeti hili wiki hii.

Kwa miaka karibu kumi kabla ya tukio hilo la Mwembeyanga, Lissu alikuwa sauti ya wananchi na wanaharakati wa Tanzania katika kudai haki yao inayotokana na utajiri wa nchi katika sekta ya madini.

Wiki hii Lissu ametangaza nia yake ya kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Singida Kusini-Mashariki lililopo wilaya ya Singida Vijijini, mkoa wa Singida.

“Nafikiri umefika wakati kwangu kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo. Kuna mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya wananchi wa Singida na Watanzania kwa ujumla na najua naweza kutoa mchango mkubwa, anasema Lissu.
“Kwa wananchi wa Singida, nataka kukomesha vitendo vya unyanyasaji, uonevu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na viongozi wa serikali kwa wananchi,” anaelza Lissu.

Anasema wananchi wananyang’anywa mifugo na baadhi ya mali zao kwa madai kuwa hawajachangia katika mambo ambayo kimsingi mwananchi halazimishwi kuchangia.

“Lakini kubwa, wananchi wa jimbo langu wameanza kuhamishwa kwa lengo la kupisha shughuli za uwekezaji katika uchimbaji wa madini na utafutaji nguvu ya nishati ya umeme kwa kutumia upepo.

“Nataka wananchi wangu wasinyanyaswe katika uwekezaji huu. Nataka wafaidike, na unajua mimi ninafahamu jinsi ya kuendesha harakati katika mambo haya.

“Kitaifa, nafahamu bunge lijalo linahitaji kuwa na mtu kama mimi. Uzoefu wangu wa zaidi ya miaka kumi katika harakati za kusaidia wananchi na kufahamu matatizo makubwa, ni nyenzo muhimu katika eneo hilo.

Mwanasheria huyu anasema yeye ni mwanasheria na bunge ni chombo cha kutunga sheria. Hivyo kuwepo kwake kutamaanisha kuwa atahakikisha serikali inapitisha sheria ambazo kweli zina manufaa kwa wananchi.

“Yale mapambano dhidi ya ufisadi niliyokuwa nayaendesha nje ya bunge; Mwembeyanga na kabla ya hapo, sasa umefika wakati wa kuyahamishia bungeni. Mimi nikiwa ndani ya bunge, kwa kushirikiana na wenzangu, naamini tutalifanya kuwa bora zaidi,” anasema.

Lissu anasema atapenda ahukumiwe miaka mitano baada ya kipindi chake kwa mchango wake katika kutetea haki za wananchi na maslahi ya taifa ndani ya bunge.

“Mimi sina fedha za kuwaahidi wananchi wa jimbo la Singida Kusini-Mashariki kwamba nitawajengea shule ngapi au zahanati ngapi katika kipindi changu. Hizi ni kazi zinazopaswa kufanywa na serikali.

“Mimi ninataka kuwaahidi wananchi wangu utumishi uliotukuka na wa kifanisi. Sina fedha za kifisadi za kuwaambia nitawanunulia hili au lile. Mimi nataka kuwatumikia kwa kiwango cha juu,” anasema.

Akizungumzia ugawanywaji wa jimbo lake uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita, Lissu alisema hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Alisema jimbo ambalo kabla ya ugawanyaji lilikuwa likifahamika kwa jina la Singida Kusini, imegawanywa kwa sababu za kisiasa ili kumlinda anayeshikilia kiti hicho kwa sasa, Mohamed Missanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Jimbo la Manyoni, mkoani kwetu, ni kubwa mara mbili kuliko la kwangu, lakini halikugawanywa. Kama kigezo ni idadi ya watu, kuna majimbo kama Ubungo na mengine mengi tu ambayo hayakuganywa lakini yana idadi kubwa ya watu kuliko la kwangu.

“Kama suala ni miundombinu, Singida Kusini lina miundombinu mizuri kuliko maeneo mengi tu mkoani Singida na kwingineko nchini. Kuligawanya ilikuwa ni siasa tu lakini nawaambia hata wafanyeje, jimbo hili litanyakuliwa na CHADEMA mwaka huu,” anasema.

Lissu anasema ana imani kubwa ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu amefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

“Mimi nimejiandaa kuanzia mwaka 2008. Nimezunguka katika vijiji vyote vilivyopo katika jimbo langu kuzungumza na wananchi na kufahamu shida zao. Kwa sasa ninafahamu shida zao na wao wananifahamu na wanajua cha kutaraji kutoka kwangu,” anasema.

Lissu anazungumziaje matumizi ya fedha katika chaguzi hapa nchini?

Anasema ni kweli kwamba kama mtu hana fedha ni vigumu sana kwake kufanya vizuri katika uchaguzi. Si kwamba haiwezekani kushiriki, lakini ni vigumu kufanya vizuri katika mazingira yaliyopo.

“Nikupe mfano. Ili niende jimboni kwangu, kutoka Dar es Salaam, nahitaji kuweka mafuta ya takribani shilingi milioni moja. Kwa wiki, nikiwa jimboni, nahitaji kutumia kiasi cha Sh. 350,000 (laki tatu na nusu). Hayo ni mafuta tu.
“Hapo sijazungumzia gharama za chakula na malazi. Kwa bahati nzuri, sisi katika CHADEMA hatulipani posho. Ninapokula na kulala ndipo watu wangu wanapokula na kulala.

“Kwa hiyo, kama ningekuwa CCM, ningekuwa na kazi kubwa zaidi kwa vile ningehitaji kuwalipa posho wale wanaonisaidia. Kwa hiyo, bila ya kuwa na fedha, ni vigumu kuwafikia wananchi. Na kama huwezi kuwafikia wananchi, watakupigiaje kura?” anahoji.

Mwanasiasa huyu aliwahi kuwania ubunge wa jimbo analowania mwaka 1995 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi. Hata hivyo kura zake hazikutosha. Alichukua mgombea wa CCM, Yona Isingo.

“Wakati huo nilikuwa na umri miaka 27 tu. Wakati nakwenda kufanya kampeni nilikuwa na kiasi cha Sh 140,000 na ndizo nilizotumia. Nilipata kura takribani 6900 ambazo si haba,” anasema.

Lissu anasema ana matumaini makubwa na uchaguzi mwaka huu kwa vile chama kimekubalika jimboni mwake wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana.

Alisema mkoa wa Singida ulikuwa haujawahi kuwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa, diwani wala mbunge kutoka vyama vya upinzani “tangu kuumbwa kwa dunia,” lakini hilo lilikwisha mwaka jana.

Katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa, CHADEMA iliibuka ya pili kwa wingi wa viti vya serikali za mitaa, idadi ambayo, kwa mujibu wa Lissu, inatia matumaini.

Tundu Antipas Lissu alizaliwa katika kijiji cha Mahambe, kata ya Ikungi, tarafa ya Ikungi, tarehe 20 Januari 1968.
Alianza shule ya msingi Mahambe mwaka 1976 na alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa darasa la saba la kwanza katika shule hiyo mwaka 1982.

Baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa masomo ya sekondari – 1983 hadi 1986.
Mwaka 1987 hadi 1989, Lissu alijiunga na shule ya sekondari ya Galanos mkoani Tanga kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Kama ilivyokuwa kwa mujibu wa sheria enzi hizo, Lissu alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka 1989, ambako alikaa katika kambi ya Mafinga mkoani Iringa kwa wiki tatu na kumalizia katika kambi ya Itende mkoani Mbeya.

Mwaka 1991, Lissu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kitivo cha Sheria kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) ambako alipata zawadi ya mwanafunzi bora kuliko wote baada ya kumaliza mwaka 1994.
Lissu ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka shule ya msingi Mahambe kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Alipokwenda Uingereza katika Chuo Kikuu cha Warwick (Warwick School of Law, kwa ajili ya masomo ya shahada ya pili, aliweka pia rekodi ya kuwa mwanafunzi wa kwanza wa shule hiyo kufikia elimu hiyo.

Zaidi ya elimu hiyo aliyokuwa nayo, Lissu pia amewahi kufanya kazi ya mtafiti katika taasisi ya World Resources Institute (WRI) iliyoko Washington, Marekani kati ya 1999 na 2002.

Kazi hiyo ndiyo iliyompa nafasi kubwa ya kuzunguka nchi mbalimbali kueleza madhila yanayowakumba wananchi wa Tanzania wanaohamishwa kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini.

Lissu anaamini kuwa kipindi hicho ndicho kilikuwa cha mafanikio makubwa kwake kama mwanataaluma, kupita kipindi kingine chochote maishani mwao.

“Nimekuwa Marekani yote, Ulaya na kwingineko. Huko nimekutana na watu wa aina na kada mbalimbali ambao kubadilishana nao mawazo na taarifa, kumekuwa kwa msaada mkubwa kwangu na kwa taifa letu,” anasema.
Mwanaharakati huyu amesema bunge linalomaliza kipindi chake lilikuwa na mazuri yanayotakiwa kuendelezwa na mabaya ambayo yanatakiwa kuachwa na kutupwa.

“Hili ndilo bunge ambalo lilisababisha serikali nzima kujiuzulu wakati wa kashfa ya Richmond. Kulikuwapo na mijadala mikali ambayo ilikuwa na maslahi kwa taifa,” anasema Lissu.

Aidha, alisema ni bunge hili ambalo limekuwa la kwanza ambamo rais mstaafu alisemwa kuhusu vitendo vyake akiwa madarakani. Hii ilikuwa haijapata kutokea.

Amesema kitu kibaya kuhusu bunge hili ni kwamba kwa vile wabunge wake wengi walikuwa wanatoka CCM, kuna mambo hayakufikia tamati. Wabunge wa CCM walinywea ndani ya chama hicho.

Dawa ya kutibu ugonjwa huo ni kuchagua wabunge wengi zaidi kutoka upinzani na “kwa wananchi wa Singida Kusini-Mashariki, dawa yake ni kumchagua Tundu Antipas Lissu,” anasema.

Tundu Lissu, mwanasheria, mwanaharakati na mwanasiasa, ameoa na ana watoto wawili.
 
Kila laheri bungeni kutawaka moto 2011 - 15, watu kama kina Tundu Lissu wanahitajika wengi
 
Hawa ndiyo tunaowategemea kuleta changamoto anuwai bungeni! Ninaamini maslahi ya taifa akishinda atayaweka mbele
 
Kila la heri jemedari ila usiende kuwa kama dogo ambaye ameshaamua ku-take side na mafisadi. Naamini umeshapata fedha za kutosha za kazi yako hiyo hivyo usibababaishwe na hao mafisadi na vibaraka wao wanaowatetea kila kukicha. Washa moto mwanzo hadi mwisho. Bravo.
 
This is a good stuff so to say. Wishing you all the best as you prepare for that. Angalia usije ukawa kigeugeu kama mdogo wako Kabwe Zito:tinfoil3:
 
Nimekuwa nikisubiri kwa hamu sana kupata habari za Tundu Lissu kugombea ubunge. Anafaa sana. kwa wananchi wa Singida Kusini - Mashariki "this is the right option"
 
Ki Ukweli Huyu Jamaaa ni mzuri. We Msikilize anapokuwa anahojiwa kwaenye TV. He is Smart. Tundu neda kagombee ili uweze kutukuomba Watanzania wenzako
 
Hii itakuwa mara ya 3 anajaribu ubnge, nafikiri amejifunza ni wapi aliteleza hadi kukosa safari zilizopita.
 
Ki Ukweli Huyu Jamaaa ni mzuri. We Msikilize anapokuwa anahojiwa kwaenye TV. He is Smart. Tundu neda kagombee ili uweze kutukuomba Watanzania wenzako
Kifimbocheza, the guy is realy smart upstairs na amauweza wa kumiliki jukwaa ipasavyo. Jamaa ni kichwa mbaya tangu Ilboru na shria ndio mwake!.

Tatizo mimi ninaloliona ni moja tuu, awareness na misimamo ya watu wa Singida kuftokana na literacy level na poverty status.

Hili la awareness nililiona Busanda na Biharamulo, ambalo pia limekwenda sambamba na umasikini uliokithiri/topea, na hii ndio hali ya Singida. Mtu yuko tayari kuuza uhuru wake wote kwa kilo ya sukari, shibe ya pilau ya siku moja au t-shirt na kofia!.

Namuaminia Lissu ni strategist mzuri na hilo analijua, hivyo atajipanga vizuri na jimbo atalitwaa kiulaini kama kumsukuma mlevi!.
 
Kwa CV yake ilivyo nafikiri atakuwa na nafasi nzuri ya kuwawakilisha wananchi wa Singida Kus-Mash. Keep on Tundu Lissu kazi yako inaonekana na wengi.
 
Kama uelewa huko singida waweza kuwa tabu kidogo, Yeye agombee hata majimbo ya DSM, hiki kichwa kiko juu na kinakubalika sana! All the best
 
Mimi namuunga mkono kabisa!!! NImekuwa nikisubiri kusikia an activist anaingia Bungeni... huyu ni mmojawapo..
 
mimi jamaa huyu namkubari sana, ningekuwa singida ningemsadia kupiga kampeni, akifanikiwa kuingia bungeni mwaka huu jua kuwa bunge la 2010-2015 itakuwa moto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom