Tunda nimelitungua!

[FONT=Times New Roman, serif]TUNDA[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelitungua, chini puu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikalichukua, mikono juu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninaling’atua, utamu huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninalilambua, uhondo mkuu![/FONT]


[FONT=Times New Roman, serif]Tunda linanizingua, kwenye miguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelibanjua, kwa utunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotungua, ni jekunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, ni tamu tuu![/FONT]


[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikaliparua, bila kisuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda sitoliumbua, kwa wenzanguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda hili siyo mua, si karafuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda langu sio bua, na si kifuu![/FONT]


[FONT=Times New Roman, serif]Tunda limejichanua, uroda huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, kwa mkoguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda msijebagua, kisa wivuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotumbua, sio vivuu![/FONT]


[FONT=Times New Roman, serif]na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)[/FONT]


Hata mimi nimelitungua......! Japo nimeshindwa kuelezea kwa uhondo huo!
 
Tunda nilotungua
Jinale sitofichua
Uale lilochanua
Kokwaye nikabanjua!

Si chungwa nawaambia,
Si fenesi naapia
Si embe mkadhania
Tunda la Kitanzania!

Mtini nililiona,kiukweli lilinona,
Nikatamani limenya,mdomoni limun'gunya
Hisia zkasema tulia'
Tunda langu tajilia.

Mwakijiji nlomjua.shaka sikumtilia,
Kuwa tunda akilona,atataka litungua,
Kumbe nayejatulia,
Ndio keshalitungua,

Mate nlilimezea,pindi macho yakilona,
Nikizidi vumilia,ipo siku talivuna,
Kila siku chekelea,nkilona siwezi nuna,
Mwakijiji katungua,analila kwa kuguna,

Tunda mithili ya epo,ama kiembe bolibo,
Natamani piga chabo,ulilapo kwa mpigo,
Labebeka kirahisi,haliwezi kuwa zigo,
Tunda sio nanasi,na halifanani na bungo,
Mwakijiji ulotungua,sio muwa wa mafundo,
 
Back
Top Bottom