Tundu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake

isango alikuwa akitoa update wakati ule wa kesi..ukisoma mtiririko na jinsi mashahidi wa ccm walivyokuwa wanahangaika na wengine kununuliwa na ccm na walipofika mahakamani wakakili kupewa hela ili waje watoe ushahidi ni dhahiri kesi hii lissu anashinda lakin kwa hila za ccm lolote laweza kutokea
 
Tumeshafika mahakamani, wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari wapo wengi sana katika eneo la mahakama. Polisi ni wengi sana, ndani na nje ya mahakama. Kilicho cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi wapo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kumkagua kila anayeingia mahakamani, tunapekuliwa hasa, hadi wabunge wanaoingia. Kuna baadhi walikatazwa kuingiza magari yao mahakamani lakini baada ya vuta nikuvute, magari yapo mahakamani, na watu wamtinga ndani tunasubiri yatakayojiri.......... tutawajuza, leo kamanda nipo gado, Mungu amenijalia afya.

Pamoja na kuchelewa sana, sasa jaji Moses Mzuna, ndo anatinga mahakamani, nitaendelea kuwajuza, ila naomba watu ambao hawapo mahakamani waache kutuma threads zingine zinawachanganya wasomaji.Ving'ora vya jeshi la polisi vinalia nje, vitisho kila kona utadhani kuna msafara wa Rais wa Marekani humu

aminia mwana, ngoja tusubiri tuone kama jaji ni wa voda fasta au vp!
 
Katika vitu ambavyo CCM wanaogopa kwa sasa ni uchaguzi mdogo maana kwa sasa wanadondoshwa hadi kwenye vijiji. Kwa maana hiyo watalazimika kuacha dhamira yao ya kumpora Lissu ubunge, au watampora na kumfungia asigombee tena. Katika haya mapambano ambayo tunakaribia kushinda hata wakimpora Lissu ubunge watakuwa wanampiga chura teke tu.
 
Hivi hii kesi Mh. Lissu anaweza kushindwa!!!!??

Kesi ambayo ccm wamekuwa wakikimbia, mara wamesahau nakala gesti!!? Mara shahidi alikuwepo hasubuhi mchana haonekani!!!?


si ndio hapo mkuu..wengi walikuwa wanakimbia na wengine kuhongwa na ccm ili watoe ushahidi lakini waliumbuana....mara nyingi walikuwa wanakimbia mahakamni halafuleo lissu akishindwa itakuwa ni hujuma kubwa sana
 
Polisi wamejaa kila kona ya mji wa Singida,hali si shwari.

Wanahofia nini? clearly ni kuwa hukumu itakuwa against Lissu. This is no doubt otherwise wangelijua kuwa Lisu atashinda wasingelileta polisi wengi. Let us wait and see!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
getini penyewe unaambiwa wamesimama maafisa wa polis wa ngazi za juu...yaani ni full vitisho

Halafu tunaambiwa kuna uhuru wa mahakama kwenye Dola yetu! Hivi mmewahi kujiuliza ni nani anapanga kalenda ya matukio kwenye dola yetu? Angalia namna watanzania wanavyohamishwa mawazo yao kutoka kwenye issues. nitarudi kufafanua. I bet hukumu hii sio rafiki kwa TL
 
Hivi hii kesi Mh. Lissu anaweza kushindwa!!!!??

Kesi ambayo ccm wamekuwa wakikimbia, mara wamesahau nakala gesti!!? Mara shahidi alikuwepo hasubuhi mchana haonekani!!!?

Mmagamba Kama kawaida yao huwa wanageuza nyeusi kuwa nyeupe,tusijipe matumani sana sababu hawa Jamaa(Serikali ya ccm) sio watu watoa haki kabisa hasa nikilikumbuka hili la Lema!!!
 
Hell no na hapo wakizingua tunawasha moto kamili sasa maana ya Arusha tumewastahi, mawaziri wamegoma kujichomoa mwiba, Pinda kawekuwa ukuta tena na mwanamke sasa huko kwa Lisu wasizingue jamani..
 
kwanini polisi mahakamani? ofisi yake pia nayo wamefunga kama ya Lema?
wakimpora ubunge mjue hakuna uhuru wa mahakama
lazima katiba mpya ianishe namna ya kuwawajibisha majaji kama walifonya Kenya
tuna kila sababu ya kuondokana na majaji wa kisiasa,jaji mkuu na makamu wake wachujwe na bunge
na ambao wanaonekana kushabikia siasa watimuliwe mara moja.katiba mpya nchi mpya
\Lissu hangoki wala msihofu
 
Halafu tunaambiwa kuna uhuru wa mahakama kwenye Dola yetu! Hivi mmewahi kujiuliza ni nani anapanga kalenda ya matukio kwenye dola yetu? Angalia namna watanzania wanavyohamishwa mawazo yao kutoka kwenye issues. nitarudi kufafanua. I bet hukumu hii sio rafiki kwa TL
Kikwete anaondoka na ccm come 2015!
Ni dhahiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom