Tunda nimelitungua!

Hata mimi nililiona,
mtini lilivyonona,
Nkatamani limung'unya,
Pasi hata lidondoa.

Muda nikalivutia,
mikononi lijetua,
Nilile kwa kupembua,
chefuchefu lisijentia.
Tahamaki nastukia,Mwakijiji katungua.
 
Tunda nilotungua
Jinale sitofichua
Uale lilochanua
Kokwaye nikabanjua!

Si chungwa nawaambia,
Si fenesi naapia
Si embe mkadhania
Tunda la Kitanzania!
 
wasifu tunda
lisilo inda
mengi huvunda
twayatupa

waliparua,
pasi kujua
utaungua
ndugu sikia

unajilamba
ndani ya chumba
huku wayumba
wafurahia

litakutenda
litavurunda
nawe kukonda
na kujutia

tunda chanua
sote twajua
limechipua
hamna jipya.

using'ang'ane
hadi manane
tupa uone
litafifia
 
tuna haja ya kulijua,
na nyumbani ulikolitua,
walozea vya kubetua,
utamuwe hawataujua.

na jinale kutupatia,
wivu tusijetia,
tusije tukazania,
la uongo kujitungia

na sifa tuzidi toa,
nawe uzidi kohoa
kimya kisije boa,
tena tusije kuzodoa.

kukupongeza yatupasa,
tena siyo kupapasa,
kwa tundalo la kisasa,
ulolipata kwa sasa.

liimarishie ulinzi,
lisijetuliwa na nzi,
usijefanyiwa mapinduzi,
na waliokubuhu na uzinzi.
 
hilo tunda lilo kati, si la kufakamia
yapo matunda laki, ruksa kukamia
ila huo mti baki, mwiko kuchumia
mwanakijiji tahamaki, tena taumia
 
What a sweet fruit,
By a skillful worker,
I salute you the gardener ,
For you are a great farmer.

You played a sole role,
To make the fruit rule,
Not only in summer,
But also in winter.

Now that its ripe,
To make a recipe,
Take a reap,
Enjoy the fruit.

Please buy a gun,
Hire the watchman,
To take the guard,
Of this great fruit.

Make an iron pillar,
with copper walls,
Build a fortified city,
To secure your fruit.

I m neither a good singer,
Nor a great narrator,
I salute you Mwanakijiji,
For the wonderful work.
{ Prince Of Aba Wa Ruba, The Son Of Africa }
 
Tunda ukilikagua kichefuchefu kitakupata
Raha ya tunda kulitia kula kama bubu
Tunda husilimenye ndio raha yake

Mkuu Kuna tunda sharti umenye,
ili uweze faidi utamu wake,
Kuna mengine mpaka upasue,
Wewe muulize nazi na jamii yake
 
Tunda nilotungua
Jinale sitofichua
Uale lilochanua
Kokwaye nikabanjua!

Si chungwa nawaambia,
Si fenesi naapia
Si embe mkadhania
Tunda la Kitanzania!

Fichua tulibaini, tunda lako ulopata,
Hataliwekwa sokoni, mafisadi kulipata,
Utaliweka mezani, na kula unapotaka,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulolipata?????
 
hilo tunda lilo kati, si la kufakamia
yapo matunda laki, ruksa kukamia
ila huo mti baki, mwiko kuchumia
mwanakijiji tahamaki, tena taumia

Companero nabaini, bayoloji wabobea
Matunda yote mitini, jinsi yanavyotokea,
Tunda la mtini gani, katikati hutokea
Tunda hilo tunda gani, Mzee alolipata??
 
Hilo tunda, Tunda Ganii?
Mbona una, Sifia ninii?

Kama tunda, kuna mengii.
Hilo tunda, Tunda ganii?

Kwako tunda, ni la ninii?
hilo tunda, ni la ninii?

Je mimi nile niniii?
Kama tunda, Siajaonaa!
 
Tunda tundagani umelila?
Tunda hilo mti wake waliwa?
Tunda tungua kula na kusaza?

Tunda hilo tundagani kuliwa?
Tunda huliwa mbegu hupandwa?
Tunda huliwa utamu huganda?
 
Hata mimi nililiona,
mtini lilivyonona,
Nkatamani limung'unya,
Pasi hata lidondoa.

Muda nikalivutia,
mikononi lijetua,
Nilile kwa kupembua,
chefuchefu lisijentia.
Tahamaki nastukia,Mwakijiji katungua.

Hata kama uliona, mtini, mezani sokoni
Jinsi lilivyonona, kutamani asilani
Kwa urefu na mapana, kuligusa si utani
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi.

Hata karne ikifika, bado tunda sio lako
Mikono haitarefuka, kuikiuka miiko
Mipaka utaivuka, kufika kule kusiko
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi

Kadi nyekundu pokea, hadi mwisho wa msimu
Mzee wamkosea, kumchukulia utamu
Usia wangu sikia, vya wazee vina sumu
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi
 
Mzee katuchemsha, tundale kulitambua,
Majumbani tumekesha, Mtego kuutegua,
Mpaka sasa imetosha, tumefeli kutambua,
Mzee atategua, siku akiamua.

Mzee atategua, siku akiamua,
siku yakaribia, jibu kututajia,
ili tuweze jua, tunda alotungua,
Wote tukitambua, mioyo itafurahi.

Wote tukitambua, Mioyo itafurahi,
Pindi tukilijua, makazini tutawahi,
Katu haitasumbua, rohoze pasi kudai,
Muda umewadia, wa tundale kubaini
 
Back
Top Bottom