Tundu Lissu afunguka bungeni

Msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu wizara Sheria na katiba Mh Tundu Lissu amedai kuwa Naibu mkurugenzi mkuu wa Usalama wa Taifa Mr Jack Zoka, ACT Ahmed Msangi na Rama ni miongoni mwa watuhumiwa ktk sakata la mateso ya Dr S. Ulimboka huku akirefer gazeti la mwanahalisi. Alielezea kuwa kutesa ama kutaka kuua ni kosa la jinai lililotendwa na watuhumiwa hao. Wakati akitaka kuelezea maoni ya Kambi rasmi ya upinzani kuhusu sakata hilo, muda uliisha. Nikipata hotuba nzima ya upinzani nitaiweka humu.
Utakuwa umefanya jambo la mbolea sana
 
Amesema mengi ila hili limenigusa zaidi;

- majaji waliopo ni wazee, wanaingia kwa kujuana zaidi na hawana vigezo vya kuwepo kwenye nafasi zao.....

Ndugai aponda na kuwapa mda Kambi rasmi ya Upinzani na kuwapa mda mpk jioni warekebishe kipengele hcho au walete adendum ya kurekebisha tamko hlo......

Binafsi sioni uvunjifu wowote wa maadili katika hlo kwn ni ukweli ulio wazi......... sna sna naona propaganda znaendelea bungeni.

Source: Bunge Live

Nawakilisha.....


Nukuu sahihi hapo kamanda ni hii hapa;

UTEUZI WA MAJAJI

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua Majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko Marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya ‘haki kwa wote na kwa wakati.’ Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, kuteua Majaji wengi ni jambo moja.

Kuteua Majaji wengi wenye uwezo, ujuzi na wanaofaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu ni jambo jingine kabisa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na dalili zinazoanza kuonekana wazi kwamba baadhi ya Majaji walioteuliwa na Rais hawana uwezo, ujuzi na/au hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji ya Mahakama Kuu. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa ibara ya 109(6) ya Katiba, mtu anaweza kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana ‘sifa maalum’, na amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi.

Sifa hizo, kwa mujibu wa ibara ndogo ya (7), maana yake “ni mtu aliye na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na mamlaka ya ithibati Tanzania na amekuwa hakimu; amefanya kazi katika utumishi wa umma akiwa na sifa za kufanya kazi ya uwakili au ni wakili wa kujitegemea; ana sifa ya kusajiliwa wakili, na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.”

Sharti la kuwa na sifa hizo kwa miaka kumi mfululizo linaweza kutenguliwa endapo Rais – baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama - atatosheka kwamba mhusika ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo. (ibara ya 109(8) Tume ya Utumishi wa Mahakama inaundwa na Jaji Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa atakayeteuliwa na Rais kwa kushauriana na Jaji Mkuu, Jaji Kiongozi na wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais.

Jukumu la kwanza la Tume hii, kufuatana na ibara ya 113(1)(a), ni “kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu.” Ni wazi kwamba utaratibu huu wa uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu ulilenga kumwezesha Rais – ambaye sio lazima awe mwanasheria na/au mwenye ufahamu wa masuala ya kisheria – kuteua Majaji baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania na pia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anawajibika kikatiba “... kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria....” (ibara ya 59(3).

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rais hana mamlaka ya kufanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu nje ya utaratibu huu uliowekwa na Katiba. Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina taarifa kwamba utaratibu huu wa kuteua Majaji umeachwa kufuatwa. Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na - kwa sababu hiyo - hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba juu ya uwezo na ujuzi wao na kama ‘wanafaa kwa kila hali kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.’

Inaelekea watu hao – wengi wao wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma – wanapewa ‘zawadi’ ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya Majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni. Matokeo yake ni kuwa na majaji ambao wamechoka na hawawezi au hawajui namna ya kufanya kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu. Mheshimiwa Spika, Madhara ya kukiuka utaratibu huu wa kikatiba wa uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu ni makubwa na yameanza kujitokeza wazi.

Kwanza, wapo Majaji ambao – kwa sababu ya kutokufanyiwa vetting na Tume ya Utumishi wa Mahakama – hawana uwezo wa kuandika mwenendo wa mashauri na hukumu zinazosomeka kwa sababu ya, ama kutokuwa na uwezo na ujuzi wa sheria, au kutokuwa na weledi wa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba wapo Majaji ambao – kwa sababu hizo hizo za kutokufanyiwa vetting juu ya uwezo na ujuzi wao na mamlaka husika ya kikatiba – wameshindwa kabisa kuandika hukumu za kesi walizozisikiliza na hivyo kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani usiokuwa na sababu yoyote ya msingi.

Kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu, kama ilivyo kazi ya mawakili na wanasheria kwa ujumla, ni kazi ya kisomi. Ni kazi inayohitaji watu wenye uwezo mkubwa kitaaluma na utafiti, weledi wa uchambuzi (analytical skills) na wa kuandika na kuzungumza kwa lugha ya kimombo fasaha. Watu hawa hawaitwi ‘wanasheria wasomi’ kama mapambo tu. Wanatakiwa kuwa wasomi kweli kweli. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuwa na Majaji wasiokuwa na sifa hizi sio tu kunafifisha utoaji wa haki kwa wadaawa katika mashauri yaliyoko mahakamani, bali pia kunaifedhehesha taaluma nzima ya sheria, Mahakama ya Tanzania na mamlaka yao ya uteuzi, yaani Rais mwenyewe.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe ufafanuzi juu ya jambo hili na pia itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu kwamba utaratibu wa uteuzi wa Majaji uliowekwa na Katiba utaheshimiwa kwa Rais kuteua Majaji watakaotokana na ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ili kuondokana na aibu na fedheha hii ya kuwa na Majaji wasiojua wanachotakiwa kufanya.
 
Jambo moja kubwa ambalo ni wazi kwa zama za sasa ni kwa wananchi kupoteza imani na taasisi nyeti kwenye nchi hii. BOT, TISS, Jeshi la Polisi, hizi zilikuwa zinaaminika sana. Uhalifu ukitokea mahali watu waliamini mhusika atapatikana mara moja maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo. BOT nako tuliona kama sehemu takatifu, sehemu iliyojaa wasomi wa uhakika na sio wenye masters za mashaka. Lakini sasa taasisi zote hizi zinaangaliwa kwa mashaka, na wananchi hawana imani tena.

Hili ni jambo la kujutiwa na kila mtanzania lakini kubwa ni jambo ambalo serikali inatakiwa kuliangalia kwa makini. Na badala ya kuendelea kulumbana kwenye majukwaa ya kisiasa na kutunisha msuli, serikali ingetafuta kampuni huru ya utafiti ili kubaini wananchi wamepoteza imani kiasi gani na hizi taasisi. Unless viongozi wetu waujue na waukubali ukweli, tutaendelea kusikia malumbano na kejele huku wananachi wakiendelea kuumia. Sasa imekuwa kawaida kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi wanapomkamata mwizi kwa sababu hawaamini tena Jeshi la Polisi. Tuna kazi kubwa.
 
C D M = Chama Daima Mipasho ndio kazi yenu bado kununua vifaa tu ili muanze kutumbuiza bungeni
 
Sasa akiteua majaji wanaopendekezwa na iyo Tume sijui kamati wasio na fadhila kwake, yeye ataifokeaje mahakama
 
C D M = Chama Daima Mipasho ndio kazi yenu bado kununua vifaa tu ili muanze kutumbuiza bungeni
Hivi kilishaacha kuwa chama cha msimu?
Endeleeni kugugo majina mengine kabla ya kifo chenu 2015
 
Mchekini Mh. Tindu Lissu anavyo kandamiza Magamba Bungeni now...


Ndugai aponda na kuwapa mda Kambi rasmi ya Upinzani na kuwapa mda mpk jioni warekebishe kipengele hcho au walete adendum ya kurekebisha tamko hlo......

Binafsi sioni uvunjifu wowote wa maadili katika hlo kwn ni ukweli ulio wazi......... sna sna naona propaganda znaendelea bungeni.


Mimi binafsi nakosa mvuto kabisa katika kufuatilia vipindi vya Bunge, kwani limekuwa la kisiasa mno hata kama mtu akisema hoja ya msingi, hapo wabunge pinzani na mtoa hoja watampinga vikali sana hata katika ukweli unaoonekana dhahiri.

Au kwa kumfunga mdomo mtoa hoja utakuta Spika au LUKUVI ataamua kupendekeza apewe adhabu fulani ili asilete tena hoja yake (Kumfunga mdomo)

Ni kweli kabisa hizi ni propaganda, Serikali iliyopo madarakani kwa sasa kusema ule ukweli ni kwamba imeshindwa kuongoza wanachokifanya ni "BORA LIENDE" hata kwa kutumia nguvu ili miaka iliyobaki imalizike.

HATA KIKWETE ANALIJUA hili.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
C D M = Chama Daima Mipasho ndio kazi yenu bado kununua vifaa tu ili muanze kutumbuiza bungeni

Nadhani elimu pekee uliyonayo ni kujua kubofya browser na kuingua jamii forum,kufagia na k***a vichakani,
ingawa nashawishika kuna mtu anakusaidia mpka uweze kuandika humu,ama hua unachukua siku nzima mpaka huweze comment,maana hata bibi yangu ambae hajaenda darasa hata 1 anakuzidi kifikra na mawazo
 
mbona mnakurupuka kuanzisha uzi hapa jamvini au mnataka kuonekana kwamba na nyie mpoo au mmeanzisha uzii?? Acheni kutuletea utoto wa FB hapa wakutaka sifa za kijinga eti ili ujulikane na watu wengi???? Kama huna mpya kaa kimya na tuliza yako shilingi a.k.a sifuri ili wenye data waanzishe nyuzi za uhakika??


Una hoja Mkuu ila Lugha yako inatia Kinyaa!! Kuna Hekima katika Uvumilivu na kuelekezana kwa Staha!!
 
Safi sana,hongera kamanda Lissu.....magamba mtajinyea ukombozi nauona ,,,,
 
Nadhani elimu pekee uliyonayo ni kujua kubofya browser na kuingua jamii forum,kufagia na k***a vichakani,
ingawa nashawishika kuna mtu anakusaidia mpka uweze kuandika humu,ama hua unachukua siku nzima mpaka huweze comment,maana hata bibi yangu ambae hajaenda darasa hata 1 anakuzidi kifikra na mawazo

Asante kwa tusi lako! Mimi sijasoma lakini nina busara kuliko wewe. Pia nina imani naijua computer zaidi yako. Nimezoea majibu yenu CDM naona na wewe unafaa kuimba mipasho. Jiandae kugombea ubunge ukaongeze mipasho bungeni

CDM = Chama Daima Mipasho
 
Back
Top Bottom