Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

mkuu,mbona hamkukaa kujadili ahadi za kikwete ambaye ndie mtawala wa nchi?mpaka mkaanza jadili ahadi za lissu?na huyo unaemuita msomi ameshindwa kujua kwanini lissu mpaka sasa hajatimiza ahadi?majungu tu tena achana jembe wewe huyo unaemuita msomi hata asome vpi hatakaa aufikie uwezo wa lisu.jezea lissu nini
Tujadili ahadi ya serikali ya CCM ya kupeleka ng'ombe 500 kwa gharama ya shs 200,000,000/=. Nimesikia wakati wa hotuba ya PM wakati anafunga kikao cha bunge, walahi, sikuamini. Halafu ng'ombe waliokufa ni zaidi ya laki nne kwa wilaya tatu!!!!! Kuwafidia wananchi wote walioathirika si ni balaa.

Hapo hatujahesabu mbuzi, kondoo, ngamia na kuku.

It happens only in Tanzania!!!!!!!
 
una orodha ya ahadi za jk alizoahidi wakati wa kampeni? kama huna wala usizifuatilie maana kama unashtuka hiyo ya Lissu, za jk utazimia

Hii haiwezi kuhalalisha kutotimiza ahadi ya yale CDM walioahidi wananchi. Kutekeleze kile ulichoahidi ni moja ya nyenzo muhimu kujiletea kuaminiwa na kuheshimika mbele ya wapiga kura na jamii kwa ujumla.

Kamwe tusiahidi tusiyoweza kutekeleza, vinginevyo hatutatofautishwa na yale tuyapingayo (ahadi hewa).
 
Makosa ya CCM hayawezi kurudiwa na CHADEMA. Tukumbuke CHADEMA wanasema CCM ni wazuri wa kuhubiri na kutoa ahadi lakini utekelezaji hakuna. Sasa kama Tundu Lissu alitoa ahadi ni vema akaitimiza vinginevyo hawezi kuisema CCM - na huu ndio mtihani walio nao CHADEMA wa kuhakikisha wanatenda tofauti na CCM.
Uko sahihi sana.
 
Badala ya kujiridhisha na ahadi hewa za mahewa sisi tuwe upande mwingine wa ukweli na uhakika. kwa maneno mengine tusiwe wavivu wa kufikiria kwa kuangalia ya mahewa. tu brain storm vya kutosha...
 
Mtoa mada anamanisha katika ahadi zooote alizotoa kwa wapiga kura wake ameshazitimiza,isipokuwa bado moja tu ya kuchimba visima kumi.kwa mantiki hiyo lisu jembe kuliko hata jkjkjkjk wake.na asitie shaka bado miaka mitatu,i'm sure atakuwa ameshachimba visima 12
 
Yaani wewe katika maendeleo ya singida mashariki umeona visima tu?

Lissu amesaidia wachimbaji wadogo wadogo wa madini jimboni kwake walikua wanasumbuliwana polisiccm lkn Lissu amekomesha hilo, watu walikua wanasingizwa kesi za uongo hilo amesimamia halitokei,na mwisho ujue kwamba Lissu ameongoza hilo jimbo kwa miezi 17tu, lakini CCM Wameongoza miezi 612 sawa na miaka 51 hawajafanya LOLOTE, pima uzito then ndo useme nani anaepaswa kulaumiwa.

UNAMJUA LISSU UNAMSIKIA?
 
M4C, POWER OF THE PEOPLE, Haitakuwa na maana kama hatuta sikiliza matatizo ya watu na kuya tatua, naomba tundu lissu apate ujumbe huu na kuuzungumzia kimatendo.
 
Ukianza la utekelezaji wa Ahadi za uchaguzi utachoma wengi hata JK AHADI Za 2005 hajazitekeleza mpaka leo!Mi nafikiri mazingira ya ahadi za Arumeru mashariki ni tofauti na singida mashariki.Lakini wananchi wanatakiwa kuwa na subira issue si aliahidi ndani ya miaka miatano?au alisema ndani ya miaka miwili?Uvumilivu sometime wakifanya hivi watageuka kichwa cha mwendawazimu kila mgombea atakuwa ni 5 miaka kisha wanamchapisha mwendo.huyo aliyemtangulia Lissu alikaa miaka mingapi?na alitekeleza ahadi zake kwa muda gani?
 
Wakuu kwanini tunapenda kuwa mediocre..?

Issue sio kwamba CCM wamefanya nini au hawakufanya nini..?, huwezi kujilinganisha au kujisifia kwa kumshinda kilema kwenye riadha.., Point ni kwamba kama kuna uwezekano wa kujenga hivyo visima na alihahidi basi avijenge.., mambo ya kwamba sio kazi yake au kwanini Serikali isifanye is non of the people concerns.. (Kama alitoa ahadi). Kwanini kama uwezo upo asifanye yale ambayo yamewashinda wengine.., ?

The greatest danger for most of us is not that our aim is too high and we miss it, but that it is too low and we reach it.
-- Michelangelo
 
Ahadi ni deni Lissu..kama ni kweli hujafanya walau kisima kimoja jitahidi utekeleze..muda hausubiri
 
Wizi mtupu! Hakuna mabadiliko tz,hao wanaojifanya wapinzani nao wakishika dola wameshaonekana wazi hawawezi badilisha chochote kwa watz wote wanaogelea kwenye mfumo ule ule wa kibepari unaohamasisha ubinafsi.Njaa tu na kutafuta umaarufu ndo kunawasumbua
 
Tundu Lissu sasa hivi anadeal na janga la Kitaifa kwanza, la kuhakikisha yeye na chama chake wanaing'oa hiyo mizizi ya Ufisadi katika Taifa letu, wakishamaliza hiyo kazi ambayo ndio kubwa kuliko hizo za kwenye majimbo kama hizo ahadi za kuchimba visima, wakishafanikisha hii kazi kubwa iliyopo mbele yao, basi hao wananchi majimboni wajue ndio watakuwa wamekomboka ki kweli kweli !

Watapata huduma zote za jamii wanazostahiri/zinazotakiwa na siyo visima peke yake tu, wawe wavumilivu kuanzia 2015 kazi itakuwa utekelezaji wa Majimboni sasa!!

PEOPLESSSSSSSSSS POWEEEEEEEEEERRRRRRRRR!!!!!!
 
Sioni ajabu ya wanasiasa kama Lisu, kama aliweza mteka nyara Mkuu wa Wilaya ya Igunga naye akiwa ni Mwanasheria, hana hekima na maadili. Singida Mashariki watamdai na kumsuta kwa kuwalaghai. CHADEMA waangalie maslahi ya Waliowaamini kwa kura Zao. Wakiuza hizo VX 3 tu watajenga visima vyote pale jimboni kwa Lisu. Si shangai Arumeri kwa sababu CHADEMA ni chama cha kaskazini.
 
Yaani wewe katika maendeleo ya singida mashariki umeona visima tu?

Lissu amesaidia wachimbaji wadogo wadogo wa madini jimboni kwake walikua wanasumbuliwana polisiccm lkn Lissu amekomesha hilo, watu walikua wanasingizwa kesi za uongo hilo amesimamia halitokei,na mwisho ujue kwamba Lissu ameongoza hilo jimbo kwa miezi 17tu, lakini CCM Wameongoza miezi 612 sawa na miaka 51 hawajafanya LOLOTE, pima uzito then ndo useme nani anaepaswa kulaumiwa.

UNAMJUA LISSU UNAMSIKIA?

Mkuu nashukuru sana yani. Umenitia sana moyo.
 
Juzi nilikutana na rafiki yangu mmoja ambaye ni msomi wa shahada ya uzamili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam na ni mzaliwa wa Singida Mashariki, jimbo linaloongozwa na Lissu. Tukiwa safarini tulianza kusimuliana mambo mbalimbali yaliyokuwa yamejiri bungeni jana yeke. Nilimsimulia rafiki yangu juu ya muongozo uliokuwa umeombwa na Lissu kwa spika baada ya spika kubatilisha hoja ya zitto kabla hoja hiyo haijafika mezani kwake. Nilimsifu Lissu nikasema yule jamaa ni JEMBE kweli.

Jamaa yangu aliniambia kweli Lissu ni jembe lakini haoneshi u-jembe wake jimboni kwake. Nilishtuka na kumwambia aache utani akaniambia habari ndo hiyo kwamba Lissu amekuwa moto bungeni lakini jimboni kwake ameshindwa kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni. Nilimuomba anithibitishie maneno hayo kwani sikuamini kama Lissu angewasaliti wapiga kura wake. Jamaa akaniambia wakati wa kampeni Lissu aliahidi visima 12 endapo angechaguliwa kuwa mbunge na kwamba chama chake cha CHADEMA kiliahidi kumuonezea nguvu ya kujenga visima hivyo, lakini takribani miaka miwili sasa Lissu hajachimba kisima hata kimoja na kwamba wananchi wengi wamekata tamaa na wameahidi kumuhukumu katika uchaguzi mkuu ujao kama hatatimiza ahadi zake.

Zaidi ya hapo niliambiwa kitu ambacho Lissu amefanya ni kuwakingia kifua wananchi wake wasichangishwe michango mbalimbali kitu ambacho kimechangia halmashauri pia kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake kwa madai kwamba wananchi wake hawachangii kuwezesha kukamilika kwa miradi hiyo. Kilichowaumiza na kuwasikitisha zaidi wananchi wa singida mashariki ni pale Joshua Nassari alipoanza kuchimba visima siku moja tu baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo la arumeru mashariki.

.

Sikulaumu mtoa maaada, naamini wewe ni mbumbumbu mkamata hapa na kutoa bila kufikiri, ila nataka nimuongelee huyo MSOMI wa Master degree(uzamili) ambaye kweli kwenye hii 2012 kuna mtu bado anaongelea visima.. analilia visima.. hatubezi ni kweli kwamba jamii yetu kwa kipande kikubwa bado iko duni sana, watu wanakunywa matope, lakini kujiita msomi na bado unashabikia watu kunywa matope usomi gani huo.. cha pili msomi gani hajui halmashauri zinavyoendeshwa.. ok fine mtu huwezi kujua kila kitu but kwanini uwe mzembe wa kuchukua lau dk kumi ukasoma miongozo na miundo ya serikali za mitaa na halmashauri zake..

Miundo ya madaraka mikoani imezipa halmashauri kubuni na kusimamia ukusanyaji wa kodi mbalimbali kwa jazilizo la maendeleo ya maeneo husika. mbali na ruzuku za serikali, mishara, na bajeti kuna ukusanyaji halali wa mapato ya ushuru ambao wananchi kwa miongo ya miaka wamekuwa wakilipa na hii haibishaniwi. halmashauri zinatakiwa kupokea asilimia ya mauzo ya zao la biashara (kama lipo) na ruzuku zake. hilo linafanyika kwa pamba, Tumbaku, Korosho na mengineyo. lakini pia Ushuru wa mkaa na mazao ya misitu ambayo pengi tu inafanyika. Mbali na hapo halmashauri zimebuni kodi ya baiskeli inayoitwa kipande, sasa kuna bodaboda ambazo nazo halmashauri zinahoji ziko chini ya nani.. na kwa maeneo mengi kadhia ya ushuru wa namna hii ipo na inaendelea..

sasa katazo wanaolikataa wanaume wenzako hawa wenye uwezo wa kufikiri ni utitiri wa ushuru wa njiani.. una kuku, bata, mayai, ndizi ambazo maskini ya mungu umejibebea unaenda kuuza lugelelo, unakuta vijana wamepaki baiskeli njiani na mmoja kavaa kama mgambo ingawa nguo zenyewe zimeshachafuka, kuchujika na kuchakachuka, wanambana mwananchi atoe mia mbili, tatu, nne za ushuru.. umebeba nafaka unawahi kuuza wanakunanga utoe ushuru.. umebeba maboga au mchicha wanakusimamisha na unatozwa ushuru, mbaya zaidi ukifika sokoni nako kule kuna ushuru.. kinachotendeka hapa lile zoezi la kamatakamata la njiani linasimamiwa na serikali za vijiji, na wao huzitafuna hela zote.. zile za sokoni hutafunwa na wakuu wa minada na masoko na kiduuchu hufikishwa kwenye halmashauri.. na mara nyingi mwenyekiti na diwani ambapo soko hilo lipo ndani ya kata yao wao hunufaika sana na ushuru huo wakishirikiana na wakuu wa masoko au minada.

sasa msomi asiyechunguza haya anabwatuka tu inasikitisha sana.. lakini simlaumu ndo wasomi wa chuo chetu cha bibi wengi tuko hivyo.. kaposho ka masomo(boom) kenyewe kiduchuu, na bado Mkono anawapa kwa kukunjiana ngumi, masomo yenyewe ni ilimradi, watu darasani naskia wanabanana sana siku hizi, supplementary za kumwaga, watu wanabebeshwa frustrations mwanzo mwisho, unategemea utapata msomi mwenye upeo wa kuwaza hapo.. usichakachue Usemi, Joshua alisema Kesho yake baada ya kupokea Cheti cha Ushindi kwamba ataanza kumfuatilia Ndesa-pesa(Mburo) aliyetoa ahadi ya Visima. Ataanza Kumfuatilia sio ataanza kuchimba .. usichakachue usemi msomi wetu..

Tukiachana na MSOMI wetu wa leo.. My Take' ...Wote wataogombea au wanaogombea Ubunge na wataogombea nafasi zozote sa kisiasa kuanzia 2014 serikali za mitaa, na 2015, Urais, ubunge na udiwani, natoa RAI hii kwenu....TOENI ahadi lukuki, hata kama ni kuwanunulia ndege wananchi semeni tu, hata kama ni kuwazawadia wake au waume zaidi semeni tu, semeni kila ambacho mnadhani wananchi watakipenda, lengo ni KUWAONDOA MAGAMBA MADARAKANI KWA VYOVYOTE VILE.. CHAMA HIKI NI ZAIDI YA BALAA.. ni wanyonyaji wasioridhika..hata watoto hunyonya miaka miwili maxmum, ila wao wananyonya tu miaka fifte sasa.. how come.??CCM should feel shame in the name of Uzalendo.

Kila kitu kizuri ukipeleleza wanakwambia cha mweshimiwa, majengo mazuri ya waheshimiwa, magari mazuri yenu, sio kwamba tunaona wivu ila roho inauma tu, sasa hadi mbuga ya katavi mmeimega na kujichakachulia.. mbona mnatutenda hivi sisi wananchi tumewakosea nini?, kweli kupokea tshirt na kanga zenu ndio mnatuadhibu namna hii, ok tembo mmeuza.. twiga mmeuza kwa njia zisizo halali, basi tupeni hata senti mbili tutengenezeee dawati hamtaki, mie sijui aliyewaroga nani nyie CCM..

Halafu naona labda mnaturoga kwa dawa kali sana, imagine Arumeru, kampeni hamkufanya bali mmetumwagia matusi ya nguoni na ya sehemu za siri kabisaa, mmefanya ujauzito kama kituko wanaume wazima hooovyo na kumzalilisha mwanamke mbele ya jamii kwa uwazi, lakini ajabu watu mliowaroga wakawapa kura takriban 24,000 hivi, aisee.. misukule tanzania haita kaa iishe..
 
Miaka mi2 ya Lissu inawauma sana nyie magamba.Je! nyie mmelitawala jimbo zaidi ya miaka50 mmeleta nini pa1 na kuwachangisha watu maskini?.

KABURI LENU LIPO TAYARI, TUNASUBIRI MKATE ROHO TUWAZIKE 2015 BILA SANDA
 
Wakuu kwanini tunapenda kuwa mediocre..?

Issue sio kwamba CCM wamefanya nini au hawakufanya nini..?, huwezi kujilinganisha au kujisifia kwa kumshinda kilema kwenye riadha.., Point ni kwamba kama kuna uwezekano wa kujenga hivyo visima na alihahidi basi avijenge.., mambo ya kwamba sio kazi yake au kwanini Serikali isifanye is non of the people concerns.. (Kama alitoa ahadi). Kwanini kama uwezo upo asifanye yale ambayo yamewashinda wengine.., ?

The greatest danger for most of us is not that our aim is too high and we miss it, but that it is too low and we reach it.
-- Michelangelo

Kumbe tupo 2014!.Ndo maana umekomalia ahadi ya kamanda ndani ya miaka mi5
 
Kamanda Uko sawa kabisa, nikosa la Jinai kuiga kwa walioshindwa CDM hatutakiwi kujifananisha na Magamba kamwe.
M4C, POWER OF THE PEOPLE, Haitakuwa na maana kama hatuta sikiliza matatizo ya watu na kuya tatua, naomba tundu lissu apate ujumbe huu na kuuzungumzia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom