Tundu Lissu aunguruma....Waziri mkuu awajibike

Nashauri mmoja wa wabunge wa CHADEMA aanzishe hoja ya kutokuwa na imani na serikali ili tupembue mchele na chuya kutoka wabunge wa CCM kama hasira wanazoonyesha ni za kweli au wanatupiga changa la macho?

Hili linatakiwa lifanywe na Zitto atakapohitimisha hoja yake. Aweke motion ya kutokuwa na imani na serikali kisha wabunge wa CDM wasibweteke wasimame kuunga mkono tuone kama magamba wataunga mkono? na wananchi waone nani kweli anawatetea.
 
Mgamba yana nia moja tu yaani kushindana na Bill Gate kwa utajili.
 
Filikunjombe leo kaua kabisa kawataja mawaziri wote wezi! Lukuvi kamuambia awataje!
Wananchi mbalimbali wanaoujua wezi unaofanywa na mawaziri wetu tumpe ushirikiano Filikunjombe ili uthibitisho wake uwe umeenda shule na kama vipi utumike kwenye kuipiga chini serikali kwa kuforce mawaziri tajwa wastep down ili kupisha uchunguzi kulingana na ushahidi/uthibitisho wa Filikunjombe. Good Enough ni maneno haya yametoka kwa mwana CCM mwenzao. Tunashkuru Mungu kwa hili maana naamin ujumbe wa CDM umeanza kuwafikia na kueleweka hata ndani ya CCM wenyewe.
 
Pinda kweli hana dhamira ya kumkomboa matanzania aliyofanyiwa ccm na anavyoyaona mambo angetoka tu
 
Punguza UDINI, tizama kweli.
Kweli nimeamini watanzania wanafiki. Wanalalamika serikali dokozi halafu wao wenyewe wanaomba rushwa!!!! Je tutafika. Anzeni wenyewe wapinzani kuwa waadilifu mtapata nguvu ya kuiangusha serikali dokozi. Vyenginevyo mnampigia mbuzi gitaa bure!!!!
 
Kwa kweli ifikie wakati sasa wabunge hawa wetu wafanye kazi kwa vitendo na si maneneo na kuogopana.

Wataleta historia mpya ya tanzania km watatkeleza yafuatayo.

1. Kumpigia kura waziri mkuu kutokuwa na imani nae hivyo kumuondoa madarakani, hii itasaidia kuitingisha serikali na kuona sasa bunge lina nia ya dhati ya kuikomboa nchi hasa wanamchi walio ktk lindi la umasikoni.

2. Kugoma kuendelea na vikao vingine au mijadala mingine hadi haya yanayojadiliwa leo yawe yamefanyiwa kazi na hatua zimechukuliwa. Na wote waliohusika kutafuna hela za serikali wamefanyiwa kazi.

3.Kama katiba inaruhusu kumwajibisha raisi au kumpa barua ya warning alert kuhusu mustakabali mzima wa mwenendo wa viongozi wetu na masilahi ya tanzania.

Unaweza ongezea.
 
Pinda kweli hana dhamira ya kumkomboa matanzania aliyofanyiwa ccm na anavyoyaona mambo angetoka tu

Pinda ndiye mnafiki na msaliti namba moja Tanzania.Huwa anaonyesha masikitiko na kutoa machozi ya kinafiki wakati anapoona matatizo yanayotokana na umasikini wa kutengenezwa.Wakati huohuo hafanyi lolote la kuwawajibisha watu wake.
 
ndugu zangu morogoo hatuna mwakilishi bungen hat jimboni hatuna pakusemea jimbo lipo "wazi" uongozi wa cdm mkoa movement yao ni very slow cdm taifa njoon pls
 
Wanachofanya baadhi ya wabunge wa CCM nikuhadaa wananchi na kujitafutia umaarufu. Jana wamepokea Juzi wamepokea rushwa na kupitisha mabozo kwenye ubunge wa east africa leo wanakemea ufisadi!!!!!!!!! Acheni upuuzi tafuteni wajinga wengine wakuwadanganya.
Mnamkumbuka Mwakyembe kwenye Tume ya inayofahamika kwa jina lake.. Alisema mengine hatuyasemi kwakulinda heshima ya serikali. Serikali haijabadilika sana na heshima yake bado inapaswa kulinda. Tusitegemee chochote kutoka kwa hawa wezi.
 
Kama kweli mna ubavu na uchungu mlioonyesha kwenye uchangiaji wenu wa report za kamati za Bunge ni wa kweli kutoka moyoni basi chukueni hatua madhubuti tuone kweli mko serious na mnacho lalamikia. Pigeni vote of no confidence to the government. Tumewazoea miaka yote kamati zinapo wasilisha taarifa zao mmekuwa mnatuletea usanii wa kuvunga mnalaumu mapungufu yaliyopo serikalini mwisho wa siku mnapulizia na kuunga hoja. Ya Jairo na kelele zenu yameishia wapi?

Tuna waangalieni tu na sidhani hata hiyo 2015 mtafika. Hatuto subiri kuingia barabarani tena kama mlivyozoea bali msituni. Tuone Jeshi letu ni la wananchi kama jina lao lilivyo au la mafisadi. Pamoja na uozo wote wa serikali wao wako kimya tu.. sasa tuna majeshi kweli au masanamu? Je, mnalinda wavamizi wasitoke nje ili walioko ndani watumalize vizuri? kuna tofauti gani ya kuvamiwa hapa? kwa mtindo huu wa magamba ni kama nchi imevamiwa tena kwa uvamizi wa aina mpya kutokea ndani wala siyo uasi kwa tafsiri halisi ya uasi, chukueni hatua. Msidhanie tunashindwa kupata silaha na kuzitumia. Kumbukeni wengine jeshini tulipitia tuna mshukuru hayati Nyerere kwa hilo. Tuna kuhesabieni siku tu..

Tulipo fikia kwa sasa serikali haiwezi tena kuchukua hatua na wala haina ubavu huo. Tuna mifano mingi ya mambo mazito ambapo wameshindwa kabisa kufanya lolote. Kilicho bakia kwa sasa ni majeshi kuingilia kati kama Guinea Bissau au kwa mara ya kwanza Tanzania iwe na waasi. Mapori tunayo mengi ya kuanzia front na vijana wasio na kazi watalianzisha. Mnapo sikia EL anawaambia vijana wasio kuwa na kazi ni bomu litakalo lipuka wakati wowote mnaona ni ndoto eh? subirini..
 
Wananchi mbalimbali wanaoujua wezi unaofanywa na mawaziri wetu tumpe ushirikiano Filikunjombe ili uthibitisho wake uwe umeenda shule na kama vipi utumikwe kwenye kuipiga chini serikali kwa kuforce mawaziri tajwa wastep down ili kupisha uchunguzi kulingana na ushahidi/uthibitisho wa Filikunjombe. Good Enough ni maneno ya mwana CCM mwenzao.

Kiongozi tutawasumbua wananchi bure!
Report ya Lema juu ya uongo wa waziri mkuu isomwe kwanza ndipo Filikunjombe alete ushahidi!
 
Hili linatakiwa lifanywe na Zitto atakapohitimisha hoja yake. Aweke motion ya kutokuwa na imani na serikali kisha wabunge wa CDM wasibweteke wasimame kuunga mkono tuone kama magamba wataunga mkono? na wananchi waone nani kweli anawatetea.
Mimi natabiri leo ni mwisho wa serikali ya JK, mana kama Zitto atatoa hoja ya kuiangusha serikali kwa vote of no confidence, naimani hata CCM wataiunga mkono mana kwa kweli wote tumechoka na hizi puluzai za serikali yetu dokozi na isiyo na dhamira ya dhati kukwamua wananchi wake kwenye lindi hili la ufukara. Na ninajua baada ya serikali yetu kuangushwa jioni ya leo wabunge wengi wa ccm watahamia chadema, so CDM Jembe litaongoza nchi na kumalizia safari ya ukombozi wa kweli waloianzisha.
 
Punguza UDINI, tizama kweli.

Hembu changanua udini niliouonyesha? Udini ni nini na unautambuaje? Mie nilichosema kwani ni uongo kwasababu nikuulize hakuna wabunge walioomba rushwa wakati wa uchaguzi wa East Africa? Wako walioomba laki 5 hadi milioni 1. Sasa wanabwata nini katika serikali iliyojaa watu wenye sifa kama zao wakati wao wenyewe walaji rushwa??? Huo ni unafiki tena wa hali ya juu ndio maana mie sina chama kwani WATANZANIA SISI NI WANAFIKI SANA!!!!!
 
Wapige kura ya kutokuwa na imani na RAISI tena sio kwa kunyosha vidole bali iwe ya siri!
 
Hakuna sehemu yoyote ambayo bunge lina mamlaka ya kufukuza zaidi ya Kumkamata Waziri mkuu... na waache usanii, huyo ndiye saizi yao... the rest ni porojo... this is according to katiba.
 
Kweli nimeamini watanzania wanafiki. Wanalalamika serikali dokozi halafu wao wenyewe wanaomba rushwa!!!! Je tutafika. Anzeni wenyewe wapinzani kuwa waadilifu mtapata nguvu ya kuiangusha serikali dokozi. Vyenginevyo mnampigia mbuzi gitaa bure!!!!

Kama huoni jitihada za wabunge wa CDM basi una matatizo. Usiseme wanaomba rshwa taja mmoja mmoja anayeomba rushwa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom