Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
Ulitaka aulize kwa sauti ya mahaba? lazima iwe kwa kejeli hasa kiongozi anapokiri wazi kuwa jambo hilo limemshinda. Tatizo la madaktari ni nyeti kwani linahusu uhai wa watu tena waliokupa uongozi,sasa ukionyesha kushindwa kwa nini usiulizwe kujiuzulu.
Hata hivyo kama ni kejeli au mahaba haina maana yeyote,muhimu ni uzito wa swali. Namshangaa spika kutaka lisijibiwe swali muhimu kama hilo.
 
Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
"kwa sauti (Tone) ya kejeli" ​this is too subjective. pinda alitakiwa kutaja sababu za kwani hatajiuzulu badala ya kakasirika kwa kuulizwa lililonyooka vile!
 
'...Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana....'

Kuheshimiana hukohuko kwenye nec mnapochekeana kwenye mambo ya msingi hapa kazi tu,hukuwa PM ili upewe heshima ulipewa uPM ili uweze kuleta tija kwa taifa kuwa na uwezo wa kutatua matatizo kama hili la madaktari.Heshima huko nec,kwa mkeo na watoto wako kwa watanzania kazi tu.
Tupa kule Pinda Toothless Dog!..
 
Wazo lako la kusubiri hadi baada ya miaka mitano ndo usuluhishe kwa kuchagua chama kingine si wazo la kidemokrasia. Demokrasia ni pamoja na kukosoana au kukubaliana kutofautiana lakini bila kugombana. Kwa hali ilivyo unataka tuamini kuwa matatizo ni kuyasubirisha 2015 ili tuje tuchague chama kingine badala ya CCM. Wazo hili upungufu wake ni kuwa tayari baada ya miaka mitano tutakuwa hatuna hata pa kusemea na uchaguzi unaweza usiitishwe tukiendelea na ubabe walionao jamaa hawa kwa sasa. Kwa hiyo lazima waelezwe mapema isijefika 2015 wakasema hatutoki ng'o

Wazo si langu mimi la kusema eti wasubiri miaka mitano nilichoongelea ni masuala ya siasa za demokrasia unapochagua mtu au kitu na unaelewa mkataba wake sharti usubiri tena mpaka utapopata fursa ya kuchagua tena (hata bidhaa unayo nunua dukani ikiisha waranty ujue pole ikiaribika solution ni kununua nyingine tu). Lazima tujifunze kuishi kwenye dunia ya ukweli kama watu wazima na ukweli wa mambo ndio huo, thus far we elect.

Hivyo hapa serikali chini ya mwongozo wa CCM haijaipa kipaumbele upande wa afya hivyo si kosa la wagonjwa ni kusubiri tu uchaguzi ujao labda kuweza badilisha serikali iliyopo labda itajali. Ningekubali sana hawa jamaa kugoma kwa kutaka kuondolewa kwa viongozi wa serikali (waziri na naibu wake kwenye secta ya afya) au ambao wapo chini ya serikali kwa utendaji na utekelezaji kama (katibu mkuu na wasaidizi wake) kwa kuzuia ufanisi au kuharibu matumizi kama wanaushahidi.

Lakini huwezi goma kwa sera ya mbovu tu, mfano waingereza nadhani kuna mgomo wa madaktari unakuja lakini si kwa sera mbovu za serikali bali kwa sababu serikali inataka kuwaamulia jinsi ya kupanga pension plans mpya madokta. Hapo ni maslahi ya madokta personal yameguswa na yanataka badilishwa bila ya idhini yao.

Lakini hawakugoma kwa sababu ya sera za privatisation ambazo ni serikali inaona zitatoa ufanisi bora ingawa madokta hawazipendi kwa sababu zitawaongezea majukumu na kufanya kazi katika mazingira magumu, hila kwa sababu wao kazi yao ni kutibu kutokana na walichonacho hawana budi ndio siasa tena.

Ukitaka serikali itakayo jali hayo subiri chaguzi zingine muwatowe waliopo, maana labda pengine wagonjwa wameridhika ndio maana hawaoni sababu ya kuandamana kwa huduma mbovu so why should the doctors intervene huwezi kazi acha. Lakini usilalamike working conditions ikawa sababu ya kuwauwa wasiopanga sera that is just immoral.

Na hata madaktari wanaotaka kugoma wa uingereza wameshasema kabisa no emergency patience will be affected or those in need of intensive care. Huko ndio kugoma responsibily sasa hawa wanakurupuka tu kutaka kuwasemea wagonjwa huku wakiwaadhibu for god sake how many professionals in our country work with limited resources lakini hawagomi ovyo. Kunahitajika mabadiliko lakini na watu wanahitaji kutambua haki zao na si sawa kuwaadhibu a majority of ignorance kwa makosa ya wengine.

Doctors should know better.
 
Mwl. Nyerere aliulizwa swali na mwandishi mmoja wa kiingereza.. wakati alipotembelea Uingereza mwaka 1984 akiwa kwenye ziara ya kuaga kabla ya kung'atuka uraisi kwamba kwa nchi kama Tanzania yeye Mwalimu angeweza kuendelea kutawala bila ya matatizo au upinzani sasa ni kitu gani kilichomfanya (Mwalimu) ang'atuke..? Mwalimu alijibu na ninanukuu hapa.. "Nilichoshindwa kukifanya ndani ya nchi yangu ndani ya miaka 23 ya utawala wangu hata nikipewa miaka mingine 40 cintoweza kukifanya..! Ni wakati wa kuachia damu mpya na yenye fikra na mawazo mapya"..!
Sasa Mr. Pinda kama umejaribu umeshindwa maana yake huna tena jipya na i think Mr. Lisu na wote wanaotaka uachie ngazi wako sahihi.. Kama mnadai mnamuenzi Mwalimu basi huu ndio wakati wako Mr. Pinda kuonyesha kwa vitendo.. Please do the right thing.. Utakumbukwa kwa ujasiri wako..
 
Kwa watu wanaoelewa na kukubali utawala wa demokrasia/vyama vingi, basi watakubaliana na kauli ya Lissu 100%. Alichosema na namna alivyosema Lissu ndivyo inavyotakiwa. Mh Pinda anafanya 'zilipendwa' akisaidiwa na Spika, lakini gharama za huu muziki wa zilipendwa zitalipwa na CCM.

Kwa kiongozi yoyote ambaye anashindwa kufanya yale anayooamini na ambayo wanachi wanamtegemea kwa sababu zozote zile (iwe mfumo, ugonjwa, whatever) basi kiongozi huyo anatakiwa ajiuzulu. Kuendelea kukalia kiti ni sawa na kugeuka jiwe. Katika hali ya sasa Pinda hawezi kusema ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari halafu akaendelea na kazi zake kama Waziri mkuu. Haiwezekani. Ama unaondoa vizingiti (mfumo mbaya) au vizingiti vinakuondoa. Lakini vyote viwili haviwezi kubaki halafu tukasema tuna uongozi bora. Tuna shida sana na mentality ya zilipendwa.
Unanalalamika nini waziri wa marekani alijiuzulu kwa kusinzia kwenye gari tu ndio itakuwa pinda kushindwa kutatua kitu kinachohitaji hekima yake?!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe.Lisu hakutenda haki.Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima.Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo.Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima,aache ulaji alionao sasa,ni sawa na kumwambia ajiue.
Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema : 'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?'.Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.Lakini Pinda alisema '...Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana....'
Kama kwelikazi imemshinda nakwa kukiri yeye mwenyewe sijui kwa nini bado ni waziri mkuu kwani hana maamuzi na yupo tu pale kama kivuli kwani hakuna anachoamua na idadi kubwa ya wananchi inaumia kwa kukosa kwake uamuzi kama waziri mkuu. Kiukweli angejiuzuru tu kwani ni dhaifu na haiwezi hiyo kazi. kwani yupo hapo kwa ajili ya kufanya kazi gani haswa kama mgomo unaoleta madhara makubwa ameshindwa kuutatua kwa kumshinikiza raisi wake kwa kufanya maamuzi?
 
Lisu siyo SHOGA kuongea na Mwanaume mwingine kwa SAUTI LAINI.

Hiyo ya kuongea na PM kwa sauti laini ni kazi ya Mamaa Tunu Pinda.

pinda.jpg

Nimecheka mpaka machozi yamenitoka
 
Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe.Lisu hakutenda haki.Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima.Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo.Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima,aache ulaji alionao sasa,ni sawa na kumwambia ajiue.
Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema : 'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?'.Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.Lakini Pinda alisema '...Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana....'
Hapo kwenye Red Kama akishindwa Kulia naamini atakesha usiku wa leo Mischozi Hinha
 
It is sad jinsi unavyo comment about doctors. Nadhani hujafanya uchunguzi why more than 700 doctors wanagraduate lakini chini ya madakatari 200 wanakubali kufanya kazi Tanzania? Kwa nini nchi kama Botswana wanajivunia madaktari kutoka TZ na kwa nini wengi wanakimbilia huko?

Wazo si langu mimi la kusema eti wasubiri miaka mitano nilichoongelea ni masuala ya siasa za demokrasia unapochagua mtu au kitu na unaelewa mkataba wake sharti usubiri tena mpaka utapopata fursa ya kuchagua tena (hata bidhaa unayo nunua dukani ikiisha waranty ujue pole ikiaribika solution ni kununua nyingine tu). Lazima tujifunze kuishi kwenye dunia ya ukweli kama watu wazima na ukweli wa mambo ndio huo, thus far we elect.

Hivyo hapa serikali chini ya mwongozo wa CCM haijaipa kipaumbele upande wa afya hivyo si kosa la wagonjwa ni kusubiri tu uchaguzi ujao labda kuweza badilisha serikali iliyopo labda itajali. Ningekubali sana hawa jamaa kugoma kwa kutaka kuondolewa kwa viongozi wa serikali (waziri na naibu wake kwenye secta ya afya) au ambao wapo chini ya serikali kwa utendaji na utekelezaji kama (katibu mkuu na wasaidizi wake) kwa kuzuia ufanisi au kuharibu matumizi kama wanaushahidi.

Lakini huwezi goma kwa sera ya mbovu tu, mfano waingereza nadhani kuna mgomo wa madaktari unakuja lakini si kwa sera mbovu za serikali bali kwa sababu serikali inataka kuwaamulia jinsi ya kupanga pension plans mpya madokta. Hapo ni maslahi ya madokta personal yameguswa na yanataka badilishwa bila ya idhini yao.

Lakini hawakugoma kwa sababu ya sera za privatisation ambazo ni serikali inaona zitatoa ufanisi bora ingawa madokta hawazipendi kwa sababu zitawaongezea majukumu na kufanya kazi katika mazingira magumu, hila kwa sababu wao kazi yao ni kutibu kutokana na walichonacho hawana budi ndio siasa tena.

Ukitaka serikali itakayo jali hayo subiri chaguzi zingine muwatowe waliopo, maana labda pengine wagonjwa wameridhika ndio maana hawaoni sababu ya kuandamana kwa huduma mbovu so why should the doctors intervene huwezi kazi acha. Lakini usilalamike working conditions ikawa sababu ya kuwauwa wasiopanga sera that is just immoral.

Na hata madaktari wanaotaka kugoma wa uingereza wameshasema kabisa no emergency patience will be affected or those in need of intensive care. Huko ndio kugoma responsibily sasa hawa wanakurupuka tu kutaka kuwasemea wagonjwa huku wakiwaadhibu for god sake how many professionals in our country work with limited resources lakini hawagomi ovyo. Kunahitajika mabadiliko lakini na watu wanahitaji kutambua haki zao na si sawa kuwaadhibu a majority of ignorance kwa makosa ya wengine.

Doctors should know better.
 
hivi hii serikali dhaifu unataka ibembelezwe hadi lini yameshindwa kutatua mgomo watu wanakufa halafu unataka wabembelezwe!!!!!!!!!
 
It is sad jinsi unavyo comment about doctors. Nadhani hujafanya uchunguzi why more than 700 doctors wanagraduate lakini chini ya madakatari 200 wanakubali kufanya kazi Tanzania? Kwa nini nchi kama Botswana wanajivunia madaktari kutoka TZ na kwa nini wengi wanakimbilia huko?
Hakuna pahala nilipo wasema vibaya Madokta hakuna pahala niliposema madai yao hayana msingi ninachosema serikari ni mbovu lakini kuna namna zingine za kuipa pressure na si kwa kuwaadhibu wasio husika.

Maana wanachokifanya si kutoa pressure or be it the pressure wanayotoa inaambata na shughuli za mungu (ndio wanachokifanya sasa) na hapo ndipo sikubaliani napo. Kwanini tupoteze watu kwa makosa ya wangine kisa madktari wameamua (kuchukua kazi ya mungu) hiwe hivyo no Sir.
 
Kuheshimiana kati ya PM na Mbunge Lissu ni jambo jema maana wote ni WaTz. Hilo haliondo nafasi ya mbunge kueleza ukweli maana huko sio kumvunjia heshima bali kuweka mambo sawa. Ikiwa anamheshimu na anatuheshimu- tena akakiri amefika mwisho wa uwezo wake. Hakuna hata chembe ya dharau kwenye kauli ya Lissu. Ajiuzulu ili ambao wana uwezo wa kufikiri kidogo zaidi ya hapo alipofika wapate nafasi ya kuokoa taifa.
 
Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!

Wtz wenzangu tuache ushabiki, kama umeishawahi kushirikia vikao vya wabunge kama mtaalam(siyo mbunge) siku zote wanajivunia kuongea kwa jaziba, nafuatilia bunge sana, unakuta mbunge anaongelea kilimo kwanza anavyofoka na kutokwa na mate mdomoni utafikiri ana lima kwa jembe yeye mwenyewe na hivyo anaomba msaada kwa kuachia hilo jembe, kauli za wabunge siku zote ni kuwa wanaendesha mambo yao kwa mijadala bila kujali style kila mmoja anayotumia (bila kuvunja) kanuni. Hivyo ndivyo ilivyo. Je kama spika ameshindwa kuona kwa utaratibu wa kuendesha bunge (kanuni) kuwa Lisu amevunja sheri je ni wajibu wetu sisi tulioko nje ya bunge kuhukumu kuwa mbunge fulani amekosea au ni mwendelezo wa makundi hata kama suala hilo halina maslahi kwa taifa?
 
Ndugu wana JF, Hii kauli ya Mh. Lisu kwa PM. PINDA... je ni stahiki kwa mzingira tuliyonayo (kisiasa, kiuchumi, kiuwajibikaji, kitamaduni nk) ama inawalakini?
Mh Lisu akifuatilia swala linalojirudia rudia la madaktari kugoma alimuuliza Pinda '" Kama umefanya kwa uwezo wako wote kutatua mgogolo wa maktali, kama ulivyoahidi kwamba utalishugulikia na halita jirudia tena lakini bado tatizo liko palepale na madaktali wamegoma tema , je kwa nini husijiuzuru?"
Pinda halionyesha wazi kutofurahia swali hilo kwa kusema anamuheshimu sana Lisu na hakutegemea approach kama hiyo.

Sikuwemo mjengoni lakin kwa ufupi haya mambo yalienda hivyo. Sasa naamini hapa tunaowatu mbalimbali wanaoweza kutusaidia kufanya uchambuzi wa jambo hili kwa nyanja zote ...kitaratibu/kimaadili, kisheria, kitamaduni nk

Binafsi nakumbuka jambo moja, kabla ya kuja kwa Makismo timu ya taifa, taifastar, ilikuwa na record mbaya ya matokeo kimataifa, lakini baada ya jitiada za new coach taifa star ilibadilika na kuanza kupata ushindi wa nje na hata kufikia kukaribishwa Dodoma Bungeni kupongezwa! Mambo mengi yaliongelewa kuhusiana bad perfomance ya team wakati huo, lakini nakumbuka kati ya mambo aliyobadili couch Maksmo ilikuwa ni kubadili fikra mnato kwamba baadhi ya wachezaji fulani wenye majina makubwa wasipokuwemo kwenye kikosi basi taifastar haiwezi kuwa taifa star! Baada ya kuliona hili, Makismo alitafuta wachezaji vijana wanaofundishika na kuachana na wachezaji wenye majina ya mpira lakini wasioweza tena kucheza mpira na kubadili record ya taifa star! Maneno mengi aliambiwa na hata kutukanwa lakini baada ya timu kuitwa bungeni kupongezwa maneno yote yaliisha.

Naitazama kauli ya Lisu kwa Pinda kuwa na mtazamo kama wa Makismo!......Kama umefanya kila unachoweza kutatua tatizo lakini umeshindwa, sasa umekimbilia mahakamani. Ni kwa nini husimwachie mwingine anayeweza kutatua tatizo hilo! Ufumbuzi hautatokana na mahakama kulazimisha madaktari kufanya kazi, polisi kutumia nguvu zidi ya madaktari, kuunda genge la mauaji zidi ya madaktari bali itahitaji altenative thinking ya busara kutumika basi! Social conflict/changes/crisis are never controlled by force from the police, mahakama nk

Kwa hiyo kama ni utamaduni/desturi zetu kuoneana aibu kwa sababu unajina kubwa, wakati watu wanateseka na kufa nafikiri utamaduni huu tuuzike kabisa na kuachana nao
 
Mheshimiwa Liszsu ana pointi. Taabu ya PM wetu wa sasa nikusema maneno bila kuyapima kabla ya kuyatamka. :spy:
 
Back
Top Bottom