Tundu Lissu atunukiwa Nishani ya Heshima Marekani

Mimibaba

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
4,557
1,291
"Wanabidii wenzangu,

Nadhani sitakosea kuwashirikisha habari njema kidogo. Leo hii tarehe 6 Mei 2011, Chuo Kikuu cha Bridgeport kilichopo mji wa Bridgeport, Jimbo la Connecticut nchini Marekani kimenitunuku nishani ya 'Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Bridgeport' (Honorary Fellow of the International College).

Citation ya nishani hii inasomeka kwamba 'Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu cheo cha Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa kwa kutambua utumishi wake uliotukuka katika kuendeleza haki za binadamu, ujenzi wa demokrasia na ulinzi wa mazingira katika Tanzania na Afrika...

' Kwa Kiingereza: 'In recognition of his inspired service for the furtherance of human rights, democratic institutions and the protection of the environment in Tanzania and in Africa..."

Tuzo hii imekabidhiwa kwangu na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa Dr. Thomas J. Ward na Rais wa Chuo Kikuu cha Bridgeport Dr. Neil Albert Salonen.

Kwa wale wote ambao wanaweza kuwa wanajiuliza kwa nini sijaonekana Mbeya na Nyanda za Juu Kusini, hii ndio sababu ya utoro wangu.

Nitajiunga na makamanda wenzangu kuanzia wiki ijayo.

Wasalaam,

Tundu"

Nimetundika hiyo msg ya Mh. Tundu Lisu iliyoko "wanabidii" kwa kufurahishwa na kutambuliwa kwake kimataifaa na kujibu tashwishwi za kutokuwepo kwake kwenye maandamano ya Mbeya.

Hongera Tundu Lisu, Hongera Chadema thamani yenu inaheshimika.

Kitaeleweka tu.
 
Vipi Tambwe hapewi jamani?teh teh teh teh,ahaaaa,maskini wavua magamba!

PIPOOO.....,ndugu yetu,mbunge wetu,Lissu,pale bungeni Mama wa Makida anatafuta kila njia uingie mkenge,but always stand smart as for us we trust u,no matter what,the truth speaks tself to reveal the essence of the truth! The ALBAMA MATCH STILL GOES ON!
 
Bora hata hiyo inatambulika kimataifa kuliko hizi wanazokabidhiana watu wenye magamba na vyuo vyao vya kata!! Tuzo za Udhamiri/Uzambivu na Uchakachuaji.

View attachment 29503
 
Hongera sana Mr Lissu usibweteke, endelea na kazi, kaza buti, jiamini na watanzania wataendelea kuwa nyuma yako
 
Tunajua lazima mambo kama hayo yaje kwako kwani tunaziona juhudi zako .kaza but usichoke we ni mzalendo wa kweli katika taifa letu.kama ilivyokuwa pale bungeni siku ya mjadala wa mahakama tuliona juhudi zako za kutete democrasia katika nchi yetu japokuwa ulishindwa lakini ukweli utabaki pale pale.
 
Hongera sana Mh.Lisu. You deserve that.
Mungu akubariki sana, akujalie afya njema, na damu ya Bwana YESU akufunike.Maadui wako washindwe kwa jina la YESU.
You are not alone, wapenda haki tuko pamoja na wewe.
Naomba wananchi wa jimbo la Mheshimiwa wampongezi mbunge wao.
 
Hongera sana Mh.Lisu. You deserve that.
Mungu akubariki sana, akujalie afya njema, na damu ya Bwana YESU akufunike.Maadui wako washindwe kwa jina la YESU.
You are not alone, wapenda haki tuko pamoja na wewe.
Naomba wananchi wa jimbo la Mheshimiwa wampongezi mbunge wao.
 
Mkuu Lissu,we ni icon ktk bunge letu. Kama alhaj dr dr dr pres.jk alisema bora dr Slaa apate kura kuliko wewe kwenda bungeni tayari alishakubariki kuwa wewe ni tishio. You are my 2rd Role model after dr Slaa ! Gud gud!
 
Back
Top Bottom