Tundu Lissu afunguka bungeni

Jamaa namuonea huruma sana kwani anaishi na jamii ambayo hiko gizani,Tanzania is still in dark ages.
 
Jamaa huwa anaongea english bungeni'sijui kule iramba wote wanajua english!!!!

Mbona wabumnge wengi wa CCM ni vilaza hata kuchangia Bungeni hawawezi na wanapitisha sheria kwa lugha ya kiingereza je kwenye majimbo wakiwamo wenyewe wanajua kiingereza ,je wajua kwamba ni lugha rasmi bungeni
 
Mchekini Mh. Tindu Lissu anavyo kandamiza Magamba Bungeni now...

Ananukuu matukio mengi sana hasa rushwa za uchaguzi, Uteuzi wa wakuu wa wilaya na Mikoa ambao woote ni wabunge wa viti maalumu. Lissu anahoji kwa mujibu wa katiba tuliyonayo saa mkuu wa wilaya au mkuu wa Mkoa ni wa mtumishi wa serikali ambayo inapaswa kujibu hoja za wabunge waliopo bungeni, (ieleweke kuwa Bunge ni mhimili tofauti na ule wa serikali) sasa je wabunge waha wa kuteuliwa wanafanya nini bungeni wakati wanapaswa kutekeleza yanayojadiliwa bungeni? Pili; wanapokuwa bungeni wanakuwa wanakosoa serikali hiyohiyo ambayo imewaajiri?

Amesema mengi ila hili limenigusa zaidi;

- majaji waliopo ni wazee, wanaingia kwa kujuana zaidi na hawana vigezo vya kuwepo kwenye nafasi zao.....

Ndugai aponda na kuwapa mda Kambi rasmi ya Upinzani na kuwapa mda mpk jioni warekebishe kipengele hcho au walete adendum ya kurekebisha tamko hlo......

Binafsi sioni uvunjifu wowote wa maadili katika hlo kwn ni ukweli ulio wazi......... sna sna naona propaganda znaendelea bungeni.

Kwa hili lakuwatukana majaji hana pa kutokea na amedhihirisha ni kilaza wa sheria kwa kutojua mipaka ya kila muhimili wa dola, mkaribishe home basi kesho mkuu

Hivi hotuba ya kambi ya upinzani inaandaliwa na mtu mmoja mwenye influence anu inaandaliwa na jopo maalumu la kambi ya upinzani? Je Bajeti hiyohiyo inaweza kutumika wakiwa madarakani? Nauliza hivi kwakuwa sijona chochote alichosema Lisu nimesikia makelele yaliyoambatana na nguvu nyingi hadi kaharibu kipasa sauti na meza yenyewe akahamia kwa mwingine. Zaidi ya hapo sijaona kitu kama bajeti ila tu kuishambulia serikali kana kwamba anafanya kampeni. Kaaaazi kwelikweli.Tunachezewa akili kwa stali ya kipropaganda
 
Wengine hawalijui hili , ngoja pro cdm uwaone watakavyo kuijia juu, ila kiukweli jamaa leo kaaibisha sana, jamaa ni mchovu sana wa sheria. Na Lissu ni mtaalam wa sheria za mazingira na si mtaalam wa sheria za katiba
 
Lisu ni Simba aneng'ata bila huruma akiwinda lazima akamate nyama,uwezo wake wa kuchambua mambo,kwa vifungu na kwa kuzingatia kanuni na sheria, uwezo wake huo wa kujenga hoja na kutokuwa na hofu, na kukosoa serikali umemfanya aonekane ni mbunge aliekuwepo bungeni kwa kipindi kirefu ,kumbe ni miaka miwili tu na nusu ya maisha yake ya bungeni.
Kiukweli tukiwa na watu kama lisu hii serikali dhaifu haitakohoa.

Hakika ni kifaa! Ila tu tumuombee ulinzi wa Mungu wasije wakamvizia kama ilivyo kwa slaa na mnyika! Mungu awalinde hawa wapiganaji wetu
 
Eng. Manyanya hii ni chungu lakini dawa ngoja mmpewe kweli yenu labda mlikuwa mjitambui kuwa mpo kwa fadhila ambayo ni kinyume na sheria.Mtajibeba...:loco:
 
Nimemshangaa MWANASHERIA MKUU kujaribu kumbeza LISSU eti si mweledi wa Sheria na pia hajui Kiingereza.Sote WANANCHI tunajua jinsi MWANASHERIA huyu asivyoweza kujieleza hata kidogo,hawezi hata kujenga HOJA ndogo tu zaidi hata KISWAHILI hakijui sembuse KIINGEREZA anajikanyaga tu.Alipokuwa JAJI bila kusoma hawezi kukudadavulia sheria yoyote hata BUNGENI mnaona jinsi akirushiwa HOJA anavyoweweseka.AIBU mwanasheria yeye naye ameonekana hiki cheo kwa kujuana tu.
 
Haya ni majibu ya hoja za Lisssu au ni kiburi na U ccm unamsumbua AG =
 
Twendeni na bado. Aibu yenu mulioichagua CCM. Japo chama nilichochagua hakikufua dafu hata 4 bora ila najivunia.
 
Hivi inakuwaje Tanzania inaweza kuwa na watu mahiri kama hawa akina Lissu halafu Nchi/Serikali inaongozwa na Mibomu? Nashindwa kuelewa. Haiyumkiniki kwa kweli! WTF?
 
Nimemshangaa MWANASHERIA MKUU kujaribu kumbeza LISSU eti si mweledi wa Sheria na pia hajui Kiingereza.Sote WANANCHI tunajua jinsi MWANASHERIA huyu asivyoweza kujieleza hata kidogo,hawezi hata kujenga HOJA ndogo tu zaidi hata KISWAHILI hakijui sembuse KIINGEREZA anajikanyaga tu.Alipokuwa JAJI bila kusoma hawezi kukudadavulia sheria yoyote hata BUNGENI mnaona jinsi akirushiwa HOJA anavyoweweseka.AIBU mwanasheria yeye naye ameonekana hiki cheo kwa kujuana tu.

Lissu ni mropokaji tu hajui sheria, isipokuwa anajua uropokaji wa sheria na kiingereza chake ni cha kuunga unga, ni janga la kitaifa Lissu, Tundu ni mfa maji haichi kutapa tapa

Record ya Judge Werema sio nzuri. Hukumu zake kibao zimetupiliwa mbali. Hawezi hata siku moja kushindana na record ya Tundu Lissu mahakamani. Na tunapokuwa na Manasheria mkuu wa serikali anayesimama bungeni badala ya kutoa ufafanuzi wa kisheria anajikita kumshambulia mbunge -persnally, ni janga la taifa.

Werema anaweza kujiinua sana kwa sababu pengine ana short memory. Angekuwa na memory nzuri angekumbuka Lissu na ule muswada wake na Celina Kombani walio-download kwenye google. Muswada ulirudi bungeni thanks to Lissu na kufanyiwa marekebisho makubwa. Na hata yeye mwenyewe Werema (hansard) alimsifia Lissu kwa uelewa wake wa sheria. Sasa keshapata chips kuku kasahau!
 
Duhh sasa hii aibu kweli. Mwanasheria asiyeweza control emotion provocation, ni Tabu tu. Je wakikutana mahakamani si atamrukia Lisu.
 
Kuna vitu vingi na vya msingi amevizungumzia hasa uteuzi wa wakuu wa mikoa/wilaya. Wengi wao wamepewa kama zawadi bila kujali uwezo na maadili ya mtu. Ameuliza kwamba hawa wakuu wa mikoa/wilaya ambao pia wamo bungeni ni nani anayefanya kazi zao wakiwa bungeni?, naona hapo angeenda mbali zaidi kwa kuwachanganya na mawaziri ambao pia ni wabunge, je nani anafanya kazi zao za uwaziri wakiwa bungeni?
 
Lissu ni mropokaji tu hajui sheria, isipokuwa anajua uropokaji wa sheria na kiingereza chake ni cha kuunga unga, ni janga la kitaifa Lissu, Tundu ni mfa maji haichi kutapa tapa

Basi wewe ndiyo unajua ndiyo maana unafanya na upo hapo ulipo mwenzako anajua anachofanya na hata wewe usipotambua pamoja na mabosi wako wanaojua mchango wake wanamtambua.
 
Nimemshangaa MWANASHERIA MKUU kujaribu kumbeza LISSU eti si mweledi wa Sheria na pia hajui Kiingereza.Sote WANANCHI tunajua jinsi MWANASHERIA huyu asivyoweza kujieleza hata kidogo,hawezi hata kujenga HOJA ndogo tu zaidi hata KISWAHILI hakijui sembuse KIINGEREZA anajikanyaga tu.Alipokuwa JAJI bila kusoma hawezi kukudadavulia sheria yoyote hata BUNGENI mnaona jinsi akirushiwa HOJA anavyoweweseka.AIBU mwanasheria yeye naye ameonekana hiki cheo kwa kujuana tu.

Hata mimi nimeshangaa sana! Halafu anamtisha kuwa ataweza kuishia kwenye kamati ya maadili as if Tundu Lissu amejihusisha na 'malpractice' yeyote. Hivi hawa watu kwa nini hatawaki watu wakosowe mfumo mbaya? Baadala ya kujenga hoja wanaanza ku'attack' wakosoaji. Wiki iliyopita alidai Tundu Lissu hajasomea Katiba as if kuchingia bungeni kuhusu Katiba mpaka uwe ume'specialise' kwenye Constitutional Law. Jamani kama mfumo kushindwa kufanya kazi sasa imefika mwisho. The current ruling system is falling apart/collapsing!
 
Back
Top Bottom