Tundu Lissu aitwa na Jeshi la Polisi: Ni kuhusiana na Sakata la Gazeti la Mawio

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.

Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.

Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu huyo au umaarufu wake kwenye jamii.

======

Wahariri wa Mawio wachiwa, Lissu kuhojiwa leo

Kwa ufupi

Waliachiwa jana saa 6.40mchana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao walisaini hati ya Sh20milioni.

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana imewaachia kwa dhamana Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa baada ya kuwashikilia tangu juzi.

Wakati wahariri hao wakiachiwa, imeelezwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ametakiwa kufika polisi leo kwa mahojiano dhidi ya tuhuma zinazowakabili Mkina na Idrissa. Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wakili wa kujitegemea, Peter Kibatala wamesema Lisu anatarajia kuhojiwa leo na polisi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuitwa kwa Lissu alisema hana taarifa hizo lakini Lissu mwenyewe alisema ameitwa na kwamba leo mchana atakwenda. Mkina na Idrisa walijisalimisha juzi mchana katika Kituo cha Polisi cha Kati baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa madai ya kuandika habari za uchochezi ambako walihojiwa kwa saa nane. Waliachiwa jana saa 6.40mchana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao walisaini hati ya Sh20milioni.

Wadhamini hao ni Robert Katula, Michael Sarungi na Josephat Isango. Wakili wa wahariri hao, Peter Kibatala alisema ni busara kuwapa muda polisi kufanya uchunguzi.

Mkina alisema wamehojiwa na wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa mbili asubuhi hadi hapo kesi yao itakapoisha. Idrissa alisema baada ya kujisalimisha, askari walianza kumhoji kuhusiana na habari iliyoandikwa katika gazeti la Mawio yenye kichwa cha habari Machafuko yaja Zanzibar.

Chanzo: Mwananchi
 
WanaJF,

Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.

Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.

Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu au umaarufu wake kwenye jamii.

Wangeanza na ile TEAM LUMUMBA inayotoa mitandaoni taarifa za vifo na magonjwa kwa viongozi wa upinzani ndipo nitaona kweli jeshi linafanya kazi kitaalamu vingine ni Tawi dogo la CCM kama ilivyo TCRA
 
WanaJF,

Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.

Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.

Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu au umaarufu wake kwenye jamii.
mambo mengine yaajabu sana hivi kama tundu lisu angekuwa mmiliki wa gari na akaajiri dereva mwisho wa siku akamwamuru dereva kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na hatimaye wakapata ajali hii imekaaje mahakamani dereva (mtaalam) anaweza kujitetea kwa madai ya kupewa amri na tundu lisu (mmiliki)
 
Kwani kusema kwamba Mgonjwa anayepumulia mashine anaweza kufa, unaambiwa ni uchochozi?
Mkuu hao wanaitwa vijana wa mitandaoni, kazi yao ni moja tu kutetea maamuzi ya wanachama wao bila kujali sheria wala nini. Ashukuriwe Mungu watanzania wa leo si kama wa zamani... wanajua baya na jema
 
Kuna habari Chamanzi,mbagala watu wanaibiwa sana majambazi yanatumia siraha nzito wao wapo busy na hao wasomi ambao madhara yake si makubwa kuriko kuuliwa watu huko..na police mpo kimya mnakuja na hoja zisizo na mashiko kabisa..
 
WanaJF,

Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.

Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.

Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu huyo au umaarufu wake kwenye jamii.
Kama kuna habari za uzushi waende tu mahakamani. Tabia ya ku-intimidate haifai na Polisi wakome.
 
WanaJF,

Baada ya polisi kumaliza mahojiano na wahariri wa gazeti la Mawio na kuwaachia huru, sasa jeshi hilo linaelekeza nguvu zake kwa Lissu, ambae inasemekana yeye (Lissu) ndio chanzo cha habari za uchochezi zilizo pelekea gazeti hilo kufutwa na waziri mwenye dhamana na habari, ndugu Nape.

Katika mahojiano ambayo jeshi la polisi limefanya na wahariri wa gazeti la Mawio, jeshi limebaini kuwa mtu ambae ametajwa mara zote na wahariri hao kuwa chanzo cha habari ya kizushi iliyopewa kichwa cha habari, "Zanzibar Pawaka" ni Tundu Lissu. Habari zinasema kuwa tayari jeshi hilo linae Tundu Lissu katika himaya yao tayari kwa ajili ya mahojiano na mwanasheria huyo wa CHADEMA na mbunge.

Aidha, Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine, limejipanga kukomesha tabia ya kueneza habari za uzushi na kushughulikia mtu yeyote anayeeneza uzushi ambao utapelekea uvunjifu wa amani bila ya kujali nyadhifa ya mtu huyo au umaarufu wake kwenye jamii.
Hapo kwenye logo naona bendera ya kijani. Wala sina shaka na wewe
 
Back
Top Bottom